Post by Admin on May 30, 2015 4:16:37 GMT
Alikuwa akitoka shuleni kuelekea
nyumbani kwao. Alikuwa na
mawazo mengi juu ya masomo
pamoja na maisha yake hakuelewa
ni kwanini toka asubuhi ya siku
hiyo alikuwa akitafakari juu ya
jambo hilo.
Akiwa tayari amekwisha yaacha
mazingira ya Shule, Ghafla
mawazo yake yalikatishwa na
sauti iliyotokea nyuma yake
“Bryan …….Bryan”. Ilikuwa ni
sauti ya kike lakini ilikuwa vigumu
kwake kuitambua, inawezekana ni
kwa sababu ya mawazo aliyokuwa
nayo. Lakini hiyo sauti kwake
haikuwa ngeni, Aligeuza shingo
taratibu ili kuona ni nani
aliyemuita, alikuwa ni Mercy
aliyemuita. Bryan alimsubiri kando
kidogo ya njia. “ Mambo vipi
Bryan? Mercy alianza kwa
kumsabahi Bryan” Ah safi tu”
alijibu Bryan.
“Mbona leo uko hivyo? Aliuliza
Mercy. Badala ya kujibu
alinyamaza kwa sekunde kadhaa
kasha naye akamuuliza kwani
nikoje? Nakuona kama una
mawazo mengi au naogopa?
Hapana ni kweli siku ya leo siko
kawaida, Sasa unawaza nini Bryan
ili hali wewe bado mwanafunzi?
Nawaza maisha Mercy “ Kwa nini
unasema hivyo wakati wewe bado
mwanafunzi tena ndio kwanza uko
kidato cha pili” Nina haki ya
kuwaza hivyo kwa sababu sina
hakika kama nitaendelea na shule
mpaka mwisho. “He! Hebu acha
utani wako Bryan” Mercy alisema
huku akionyesha kutoamini Bryan
kwa kile alichokiongea.
Ni kweli Mercy kwa sababu
maisha ya nyumbani kwetu ni
magumu mno, Mama yangu hana
kipato cha kutosha kuweza
kuniendeleza na masomo yangu ya
Sekondari na isitoshe hana karo
ya term hii kuipata kwake
kwenyewe ilikuwa shida, yaani
mpaka mama auze
mandazi,vijisenti
atakavyodunduliza ndio aniwekee
kwa ajili ya karo, hapo bado
nyumbani hatujala wala
hatujavaa. Na isitoshe safari hii
ngano imepanda bei na mama
yangu hata hela ya mtaji
hajafikisha, Yaani hata sielewi
tutaishije maisha haya.
Bryan alijaribu kumuelezea Mercy
maisha ya kwao kwa uchungu
mwingi mno. Muda wote huo
Mercy alikuwa akimsikiliza Bryan
kwa makini huruma ilimjaa ila
hakuelewa ni vipi angemsaidia
Bryan.
“Bryan” Mercy aliita “Ndio
nakusikiliza unasemaje aliita na
kuuliza.
“kuna kitu kimoja naomba
nikuulize kama hutojali” “hakuna
shida we uliza tu”
“Hivi bana yako alishafariki au
bado yupo hai? Bryan alinyamaza
kama sekunde kadhaa kisha
akaguna “Duh” ni story ndefu sana
lakini nitakueleza kwa ufupi tu.
“Hakuna shida kwani shida yangu
ni kutaka kujua kuhusu hilo tu.
Lakini kabla hata Bryan hajaanza
kumsimulia Mercy juu ya Baba
yake walikuwa tayari wamefika
kwenye kituo cha daladala.
“Oya nyie madent hamuendi?Sauti
ya konda iliwashitua .
“Mercy twende tupande hii” Bryan
alimwambia Mercy. Hapana ngoja
kwanza mpakatumalize maongezi
yetu Bryan alikubali na kumruhusu
konda waende.
Mercy ni binti wa pekee katika
familia ya Mzee Josephat. Familia
hiyo ilikuwa na watoto wa nne, wa
kwanza Irene na wa pili Jacobo
akifuatiwa na Isack na
kitindamimba ambaye ni Mercy.
Hawa wote walikuwa na maisha
mazuri kwa sababu wote walikuwa
na Elimu nzuri na kila mmoja
alikuwa anakazi yake kasoro
Mercy ambae alikuwa bado
anasoma ndo kwanza yupo kidato
cha pili.
Mzee Josephati pamoja na Mkewe
Mama Irene walijitahidi kumpatia
Mercy kila hitaji ilimradi tu Binti
yao asome kama ndugu zake.
Mercy na Bryan hawakuwa
wakisoma darasa moja, Mercy
alisoma kidato cha pili B, wakati
Bryan alisoma kidato cha pili
mkondo A .Lakini wote walikuwa
kidato kimoja. Hawakuwa marafiki
kiasi kwamba wakutane na kuanza
kuongea zaidi ya dakika tano,hiyo
haikuwahi kutokea. Ilikuwa kila
walipokutana ni salamu na kila
mtu anaendelea na shughuli zake.
Toka siku nyingi Mercy alikuwa
akimpenda Bryan lakini tatizo
lilikuwa likimtatiza ni vipi ataweza
kumueleza Bryan anavyojisikia juu
yake.Alihofia kuwa baada ya
kumueleza Bryan jinsi
anavyojisikia juu yake
angeonekana kuwa yeye Malaya,
Lakini alijiapiza ipo siku lazima
angemtobolea.
