Post by Admin on May 30, 2015 4:32:37 GMT
Saa moja baadaye, aliwasili Bi
Kibena akitokea
maeneo ya Kakonko. Huyu
alitumainiwa kuwa
angeweza kumtapisha Bi
Masonganya ile ‘mpigi’
aliyomeza ili akazikwe maana Bi
Kibena naye ni
kiboko kwa uchawi. Baada ya
kusalimiana na
wafiwa aliingia mpaka chumbani
ilipolala maiti na
kuwaamuru watu wote watoke nje,
walipotoka tu
akaanza vimbwanga vyake!
Laahaullah!
Kilichomkuta Bi Kibena alikijua
yeye na Mungu
wake, watu walisikia kukurukakara
ya haja
ikiendelea mle chumbani mpaka
ikabidi wafungue
haraka mlango. Ndipo wakamkuta
bi kibena akiwa
kama mchawi aliyeenda kucheza
mahepe kwenye
nyumba iliyozindikwa na hatimaye
akaya-bhula…
haja kubwa na ndogo vilihitimisha
kifo cha bi
Kibena alipofikishwa nyumbani
kwake!
“Jamani ndugu wafiwa na majirani,
maziko
yameakhirishwa mpaka hapo
mtakapotangaziwa
vinginevyo.” Sauti ya Mzee Mtandi
ambaye ndiye
msimamizi wa msiba ilihitimisha
na watu wote
kusambaa.
Kifo cha Bi Masonganya kilijizolea
umaarufu
kutoka kila pembe ya mkoa wa
Kigoma huku kila
mmoja akiwana mshawasha wa
kutaka kujua nini
hatma yake…ikawa kama mchezo
sasa, haipiti japo
saa moja bila ya Bi Masonganya
kufumbua macho
japo vipimo vyote vya waganga na
hata madaktari
wa kawaida walioshirikishwa
vilionesha kuwa
amekwishafariki.
Zikapita takribani siku tatu bila ya
mwili wa Bi
Masonganya kuzikwa, huku ndugu
wakiswampa
kila uchao kutafuta waganga wa
kulitatua tatizo
lililoikumba familia yao, kila
mganga aliyefuatwa
alipokaribia tu na nyumba ilimo
maiti aliishia nje
na kuingia mitini! Haikuwa kazi
rahisi.
Siku ya tano, mwili wa marehemu
ukiwa
umekwishaanza kutahayari ndipo
wana-ukoo
walipofanikiwa kumpata mganga
maeneo ya vijiji
vya mbali kidogo tokea Kibondo
mjini.
Ilichukuwa karibu saa saba
kutokea huko vijini kwa
mwendo wa gari mpaka kufika
hapo Kibondo mjini.
Wakiwa bado hawajafika nyumbani
ulipo msiba
ghafla mkwara wa Babu-mganga
ukaanza,
akapandisha mashetani yake
kichwani na kuanza
kufanya vurugu kubwa ndani ya
gari. Alipotulia
akamuamuru dereva asimamishe
gari kisha yeye
akashuka na kikapu chake kichafu
na kilichochakaa
kama nguo zake alizozivaa…
wafiwa waliomuendea
nao wakashuka.
“Vipi babu?”
“Mizimu imenikatalia kwenda kwa
gari huko
nyumbani kwenu…yaonekana huyo
aliyekufa
hakuwa mtu wa kawaida asilani.”
Wafiwa
wakaangaliana, kisha mmoja
akamsaili tena.
“Kwahiyo tunafanyaje?”
“Hakuna cha tunafanyaje hapa…
twendeni kwa
miguu tu!”
Haikuwa mbali sana na nyumba,
hivyo walitembea
kwa karibu nusu saa wakawasili
na kupokelewa na
ndugu na majirani walioanza
kufurika.
“Jamanimi’ si mkaaji hapa…”
alianza kuongea
mganga. “…nataka kufanya kazi
yangu haraka
iwezekanavyo ili niondoke zangu.”
“Sawa babu karibu ndani,” Alijibu
mtoto wa kiume
wa marehemu huku akifungua
mlango mkubwa wa
mbele na kumpisha Babu-mganga
aingie ndani.
“Hapana mi’ sipitii mlangoni,
naomba mniruhusu
nipande juu ya bati la nyumba
yenu kisha nipitie
huko kwa juu.”
Heh!
“Sasa utapitiaje kwa juu babu?”
