Post by Admin on May 30, 2015 4:37:29 GMT
Yaani wamemsikia hivihivi ndugu
yao
waliokwishamzika, akilia kwa
uchungu huku
akiteswa sana, hakika siku
iliwaharibikia. Kilio
kikaanza upya, hata wanaume
walishindwa kujizuia
nao wakawa wanalia. Inaonekana
hao
wanaomtesa Nyanzala waliamua
kwa makusudi
kabisa kuja kumtesa mbele yao
wakiwaoneshea
umwamba wao. Hawakua na la
kufanya,
wakanyamazishana na kwenda
kulala! Vitanda
vilikuwa vichungu.
***
“Heeh! NYA-NZALA?” Mama
Kaguba aliyekuwa
akipika uani alihamaki baada ya
kumuona Nyazala
akiingia mle uani akiwa mchovu,
mchafu, hoi bin
ta’aaban.
“Abee dada.”
“Ni wewe kweli?”
“Ni mimi dada yangu, nimepigwa
sana, hapa sina
hali.”
“Enhee Ulikuwa wapi kwanza? Na
ninani huyo
aliykupiga hivi? Mbona umeumia
hivi jamani
mdogo wangu?” Maswali mfululizo
yalimtoka
mama Kaguba.
“Nilichukuliwa kwa Binti Sambayu
nd’o nimewekwa
huko, napigwa sana na kupewa
kila aina ya
mateso!”
“Heeh! Binti Sambayu?” Mama
Kaguba alishangaa
kusikia kumbe siku zote zile
Nyanzala alikuwa kwa
Binti Sambayu japo hakuelewa
kuwa kwanini Bi
mkubwa yule amchukue ndugu
yao na kumtesa
vile. Binti Sambayu ni mdogo’ake
na hayati Bi
Kibena, yule mchawi aliyeshindwa
kumtapisha
mpigi hayati Bi Masonganya
mpaka naye kifo cha
kidhalili kikamkumba.
“Sasa kwanini anakutesa kiasi
hiki?”
“Anasema kuwa mi’ nisingeshiriki
kumuua Bi
Masonganya nisingesababisha
ndugu yake akafa
kifo cha fadhaa namna ile hivyo
anamalizia hasira
zake kwangu…sasa leo kuna kazi
alinipa ya
kufyeka ile michongoma
inayozunguka nyumba
yake, nilipofika karibu na kule
chooni kwake
nikaangusha upanga niliokuwa
nikiutumia kufyekea
majani, nilipouangalia chini
sikuuona kabisa ndipo
akaja yeye mwenyewe na kuanza
kunipiga sana na
kunichoma na vijinga vya moto…
akaniambia
niondoke haraka nije kuwaambieni
kuwa anataka
upanga wake hivyo ninyi mumlipe
Laa sivyo
atanitesa sana na hata ikibidi
kumuua mtu
mwingine humu ndani.” Nyanzala
alikuwa akiongea
huku akilia kiasi cha kumfanya
mama Kaguba naye
alie sana kwa uchungu wa
mdogo’ake.
“Sasa mbona umevaa ndala mguu
mmoja?” Mama
Kaguba alimsaili mdogo wake
baada ya kumtupia
jicho mguuni.
“Wakati nakimbia kipigo cha Binti
Sambayu nd’o
nikaangusha ndala moja kulekule
nyumbani kwake,
nyuma ya choo nilipokuwa
nikifyeka michongoma
yake…Dada acha mimi niondoke
nisije kufuatwa
tena huku ikawa balaa jingine.”
“HA-PA-NA Nyanzala, usiondoke
tafadhali,watak
uua huko mdogo’angu..” Kabla
mama Kaguba
hajamilizia sentensi yake, tayari
Nyanzala
alikwishatoweka mbele ya upeo
wa macho yake.
“NOOO, NYANZALAAAAAA,
USIENDE HUKOOOO.”
Sauti kali aliyoitoa mama Kaguma
nd’o ikamtoa
usingizini, na kujikuta akiwa
kitanda amelala.
Kumbe ilikuwa ni ndoto tu.
Sauti yake hiyo iliwafanya karibu
nyumba nzima
washituke, wote wakihamaki
kumsikia ndugu yao
akiweweseka kwa kumtaja
marehemu.
Wakamkimbilia chumbani mwake
ambapo
walimkuta ameketi juu ya kitanda,
akihema kwa
kasi sana kama aliyekimbizwa.