Wakati Mama yuko kidato cha nne
alipewa namba na mvulana mmoja
aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu
Dar –es-salaam aliitwa Enock
Mwansasu.Mama yangu
alifukuzwa Shule baada ya
kugundulika kuwa ni
Mjamzito.Baada ya kufukuzwa
Shule Mama alimuendea yule
Mwanaume aliye mpa Mimba na
kumueleza kuwa ana mamba
yake.
Yule Mwanaume ambaye ndio Baba
yangu alikubali ile Mimba na
kuhaidi kuwa atamtunza yeye na
kiumbe kilichokuwa Tumboni.
Baba aliendelea kumtunza Mama
na kumtimizia kila hitaji ambalo
mama alihitaji mpaka nilipozaliwa
mimi. Baadaye baba alihitajika
aende Urusi kwa Masomo yake
kwa kipindi cha miaka mitano,
Lakini Baba alimuomba Mama
asijali kwani safari sio kifo, kwa
hiyo ipo siku atarudi kama Mungu
akijalia basi watafunga ndoa.
Kwahiyo waliagana na kila mmoja
akiwa na majonzi ya kumkosa
mwenziwe kila mmoja alionyesha
kuwa ana penzi la dhati kwa
mwenziwe. Baada ya hapo Baba
alisafiri na kwenda nje kusoma.
Huku nyuma Mama aliendelea
kutumiwa misaada mbalimbali na
baba.Hali hiyo iliendelea takribani
miezi sita (6) halafu hali hiyo
ikakatika ghafla, kukawa hakuna
msaada wala msaidizi. Mama
kuona hivyo akaamua kufungua
genge kwa akiba ndogo aliyokuwa
nayo. Hilo banda ndio lilimsukuma
mpaka akajenga nyumba ndogo ya
udongo yenye vyumba viwili na
sebule na hilohilo banda
limenisomesha shule.
Tuliendelea kuishi hivyo na Mama
yangu huku tukiwa tumepoteza
matumaini ya kumuona Baba
katika maisha yetu.
Ilipofika mwaka 1994 tulivamiwa
na wezi wakavunja nyumba yetu
pamoja na genge letu wakachukua
kila kitu walichokiona kuwa kwao
ni cha thamani na kasha
wakatokomea.
Hali hiyo ilimlazimu Mama yangu
awe omba omba tuliendelea kuishi
kwa kazi hiyo mpaka Mama
alipopata mtaji wa kuanzisha
biashara yake ya maandazi
ambayo mpaka sasa ndiyo
inatusaidia. Na sasa hivi
ninavyoongea na wewe Mama
yangu ni Mgonjwa sana na mimi
peke ndio tegemeo lake sijui
nitafanya nini.
Bryan alipomaliza kusema hayo
macho yake yalilengwalengwa na
machozi. Na kwa upande wa
Mercy yeye uso wake uliingiliwa na
simanzi kuu. “Pole sana Bryan
kwa matatizo hayo”.Alisema Mercy
kwa upole huku akimtazama Bryan
machoni. “Asante japo sijapoa”.
“Usijali sana Bryan kwani Mungu
hamtupi mja wake”Mercy alijitaidi
kumfariji Bryan.
Maneno yale kidogo yalimtia
nguvu Bryan, Muda ulikuwa
umekwenda sana kwa hiyo wote
wakakubaliana wapande Hice
lakini kabla ya kupanda kwenye
daladala Mercy alitoa noti ya
shilingi Elfu mbili na kumpatia
Bryan. Nashukuru sana Mercy kwa
wema wako naomba Mungu
akuongezee. “Usijali Bryan”
Alisema Mercy huku akitabasamu.
Mercy na Wazazi wake walikuwa
wakiishi mtaa wa Area D Mkoani
Dodoma na Bryan alikuwa akiishi
katika mtaa wa Chadulu katika
Mkoa huohuo.
Daladala ilipofika njia panda area
D Bryan alimuaga Mercy na
kuteremka kuelekea kwao. Moyo
wake ulikuwa ukimuenda kasi
ambavyo si kawaida yake.
“Hivi kwa nini moyo wangu uko
hivi? Mh Sio bure huko nyumbani
lazima kutakuwa na
jambo”Aliwaza Bryan na kuanza
kuongeza ukubwa wa hatua.
Alipofika hatua chache kabla ya
kufika kwao alisikia kelele.
“Jamani majirani naombeni
msaada.”Alikuwa ni mama wa
Makamo alikuwa ni jirani yao
Mama Musa. Alionekana akitokea
upande wa Maliwatoni kwa akina
Bryan huku akiwa anamkokota
mtu. Mtu huyo alionekana
amelegea mno na mdomo wake
ukiwa wazi huku povu jingi
likimtoka.
Alionekana anahema kwa taabu
sana. Mtu aliyekokotwa hakuwa
mwingine bali ni Bi Sara ambaye
alikuwa ndiye Mama yake Bryan.
Bryan alishituka sana alipomuona
Mama yake yupo katika hali ile.
Akaanza kukimbilia kule aliko
Mama Musa na Mama ili
kufahamu kumetokea nini.
“Hah Mama amekuwaje? Bryan
alishitukiaamemuuliza Mama yake
swali hilo bila kujali hali
aliyokuwa nayo.
“Fanya haraka kaite Taksi”
Alisema Mama Musa huku akiwa
anaendelea kumkokota Bi Sara
kuelekea kiliko kituo cha taksi.
