Post by Admin on May 30, 2015 4:22:42 GMT
Ilikuwa ghafla tu, Pepo kali
zilipovuma karibu kila
kona ya wilaya ya Kibondo,
mkoani kigoma.
Taratibu mawingu mazito
yakalifunika anga kiasi
cha kuifanya saa tisa ile ya
alasiri ifanane na usiku
wa manane, usiku wa kiza, usiku
wa hofu.
Ingawaje ilikuwa ni msimu wa
kiangazi na kwamba
ni aghalabu mvua kunyesha,
lakini hakuna
aliyeipuuza dalili ya mvua ile
ambayo ni mawingu.
Kilichowafanya wakaazi waogope
zaidi ni jinsi giza
lilivyozidi kuumeza mwanga,
maana hata kama
nd’o dalili yenyewe ya mvua, hii
sasa ilizidi!
Baadhi ya wafanyabiashara
wakaanza kufunga
maduka yao, wanafunzi
wakikimbilia makwao, na
hata mifugo nayo ikaanza
kurejea mabandani ikijua
kuwa usiku umewadia. Wale
wenzangu na mimi
wenye nyumba za udongo
zilizosheheni ‘mawakili’
karibu katika kila ukuta walianza
‘kudhikiri’
vyumbani mwao wakimuomba
mola awasitiri…
maana bila hata ya mvua tu, kila
siku ukuta
unakuuliza ‘Nikuuwe?’ sasa je
ikishuka si kuta
zitageuka biskuti?
Upepo mkali uliendelea kuvuma
mithili ya
kimbingunga huku baridi kali
ikiwa imeshtadi
kwelikweli, cha jabu hapakuwa
na mingurumo, radi,
wala manyunyu…ni upepo, Baridi
na giza tu.
***
Wakati hali hiyo ya hewa ikizidi
kuchafuka, katika
wilaya hiyohiyo ya Kibondo
nyumba ya Bi
Masonganya binti Kalukalange
ilifurika umati
mkubwa wa wana-ukoo kutoka
sehemu mbalimbali. Watoto,
wajukuu, vitukuu na vilembwe
wakiwa wamekusanyika kwa
kukizunguka kitanda
cha chuma alipolala Bi
Masonganya.
Ni wana-ukoo hao pekee ndiyo
waliokuwa wakijua
siri ya hali ya hewa kubadilika
ghafla katika eneo
lote la kibondo. Ni kwamba bibi
na mama yao
kipenzi, Bi Masonganya alikuwa
akikaribia kukata
roho baada ya kuishi kwa
takribani miaka miamoja
na sitini! Kwa kawaida kifo huja
ghafla tu na hakuna anayeweza
kupata taarifa kabla…ila kwa
wana-ukoo hawa walikitumainia
kifo cha mama na bibi yao yule.
“Yreeeeeeeew! Watemi woseeee!
mizimu yoose!
Makulwa na madoto, na
makashindyeee!
Mumsaidie mtu wenu.” Maneno
hayo yalitamkwa
kwa sauti kali na babu mmoja
aliyekuwa
amesimama pamoja na wana-
ukoo wale kisha
akatoa chafya kwa nguvu na
sauti kali sana!
Nje ya chumba hicho, usawa wa
dirisha alikuwa
amesimama binti wa mwisho wa
Bi Masonganya,
akiwa ameshika mwichi mkononi
akisubiri ishara
aliyoelekezwa ili atekeleze zoezi
muhimu…na ishara
hiyo ilikuwa ni ile chafya
aliyoisikia ikitokea ndani.
Kitendo bila kuchelewa akauinua
juu ule mwichi
aliokuwa ameushikilia, kisha
akaukita kwa nguvu
chini ya ukuta ambao kwa ndani
amelala mama
yake akiwa amezungukwa na
wana-ukoo.
Baada tu ya kuukita mchi ule
chini ya ukuta, kule
chumbani wana ukoo
wakashuhudia mama yao
akihangaika kitandani kwa
sekunde kadhaa huku
akikakamaa kama askari wa
kikoloni akijiandaa
kupiga saluti kwa bwana wake,
haikuchukua hata
dakika mbili, Bi Masonganya
akanena kwa sauti
kavu ya kukoroma.