“Nini tena mama Kaguba?” alisaili
dada yake na
mama Kaguba.
“Nimeota Ndoto…mbaya sana!”
“Ndoto gani hiyo?” Kabla mama
Kaguba hajaanza
kusimulia ndoto yenyewe. Ndipo
Kaguba aliyekuwa
ameshaamka akaingilia kati kama
kawaida yake.
“Halafu huyu ma’mdogo Nyanzala
tatizo lake ni
kiburi sana, shauri yake watamuua
bure…ye’
ameambiwa awaambie tu mumlipie
upanga wa
watu alioupoteza halafu ye’
anakuja kusema
mpaka hayo mambo mengine ya
kuteswa na Bi
Kibena. Wakimsikia shauri yake
tuu.”
Laah!
Damu zikawasisimka wote mle
chumbani, hakuna
aliyeamini kusikia tena maneno ya
mtoto Kaguba.
Ikabidi wamgeukie mama Kaguba
aliyepigwa na
Butwaa kuona mwanaye
anasimulia kitu ambacho
amekiota yeye. Hapo ndipo akajua
kuwa ile
haikuwa ndoto ya kawaida na pia
sasa ikazidi
kuwadhihirikia kuwa Kaguba si
mtu kawaida. Kwa
hofu na kihoro cha hali ya
juuakaanza kuwasimulia
ndoto aliyoota, kila moja alihisi
mwili ukimfa ganzi
kwa woga.
Hapakulalika tena mapa
kulipopambazuka.
Walijaribu kumbana sana Kaguba
bila mafanikio.
Walipoona jitihada zao
zimeshindikana ndipo
wakakubaliana watafute mganga
awasaidie.
“Jamani pamoja na kuwa
mmependekeza kuwa
twende kwa waganga ila mi’nina
rai moja…”
alinena Mzee Mtandi. “…Tusilikalie
kimya jambo
hili la kuteswakwa ndugu yenu…”
“Mjomba, si nd’o tunataka kumleta
mganga
kwakuwa hatujakubali kulikalia
kimya hili!” alijibu
kwa haraka bwana Kungurume,
mtoto wa kiume
wa hayati Bi Masonganya.
“Sina maana hiyo…” wote
wakamgeukia mjomba
wao ili wajue ni nini azma yake
hasa. “…nashauri
asubuhi hii tukanunue upanga
mpya kisha
tumfuate bila uoga huyo binti
Sambayu
tukamkabidhi ili aache kumtesa
mtoto wetu.”
“Aah mjomba hiyo haiwezakani
kabisa, hivi hata
huyo bibi si atatushangaa
kuyabeba mambo ya
kwenye ndoto halafu
tukampelekee yeye!” Alipinga
Kungurume.
“Na tutanzia wapi sasa kufanya
hivyo jamani?
Tutaonekana vituko..” Aliongezea
Kabinga, mjukuu
wa hayati Masonganya.
“Mnaona haiwezekani eeh? Lakini
nachowaambieni
mimi ni kwamba hii siyo ndoto ya
kawaida bali ni
ujumbe maalumu tuliotumiwa na
kama mko radhi
kuona ndugu yenu anaadhirika
kila siku haya
shauri yenu…mi’ mwenzenu
nimekuwa zamani
nimeona mambo mengi sana.
Waswahili wanasema
Awashwaye, ndiye ajikunaye…ni
lazima tujikune
wenyewe!” Rai hiyo ilikuwa ngumu
sana ila baada
ya majadiliano ya kina, na
kutokana na heshma na
imani waliyonayo wanafamilia kwa
mjomba na
babu yao mzee Mtandi,
waliafikiana.
***
Nje ya nyumba ya Binti Sambayu
walisimama watu
watatu; Mama Kaguba, Mzee
Saadallah, na
Kungurume wakiwa na upanga
wao mkononi. Ila
kabla hawajaingia wakawa
wanastaajabu kuona ni
kweli michongoma ilikuwa
inaonekana kufyekwa
siku si nyingi,bila shaka nd’o kazi
aliyokuwa
akiifanya Nyanzala.
Roho ziliwachinyota sanakwa
uchungu.
Wakapatwa na wazo jipya, kabla
ya kuingia ndani
wakazunguka nyuma ya choo
walipotajiwa na
Nyanza kupitia ndoto ya mama
Kaguba.
Hamaad!