“N’tafumua bati pamoja na
singibodi kama iko
kisha n’taibukia chumbani kwa
mtuhumiwa
wenu.”Ilikuwa ni mzaha mwingine
msibani hapo,
ila kwakuwa walikuwa wanashida
wakamkubalia,
Babu akapanda juu ya nyumba
huku watu
wakimshangaa na baadhi ya
wafiwa wakitangulia
chumba chenye maiti.
Watu walimshuhudia babu
akipanda mpaka juu na
kufumua bati kisha akidumbukia
kwa ndani kiasi
cha kuachia kishindo kizito…
nyumba nzima
ikatulia, walio nje wakisubiri
taarifa ya kitakachojiri
huko chumbani.
Zilipita dakika takribani thelathini
nyumba ikiwa
kimya kila mmoja akijiandaa
kutimua mbio endapo
maiti itazua songombingo.
Haikuwa hivyo,badala
yake zilisikika sauti za vigeregere
na shangwe
kutokea chumbani, ikiwa ni ishara
ya kazi
kukamilika. Bi Masonganya
alitapishwa mpigi yake.
Haikuchukuwa muda mrefu Babu
akatoka akiwa na
kikapu chake mkononi akifuatiwa
na wafiwa.
Akaaga na kuondoka zake.
Bi Masonganya akaandaliwa na
kwenda kuzikwa
kimila, akiwa ameviringishwa
ndani ya ngozi ya
Ng’ombe mweusi.
Msiba ukaisha.
Majirani wakasambaa, na wafiwa
wakarejea kwao
kumalizia siku tatu zamsiba kabla
na wao
hawajasambaana!
***
“Mamaa…mamaa.” Kaguba alikuwa
akimgasi kwa
kumuita mama yake wakati kikao
cha kumalizia
msiba wa Bi Masonganya
kikiendelea. Kaguba ni
mjukuu wa marehemu Bi
Masonganya, mtoto wa
kike wa mwanaye wa pili kutoka
mwisho.
“Mamaaa…mama.” Kaguba
aliendelea kumgasi
mama yake aliyekuwa
amempakata miguuni.
Mama Kaguba alimpuuza
mwanaye akiamini hana
jipya pengine na umri wake kuwa
mdogo. Kaguba
alikuwa ni mtoto wa miaka
takribani minne tu.
“Mama ujue mi’ n’namuonea
huruma sana
ma’mdogo Nyanzala,” alisema
Kaguba na kufanya
kikao kipige kimya kidogo huku
watu wote
wakimuangalia kama kituko vile
kwa ile kauli yake
aliyoitoa baada ya kuona mama
yake hamjibu
chochote akiendelea kufuatilia
kikao. Wakajikuta
wote wamecheka!
“Unamuonea huruma ya nini
mama?” Mama
Kaguba alimuuliza kimzaha
Kaguba wake huku
wengine wakimsikiliza.
“Hivi kwanini sasa ma’mdogo
Nyanzala alikubali
kupiga mwichi chini ya ukuta ili
amuue bibi?”
alisaili mtoto Kaguba na kuwaacha
midomo wazi
wote mle ndani.
Haikuwa jambo la kawaida kwa
mtoto mdogo wa
umri wa Kaguba kutambua jambo
lile lililofanyika
kisiri. Na hata wakati yote hayo
yalipokuwa
yakitendeka yeye(Kaguba) alikuwa
uani huko
akicheza na wenziye, sasa
ameyajuaje haya.
“Shauri yenu, mjue wamekasirika
sana huko.”
Kaguba aliropoka tena.
Ama!
“We’Kaguba, akina nani hao
wamekasirika?
amekwambia maneno hayo?” Mzee
Mtandi ambaye
ni kaka wa marehemu alimsaili
mjukuu wake kwa
kihoro kikubwa.
“Eeenh…nyie ngojeni tu! Kesho
mtaona tu
ma’mdogo Nyanzala naye
anakufa!”
SEHEMU YA PILI
Ukumbi mzima ulizizima kwa hofu
na mashaka.
Hali ile haikuwa ya kawaida hata
kidogo.
Walipojaribu kumdodosa Kaguba
wao tena
hakuendelea kusema chochote
cha maana zaidi ya
kubwabwaja maneno yasiyo na
maana yoyote,
maneno ya kitoto tu!
Raha ikawaisha, kikao kikafa
kimyakimya!
