Post by Admin on May 30, 2015 4:27:03 GMT
Kifo cha Jaji kwa kuumwa na
nyuki mahakamani
kikazagaa kama moto wa pumba,
huku kila mmoja
akijifanya ni fanani wa mkasa ule.
Kesi ya ndoza ikatulia kama maji
ya mtungi.
Kama ilivyo kawaida ya mawingu,
huwa hayatandi
milele…kuna siku husambazwa na
kutawanywa
kwa upepo! Na hivyo ndivyo
habari ile ya kifo cha
Jaji ilivyosahaulika na kisha
baadaye ikapangwa
tena upya tarehe ya kuendelea
kwa kesi ya ubakaji
inayomkabili Ndoza na
kukabidhiwa kwa Jaji
mwingine.
Huyu sasa naona alikuwa
mwepesi kama tishu
maana kazi ya Bi Masonganya
ilikuwa ni kama
kupuliza kibatali tu na kukizima
kabisa. Ilitokea
kama maskhara tu, siku ya
hukumu Jaji akiwa
anatoka nyumbani kwake, kwa
bahati mbaya
akajikwaa na kuanguka mpaka
chini, hakuinuka
akiwa hai bali alinyanyuliwa na
kubebwa akiwa
maiti!
Wakati huohuo Jaji anaanguka,
binti aliyebakwa na
Ndoza naye alijikwaa kama
ilivyokuwa kwa Jaji!
Na wakati maiti ya Jaji
inanyanyulia, na ya binti
yule naye ilinyanyuliwa tokea pale
alipoangukia.
Vifo viwili, vilivyofanana japo
vimetokea sehemu
tofauti kwa watu wanaohusika na
kesi moja vilizua
gumzo mjini Kibondo…kesi hata
ilkopotelea!
Unadhani Jaji gani asiyependa
kuishi?
Yapo mengi ya kumhusu Bi
Masonganya, hata
humohumo kwenye ukoo wake
mbali ya
kuwasaidia pindi wapatwapo na
matatizo, pia
ameshawamaliza sana watoto na
wajukuu kwa
kuwachukua kichawi.
Mbali ya vimbwanga hivyo vya
uchawi, pia
inasemekana Bi Masonganya
alipata kumeza
‘mpigi’. Mpigi ni dawa ya
mtishamba ambayo
ukiimeza basi haufi kirahisi mpaka
utapishwe
kwanza dawa hiyo, vinginevyo
utazeeka mpaka
ubakie kama mzoga huku ukiwa
hai.
Sasa tayari Bi Masonganya
alikuwa
amekwishazeeka kiasi hata cha
kushindwa hata
kutembea mwenyewe, na
kuwafanya wajukuu zake
kuwa wanamtoa nje kumuanika
mara mojamoja…
na siku akitolewa kuanikwa,
utafikiri alikuwa akitoa
sumu angani maana kama kuna
wagonjwa au
watoto wadogo maeneo ya jirani,
basi siku hiyo
watashinda ovyoovyo tu wakiwa
ta’abani mpaka Bi
Masonganya atakaporejeshwa
ndani.
Hata yeye mwenyewe Bi
Masonganya alitamani
sana tu kufa sasa ili akapumzike
kama kweli
atapata nafasi hiyo, lakini
inasemekana kabla
hajaitapika ile ‘mpigi’ pia kuna
fununu kwa
nduguze kuwa alitaka kwanza
aache amemrithisha
mtu mmoja uchawi wake wote
kabla hajafa…hilo
nd’o lililowagutua wana-ukoo na
kuamua
kumsaidia kufa mapema kabla
hajarithishwa mtu
mwingine huo mzigo wa ulozi.
Ndipo akaitwa
mtaalamu ambaye aliusuka
mpango mzima wa
kumuondoa duniani bi mkubwa
yule. Hivyo ule
mwichi uliokitwa chini ya ukuta
baada ya maneno
yale ya kimila yaliyofuatiwa na
chafya ya bila
kunusa ugoro ulikuwa nd’o pigo la
mwisho la
kummaliza, na kweli
wakammaliza…sasa kwanini
wasipige vigeregere?
Ambacho hawakukikumbuka ni
kimoja tu, kwamba
Bi Masonganya amekufa na ‘mpigi’
yake kifuani…
hawakuijua hekaheka yake.