Wakaikuta ile ndala moja ya mguu
wa kushoto
ambayo ya kulia yake ilikuwa
imevaliwa na
Nyanzala kule ndotoni. Kufikia
hapo sasa
hawakuwa na pingamizi kuwa
Nyanzala hakufa
kamwe, na kwamba anateswa na
Bi mkubwa yule.
Wakabisha hodibaada ya kuutwaa
mlangowa
kuingilia ndani kwa Binti Sambayu,
wakakaribishwa
na kuingia ndani. Wakamkuta Bi
mkubwa yule
mweusi kama pampu mpya akiwa
ametuna juu ya
kiti cha uvivu akiwa ameliatamia
jiko lake la mkaa
akiota moto licha ya joto kali
lililotamalaki karibu
Kibodo nzima.Kwa jinsi
alivyousokota uso wake
kwa ghadhabu na ule mdomo
alivyouvuta kama
Ndomolomo hakika kama
ungepata nafasi ya
kumtupia jicho mara moja,
usingekuwa na hamu
ya kumtazama kwa mara ya pili.
Wakamsalimu na kuketi.
“Mama siye tumekuja tunaomba
utupokee, na
tunaomba utuwie radhi kwa hili
kama tutakosea.
Tumepoea salamu zako kutoka
kwa Nyanzala
kuwa kuna upanga wako
aliupoteza hivyo
unamuadhibu sana…tumeleta
upanga mpya,
tunaomba sana mama yetu
uupokee na umpe
ahueni binti huyo ili apumzike
japo kidogo.” Mzee
Mtandi aliongea kwa niaba ya
wenziye.
Kikapita kimya cha kama dakika
moja hivi! Mzee
Mtandi akainuka na kumkabidhi
Binti Sambayu
upanga ule mpya.
Bila aibu wa soni, Binti Sambayu
akaupokea
upanga ule kisha akainuka na
kuelekea naousawa
wa chumba chake ambacho
kimefunikwa gunia
zito kama nd’o pazia. Akapotelea
humo.
“NIMEWAELEWA, MNAWEZA
KWENDA.” Sauti kali
ya binti Sambayu ikitokea kule
chumbani iliwaijia
mpaka pale sebuleni walipoketi.
Wakatazamana
kisha Mzee Mtandi akajibu kwa
nidhamu.
“Ahsante bi mkubwa,
tunakwenda.” Hawakujibiwa.
Wakasimama na kuondoka
kimyakimya mpaka
nyumbani kwao ambako walizua
kilio kipya,hakika
ilikuwa ni simanzi kubwa kwao.
SEHEMU YA TATU
Baada ya siku kadhaa kupita bila
mauzauza yoyote
kuwakuta ndipo wakaketi kikao
tena ambapoKwa
kauli moja wakaafikiana kuwa
wamuendee Babu
Gao, yule mganga bingwa
aliyemtapisha ‘mpigi’
hayati Bi Masonganya. Wakajiteua
baadhi na
kumfuata Babu Gao ambaye
aliwakubalia ombi lao
la kwenda huko kwao. akawaahidi
kuwa
angekwenda kesho yake hivyo
wao warejee tu
Kibondo mjini.
Ndugu waliokuwa wakiishi mbali
na Kibondo
walishindwa hata kuondoka tena
kutokana na si tu
vimbwanga vya mtoto wao,
Kaguba bali msiba
mpya wa ndugu yao Bi Nyanzala.
Japo watoto wa
mzee Mtandi waishio Kigoma, wao
iliwabidi
kuondoka kutokana na majukumu
ya ajira zao.
Wafiwa waliobaki wkiwa hapo
nyumbani ndipo
bingwa akawasili, Babu Gao akiwa
na kilekile
kikapu chake japo safari hii
aliingilia mlangoni
tofauti na awali.
“Karibu sana bwana mkubwa!”
Mzee Mtandi kama
kiongozi wa familia alimkaribisha
Babu Gao, wakati
huo wanafamilia wote wakiwa
wamejumuika
pamoja hapo sebuleni.
“Karibu…ahsante, karibu…ahsante,”
alijibu Babu
Gao kwa mkwara na mbwebwe za
kiganga huku
akitoa dawa zake na kuanza
kumwaga huku na
kule ikiwa kama ni kinga yake na
familia yote
katika muda atakaokuwa hapo.
Baada ya utulivu, mzee Mtandi
alitaka kutoa
muhtasari wa kilichojiri hapo
nyumbani lakini Babu
Gao akamzuia na kuanza kuongea.