Bryan hakuuliza swali zaidi alitoka
pale mbio kuelekea kwenye kituo
ch Taksi.Ulikuwa ni mwendo wa
dakika. Ulikuwa mwendo wa
dakika tano kutoka kwao mpaka
kituo cha taksi.
Huku nyuma wakina mama
wajirani walishakwishafika
kumsaidia Mama Musa.Baada ya
muda mfupi taksi ilifunga breki
miguuni kwao kwa kundi la
wakina mama “Tufikishe General”
Alisema Mama Musa huku
akifungua mlango wa wa siti ya
nyuma ya taksi alisaidiana na
wakina mama wenzake kumpakia
ndani ya taksi.Bryan alikaa siti ya
mbele.Mma Musa na jirani yake
Mama Rashidi pamoja na Mgonjwa
Bi sara wlikaa nyuma. Na safari
yakwenda hospitali ikaanza.
“Jikaze bwana wewe ni mtoto wa
kiume”Alisema Dereva walipokuwa
njiani, baada ya kumuona Bryan
analia. Bryan hakujibu zaidi ya
kuendelea kulia kilio cha kwikwi.
Mama Bryan alikuwa mgonjwa
takribani wiki sasa. Japo hakuwa
serious sana alikuwa ansumbuliwa
na BP pamoja na Athima.
Siku moja akiwa ndani
amejipumzisha akaja jirani yake
mama Musa kumtakia hali, “Haya
wajionaje leo mama Bryan” Mama
Musa alianza kwa kumsabahi
jirani yake.
“Namshukuru jalia leo ahueni”
alimjibu mama Bryan. Waliendelea
na maongezi kwa muda kama
robo saa. Baadae Mama Bryan
alimtaka radhi mama Musa kuwa
anaomba amsubiri kwa nukta
chache anaenda chooni mara
moja. Naomba nikusindikize kwa
sababu siamini kama utajiweza”
Alisema mama Musa. “Usijali
nitajikongoja”Alijibu mama Bryan.
Mama Musa alimuacha mama
Bryan aende peke yake japokuwa
alikuwa hamuamini sana hali
yake.
Baada ya Mama Bryan kutoka nje
kwa kulegalega hukunyuma Mama
Musa hisia zake zikawa hazimpi
kabisa kuendelea kubaki mule
sebuleni, akatoka nje na
kusimama mlangoni. Zilipita
dakika 5 bila Mama Bryan kutoka
msalani. Baada ya dakika hizo
kupita Mama Musa alisikia
kishindo kutoka msalani kama
mtu amedondoka vile.
Mama Musa aliuendea ule mlango
wa choo kwa haraka na kusukuma
kwa bahati nzuri ulikuwa
umerudishiwa, ulipofunguliwa
hakuamini kile alichokiona kwani
Mama Bryan alikuwa ameanguka
pembeni ya shimo la choo huku
povu likimtoka mdomoni. Mama
Musa alimuinua na kumbeba
mpaka nje.
Ndani ya taksi wakielekea
hospitali Mgonjwa alikuwa bado
hajazinduka, kufika maeneo ya
bunge Mama Musa na Mama
Rashidi wakamuona mgonjwa kwa
taabu anafumbua macho. Mioyoni
mwao wakaanza kupata
matumaini kuwa mgonjwa wao
anapata ahueni katika siti ya
mbele hakuna aliyeelewa
kinachoendelea nyuma si Bryan
wala Dereva.
Katika siti ya nyuma mambo
yakawa sivyo na matarajio kwani
Mama Bryan alianza kutupa miguu
pamoja na mikono na baadaye
akaanza kugeuzageuza macho
halafu akajinyoosha na kisha
kukakamaa.
Mama Musa alikuwa kaduwaa na
Mama Rashidi kubung’aa wasijue
cha kufanya.
Mzee Josephati na Mkewe Bi Maua
walikuwa wamepumzika sebuleni
wakiangalia TV na mara wakasikia
hodi, “karibu mlango
umeludishiwa tu” alijibu Bi maua
na mara akaingia Mercy. Usoni
mwake alivaa sura ya simanzi
kana kwamba kulikuwa na msiba
mkubwa mno.
“Shikamooni” aliwasalimu wazazi
wake “Marahaba” waliitikia kwa
pamoja. “Vipi huko utokapo ni
kheri au shari”? Bi maua
alimuuliza binti yake baada ya
kugundua hayuko katika hali yake
ya kawaida. “Heri tu mama”
alijibu Mercy huku akijilazimisha
kutabasamu.
Mama yake alielewa kuwa kuna
tatizo linalomtatiza binti yake
lakini hakutaka kumsonga sana
kwa maswali alimuacha aende
kwanza akapumzike.
Mercy alipoingia chumbani kwake
alijitupa kitandani bila hata
kubadili uniform hata kula chakula
hakikukumbuka tena kwa kipindi
hicho. Hiyo yote ilisababishwa na
fikra juu ya Bryan ni jinsi gani
ataweza kumsaidia?. Ni vipi
ataweza kumtatulia matatizo yake
aliyonayo na kumfanya aweze
kuishi kwa furaha na ni vipi
ajieleze mpaka aeleweke juu ya
hisia zake kwa Bryan. Na si hivyo
tu alikuwa anatamani siku iishe
upesi akaonane na Bryan.
Dereva hakujua kilichotokea bali
aliendelea kutereza akielekea
hospitali.