Nyanzala alichanganyikiwa
maradufu, hofu kuu
ilimvaa, mishipa ya shingo ikawa
inampwita kama
moyo wa chura. Kila mara alikuwa
akilia tu
akihofia kifo alichobashiriwa na
mtoto wa dada
yake. Ndugu walijaribu kumfariji
na kumsihi kuwa
yale yalikuwa ni maneno ya mtoto
tu ambaye
pengine ilitokezea akawasikia
wakiongelea juu ya
mpango wao huo. Haikumuingia
akilini kamwe!
Siku hiyo walishinda ovyoovyo tu,
chakula
hakikulika. Hatimaye usiku
ukaingia na kuzidisha
simanzi kwa wanafamilia.
Nyanzala akiogopa kufa,
mama Kaguba naye akiogopa hata
kulala na
mwanaye, huku ndugu wengine
wakihofia balaa
inayotaka kuukumba ukoo wao.
Usingizi ukaota
mbawa. Lakini hali hiyo ya
mang’amng’am iliduma
kwa muda tu. Baadaye usingizi
ukawapitia.
Siku hiyo usingizi ulikuwa mzito
kwa karibu kila
mmoja wa wanafamilia wale, kama
ungebahatika
kukatiza nje ya nyumba yao kwa
usiku ule,
ungedhani kuna helkopta
zinajiandaa kuruka kwa
jinsi walivyokua wakikoroma.
Walilala fofofo!
Kilichowashitua asubuhi na
mapema ni TANZIA
(Tangazo la kifo) iliyokuwa
ikinadiwa kutoka katika
spika kubwa za msikitini. Haikuwa
jambo la ajabu
sana kusikia Tanzia kutoka katika
spika za
msikitini maana huo ni utaratibu
wa kawaida kwa
waumini wa dini zote kubwa
kupashania habari
kupitia spika hizo bila kujali
tofauti ya dini zao, ila
hii ilikuwa ni taarifa ya kushitua
kwao.
“…ifuatayo ni Tanzia, familia ya
hayati Bi
Masonganya wa kilogho, Kibondo
inasikitika
kutangaza kifo cha mtoto wao, Bi
Nyazala.
Kilichotokea usiku wa kuamkia
leo…maziko
yatafanyika leo saa kumi Alasiri.”
Sehemu ya
Tanzia hiyo ilisikika ikinadi.
Heeh!
Nyanzala amekufa?
Familia nzima ilikumbwa na
mshituko na woga
kutokana na tangazo hilo.
ukizingatia kuna hadhari
ambayo ilikuwa ni kama Tanzia
kabla ya tukio
waliyopewa na mtoto Kaguba na
sasa kimeibuka
kioja kipya kwamba tangazo
limenadiwa kuhusu
kifo cha Nyanzala bila ya hata wao
kama ndugu na
wahusikawa karibu kujua lolote!
“Mama Kaguba…” Aliita Mzee
Mtandi kwa sauti ya
mashaka na wahka. “…Mama
Kagubaaa..” aliita
tena Mzee yule kutokea chumbani
kwake.
“Abee Mjomba,” Alijibu Mama
Kaguba.
“Umesikia hilo Tangazo la kifo?”
“Kumbe nawe’ umelisikia?” Jibu
hilo la mama
Kaguba liliwafanya familia nzima
ishituke, kumbe
kila mmoja kutokea chumbani
kwake alilisikia
vyema Tangazo lile. Wote
wakatoka wakiwa bado
na mang’amng’am ya usingizi
mpaka sebuleni,
wakautwaa mlango wa chumba
cha Nyanzala na
kuugonga zaidi ya mara tatu bila
kujibiwa.
Hofu ikiwazidia!
Hapakuwa na la ziada, wakauvunja
mlango kisha
wote wakakivamia kitanda cha
Nyanzala na
kumkuta akiwa amejilaza kiubavu
huku roho
ikionesha dalili kuwa iliuacha
mwili ule karibu hata
saa tano mbele. Alitulia tuli akiwa
amepoa kabisa!
Vilio vikalipuka. Ndugu walilia kwa
maombolezo na
vihoro vya hali ya juu, hakika
msiba ule wa
maajabu uliwaumiza sana.
Haya sasa Nyanzala ni kweli
amekwishaaga dunia
lakini sasa kwanini kifo chake
kilibashiriwa na
mtoto mdogo Kaguba? Na kwanini
Tangazo la kifo
(Tanzia) linadiwe huko kwenye
vipaza sauti ilhali
wao kama wanafamilia waliolala
naye nyumba
moja wakiwa hawajapata taarifa ya
kifo hicho?