“Kwanza poleni sana kwa msiba
mpya na kila
lililotokea…jana usiku sikulala
kabisa ilinibidi
kwanza niyaangalie haya mambo
yenu kwa jicho la
mwewe ili kabla ya kuja huku niwe
ninajua cha
kuwaelezeni…” alianza kutiririka
Babu Gao. “…najua
nyote mlifurahia kuwa Bi
Masonganya amekufa
akiwa hajamrithisha yeyote uchawi
wake, hapo
ndipo mlipokosea…
alikwishamrithisha mtu siku
nyingi, na mtu mwenyewe
mwenyewe mnaye
humuhumu ndani...”
Wakatazamana wanafamilia
kwa macho ya mashaka huku kila
mmojaakimhisi
mwenziye. Babu Gao akaendelea
tena kufunguka.
“Aliyerithishwa uchawi ni huyo
mtoto wenu
Kaguba!”
Loohsalalee!
“KA-GU-BA?...haiwezekani!
amewezaje kumrithisha
mtoto mdogo kama huyu?” alijibu
kwa wahka na
kihoro mama Kaguba.
Ukumbi mzima ukatulia na
kumtupia macho Babu
Gao ili kumsikia akijibu swali
pingamizi kutoka kwa
mama Kaguba.
“Hilo ni jambo la kawaida sana
kwa wachawi
wengi tu duniani kuwarithisha
vitunga vyao watoto
wadogo kutokana na ukubwa wa
uchawi
wenyewe…kama uchawi ni mzito
sana hulazimika
kumkabidhi mtoto mdogo
kwakuwa hatoukataa,
tofauti na mtu mzima ambaye
anaweza kuogopa
masharti yaliyomo ndani ya
vitunga hivyo vizito
vya uchawi…” Aliongea kwa
utulivu mkubwa Babu
Gao kisha akatulia ili maneno yake
yakite katika
vichwa ya wateja wake, halafu
akaendelea tena “…
Iko hivi kama kuna mchawi
mkubwa katika ukoo
na anataka kuurithisha kwa mtoto
mdogo basi
hufanya hivi…kila anapozaliwa
mtoto ndani ya
ukoo yeye hufika mapema akiwa
na dawa fulani ya
uchawi aliyoifunga kwenye pindo
la kanga yake,
kisha anapopata nafasi ya
kukibeba kichanga hicho
kuna jambo hufanyika hapo
kisirisiri ila ya
kuonekana na mtu…si mnajua
mtoto akiwa
mchanga, muda wote hukunja
viganja vyake vya
mikono kama aliyekunja ngumi
eenh?” alisaili Babu
Gao na kuitikiwa kwa vichwa tu
wanafamilia
waliokuwa wameingiwa na hofu,
kisha
akaendelea.“…Vizuri, sasa huyo
mchawi humkunjua
vidole mtoto huyo na kumwekea
dawa hiyo na
hapo ndipo miujiza hutokea…
mtoto huyo yeye
mwenyewe huukubali uchawi huo
ama kuukataa!”
“Kivipi mtoto mchanga asiyejua
lolote akubali ama
kukataa huo uchawi ambao
kwanza hata haujui?”
aliuliza Mzee Mtandi.
“Swali zuri, sasa iko hivi endapo
mtoto huyo
ataukataa uchawi huo basi
hutokea tu hatokifunga
kiganja chake cha mkono baada
ya kuwekea dawa
na huyo mchawi…na hapo
utamuona huyo mchawi
akiwa amekasirika kabisa na
huenda hata
akaondoka na kumwacha mtoto
akiumwa ovyo tu.
Na endapo mtoto huyo ataukubali
uchawi huo,
basi atakapoachiwa tu mkono
wake baada ya
kukunjuliwa kiganja chake na
kuwekewa ile dawa
ya kichawi, hapohapo huukunja
mkono wake na
kuifumbata vizuri dawa ile ambayo
hupotelea
katikati ya kiganja chake…hivyo
ndivyo ilivyokuwa
kwa Kaguba alipozaliwa, baada ya
kuupokea
uchawi ule akawa ni miongoni
mwao hivyo
haikuwa taabu kwake kujifunza
vitu vya jamii yake
hiyo ya kichawi maana wahenga
walinena;Kifara
nga hakifunzwi kuchakura,”
Alinena kwa utuo Babu
Gao.