“…Akkh…wana-ngu…mme-niwe-
zaa mme-ni-u-
waaa!” Hapohapo Bi
Masonganya akakata roho.
Sauti za vigeregere, nderemo na
vifijo kutoka kwa
wana-ukoo vilizizima chumbani
humo, japo
havikuwa vigeregere vya furaha
bali viashiria vya
kukamilika kwa kifo kile
kilichowabidi
kukilazimisha. Laiti wangejua
kilichokua
kikiwanyemelea, wala
wasingenyanyua vinywa
vyao kupiga vigeregere. Lakini
nd’o hivyo tena
hakuna aijuaye kesho hata
mtunzi wa kalenda.
Baada tu ya Bi Masonganya
kukata roho, muda
huohuo hali ya hewa ikabidilika
tena, mwanga
ukarejea na upepo ukatulia kiasi
cha
kuwastaajabisha wakazi wa
Kibondo.
***
Sifa kubwa ya Bi Masonganya
ilikuwa ni uchawi.
Uchawi uliokubuhu, aliorithishwa
na marehemu bibi
yake mzaa mama ambaye kwa
asili ni mtu kutoka
Kongo. Uchawi huo ulimfanya Bi
Masonganya
aheshimike na kuogopwa karibu
na kila mtu. Wapo
aliowaangamiza kutokana na
uchawi wake, na
wapo aliowasaidia, lakini mchawi
ni mchawi tu
hana muamana asilani.
Ilikuwa Bi Masonganya
akaikwambia kuwa
hautoliona jua la jioni basi
kimbia haraka
ukamtake radhi, vinginevyo
utakufa kweli. Na hata
uwe na kesi ya namna gani
endapo utamfuata
kumtaka msaada na akaamua
kuivalia njuga basi
piga geuza utashinda tu. Mpaka
viongozi wakubwa
serikalini wanaouhusudu
ushirikina huwasili kwa Bi
Masonganya kufanyiwa ndumba.
Kuna madhila yaliwahi kumpata
Jaji aliyekuwa
akisikiliza kesi ya ubakaji
iliyokuwa ikimkabili
mjukuu wa Bi Masonganya
aitwaye Ndoza, hiyo
nayo ikawa ni historia ya
kushangaza na
kusikitisha! Ni kweli Ndoza
alibaka haswa tena saa
saba mchana watu wakishuhudia
dhahiri
akimng’ang’ania binti wa watu
aliyekuwa akipita
na safari zake, akamvutia
kwenye pagara lilikouwa
jirani na kumfanyia ushenzi.
Sasa kesi ilipoonesha
dalili zote za kumuelemea
Ndoza, ndipo Bi
Masonganya akaibuka na
kuikingia kifua.
Akamfuata jaji, akamkanya kwa
maneno makali ya
vitisho kuwa endapo ataendelea
na mpango wake
wa kutaka kumfunga jela mjukuu
wake basi
atakiona kilichomfanya kuku
aanze kuota manyoa
mkiani…Jaji akapuuza, pengine
kwakuwa naye
alikuwa amejiganga.
Siku ya hukumu sasa Jaji akiwa
anaingia
mahakamani baada ya umati
kufurika ndipo ghafla
walipoibuka nyuki hata
wasijulikane walipotokea,
ikawa ni patashika ya nguo
kuchanika kila mmoja
akitafuta njia yake. Kama Nyuki
nao huwa na
kichaa, basi hawa nao walihitaji
chanjo. Walikua
wanauma ovyoovyo, na
wakikuuma, hayo maumivu
yake ni kama umegongwa na
koboko.
Matokeo ya hila za nyuki wale ni
pamoja na
mafaili yote yaliyobeba kesi ya
Ndoza kupotea japo
hilo halikuwa kubwa sana.
Lililoshitua zaidi ni
kitendo cha wale nyuki
kumfakamia Jaji licha ya
kelele za kutaka msaada
alizokuwa akipiga bila
mafanikio mpaka walipomtoa
roho.
Kifo cha Jaji kwa kuumwa na
nyuki mahakamani
kikazagaa kama moto wa pumba,
huku kila mmoja
akijifanya ni fanani wa mkasa
ule.
Kesi ya ndoza ikatulia kama maji
ya mtungi.