Maana kwa kawaida wao kama
ndugu ndiyo
walipaswa kupeleka taarifa za
msiba wao msikitini
ili watangaziwe watu…hapakuwa
na majibu ya
kutosha zaidi vilio vikali
vilivyogubikwa na hofu na
mashaka.
Majirani kama ilivyo kawaida yao
wakajaa tele
kama pishi la mchele
wakishirikiana bega kwa
bega mpaka walipohitimisha safari
ya mwisho ya
Nyanzala. Familia ilijitahidi kuficha
ukweli
uliokigubika kifo kile kuwa
ulibashiriwa na Kaguba,
ila hawakuwa wapuuzi wa
kulipuuzia jambo lile
zito. Wakaendelea kumuandama
kwa maswali
Kaguba huku wakimtishia
kumchapa viboko lakini
walaa hakusema lolote la maana,
ni kama hakuwa
yeye aliyeropoka maneno mazito
juzi yake tu. Na
hata walipowakabili viongozi wa
msikitini kuhusu ni
nani aliyepeleka tangazo lile bila
ya wao kuhusika?
Majibu yalizidi kutatanisha, hata
wao hawakumjua
aliyetangaza maana japo walikuwa
wameufunga
msikiti lakini waliweza kusikia
tangazo hilo
likitokea katika spika hizo…na
kweli sauti ya
aliyetangaza haikuwa ile ya siku
zote.
Utata!
Hatimaye katika hali hiyohiyo ya
sintofaamu,
Nyanzala akazikwa…na shughuli
za msiba
zikaendelea kama ilivyo ada.
“Ebyomunyumba tebi totolwa!”
Mzee Mtandi
aliwasihi wanawe kwa lugha ya
Kinyankole. Wote
walimuelewa kwakuwa alipendelea
sana kulitumia
neno hilo kwenye muktadha wa
namna ile. Msemo
huo ulimaanisha kwamba ‘Ya
vyumbani,
hayajadiliwi hadharani.’ Hivyo siri
zilizogubika kifo
hicho wasiweke hadharani.
***
Siku moja ndugu kadhaa wa
familia ya Bi
Masonganya wakiwa wameketi nje
ya nyumba yao
kwa upande wa barabarani huku
wengine wakiwa
wameketi juu ya viti na wengine
juu ya daraja
kubwa la maji linalotenganisha
nyumba na
barabara kubwa, ikiwa ni siku
kadhaa tangu
wamalize msiba wa ndugu yao
kipenzi, ndipo
wakasikia sauti iliyowashitua
sana…sauti ya
mwanamke anayeonekana
kuchoka sana.
“Uuuh…uuh ja-maaa-ni ni-sa-me-
he-ni, msi-ni-pi-
ge…nipelekeni taratibu.” Ilikuwa ni
sauti
waliyoifahamu fika, sauti ya ndugu
yao kipenzi
hayati Nyanzala. Sauti hiyo ya
kulalamika kutoka
kwa Nyanzala ilitokea usawa wa
chini ya lile
daraja kubwa walilokuwa wameketi
juu yake huku
wamening’iniza miguu yao kwa
starehe. Wakiwa
wameduwaa ndipo tena ikafuatia
sauti nyingine
wasiyoifahamu ikimkemea
Nyanzala kwa
ghadhabu.
“Tulia mbwa we’.. tembea
haraka…” Sauti hiyo
ilifuatiwa na milio ya mijeredi ya
nguvu kama kuna
ng’ombe au punda anayeadhibiwa.
“Uwiiii…naku-faa.. jamani mtaniua,
nioneeni
huruma jamani.” Baada ya hapo
familia nzima
ilipitiana mieleka, wa huku, kule!
Na wakule huko!
Wote wakigombea mlango ili
waingie ndani. Hakika
hofu iliwavaa.
Yaani wamemsikia hivihivi ndugu
yao
waliokwishamzika, akilia kwa
uchungu huku
akiteswa sana, hakika siku
iliwaharibikia. Kilio
kikaanza upya, hata wanaume
walishindwa kujizuia
nao wakawa wanalia. Inaonekana
hao
wanaomtesa Nyanzala waliamua
kwa makusudi
kabisa kuja kumtesa mbele yao
wakiwaoneshea
umwamba wao. Hawakua na la
kufanya,
wakanyamazishana na kwenda
kulala! Vitanda
vilikuwa vichungu.
***
“Heeh! NYA-NZALA?” Mama
Kaguba aliyekuwa
akipika uani alihamaki baada ya
kumuona Nyazala
akiingia mle uani akiwa mchovu,
mchafu, hoi bin
ta’aaban.