ITAENDELEAAA....
yao
waliokwishamzika, akilia kwa
uchungu huku
akiteswa sana, hakika siku
iliwaharibikia. Kilio
kikaanza upya, hata wanaume
walishindwa kujizuia
nao wakawa wanalia. Inaonekana
hao
wanaomtesa Nyanzala waliamua
kwa makusudi
kabisa kuja kumtesa mbele yao
wakiwaoneshea
umwamba wao. Hawakua na la
kufanya,
wakanyamazishana na kwenda
kulala! Vitanda
vilikuwa vichungu.
***
“Heeh! NYA-NZALA?” Mama
Kaguba aliyekuwa
akipika uani alihamaki baada ya
kumuona Nyazala
akiingia mle uani akiwa mchovu,
mchafu, hoi bin
ta’aaban.
“Abee dada.”
“Ni wewe kweli?”
“Ni mimi dada yangu, nimepigwa
sana, hapa sina
hali.”
“Enhee Ulikuwa wapi kwanza? Na
ninani huyo
aliykupiga hivi? Mbona umeumia
hivi jamani
mdogo wangu?” Maswali mfululizo
yalimtoka
mama Kaguba.
“Nilichukuliwa kwa Binti Sambayu
nd’o nimewekwa
huko, napigwa sana na kupewa
kila aina ya
mateso!”
“Heeh! Binti Sambayu?” Mama
Kaguba alishangaa
kusikia kumbe siku zote zile
Nyanzala alikuwa kwa
Binti Sambayu japo hakuelewa
kuwa kwanini Bi
mkubwa yule amchukue ndugu
yao na kumtesa
vile. Binti Sambayu ni mdogo’ake
na hayati Bi
Kibena, yule mchawi aliyeshindwa
kumtapisha
mpigi hayati Bi Masonganya
mpaka naye kifo cha
kidhalili kikamkumba.
“Sasa kwanini anakutesa kiasi
hiki?”
“Anasema kuwa mi’ nisingeshiriki
kumuua Bi
Masonganya nisingesababisha
ndugu yake akafa
kifo cha fadhaa namna ile hivyo
anamalizia hasira
zake kwangu…sasa leo kuna kazi
alinipa ya
kufyeka ile michongoma
inayozunguka nyumba
yake, nilipofika karibu na kule
chooni kwake
nikaangusha upanga niliokuwa
nikiutumia kufyekea
majani, nilipouangalia chini
sikuuona kabisa ndipo
akaja yeye mwenyewe na kuanza
kunipiga sana na
kunichoma na vijinga vya moto…
akaniambia
niondoke haraka nije kuwaambieni
kuwa anataka
upanga wake hivyo ninyi mumlipe
Laa sivyo
atanitesa sana na hata ikibidi
kumuua mtu
mwingine humu ndani.” Nyanzala
alikuwa akiongea
huku akilia kiasi cha kumfanya
mama Kaguba naye
alie sana kwa uchungu wa
mdogo’ake.
“Sasa mbona umevaa ndala mguu
mmoja?” Mama
Kaguba alimsaili mdogo wake
baada ya kumtupia
jicho mguuni.
“Wakati nakimbia kipigo cha Binti
Sambayu nd’o
nikaangusha ndala moja kulekule
nyumbani kwake,
nyuma ya choo nilipokuwa
nikifyeka michongoma
yake…Dada acha mimi niondoke
nisije kufuatwa
tena huku ikawa balaa jingine.”
“HA-PA-NA Nyanzala, usiondoke
tafadhali,watak
uua huko mdogo’angu..” Kabla
mama Kaguba
hajamilizia sentensi yake, tayari
Nyanzala
alikwishatoweka mbele ya upeo
wa macho yake.
“NOOO, NYANZALAAAAAA,
USIENDE HUKOOOO.”
Sauti kali aliyoitoa mama Kaguma
nd’o ikamtoa
usingizini, na kujikuta akiwa
kitanda amelala.
Kumbe ilikuwa ni ndoto tu.
Sauti yake hiyo iliwafanya karibu
nyumba nzima
washituke, wote wakihamaki
kumsikia ndugu yao
akiweweseka kwa kumtaja
marehemu.
Wakamkimbilia chumbani mwake
ambapo
walimkuta ameketi juu ya kitanda,
akihema kwa
kasi sana kama aliyekimbizwa.