Walipita getini na kuingia ndani
kabisa hospitalini. Dereva alifunga
breki na kufungua mlango wa
upande wake alishuka na kasha
akazunguka upande wa pili na
kumfungulia Bryan.
Huku nyuma Mama Rashidi na
Mama Musa walishuka na
kumuomba dereva awasaidie
kumbeba mgonjwa. Na Bryan naye
bila kuambiwa alitaka kushiriki
katika hatua hiyo. “Ah hapana
Bryan we acha pumzika tu” Mama
Rashidi alimkataza Bryan.
“Kwanza shika hii mia tano ukale
mgahawani kwa sababu toka
utoke shule haujagusa chakula
aliongea Mama Musa.
Bryan ikamlazimu aichukue ile
hela japo kwa shingo upande.
Lakini akili na mawazo yote ni juu
ya mama yake ambaye kwa yeye
anavyomfahamu ni Mgonjwa
Mahututi alianza kutembea kwa
hatua ndogondogo huku akiwa
amenyong’onyea kuelekea kwenye
mgahawa uliopo pembeni kidogo
na hospitali ya General. Alipofika
Mgahawani akaagiza chakula na
badala ya kukila akawepo
anakitazama utafikiri ndo kwanza
anakiona.
Aliendelea kukitazama kile chakula
takribani dakika tano kana
kwamba kile chakula hakikuagiza
yeye.
Mercy alikuwa ndani ya daladala
akielekea Dodoma Sekondari shule
ambayo alikuwa akisoma. Moyoni
mwake alikuwa na furaha tele
akiamini hiyo akiamini ni siku
nyingine tena ya kwenda kuonana
na Bryan. “Oya kuna anaeshuka
hapa bohari”? ilikuwa ni sauti ya
konda.
“Shusha” Mercy alijibu. Mercy
alishuka na kumlipa konda nauli
kisha akavuka barabara akielekea
shuleni kwao.
Alipofika shule alikuta wenzake
wametawanyika kutoka assembly
kuelekea madarasani. Aliangaza
macho yake huku na kule asijue
wapi kwa kumpata Bryan.
Baadaye akaamua kwenda
darasani kwa akina Bryan ili
kuuliza kama amekuja.
Alipofika darasani kwa akina
Bryan alimuendea moja kwa moja
rafiki yake Martha ambaye ni
Monntress wa darasa hilo. “Sema
shoga mambo vipi”? Mercy
alimsabahi shoga yake huo. “Safi
tu, issue vipi?” Martha alijibu na
kuuliza, “Poa alijibu Mercy”.
“Bryan ameshafika?” “hapana
naona leo kachelewa kidogo lakini
atafika muda si mrefu” kwa
maneno yale alinyong’onyea lakini
alijipa moyo kuwa bado nukta
chache Bryan angetokea kipindi
kipindi cha kwanza kiliisha,
hakuna Bryan kuonekana cha pili
na hatimaye cha tatu Bryan
hakutokea.
Mercy ilikuwa ni huzuni kubwa
mno kwani alijihisi ni ni mpweke
kuliko.Katika vipindi vyote hivyo
vitatu hakuelewa somo hata moja
na zaidi aliona walimu wote
wanaofundisha ni kero kwake.
Alijishangaa kwa nini Bryan
amemuingia kiasi kile, ukizingatia
Bryan mwenyewe hawana siku
nyingi toka wazoeane.
Alizikusanya daftari zilizokuwa juu
ya meza yake na taratibu
alinyanyuka kwenye kiti
alichokuwa amekalia na taratibu
akaulenga mlango wa kutokea
kwenye ofisi ya walimu.
Alipoingia Ofisini alimkuta
mwalimu wake wa darasa Mr
Innocent “Morning Sir”
“Have a good day what’s ya
problem”, “I’m not feel well I think
this is Malaria” “So you want go
to the hospital”, “Yes Sir” Okay
you may”.
Alikula robo ya chakula kile kasha
akalipa hela na kunyanyuka.
Mapigo yake ya Moyo yalikuwa
yakienda mbio mno. Mwendo wake
ulikuwa wa haraka mno pindi
alipotoka mgahawani hapo
akielekea hospitalini.
Pengine ungemuona usingeweza
kuelewa anatembea au ankimbia.
Ilikuwa nusu kutembea nusu
kukimbia akaingia hospitalini na
moja kwa moja akaenda
mapokezi. “Samahani dada sijui
mgonjwa aliyeletwa muda mfupi
kabla ya sasa sijui yupo sehemu
gani? “Salamu kwanza kaka angu.
Lakini usijali sana wameingia
katika chumba cha docta”
“Samahani kwa hilo dada angu,
shukrani” Bryan alijibu na
kuondoka kwa mwendo wake
uleule kabla hajasukuma mlango
wa docta, mlango huo ulifunguliwa
na Mama Musa pamoja na Mama
Rashidi walitoka ndani ya chumba
hicho.”Vipi?”Akina mama hao
walimuuliza Bryan kwa pamoja.
Bryan kabla hajajibu aliwatazama
wakina mama hao machoni kwa
nucta kadhaa, Na kugundua
macho yao yameiva na kuwa
mekundu kuliko kawaida. Hivi
ilimaanisha wametoka kulia muda
si mrefu na hilo alilitambua na
mara ghafla fikra zake zikaunda
picha nyingine katika ubongo wake
“Nataka kumuona mama yangu”
alijibu Bryan huku mapigo yake ya
moyo yakizidi kumuenda kasi.