ITAENDELEA
Kibena akitokea
maeneo ya Kakonko. Huyu
alitumainiwa kuwa
angeweza kumtapisha Bi
Masonganya ile ‘mpigi’
aliyomeza ili akazikwe maana Bi
Kibena naye ni
kiboko kwa uchawi. Baada ya
kusalimiana na
wafiwa aliingia mpaka chumbani
ilipolala maiti na
kuwaamuru watu wote watoke nje,
walipotoka tu
akaanza vimbwanga vyake!
Laahaullah!
Kilichomkuta Bi Kibena alikijua
yeye na Mungu
wake, watu walisikia kukurukakara
ya haja
ikiendelea mle chumbani mpaka
ikabidi wafungue
haraka mlango. Ndipo wakamkuta
bi kibena akiwa
kama mchawi aliyeenda kucheza
mahepe kwenye
nyumba iliyozindikwa na hatimaye
akaya-bhula…
haja kubwa na ndogo vilihitimisha
kifo cha bi
Kibena alipofikishwa nyumbani
kwake!
“Jamani ndugu wafiwa na majirani,
maziko
yameakhirishwa mpaka hapo
mtakapotangaziwa
vinginevyo.” Sauti ya Mzee Mtandi
ambaye ndiye
msimamizi wa msiba ilihitimisha
na watu wote
kusambaa.
Kifo cha Bi Masonganya kilijizolea
umaarufu
kutoka kila pembe ya mkoa wa
Kigoma huku kila
mmoja akiwana mshawasha wa
kutaka kujua nini
hatma yake…ikawa kama mchezo
sasa, haipiti japo
saa moja bila ya Bi Masonganya
kufumbua macho
japo vipimo vyote vya waganga na
hata madaktari
wa kawaida walioshirikishwa
vilionesha kuwa
amekwishafariki.
Zikapita takribani siku tatu bila ya
mwili wa Bi
Masonganya kuzikwa, huku ndugu
wakiswampa
kila uchao kutafuta waganga wa
kulitatua tatizo
lililoikumba familia yao, kila
mganga aliyefuatwa
alipokaribia tu na nyumba ilimo
maiti aliishia nje
na kuingia mitini! Haikuwa kazi
rahisi.
Siku ya tano, mwili wa marehemu
ukiwa
umekwishaanza kutahayari ndipo
wana-ukoo
walipofanikiwa kumpata mganga
maeneo ya vijiji
vya mbali kidogo tokea Kibondo
mjini.
Ilichukuwa karibu saa saba
kutokea huko vijini kwa
mwendo wa gari mpaka kufika
hapo Kibondo mjini.
Wakiwa bado hawajafika nyumbani
ulipo msiba
ghafla mkwara wa Babu-mganga
ukaanza,
akapandisha mashetani yake
kichwani na kuanza
kufanya vurugu kubwa ndani ya
gari. Alipotulia
akamuamuru dereva asimamishe
gari kisha yeye
akashuka na kikapu chake kichafu
na kilichochakaa
kama nguo zake alizozivaa…
wafiwa waliomuendea
nao wakashuka.
“Vipi babu?”
“Mizimu imenikatalia kwenda kwa
gari huko
nyumbani kwenu…yaonekana huyo
aliyekufa
hakuwa mtu wa kawaida asilani.”
Wafiwa
wakaangaliana, kisha mmoja
akamsaili tena.
“Kwahiyo tunafanyaje?”
“Hakuna cha tunafanyaje hapa…
twendeni kwa
miguu tu!”
Haikuwa mbali sana na nyumba,
hivyo walitembea
kwa karibu nusu saa wakawasili
na kupokelewa na
ndugu na majirani walioanza
kufurika.
“Jamanimi’ si mkaaji hapa…”
alianza kuongea
mganga. “…nataka kufanya kazi
yangu haraka
iwezekanavyo ili niondoke zangu.”
“Sawa babu karibu ndani,” Alijibu
mtoto wa kiume
wa marehemu huku akifungua
mlango mkubwa wa
mbele na kumpisha Babu-mganga
aingie ndani.
“Hapana mi’ sipitii mlangoni,
naomba mniruhusu
nipande juu ya bati la nyumba
yenu kisha nipitie
huko kwa juu.”
Heh!
“Sasa utapitiaje kwa juu babu?”