***
Baaada ya taarifa kusambaa kila
kona kuwa Bi
Masonganya amefariki, kila mmoja
alifurahi. Ndugu
kutoka sehemu mbalimbali
wakajumuika kwa ajili
ya maziko. Ulikuwa ni msiba wa
kimila zaidi,
wafiwa wote walipakwa pemba
usoni na ilikuwa ni
marufuku kwa mfiwa yeyote kulia.
Na katika
kipindi chote maiti ikiwa ndani,
palikuwa na ngoma
maalum ikipigwa taratibu bila
kuzimwa, endapo
mpigaji wa ngoma akichoka basi
anampasia aliye
jirani yake naye anaendelea
kuipiga mpaka
atakapochoka na kumpa mwingine
aendeleze.
Siku ya maziko ilipowadia ndipo
kikaibuka
kizaazaa kipya, ndugu walipoingia
chumbani ili
kuubeba mwili wa marehemu,
wakaikuta maiti
ikiwa imefumbua macho!
TOBAA!
Ilikuwa ni mpishempishe kila
mmoja akigombea
mlango wa kutokea…ilikuwa ni hali
ya ajabu na
kuogofya japo kwa wajuvi wa
mambo waliitegemea
hali ile.
“Hebu kaeni chini tusikilizane…”
aliongea mzee
mmoja aliyetapakaa mvi karibu
robo tatu ya
kichwa chake. Mzee huyo ni kaka
wa Bi
Masonganya aitwaye mzee Mtandi
bin
Kalukalange. Umati ukamsogelea
na kumsikiliza,
kisha akaendelea “…Iko hivi, haya
ni mambo
makubwa lakini ni ya kawaida
hasa anapokufa
kiongozi mkubwa wa kimila kama
Bi Masonganya…
hivyo kuna mambo
yanarekebishwa na wakubwa
kisha kila kitu kitatengemaa na
sote tutakwenda
malaloni kumsitiri bi mkubwa, cha
msingi ni utulivu
wenu tu.” Akamaliza kuzungumza
babu yule.
“Ni mambo gani hayo
yanayorekebishwa na
wakubwa huko ndani?” Aliuliza
mmoja wa majirani
waliojumuika msibani pale “…Na ni
wakubwa gani
hao?” akaongezea huku
akimtazama jirani
mwenziye.
“Mtoto yasiyokuhusu waachie
baba na…”
“Na mama..” Wakaachia kicheko
cha kimbea
kilichokatizwa na majibu ya swali
lao kutoka kwa
Bi mkubwa mmoja aliyebarizi
pembezoni mwa
mpera.
“Kuna kitu alimeza kitambo kirefu
sana, hivyo bila
ya kutapishwa itakuwa kama
mchezo…atafumbua
macho kila atakapokaribia
kupelekwa kuzikwa, na
hao wakubwa waliotajwa ni
wachawi magwiji nd’o
wanasubiriwa kama wataweza
kumtapisha!”
“Heh…makubwa!”
“…madogo yana nafuu.”
“Hivi kuna gwiji wa uchawi kuliko
Bi
Masonganya?”
“Avumaye baharini ni Papa, na
wengine pia wamo…
magwiji wapo japo hawajavuma
kama yeye!”
“Sasa je kama watamzika
hivyohivyo akiwa macho
itakuwaje?” mpambe mwingine
alisaili.
“unataka wapitiane ukoo mzima
kama kuku wenye
mdondo? Chezea wachawi wewe!”
“Na ikitokezea hao magwiji
wakashindwa
kumtapisha, itakuwaje jamani?”
“Hapo nd’o watakapocheza naye
makida.”
Saa moja baadaye, aliwasili Bi
Kibena akitokea
maeneo ya Kakonko. Huyu
alitumainiwa kuwa
angeweza kumtapisha Bi
Masonganya ile ‘mpigi’
aliyomeza ili akazikwe maana Bi
Kibena naye ni
kiboko kwa uchawi. Baada ya
kusalimiana na
wafiwa aliingia mpaka chumbani
ilipolala maiti na
kuwaamuru watu wote watoke nje,
walipotoka tu
akaanza vimbwanga vyake!
***Mnh! Haya Bi. Kibena...una
vimbaga gani zaidi?