“Nini tena mama Kaguba?” alisaili
dada yake na
mama Kaguba.
“Nimeota Ndoto…mbaya sana!”
“Ndoto gani hiyo?” Kabla mama
Kaguba hajaanza
kusimulia ndoto yenyewe. Ndipo
Kaguba aliyekuwa
ameshaamka akaingilia kati kama
kawaida yake.
“Halafu huyu ma’mdogo Nyanzala
tatizo lake ni
kiburi sana, shauri yake watamuua
bure…ye’
ameambiwa awaambie tu mumlipie
upanga wa
watu alioupoteza halafu ye’
anakuja kusema
mpaka hayo mambo mengine ya
kuteswa na Bi
Kibena. Wakimsikia shauri yake
tuu.”
Laah!
Damu zikawasisimka wote mle
chumbani, hakuna
aliyeamini kusikia tena maneno ya
mtoto Kaguba.
Ikabidi wamgeukie mama Kaguba
aliyepigwa na
Butwaa kuona mwanaye
anasimulia kitu ambacho
amekiota yeye. Hapo ndipo akajua
kuwa ile
haikuwa ndoto ya kawaida na pia
sasa ikazidi
kuwadhihirikia kuwa Kaguba si
mtu kawaida. Kwa
hofu na kihoro cha hali ya
juuakaanza kuwasimulia
ndoto aliyoota, kila moja alihisi
mwili ukimfa ganzi
kwa woga.
Hapakulalika tena mapa
kulipopambazuka.
Walijaribu kumbana sana Kaguba
bila mafanikio.
Walipoona jitihada zao
zimeshindikana ndipo
wakakubaliana watafute mganga
awasaidie.
“Jamani pamoja na kuwa
mmependekeza kuwa
twende kwa waganga ila mi’nina
rai moja…”
alinena Mzee Mtandi. “…Tusilikalie
kimya jambo
hili la kuteswakwa ndugu yenu…”
“Mjomba, si nd’o tunataka kumleta
mganga
kwakuwa hatujakubali kulikalia
kimya hili!” alijibu
kwa haraka bwana Kungurume,
mtoto wa kiume
wa hayati Bi Masonganya.
“Sina maana hiyo…” wote
wakamgeukia mjomba
wao ili wajue ni nini azma yake
hasa. “…nashauri
asubuhi hii tukanunue upanga
mpya kisha
tumfuate bila uoga huyo binti
Sambayu
tukamkabidhi ili aache kumtesa
mtoto wetu.”
“Aah mjomba hiyo haiwezakani
kabisa, hivi hata
huyo bibi si atatushangaa
kuyabeba mambo ya
kwenye ndoto halafu
tukampelekee yeye!” Alipinga
Kungurume.
“Na tutanzia wapi sasa kufanya
hivyo jamani?
Tutaonekana vituko..” Aliongezea
Kabinga, mjukuu
wa hayati Masonganya.
“Mnaona haiwezekani eeh? Lakini
nachowaambieni
mimi ni kwamba hii siyo ndoto ya
kawaida bali ni
ujumbe maalumu tuliotumiwa na
kama mko radhi
kuona ndugu yenu anaadhirika
kila siku haya
shauri yenu…mi’ mwenzenu
nimekuwa zamani
nimeona mambo mengi sana.
Waswahili wanasema
Awashwaye, ndiye ajikunaye…ni
lazima tujikune
wenyewe!” Rai hiyo ilikuwa ngumu
sana ila baada
ya majadiliano ya kina, na
kutokana na heshma na
imani waliyonayo wanafamilia kwa
mjomba na
babu yao mzee Mtandi,
waliafikiana.
***
Nje ya nyumba ya Binti Sambayu
walisimama watu
watatu; Mama Kaguba, Mzee
Saadallah, na
Kungurume wakiwa na upanga
wao mkononi. Ila
kabla hawajaingia wakawa
wanastaajabu kuona ni
kweli michongoma ilikuwa
inaonekana kufyekwa
siku si nyingi,bila shaka nd’o kazi
aliyokuwa
akiifanya Nyanzala.
Roho ziliwachinyota sanakwa
uchungu.
Wakapatwa na wazo jipya, kabla
ya kuingia ndani
wakazunguka nyuma ya choo
walipotajiwa na
Nyanza kupitia ndoto ya mama
Kaguba.
Hamaad!