***JE? Nini kitaendelea…..
nyumbani kwao. Alikuwa na
mawazo mengi juu ya masomo
pamoja na maisha yake hakuelewa
ni kwanini toka asubuhi ya siku
hiyo alikuwa akitafakari juu ya
jambo hilo.
Akiwa tayari amekwisha yaacha
mazingira ya Shule, Ghafla
mawazo yake yalikatishwa na
sauti iliyotokea nyuma yake
“Bryan …….Bryan”. Ilikuwa ni
sauti ya kike lakini ilikuwa vigumu
kwake kuitambua, inawezekana ni
kwa sababu ya mawazo aliyokuwa
nayo. Lakini hiyo sauti kwake
haikuwa ngeni, Aligeuza shingo
taratibu ili kuona ni nani
aliyemuita, alikuwa ni Mercy
aliyemuita. Bryan alimsubiri kando
kidogo ya njia. “ Mambo vipi
Bryan? Mercy alianza kwa
kumsabahi Bryan” Ah safi tu”
alijibu Bryan.
“Mbona leo uko hivyo? Aliuliza
Mercy. Badala ya kujibu
alinyamaza kwa sekunde kadhaa
kasha naye akamuuliza kwani
nikoje? Nakuona kama una
mawazo mengi au naogopa?
Hapana ni kweli siku ya leo siko
kawaida, Sasa unawaza nini Bryan
ili hali wewe bado mwanafunzi?
Nawaza maisha Mercy “ Kwa nini
unasema hivyo wakati wewe bado
mwanafunzi tena ndio kwanza uko
kidato cha pili” Nina haki ya
kuwaza hivyo kwa sababu sina
hakika kama nitaendelea na shule
mpaka mwisho. “He! Hebu acha
utani wako Bryan” Mercy alisema
huku akionyesha kutoamini Bryan
kwa kile alichokiongea.
Ni kweli Mercy kwa sababu
maisha ya nyumbani kwetu ni
magumu mno, Mama yangu hana
kipato cha kutosha kuweza
kuniendeleza na masomo yangu ya
Sekondari na isitoshe hana karo
ya term hii kuipata kwake
kwenyewe ilikuwa shida, yaani
mpaka mama auze
mandazi,vijisenti
atakavyodunduliza ndio aniwekee
kwa ajili ya karo, hapo bado
nyumbani hatujala wala
hatujavaa. Na isitoshe safari hii
ngano imepanda bei na mama
yangu hata hela ya mtaji
hajafikisha, Yaani hata sielewi
tutaishije maisha haya.
Bryan alijaribu kumuelezea Mercy
maisha ya kwao kwa uchungu
mwingi mno. Muda wote huo
Mercy alikuwa akimsikiliza Bryan
kwa makini huruma ilimjaa ila
hakuelewa ni vipi angemsaidia
Bryan.
“Bryan” Mercy aliita “Ndio
nakusikiliza unasemaje aliita na
kuuliza.
“kuna kitu kimoja naomba
nikuulize kama hutojali” “hakuna
shida we uliza tu”
“Hivi bana yako alishafariki au
bado yupo hai? Bryan alinyamaza
kama sekunde kadhaa kisha
akaguna “Duh” ni story ndefu sana
lakini nitakueleza kwa ufupi tu.
“Hakuna shida kwani shida yangu
ni kutaka kujua kuhusu hilo tu.
Lakini kabla hata Bryan hajaanza
kumsimulia Mercy juu ya Baba
yake walikuwa tayari wamefika
kwenye kituo cha daladala.
“Oya nyie madent hamuendi?Sauti
ya konda iliwashitua .
“Mercy twende tupande hii” Bryan
alimwambia Mercy. Hapana ngoja
kwanza mpakatumalize maongezi
yetu Bryan alikubali na kumruhusu
konda waende.
Mercy ni binti wa pekee katika
familia ya Mzee Josephat. Familia
hiyo ilikuwa na watoto wa nne, wa
kwanza Irene na wa pili Jacobo
akifuatiwa na Isack na
kitindamimba ambaye ni Mercy.
Hawa wote walikuwa na maisha
mazuri kwa sababu wote walikuwa
na Elimu nzuri na kila mmoja
alikuwa anakazi yake kasoro
Mercy ambae alikuwa bado
anasoma ndo kwanza yupo kidato
cha pili.
Mzee Josephati pamoja na Mkewe
Mama Irene walijitahidi kumpatia
Mercy kila hitaji ilimradi tu Binti
yao asome kama ndugu zake.
Mercy na Bryan hawakuwa
wakisoma darasa moja, Mercy
alisoma kidato cha pili B, wakati
Bryan alisoma kidato cha pili
mkondo A .Lakini wote walikuwa
kidato kimoja. Hawakuwa marafiki
kiasi kwamba wakutane na kuanza
kuongea zaidi ya dakika tano,hiyo
haikuwahi kutokea. Ilikuwa kila
walipokutana ni salamu na kila
mtu anaendelea na shughuli zake.
Toka siku nyingi Mercy alikuwa
akimpenda Bryan lakini tatizo
lilikuwa likimtatiza ni vipi ataweza
kumueleza Bryan anavyojisikia juu
yake.Alihofia kuwa baada ya
kumueleza Bryan jinsi
anavyojisikia juu yake
angeonekana kuwa yeye Malaya,
Lakini alijiapiza ipo siku lazima
angemtobolea.