“N’tafumua bati pamoja na
singibodi kama iko
kisha n’taibukia chumbani kwa
mtuhumiwa
wenu.”Ilikuwa ni mzaha mwingine
msibani hapo,
ila kwakuwa walikuwa wanashida
wakamkubalia,
Babu akapanda juu ya nyumba
huku watu
wakimshangaa na baadhi ya
wafiwa wakitangulia
chumba chenye maiti.
Watu walimshuhudia babu
akipanda mpaka juu na
kufumua bati kisha akidumbukia
kwa ndani kiasi
cha kuachia kishindo kizito…
nyumba nzima
ikatulia, walio nje wakisubiri
taarifa ya kitakachojiri
huko chumbani.
Zilipita dakika takribani thelathini
nyumba ikiwa
kimya kila mmoja akijiandaa
kutimua mbio endapo
maiti itazua songombingo.
Haikuwa hivyo,badala
yake zilisikika sauti za vigeregere
na shangwe
kutokea chumbani, ikiwa ni ishara
ya kazi
kukamilika. Bi Masonganya
alitapishwa mpigi yake.
Haikuchukuwa muda mrefu Babu
akatoka akiwa na
kikapu chake mkononi akifuatiwa
na wafiwa.
Akaaga na kuondoka zake.
Bi Masonganya akaandaliwa na
kwenda kuzikwa
kimila, akiwa ameviringishwa
ndani ya ngozi ya
Ng’ombe mweusi.
Msiba ukaisha.
Majirani wakasambaa, na wafiwa
wakarejea kwao
kumalizia siku tatu zamsiba kabla
na wao
hawajasambaana!
***
“Mamaa…mamaa.” Kaguba alikuwa
akimgasi kwa
kumuita mama yake wakati kikao
cha kumalizia
msiba wa Bi Masonganya
kikiendelea. Kaguba ni
mjukuu wa marehemu Bi
Masonganya, mtoto wa
kike wa mwanaye wa pili kutoka
mwisho.
“Mamaaa…mama.” Kaguba
aliendelea kumgasi
mama yake aliyekuwa
amempakata miguuni.
Mama Kaguba alimpuuza
mwanaye akiamini hana
jipya pengine na umri wake kuwa
mdogo. Kaguba
alikuwa ni mtoto wa miaka
takribani minne tu.
“Mama ujue mi’ n’namuonea
huruma sana
ma’mdogo Nyanzala,” alisema
Kaguba na kufanya
kikao kipige kimya kidogo huku
watu wote
wakimuangalia kama kituko vile
kwa ile kauli yake
aliyoitoa baada ya kuona mama
yake hamjibu
chochote akiendelea kufuatilia
kikao. Wakajikuta
wote wamecheka!
“Unamuonea huruma ya nini
mama?” Mama
Kaguba alimuuliza kimzaha
Kaguba wake huku
wengine wakimsikiliza.
“Hivi kwanini sasa ma’mdogo
Nyanzala alikubali
kupiga mwichi chini ya ukuta ili
amuue bibi?”
alisaili mtoto Kaguba na kuwaacha
midomo wazi
wote mle ndani.
Haikuwa jambo la kawaida kwa
mtoto mdogo wa
umri wa Kaguba kutambua jambo
lile lililofanyika
kisiri. Na hata wakati yote hayo
yalipokuwa
yakitendeka yeye(Kaguba) alikuwa
uani huko
akicheza na wenziye, sasa
ameyajuaje haya.
“Shauri yenu, mjue wamekasirika
sana huko.”
Kaguba aliropoka tena.
Ama!
“We’Kaguba, akina nani hao
wamekasirika?
amekwambia maneno hayo?” Mzee
Mtandi ambaye
ni kaka wa marehemu alimsaili
mjukuu wake kwa
kihoro kikubwa.
“Eeenh…nyie ngojeni tu! Kesho
mtaona tu
ma’mdogo Nyanzala naye
anakufa!”
SEHEMU YA PILI
Ukumbi mzima ulizizima kwa hofu
na mashaka.
Hali ile haikuwa ya kawaida hata
kidogo.
Walipojaribu kumdodosa Kaguba
wao tena
hakuendelea kusema chochote
cha maana zaidi ya
kubwabwaja maneno yasiyo na
maana yoyote,
maneno ya kitoto tu!
Raha ikawaisha, kikao kikafa
kimyakimya!
Nyanzala alichanganyikiwa
maradufu, hofu kuu
ilimvaa, mishipa ya shingo ikawa
inampwita kama
moyo wa chura. Kila mara alikuwa
akilia tu
akihofia kifo alichobashiriwa na
mtoto wa dada
yake. Ndugu walijaribu kumfariji
na kumsihi kuwa
yale yalikuwa ni maneno ya mtoto
tu ambaye
pengine ilitokezea akawasikia
wakiongelea juu ya
mpango wao huo. Haikumuingia
akilini kamwe!