ITAENDELEA......
zilipovuma karibu kila
kona ya wilaya ya Kibondo,
mkoani kigoma.
Taratibu mawingu mazito
yakalifunika anga kiasi
cha kuifanya saa tisa ile ya
alasiri ifanane na usiku
wa manane, usiku wa kiza, usiku
wa hofu.
Ingawaje ilikuwa ni msimu wa
kiangazi na kwamba
ni aghalabu mvua kunyesha,
lakini hakuna
aliyeipuuza dalili ya mvua ile
ambayo ni mawingu.
Kilichowafanya wakaazi waogope
zaidi ni jinsi giza
lilivyozidi kuumeza mwanga,
maana hata kama
nd’o dalili yenyewe ya mvua, hii
sasa ilizidi!
Baadhi ya wafanyabiashara
wakaanza kufunga
maduka yao, wanafunzi
wakikimbilia makwao, na
hata mifugo nayo ikaanza
kurejea mabandani ikijua
kuwa usiku umewadia. Wale
wenzangu na mimi
wenye nyumba za udongo
zilizosheheni ‘mawakili’
karibu katika kila ukuta walianza
‘kudhikiri’
vyumbani mwao wakimuomba
mola awasitiri…
maana bila hata ya mvua tu, kila
siku ukuta
unakuuliza ‘Nikuuwe?’ sasa je
ikishuka si kuta
zitageuka biskuti?
Upepo mkali uliendelea kuvuma
mithili ya
kimbingunga huku baridi kali
ikiwa imeshtadi
kwelikweli, cha jabu hapakuwa
na mingurumo, radi,
wala manyunyu…ni upepo, Baridi
na giza tu.
***
Wakati hali hiyo ya hewa ikizidi
kuchafuka, katika
wilaya hiyohiyo ya Kibondo
nyumba ya Bi
Masonganya binti Kalukalange
ilifurika umati
mkubwa wa wana-ukoo kutoka
sehemu mbalimbali. Watoto,
wajukuu, vitukuu na vilembwe
wakiwa wamekusanyika kwa
kukizunguka kitanda
cha chuma alipolala Bi
Masonganya.
Ni wana-ukoo hao pekee ndiyo
waliokuwa wakijua
siri ya hali ya hewa kubadilika
ghafla katika eneo
lote la kibondo. Ni kwamba bibi
na mama yao
kipenzi, Bi Masonganya alikuwa
akikaribia kukata
roho baada ya kuishi kwa
takribani miaka miamoja
na sitini! Kwa kawaida kifo huja
ghafla tu na hakuna anayeweza
kupata taarifa kabla…ila kwa
wana-ukoo hawa walikitumainia
kifo cha mama na bibi yao yule.
“Yreeeeeeeew! Watemi woseeee!
mizimu yoose!
Makulwa na madoto, na
makashindyeee!
Mumsaidie mtu wenu.” Maneno
hayo yalitamkwa
kwa sauti kali na babu mmoja
aliyekuwa
amesimama pamoja na wana-
ukoo wale kisha
akatoa chafya kwa nguvu na
sauti kali sana!
Nje ya chumba hicho, usawa wa
dirisha alikuwa
amesimama binti wa mwisho wa
Bi Masonganya,
akiwa ameshika mwichi mkononi
akisubiri ishara
aliyoelekezwa ili atekeleze zoezi
muhimu…na ishara
hiyo ilikuwa ni ile chafya
aliyoisikia ikitokea ndani.
Kitendo bila kuchelewa akauinua
juu ule mwichi
aliokuwa ameushikilia, kisha
akaukita kwa nguvu
chini ya ukuta ambao kwa ndani
amelala mama
yake akiwa amezungukwa na
wana-ukoo.
Baada tu ya kuukita mchi ule
chini ya ukuta, kule
chumbani wana ukoo
wakashuhudia mama yao
akihangaika kitandani kwa
sekunde kadhaa huku
akikakamaa kama askari wa
kikoloni akijiandaa
kupiga saluti kwa bwana wake,
haikuchukua hata
dakika mbili, Bi Masonganya
akanena kwa sauti
kavu ya kukoroma.