Wakati Mama yuko kidato cha nne
alipewa namba na mvulana mmoja
aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu
Dar –es-salaam aliitwa Enock
Mwansasu.Mama yangu
alifukuzwa Shule baada ya
kugundulika kuwa ni
Mjamzito.Baada ya kufukuzwa
Shule Mama alimuendea yule
Mwanaume aliye mpa Mimba na
kumueleza kuwa ana mamba
yake.
Yule Mwanaume ambaye ndio Baba
yangu alikubali ile Mimba na
kuhaidi kuwa atamtunza yeye na
kiumbe kilichokuwa Tumboni.
Baba aliendelea kumtunza Mama
na kumtimizia kila hitaji ambalo
mama alihitaji mpaka nilipozaliwa
mimi. Baadaye baba alihitajika
aende Urusi kwa Masomo yake
kwa kipindi cha miaka mitano,
Lakini Baba alimuomba Mama
asijali kwani safari sio kifo, kwa
hiyo ipo siku atarudi kama Mungu
akijalia basi watafunga ndoa.
Kwahiyo waliagana na kila mmoja
akiwa na majonzi ya kumkosa
mwenziwe kila mmoja alionyesha
kuwa ana penzi la dhati kwa
mwenziwe. Baada ya hapo Baba
alisafiri na kwenda nje kusoma.
Huku nyuma Mama aliendelea
kutumiwa misaada mbalimbali na
baba.Hali hiyo iliendelea takribani
miezi sita (6) halafu hali hiyo
ikakatika ghafla, kukawa hakuna
msaada wala msaidizi. Mama
kuona hivyo akaamua kufungua
genge kwa akiba ndogo aliyokuwa
nayo. Hilo banda ndio lilimsukuma
mpaka akajenga nyumba ndogo ya
udongo yenye vyumba viwili na
sebule na hilohilo banda
limenisomesha shule.
Tuliendelea kuishi hivyo na Mama
yangu huku tukiwa tumepoteza
matumaini ya kumuona Baba
katika maisha yetu.
Ilipofika mwaka 1994 tulivamiwa
na wezi wakavunja nyumba yetu
pamoja na genge letu wakachukua
kila kitu walichokiona kuwa kwao
ni cha thamani na kasha
wakatokomea.
Hali hiyo ilimlazimu Mama yangu
awe omba omba tuliendelea kuishi
kwa kazi hiyo mpaka Mama
alipopata mtaji wa kuanzisha
biashara yake ya maandazi
ambayo mpaka sasa ndiyo
inatusaidia. Na sasa hivi
ninavyoongea na wewe Mama
yangu ni Mgonjwa sana na mimi
peke ndio tegemeo lake sijui
nitafanya nini.
Bryan alipomaliza kusema hayo
macho yake yalilengwalengwa na
machozi. Na kwa upande wa
Mercy yeye uso wake uliingiliwa na
simanzi kuu. “Pole sana Bryan
kwa matatizo hayo”.Alisema Mercy
kwa upole huku akimtazama Bryan
machoni. “Asante japo sijapoa”.
“Usijali sana Bryan kwani Mungu
hamtupi mja wake”Mercy alijitaidi
kumfariji Bryan.
Maneno yale kidogo yalimtia
nguvu Bryan, Muda ulikuwa
umekwenda sana kwa hiyo wote
wakakubaliana wapande Hice
lakini kabla ya kupanda kwenye
daladala Mercy alitoa noti ya
shilingi Elfu mbili na kumpatia
Bryan. Nashukuru sana Mercy kwa
wema wako naomba Mungu
akuongezee. “Usijali Bryan”
Alisema Mercy huku akitabasamu.
Mercy na Wazazi wake walikuwa
wakiishi mtaa wa Area D Mkoani
Dodoma na Bryan alikuwa akiishi
katika mtaa wa Chadulu katika
Mkoa huohuo.
Daladala ilipofika njia panda area
D Bryan alimuaga Mercy na
kuteremka kuelekea kwao. Moyo
wake ulikuwa ukimuenda kasi
ambavyo si kawaida yake.
“Hivi kwa nini moyo wangu uko
hivi? Mh Sio bure huko nyumbani
lazima kutakuwa na
jambo”Aliwaza Bryan na kuanza
kuongeza ukubwa wa hatua.
Alipofika hatua chache kabla ya
kufika kwao alisikia kelele.
“Jamani majirani naombeni
msaada.”Alikuwa ni mama wa
Makamo alikuwa ni jirani yao
Mama Musa. Alionekana akitokea
upande wa Maliwatoni kwa akina
Bryan huku akiwa anamkokota
mtu. Mtu huyo alionekana
amelegea mno na mdomo wake
ukiwa wazi huku povu jingi
likimtoka.
Alionekana anahema kwa taabu
sana. Mtu aliyekokotwa hakuwa
mwingine bali ni Bi Sara ambaye
alikuwa ndiye Mama yake Bryan.
Bryan alishituka sana alipomuona
Mama yake yupo katika hali ile.
Akaanza kukimbilia kule aliko
Mama Musa na Mama ili
kufahamu kumetokea nini.
“Hah Mama amekuwaje? Bryan
alishitukiaamemuuliza Mama yake
swali hilo bila kujali hali
aliyokuwa nayo.
“Fanya haraka kaite Taksi”
Alisema Mama Musa huku akiwa
anaendelea kumkokota Bi Sara
kuelekea kiliko kituo cha taksi.