Siku hiyo walishinda ovyoovyo tu,
chakula
hakikulika. Hatimaye usiku
ukaingia na kuzidisha
simanzi kwa wanafamilia.
Nyanzala akiogopa kufa,
mama Kaguba naye akiogopa hata
kulala na
mwanaye, huku ndugu wengine
wakihofia balaa
inayotaka kuukumba ukoo wao.
Usingizi ukaota
mbawa. Lakini hali hiyo ya
mang’amng’am iliduma
kwa muda tu. Baadaye usingizi
ukawapitia.
Siku hiyo usingizi ulikuwa mzito
kwa karibu kila
mmoja wa wanafamilia wale, kama
ungebahatika
kukatiza nje ya nyumba yao kwa
usiku ule,
ungedhani kuna helkopta
zinajiandaa kuruka kwa
jinsi walivyokua wakikoroma.
Walilala fofofo!
Kilichowashitua asubuhi na
mapema ni TANZIA
(Tangazo la kifo) iliyokuwa
ikinadiwa kutoka katika
spika kubwa za msikitini. Haikuwa
jambo la ajabu
sana kusikia Tanzia kutoka katika
spika za
msikitini maana huo ni utaratibu
wa kawaida kwa
waumini wa dini zote kubwa
kupashania habari
kupitia spika hizo bila kujali
tofauti ya dini zao, ila
hii ilikuwa ni taarifa ya kushitua
kwao.
“…ifuatayo ni Tanzia, familia ya
hayati Bi
Masonganya wa kilogho, Kibondo
inasikitika
kutangaza kifo cha mtoto wao, Bi
Nyazala.
Kilichotokea usiku wa kuamkia
leo…maziko
yatafanyika leo saa kumi Alasiri.”
Sehemu ya
Tanzia hiyo ilisikika ikinadi.
Heeh!
Nyanzala amekufa?
Familia nzima ilikumbwa na
mshituko na woga
kutokana na tangazo hilo.
ukizingatia kuna hadhari
ambayo ilikuwa ni kama Tanzia
kabla ya tukio
waliyopewa na mtoto Kaguba na
sasa kimeibuka
kioja kipya kwamba tangazo
limenadiwa kuhusu
kifo cha Nyanzala bila ya hata wao
kama ndugu na
wahusikawa karibu kujua lolote!
“Mama Kaguba…” Aliita Mzee
Mtandi kwa sauti ya
mashaka na wahka. “…Mama
Kagubaaa..” aliita
tena Mzee yule kutokea chumbani
kwake.
“Abee Mjomba,” Alijibu Mama
Kaguba.
“Umesikia hilo Tangazo la kifo?”
“Kumbe nawe’ umelisikia?” Jibu
hilo la mama
Kaguba liliwafanya familia nzima
ishituke, kumbe
kila mmoja kutokea chumbani
kwake alilisikia
vyema Tangazo lile. Wote
wakatoka wakiwa bado
na mang’amng’am ya usingizi
mpaka sebuleni,
wakautwaa mlango wa chumba
cha Nyanzala na
kuugonga zaidi ya mara tatu bila
kujibiwa.
Hofu ikiwazidia!
Hapakuwa na la ziada, wakauvunja
mlango kisha
wote wakakivamia kitanda cha
Nyanzala na
kumkuta akiwa amejilaza kiubavu
huku roho
ikionesha dalili kuwa iliuacha
mwili ule karibu hata
saa tano mbele. Alitulia tuli akiwa
amepoa kabisa!
Vilio vikalipuka. Ndugu walilia kwa
maombolezo na
vihoro vya hali ya juu, hakika
msiba ule wa
maajabu uliwaumiza sana.
Haya sasa Nyanzala ni kweli
amekwishaaga dunia
lakini sasa kwanini kifo chake
kilibashiriwa na
mtoto mdogo Kaguba? Na kwanini
Tangazo la kifo
(Tanzia) linadiwe huko kwenye
vipaza sauti ilhali
wao kama wanafamilia waliolala
naye nyumba
moja wakiwa hawajapata taarifa ya
kifo hicho?
Maana kwa kawaida wao kama
ndugu ndiyo
walipaswa kupeleka taarifa za
msiba wao msikitini
ili watangaziwe watu…hapakuwa
na majibu ya
kutosha zaidi vilio vikali
vilivyogubikwa na hofu na
mashaka.