Wakaikuta ile ndala moja ya mguu
wa kushoto
ambayo ya kulia yake ilikuwa
imevaliwa na
Nyanzala kule ndotoni. Kufikia
hapo sasa
hawakuwa na pingamizi kuwa
Nyanzala hakufa
kamwe, na kwamba anateswa na
Bi mkubwa yule.
Wakabisha hodibaada ya kuutwaa
mlangowa
kuingilia ndani kwa Binti Sambayu,
wakakaribishwa
na kuingia ndani. Wakamkuta Bi
mkubwa yule
mweusi kama pampu mpya akiwa
ametuna juu ya
kiti cha uvivu akiwa ameliatamia
jiko lake la mkaa
akiota moto licha ya joto kali
lililotamalaki karibu
Kibodo nzima.Kwa jinsi
alivyousokota uso wake
kwa ghadhabu na ule mdomo
alivyouvuta kama
Ndomolomo hakika kama
ungepata nafasi ya
kumtupia jicho mara moja,
usingekuwa na hamu
ya kumtazama kwa mara ya pili.
Wakamsalimu na kuketi.
“Mama siye tumekuja tunaomba
utupokee, na
tunaomba utuwie radhi kwa hili
kama tutakosea.
Tumepoea salamu zako kutoka
kwa Nyanzala
kuwa kuna upanga wako
aliupoteza hivyo
unamuadhibu sana…tumeleta
upanga mpya,
tunaomba sana mama yetu
uupokee na umpe
ahueni binti huyo ili apumzike
japo kidogo.” Mzee
Mtandi aliongea kwa niaba ya
wenziye.
Kikapita kimya cha kama dakika
moja hivi! Mzee
Mtandi akainuka na kumkabidhi
Binti Sambayu
upanga ule mpya.
Bila aibu wa soni, Binti Sambayu
akaupokea
upanga ule kisha akainuka na
kuelekea naousawa
wa chumba chake ambacho
kimefunikwa gunia
zito kama nd’o pazia. Akapotelea
humo.
“NIMEWAELEWA, MNAWEZA
KWENDA.” Sauti kali
ya binti Sambayu ikitokea kule
chumbani iliwaijia
mpaka pale sebuleni walipoketi.
Wakatazamana
kisha Mzee Mtandi akajibu kwa
nidhamu.
“Ahsante bi mkubwa,
tunakwenda.” Hawakujibiwa.
Wakasimama na kuondoka
kimyakimya mpaka
nyumbani kwao ambako walizua
kilio kipya,hakika
ilikuwa ni simanzi kubwa kwao.
SEHEMU YA TATU
Baada ya siku kadhaa kupita bila
mauzauza yoyote
kuwakuta ndipo wakaketi kikao
tena ambapoKwa
kauli moja wakaafikiana kuwa
wamuendee Babu
Gao, yule mganga bingwa
aliyemtapisha ‘mpigi’
hayati Bi Masonganya. Wakajiteua
baadhi na
kumfuata Babu Gao ambaye
aliwakubalia ombi lao
la kwenda huko kwao. akawaahidi
kuwa
angekwenda kesho yake hivyo
wao warejee tu
Kibondo mjini.
Ndugu waliokuwa wakiishi mbali
na Kibondo
walishindwa hata kuondoka tena
kutokana na si tu
vimbwanga vya mtoto wao,
Kaguba bali msiba
mpya wa ndugu yao Bi Nyanzala.
Japo watoto wa
mzee Mtandi waishio Kigoma, wao
iliwabidi
kuondoka kutokana na majukumu
ya ajira zao.
Wafiwa waliobaki wkiwa hapo
nyumbani ndipo
bingwa akawasili, Babu Gao akiwa
na kilekile
kikapu chake japo safari hii
aliingilia mlangoni
tofauti na awali.
“Karibu sana bwana mkubwa!”
Mzee Mtandi kama
kiongozi wa familia alimkaribisha
Babu Gao, wakati
huo wanafamilia wote wakiwa
wamejumuika
pamoja hapo sebuleni.
“Karibu…ahsante, karibu…ahsante,”
alijibu Babu
Gao kwa mkwara na mbwebwe za
kiganga huku
akitoa dawa zake na kuanza
kumwaga huku na
kule ikiwa kama ni kinga yake na
familia yote
katika muda atakaokuwa hapo.
Baada ya utulivu, mzee Mtandi
alitaka kutoa
muhtasari wa kilichojiri hapo
nyumbani lakini Babu
Gao akamzuia na kuanza kuongea.