“…Akkh…wana-ngu…mme-niwe-
zaa mme-ni-u-
waaa!” Hapohapo Bi
Masonganya akakata roho.
Sauti za vigeregere, nderemo na
vifijo kutoka kwa
wana-ukoo vilizizima chumbani
humo, japo
havikuwa vigeregere vya furaha
bali viashiria vya
kukamilika kwa kifo kile
kilichowabidi
kukilazimisha. Laiti wangejua
kilichokua
kikiwanyemelea, wala
wasingenyanyua vinywa
vyao kupiga vigeregere. Lakini
nd’o hivyo tena
hakuna aijuaye kesho hata
mtunzi wa kalenda.
Baada tu ya Bi Masonganya
kukata roho, muda
huohuo hali ya hewa ikabidilika
tena, mwanga
ukarejea na upepo ukatulia kiasi
cha
kuwastaajabisha wakazi wa
Kibondo.
***
Sifa kubwa ya Bi Masonganya
ilikuwa ni uchawi.
Uchawi uliokubuhu, aliorithishwa
na marehemu bibi
yake mzaa mama ambaye kwa
asili ni mtu kutoka
Kongo. Uchawi huo ulimfanya Bi
Masonganya
aheshimike na kuogopwa karibu
na kila mtu. Wapo
aliowaangamiza kutokana na
uchawi wake, na
wapo aliowasaidia, lakini mchawi
ni mchawi tu
hana muamana asilani.
Ilikuwa Bi Masonganya
akaikwambia kuwa
hautoliona jua la jioni basi
kimbia haraka
ukamtake radhi, vinginevyo
utakufa kweli. Na hata
uwe na kesi ya namna gani
endapo utamfuata
kumtaka msaada na akaamua
kuivalia njuga basi
piga geuza utashinda tu. Mpaka
viongozi wakubwa
serikalini wanaouhusudu
ushirikina huwasili kwa Bi
Masonganya kufanyiwa ndumba.
Kuna madhila yaliwahi kumpata
Jaji aliyekuwa
akisikiliza kesi ya ubakaji
iliyokuwa ikimkabili
mjukuu wa Bi Masonganya
aitwaye Ndoza, hiyo
nayo ikawa ni historia ya
kushangaza na
kusikitisha! Ni kweli Ndoza
alibaka haswa tena saa
saba mchana watu wakishuhudia
dhahiri
akimng’ang’ania binti wa watu
aliyekuwa akipita
na safari zake, akamvutia
kwenye pagara lilikouwa
jirani na kumfanyia ushenzi.
Sasa kesi ilipoonesha
dalili zote za kumuelemea
Ndoza, ndipo Bi
Masonganya akaibuka na
kuikingia kifua.
Akamfuata jaji, akamkanya kwa
maneno makali ya
vitisho kuwa endapo ataendelea
na mpango wake
wa kutaka kumfunga jela mjukuu
wake basi
atakiona kilichomfanya kuku
aanze kuota manyoa
mkiani…Jaji akapuuza, pengine
kwakuwa naye
alikuwa amejiganga.
Siku ya hukumu sasa Jaji akiwa
anaingia
mahakamani baada ya umati
kufurika ndipo ghafla
walipoibuka nyuki hata
wasijulikane walipotokea,
ikawa ni patashika ya nguo
kuchanika kila mmoja
akitafuta njia yake. Kama Nyuki
nao huwa na
kichaa, basi hawa nao walihitaji
chanjo. Walikua
wanauma ovyoovyo, na
wakikuuma, hayo maumivu
yake ni kama umegongwa na
koboko.
Matokeo ya hila za nyuki wale ni
pamoja na
mafaili yote yaliyobeba kesi ya
Ndoza kupotea japo
hilo halikuwa kubwa sana.
Lililoshitua zaidi ni
kitendo cha wale nyuki
kumfakamia Jaji licha ya
kelele za kutaka msaada
alizokuwa akipiga bila
mafanikio mpaka walipomtoa
roho.
Kifo cha Jaji kwa kuumwa na
nyuki mahakamani
kikazagaa kama moto wa pumba,
huku kila mmoja
akijifanya ni fanani wa mkasa
ule.
Kesi ya ndoza ikatulia kama maji
ya mtungi.
ITAENDELEA......