Majirani kama ilivyo kawaida yao
wakajaa tele
kama pishi la mchele
wakishirikiana bega kwa
bega mpaka walipohitimisha safari
ya mwisho ya
Nyanzala. Familia ilijitahidi kuficha
ukweli
uliokigubika kifo kile kuwa
ulibashiriwa na Kaguba,
ila hawakuwa wapuuzi wa
kulipuuzia jambo lile
zito. Wakaendelea kumuandama
kwa maswali
Kaguba huku wakimtishia
kumchapa viboko lakini
walaa hakusema lolote la maana,
ni kama hakuwa
yeye aliyeropoka maneno mazito
juzi yake tu. Na
hata walipowakabili viongozi wa
msikitini kuhusu ni
nani aliyepeleka tangazo lile bila
ya wao kuhusika?
Majibu yalizidi kutatanisha, hata
wao hawakumjua
aliyetangaza maana japo walikuwa
wameufunga
msikiti lakini waliweza kusikia
tangazo hilo
likitokea katika spika hizo…na
kweli sauti ya
aliyetangaza haikuwa ile ya siku
zote.
Utata!
Hatimaye katika hali hiyohiyo ya
sintofaamu,
Nyanzala akazikwa…na shughuli
za msiba
zikaendelea kama ilivyo ada.
“Ebyomunyumba tebi totolwa!”
Mzee Mtandi
aliwasihi wanawe kwa lugha ya
Kinyankole. Wote
walimuelewa kwakuwa alipendelea
sana kulitumia
neno hilo kwenye muktadha wa
namna ile. Msemo
huo ulimaanisha kwamba ‘Ya
vyumbani,
hayajadiliwi hadharani.’ Hivyo siri
zilizogubika kifo
hicho wasiweke hadharani.
***
Siku moja ndugu kadhaa wa
familia ya Bi
Masonganya wakiwa wameketi nje
ya nyumba yao
kwa upande wa barabarani huku
wengine wakiwa
wameketi juu ya viti na wengine
juu ya daraja
kubwa la maji linalotenganisha
nyumba na
barabara kubwa, ikiwa ni siku
kadhaa tangu
wamalize msiba wa ndugu yao
kipenzi, ndipo
wakasikia sauti iliyowashitua
sana…sauti ya
mwanamke anayeonekana
kuchoka sana.
“Uuuh…uuh ja-maaa-ni ni-sa-me-
he-ni, msi-ni-pi-
ge…nipelekeni taratibu.” Ilikuwa ni
sauti
waliyoifahamu fika, sauti ya ndugu
yao kipenzi
hayati Nyanzala. Sauti hiyo ya
kulalamika kutoka
kwa Nyanzala ilitokea usawa wa
chini ya lile
daraja kubwa walilokuwa wameketi
juu yake huku
wamening’iniza miguu yao kwa
starehe. Wakiwa
wameduwaa ndipo tena ikafuatia
sauti nyingine
wasiyoifahamu ikimkemea
Nyanzala kwa
ghadhabu.
“Tulia mbwa we’.. tembea
haraka…” Sauti hiyo
ilifuatiwa na milio ya mijeredi ya
nguvu kama kuna
ng’ombe au punda anayeadhibiwa.
“Uwiiii…naku-faa.. jamani mtaniua,
nioneeni
huruma jamani.” Baada ya hapo
familia nzima
ilipitiana mieleka, wa huku, kule!
Na wakule huko!
Wote wakigombea mlango ili
waingie ndani. Hakika
hofu iliwavaa.
Yaani wamemsikia hivihivi ndugu
yao
waliokwishamzika, akilia kwa
uchungu huku
akiteswa sana, hakika siku
iliwaharibikia. Kilio
kikaanza upya, hata wanaume
walishindwa kujizuia
nao wakawa wanalia. Inaonekana
hao
wanaomtesa Nyanzala waliamua
kwa makusudi
kabisa kuja kumtesa mbele yao
wakiwaoneshea
umwamba wao. Hawakua na la
kufanya,
wakanyamazishana na kwenda
kulala! Vitanda
vilikuwa vichungu.
***
“Heeh! NYA-NZALA?” Mama
Kaguba aliyekuwa
akipika uani alihamaki baada ya
kumuona Nyazala
akiingia mle uani akiwa mchovu,
mchafu, hoi bin
ta’aaban.
ITAENDELEA