“Kwanza poleni sana kwa msiba
mpya na kila
lililotokea…jana usiku sikulala
kabisa ilinibidi
kwanza niyaangalie haya mambo
yenu kwa jicho la
mwewe ili kabla ya kuja huku niwe
ninajua cha
kuwaelezeni…” alianza kutiririka
Babu Gao. “…najua
nyote mlifurahia kuwa Bi
Masonganya amekufa
akiwa hajamrithisha yeyote uchawi
wake, hapo
ndipo mlipokosea…
alikwishamrithisha mtu siku
nyingi, na mtu mwenyewe
mwenyewe mnaye
humuhumu ndani...”
Wakatazamana wanafamilia
kwa macho ya mashaka huku kila
mmojaakimhisi
mwenziye. Babu Gao akaendelea
tena kufunguka.
“Aliyerithishwa uchawi ni huyo
mtoto wenu
Kaguba!”
Loohsalalee!
“KA-GU-BA?...haiwezekani!
amewezaje kumrithisha
mtoto mdogo kama huyu?” alijibu
kwa wahka na
kihoro mama Kaguba.
Ukumbi mzima ukatulia na
kumtupia macho Babu
Gao ili kumsikia akijibu swali
pingamizi kutoka kwa
mama Kaguba.
“Hilo ni jambo la kawaida sana
kwa wachawi
wengi tu duniani kuwarithisha
vitunga vyao watoto
wadogo kutokana na ukubwa wa
uchawi
wenyewe…kama uchawi ni mzito
sana hulazimika
kumkabidhi mtoto mdogo
kwakuwa hatoukataa,
tofauti na mtu mzima ambaye
anaweza kuogopa
masharti yaliyomo ndani ya
vitunga hivyo vizito
vya uchawi…” Aliongea kwa
utulivu mkubwa Babu
Gao kisha akatulia ili maneno yake
yakite katika
vichwa ya wateja wake, halafu
akaendelea tena “…
Iko hivi kama kuna mchawi
mkubwa katika ukoo
na anataka kuurithisha kwa mtoto
mdogo basi
hufanya hivi…kila anapozaliwa
mtoto ndani ya
ukoo yeye hufika mapema akiwa
na dawa fulani ya
uchawi aliyoifunga kwenye pindo
la kanga yake,
kisha anapopata nafasi ya
kukibeba kichanga hicho
kuna jambo hufanyika hapo
kisirisiri ila ya
kuonekana na mtu…si mnajua
mtoto akiwa
mchanga, muda wote hukunja
viganja vyake vya
mikono kama aliyekunja ngumi
eenh?” alisaili Babu
Gao na kuitikiwa kwa vichwa tu
wanafamilia
waliokuwa wameingiwa na hofu,
kisha
akaendelea.“…Vizuri, sasa huyo
mchawi humkunjua
vidole mtoto huyo na kumwekea
dawa hiyo na
hapo ndipo miujiza hutokea…
mtoto huyo yeye
mwenyewe huukubali uchawi huo
ama kuukataa!”
“Kivipi mtoto mchanga asiyejua
lolote akubali ama
kukataa huo uchawi ambao
kwanza hata haujui?”
aliuliza Mzee Mtandi.
“Swali zuri, sasa iko hivi endapo
mtoto huyo
ataukataa uchawi huo basi
hutokea tu hatokifunga
kiganja chake cha mkono baada
ya kuwekea dawa
na huyo mchawi…na hapo
utamuona huyo mchawi
akiwa amekasirika kabisa na
huenda hata
akaondoka na kumwacha mtoto
akiumwa ovyo tu.
Na endapo mtoto huyo ataukubali
uchawi huo,
basi atakapoachiwa tu mkono
wake baada ya
kukunjuliwa kiganja chake na
kuwekewa ile dawa
ya kichawi, hapohapo huukunja
mkono wake na
kuifumbata vizuri dawa ile ambayo
hupotelea
katikati ya kiganja chake…hivyo
ndivyo ilivyokuwa
kwa Kaguba alipozaliwa, baada ya
kuupokea
uchawi ule akawa ni miongoni
mwao hivyo
haikuwa taabu kwake kujifunza
vitu vya jamii yake
hiyo ya kichawi maana wahenga
walinena;Kifara
nga hakifunzwi kuchakura,”
Alinena kwa utuo Babu
Gao.
ITAENDELEAAA....