ITAENDELEA....
nyuki mahakamani
kikazagaa kama moto wa pumba,
huku kila mmoja
akijifanya ni fanani wa mkasa ule.
Kesi ya ndoza ikatulia kama maji
ya mtungi.
Kama ilivyo kawaida ya mawingu,
huwa hayatandi
milele…kuna siku husambazwa na
kutawanywa
kwa upepo! Na hivyo ndivyo
habari ile ya kifo cha
Jaji ilivyosahaulika na kisha
baadaye ikapangwa
tena upya tarehe ya kuendelea
kwa kesi ya ubakaji
inayomkabili Ndoza na
kukabidhiwa kwa Jaji
mwingine.
Huyu sasa naona alikuwa
mwepesi kama tishu
maana kazi ya Bi Masonganya
ilikuwa ni kama
kupuliza kibatali tu na kukizima
kabisa. Ilitokea
kama maskhara tu, siku ya
hukumu Jaji akiwa
anatoka nyumbani kwake, kwa
bahati mbaya
akajikwaa na kuanguka mpaka
chini, hakuinuka
akiwa hai bali alinyanyuliwa na
kubebwa akiwa
maiti!
Wakati huohuo Jaji anaanguka,
binti aliyebakwa na
Ndoza naye alijikwaa kama
ilivyokuwa kwa Jaji!
Na wakati maiti ya Jaji
inanyanyulia, na ya binti
yule naye ilinyanyuliwa tokea pale
alipoangukia.
Vifo viwili, vilivyofanana japo
vimetokea sehemu
tofauti kwa watu wanaohusika na
kesi moja vilizua
gumzo mjini Kibondo…kesi hata
ilkopotelea!
Unadhani Jaji gani asiyependa
kuishi?
Yapo mengi ya kumhusu Bi
Masonganya, hata
humohumo kwenye ukoo wake
mbali ya
kuwasaidia pindi wapatwapo na
matatizo, pia
ameshawamaliza sana watoto na
wajukuu kwa
kuwachukua kichawi.
Mbali ya vimbwanga hivyo vya
uchawi, pia
inasemekana Bi Masonganya
alipata kumeza
‘mpigi’. Mpigi ni dawa ya
mtishamba ambayo
ukiimeza basi haufi kirahisi mpaka
utapishwe
kwanza dawa hiyo, vinginevyo
utazeeka mpaka
ubakie kama mzoga huku ukiwa
hai.
Sasa tayari Bi Masonganya
alikuwa
amekwishazeeka kiasi hata cha
kushindwa hata
kutembea mwenyewe, na
kuwafanya wajukuu zake
kuwa wanamtoa nje kumuanika
mara mojamoja…
na siku akitolewa kuanikwa,
utafikiri alikuwa akitoa
sumu angani maana kama kuna
wagonjwa au
watoto wadogo maeneo ya jirani,
basi siku hiyo
watashinda ovyoovyo tu wakiwa
ta’abani mpaka Bi
Masonganya atakaporejeshwa
ndani.
Hata yeye mwenyewe Bi
Masonganya alitamani
sana tu kufa sasa ili akapumzike
kama kweli
atapata nafasi hiyo, lakini
inasemekana kabla
hajaitapika ile ‘mpigi’ pia kuna
fununu kwa
nduguze kuwa alitaka kwanza
aache amemrithisha
mtu mmoja uchawi wake wote
kabla hajafa…hilo
nd’o lililowagutua wana-ukoo na
kuamua
kumsaidia kufa mapema kabla
hajarithishwa mtu
mwingine huo mzigo wa ulozi.
Ndipo akaitwa
mtaalamu ambaye aliusuka
mpango mzima wa
kumuondoa duniani bi mkubwa
yule. Hivyo ule
mwichi uliokitwa chini ya ukuta
baada ya maneno
yale ya kimila yaliyofuatiwa na
chafya ya bila
kunusa ugoro ulikuwa nd’o pigo la
mwisho la
kummaliza, na kweli
wakammaliza…sasa kwanini
wasipige vigeregere?
Ambacho hawakukikumbuka ni
kimoja tu, kwamba
Bi Masonganya amekufa na ‘mpigi’
yake kifuani…
hawakuijua hekaheka yake.