Bryan hakuuliza swali zaidi alitoka
pale mbio kuelekea kwenye kituo
ch Taksi.Ulikuwa ni mwendo wa
dakika. Ulikuwa mwendo wa
dakika tano kutoka kwao mpaka
kituo cha taksi.
Huku nyuma wakina mama
wajirani walishakwishafika
kumsaidia Mama Musa.Baada ya
muda mfupi taksi ilifunga breki
miguuni kwao kwa kundi la
wakina mama “Tufikishe General”
Alisema Mama Musa huku
akifungua mlango wa wa siti ya
nyuma ya taksi alisaidiana na
wakina mama wenzake kumpakia
ndani ya taksi.Bryan alikaa siti ya
mbele.Mma Musa na jirani yake
Mama Rashidi pamoja na Mgonjwa
Bi sara wlikaa nyuma. Na safari
yakwenda hospitali ikaanza.
“Jikaze bwana wewe ni mtoto wa
kiume”Alisema Dereva walipokuwa
njiani, baada ya kumuona Bryan
analia. Bryan hakujibu zaidi ya
kuendelea kulia kilio cha kwikwi.
Mama Bryan alikuwa mgonjwa
takribani wiki sasa. Japo hakuwa
serious sana alikuwa ansumbuliwa
na BP pamoja na Athima.
Siku moja akiwa ndani
amejipumzisha akaja jirani yake
mama Musa kumtakia hali, “Haya
wajionaje leo mama Bryan” Mama
Musa alianza kwa kumsabahi
jirani yake.
“Namshukuru jalia leo ahueni”
alimjibu mama Bryan. Waliendelea
na maongezi kwa muda kama
robo saa. Baadae Mama Bryan
alimtaka radhi mama Musa kuwa
anaomba amsubiri kwa nukta
chache anaenda chooni mara
moja. Naomba nikusindikize kwa
sababu siamini kama utajiweza”
Alisema mama Musa. “Usijali
nitajikongoja”Alijibu mama Bryan.
Mama Musa alimuacha mama
Bryan aende peke yake japokuwa
alikuwa hamuamini sana hali
yake.
Baada ya Mama Bryan kutoka nje
kwa kulegalega hukunyuma Mama
Musa hisia zake zikawa hazimpi
kabisa kuendelea kubaki mule
sebuleni, akatoka nje na
kusimama mlangoni. Zilipita
dakika 5 bila Mama Bryan kutoka
msalani. Baada ya dakika hizo
kupita Mama Musa alisikia
kishindo kutoka msalani kama
mtu amedondoka vile.
Mama Musa aliuendea ule mlango
wa choo kwa haraka na kusukuma
kwa bahati nzuri ulikuwa
umerudishiwa, ulipofunguliwa
hakuamini kile alichokiona kwani
Mama Bryan alikuwa ameanguka
pembeni ya shimo la choo huku
povu likimtoka mdomoni. Mama
Musa alimuinua na kumbeba
mpaka nje.
Ndani ya taksi wakielekea
hospitali Mgonjwa alikuwa bado
hajazinduka, kufika maeneo ya
bunge Mama Musa na Mama
Rashidi wakamuona mgonjwa kwa
taabu anafumbua macho. Mioyoni
mwao wakaanza kupata
matumaini kuwa mgonjwa wao
anapata ahueni katika siti ya
mbele hakuna aliyeelewa
kinachoendelea nyuma si Bryan
wala Dereva.
Katika siti ya nyuma mambo
yakawa sivyo na matarajio kwani
Mama Bryan alianza kutupa miguu
pamoja na mikono na baadaye
akaanza kugeuzageuza macho
halafu akajinyoosha na kisha
kukakamaa.
Mama Musa alikuwa kaduwaa na
Mama Rashidi kubung’aa wasijue
cha kufanya.
Mzee Josephati na Mkewe Bi Maua
walikuwa wamepumzika sebuleni
wakiangalia TV na mara wakasikia
hodi, “karibu mlango
umeludishiwa tu” alijibu Bi maua
na mara akaingia Mercy. Usoni
mwake alivaa sura ya simanzi
kana kwamba kulikuwa na msiba
mkubwa mno.
“Shikamooni” aliwasalimu wazazi
wake “Marahaba” waliitikia kwa
pamoja. “Vipi huko utokapo ni
kheri au shari”? Bi maua
alimuuliza binti yake baada ya
kugundua hayuko katika hali yake
ya kawaida. “Heri tu mama”
alijibu Mercy huku akijilazimisha
kutabasamu.
Mama yake alielewa kuwa kuna
tatizo linalomtatiza binti yake
lakini hakutaka kumsonga sana
kwa maswali alimuacha aende
kwanza akapumzike.
Mercy alipoingia chumbani kwake
alijitupa kitandani bila hata
kubadili uniform hata kula chakula
hakikukumbuka tena kwa kipindi
hicho. Hiyo yote ilisababishwa na
fikra juu ya Bryan ni jinsi gani
ataweza kumsaidia?. Ni vipi
ataweza kumtatulia matatizo yake
aliyonayo na kumfanya aweze
kuishi kwa furaha na ni vipi
ajieleze mpaka aeleweke juu ya
hisia zake kwa Bryan. Na si hivyo
tu alikuwa anatamani siku iishe
upesi akaonane na Bryan.
Dereva hakujua kilichotokea bali
aliendelea kutereza akielekea
hospitali.