***
Baaada ya taarifa kusambaa kila
kona kuwa Bi
Masonganya amefariki, kila mmoja
alifurahi. Ndugu
kutoka sehemu mbalimbali
wakajumuika kwa ajili
ya maziko. Ulikuwa ni msiba wa
kimila zaidi,
wafiwa wote walipakwa pemba
usoni na ilikuwa ni
marufuku kwa mfiwa yeyote kulia.
Na katika
kipindi chote maiti ikiwa ndani,
palikuwa na ngoma
maalum ikipigwa taratibu bila
kuzimwa, endapo
mpigaji wa ngoma akichoka basi
anampasia aliye
jirani yake naye anaendelea
kuipiga mpaka
atakapochoka na kumpa mwingine
aendeleze.
Siku ya maziko ilipowadia ndipo
kikaibuka
kizaazaa kipya, ndugu walipoingia
chumbani ili
kuubeba mwili wa marehemu,
wakaikuta maiti
ikiwa imefumbua macho!
TOBAA!
Ilikuwa ni mpishempishe kila
mmoja akigombea
mlango wa kutokea…ilikuwa ni hali
ya ajabu na
kuogofya japo kwa wajuvi wa
mambo waliitegemea
hali ile.
“Hebu kaeni chini tusikilizane…”
aliongea mzee
mmoja aliyetapakaa mvi karibu
robo tatu ya
kichwa chake. Mzee huyo ni kaka
wa Bi
Masonganya aitwaye mzee Mtandi
bin
Kalukalange. Umati ukamsogelea
na kumsikiliza,
kisha akaendelea “…Iko hivi, haya
ni mambo
makubwa lakini ni ya kawaida
hasa anapokufa
kiongozi mkubwa wa kimila kama
Bi Masonganya…
hivyo kuna mambo
yanarekebishwa na wakubwa
kisha kila kitu kitatengemaa na
sote tutakwenda
malaloni kumsitiri bi mkubwa, cha
msingi ni utulivu
wenu tu.” Akamaliza kuzungumza
babu yule.
“Ni mambo gani hayo
yanayorekebishwa na
wakubwa huko ndani?” Aliuliza
mmoja wa majirani
waliojumuika msibani pale “…Na ni
wakubwa gani
hao?” akaongezea huku
akimtazama jirani
mwenziye.
“Mtoto yasiyokuhusu waachie
baba na…”
“Na mama..” Wakaachia kicheko
cha kimbea
kilichokatizwa na majibu ya swali
lao kutoka kwa
Bi mkubwa mmoja aliyebarizi
pembezoni mwa
mpera.
“Kuna kitu alimeza kitambo kirefu
sana, hivyo bila
ya kutapishwa itakuwa kama
mchezo…atafumbua
macho kila atakapokaribia
kupelekwa kuzikwa, na
hao wakubwa waliotajwa ni
wachawi magwiji nd’o
wanasubiriwa kama wataweza
kumtapisha!”
“Heh…makubwa!”
“…madogo yana nafuu.”
“Hivi kuna gwiji wa uchawi kuliko
Bi
Masonganya?”
“Avumaye baharini ni Papa, na
wengine pia wamo…
magwiji wapo japo hawajavuma
kama yeye!”
“Sasa je kama watamzika
hivyohivyo akiwa macho
itakuwaje?” mpambe mwingine
alisaili.
“unataka wapitiane ukoo mzima
kama kuku wenye
mdondo? Chezea wachawi wewe!”
“Na ikitokezea hao magwiji
wakashindwa
kumtapisha, itakuwaje jamani?”
“Hapo nd’o watakapocheza naye
makida.”
Saa moja baadaye, aliwasili Bi
Kibena akitokea
maeneo ya Kakonko. Huyu
alitumainiwa kuwa
angeweza kumtapisha Bi
Masonganya ile ‘mpigi’
aliyomeza ili akazikwe maana Bi
Kibena naye ni
kiboko kwa uchawi. Baada ya
kusalimiana na
wafiwa aliingia mpaka chumbani
ilipolala maiti na
kuwaamuru watu wote watoke nje,
walipotoka tu
akaanza vimbwanga vyake!
***Mnh! Haya Bi. Kibena...una
vimbaga gani zaidi?
ITAENDELEA....