Walipita getini na kuingia ndani
kabisa hospitalini. Dereva alifunga
breki na kufungua mlango wa
upande wake alishuka na kasha
akazunguka upande wa pili na
kumfungulia Bryan.
Huku nyuma Mama Rashidi na
Mama Musa walishuka na
kumuomba dereva awasaidie
kumbeba mgonjwa. Na Bryan naye
bila kuambiwa alitaka kushiriki
katika hatua hiyo. “Ah hapana
Bryan we acha pumzika tu” Mama
Rashidi alimkataza Bryan.
“Kwanza shika hii mia tano ukale
mgahawani kwa sababu toka
utoke shule haujagusa chakula
aliongea Mama Musa.
Bryan ikamlazimu aichukue ile
hela japo kwa shingo upande.
Lakini akili na mawazo yote ni juu
ya mama yake ambaye kwa yeye
anavyomfahamu ni Mgonjwa
Mahututi alianza kutembea kwa
hatua ndogondogo huku akiwa
amenyong’onyea kuelekea kwenye
mgahawa uliopo pembeni kidogo
na hospitali ya General. Alipofika
Mgahawani akaagiza chakula na
badala ya kukila akawepo
anakitazama utafikiri ndo kwanza
anakiona.
Aliendelea kukitazama kile chakula
takribani dakika tano kana
kwamba kile chakula hakikuagiza
yeye.
Mercy alikuwa ndani ya daladala
akielekea Dodoma Sekondari shule
ambayo alikuwa akisoma. Moyoni
mwake alikuwa na furaha tele
akiamini hiyo akiamini ni siku
nyingine tena ya kwenda kuonana
na Bryan. “Oya kuna anaeshuka
hapa bohari”? ilikuwa ni sauti ya
konda.
“Shusha” Mercy alijibu. Mercy
alishuka na kumlipa konda nauli
kisha akavuka barabara akielekea
shuleni kwao.
Alipofika shule alikuta wenzake
wametawanyika kutoka assembly
kuelekea madarasani. Aliangaza
macho yake huku na kule asijue
wapi kwa kumpata Bryan.
Baadaye akaamua kwenda
darasani kwa akina Bryan ili
kuuliza kama amekuja.
Alipofika darasani kwa akina
Bryan alimuendea moja kwa moja
rafiki yake Martha ambaye ni
Monntress wa darasa hilo. “Sema
shoga mambo vipi”? Mercy
alimsabahi shoga yake huo. “Safi
tu, issue vipi?” Martha alijibu na
kuuliza, “Poa alijibu Mercy”.
“Bryan ameshafika?” “hapana
naona leo kachelewa kidogo lakini
atafika muda si mrefu” kwa
maneno yale alinyong’onyea lakini
alijipa moyo kuwa bado nukta
chache Bryan angetokea kipindi
kipindi cha kwanza kiliisha,
hakuna Bryan kuonekana cha pili
na hatimaye cha tatu Bryan
hakutokea.
Mercy ilikuwa ni huzuni kubwa
mno kwani alijihisi ni ni mpweke
kuliko.Katika vipindi vyote hivyo
vitatu hakuelewa somo hata moja
na zaidi aliona walimu wote
wanaofundisha ni kero kwake.
Alijishangaa kwa nini Bryan
amemuingia kiasi kile, ukizingatia
Bryan mwenyewe hawana siku
nyingi toka wazoeane.
Alizikusanya daftari zilizokuwa juu
ya meza yake na taratibu
alinyanyuka kwenye kiti
alichokuwa amekalia na taratibu
akaulenga mlango wa kutokea
kwenye ofisi ya walimu.
Alipoingia Ofisini alimkuta
mwalimu wake wa darasa Mr
Innocent “Morning Sir”
“Have a good day what’s ya
problem”, “I’m not feel well I think
this is Malaria” “So you want go
to the hospital”, “Yes Sir” Okay
you may”.
Alikula robo ya chakula kile kasha
akalipa hela na kunyanyuka.
Mapigo yake ya Moyo yalikuwa
yakienda mbio mno. Mwendo wake
ulikuwa wa haraka mno pindi
alipotoka mgahawani hapo
akielekea hospitalini.
Pengine ungemuona usingeweza
kuelewa anatembea au ankimbia.
Ilikuwa nusu kutembea nusu
kukimbia akaingia hospitalini na
moja kwa moja akaenda
mapokezi. “Samahani dada sijui
mgonjwa aliyeletwa muda mfupi
kabla ya sasa sijui yupo sehemu
gani? “Salamu kwanza kaka angu.
Lakini usijali sana wameingia
katika chumba cha docta”
“Samahani kwa hilo dada angu,
shukrani” Bryan alijibu na
kuondoka kwa mwendo wake
uleule kabla hajasukuma mlango
wa docta, mlango huo ulifunguliwa
na Mama Musa pamoja na Mama
Rashidi walitoka ndani ya chumba
hicho.”Vipi?”Akina mama hao
walimuuliza Bryan kwa pamoja.
Bryan kabla hajajibu aliwatazama
wakina mama hao machoni kwa
nucta kadhaa, Na kugundua
macho yao yameiva na kuwa
mekundu kuliko kawaida. Hivi
ilimaanisha wametoka kulia muda
si mrefu na hilo alilitambua na
mara ghafla fikra zake zikaunda
picha nyingine katika ubongo wake
“Nataka kumuona mama yangu”
alijibu Bryan huku mapigo yake ya
moyo yakizidi kumuenda kasi.
***JE? Nini kitaendelea…..