Post by Admin on May 30, 2015 4:44:33 GMT
SEHEMU YA TANO
“Swali zuri, sasa iko hivi endapo
mtoto huyo
ataukataa uchawi huo basi
hutokea tu hatokifunga
kiganja chake cha mkono baada
ya kuwekea dawa
na huyo mchawi…na hapo
utamuona huyo mchawi
akiwa amekasirika kabisa na
huenda hata
akaondoka na kumwacha mtoto
akiumwa ovyo tu.
Na endapo mtoto huyo ataukubali
uchawi huo,
basi atakapoachiwa tu mkono
wake baada ya
kukunjuliwa kiganja chake na
kuwekewa ile dawa
ya kichawi, hapohapo huukunja
mkono wake na
kuifumbata vizuri dawa ile ambayo
hupotelea
katikati ya kiganja chake…hivyo
ndivyo ilivyokuwa
kwa Kaguba alipozaliwa, baada ya
kuupokea
uchawi ule akawa ni miongoni
mwao hivyo
haikuwa taabu kwake kujifunza
vitu vya jamii yake
hiyo ya kichawi maana wahenga
walinena;Kifara
nga hakifunzwi kuchakura,”
Alinena kwa utuo Babu
Gao.
Wanafamilia wakaanagaliana,
hakuna aliyekuwa na
cha kubisha maana ni kweli
marehemu Bi
Masonganya alikuwa akipenda
sana kumtembelea
mtoto wake yeyote punde tu mara
baada ya
kujifungua, na hata yeye mama
Kaguba aishiye
wilayani Kasulu alipojifungua huyo
Kaguba wake, Bi
Masonganya aliwasili huko na
haraka aliwahi
kumbeba mtoto yule kama ilivyo
ada, hakuna
aliyemzuia wala kumshitukia. Bila
shaka hapo
ndipo alipopata fursa ya kutenda
huo ufedhuli
wake!
“Uchawi aliokabidhiwa huyu mtoto
wenu ni
mkubwa sana, hivi sasa yeye
ndiye kiongozi mkuu
wa wachawi wote wa ukanda huu
wa magharibi
licha ya umri wake huo mdogo…na
ameshauwa
watu wengi sana ambao hata
mkitajiwa
hamtoamini,na hata huyu
aliyefariki juzi naye
amemalizwa na mtoto wenu huyo
kwa maelekezo
au tuseme maombi aliypewa na
mmoja kati ya
watendaji wake wakubwa wa
kichawi. Ila angalizo
tu kwenu ni kwamba mtoto huyo
bado ni mdogo
sana asiyetambua lolote na
anayeongozwa na kiini
tu cha uchawi kilichomo ndani
yake sasa
mkimwendea vibaya kwanza
hatowajibu lolote
kwani kuna muda anakuwa na akili
za kitoto kama
walivyo watoto wengine na pia
zitakapomjia akili
zake za kichawi anaweza hata
kuwateketeza
nyumba nzima…” Babu Gao akiwa
anaendelea
kuongea, uzalendo ukamshinda
mama Kaguba na
kuanza kulia kwa uchungu na
fadhaa! Ikaanzaa
sasa kazi mpya ya kumbembeleza.
“Hebu mleteni hapa huyo mtoto,”
aliagiza Babu
Gao, na hapohapo akatoka mtu
mmoja mpaka uani
walipokuwa wakicheza watoto
wengi. Akamchukua
Kaguba na kurejea ndani.
Cha ajabu, Kaguba aliingia huku
akirukaruka ki-
mchezo kama wafanyavyo watoto,
ila alipoingia tu
mle sebuleni na kutupa macho
yake kwa mganga,
hapohapo akaanza kulia kwa hofu
huku
akitetemeka kwa woga.
“Unalia nini sasa wewe?” Mzee
Mtandi alimhoji
Kaguba wakati alipofikishwa pale
sebuleni.
“Namuogopa huyo…naomba
mnisamehe
msinipige.” Kila mtu alielewa kuwa
mtoto Kaguba
ni mchawi na nd’o maana
ameweza hata
kumtambua mganga. Babu Gao
hakuongea lolote,
akaingiza mkono kwenye kile
kikapu chake akatoa
kitu kama kibuyu hivi akiwa
amekizungushia
shanga za rangi za njano,
nyekundu na nyeusi…
“Nami’ ninacho sasa ukileta
mchezo nitakuua sasa
hivi hapa, haya tueleze ukweli
kwanini umemuua
ma’mdogo Nyanzala?” Babu Gao
alimfokea na
kumtisha Kaguba.
“Nisameheni Babu, mi’
nililazimishwa tu kumuua
kwakuwa yeye ndiye aliyemuua
Bibi!” Kaguba
alijibu huku akilia kwa sauti yenye
kitetemeshi cha
uoga.
“Ni kina nani hao
walokulazimisha?”
“Wale wachawi ninao waongozaga
usiku nd’o
waliniambia ni lazima tulipize
kisasi!”
“Umeshawaua watu wangapi?”
“awwwh..niii.. ni wengi tu!”
“Wataje haraka.”
“Dada Shumbana, mjomba
Makanya, kaka Ndugai,
mjomba Zumbe, ma’mdogo
Nyanzala na majirani”
Balaa!
Nyanzala, Makanya na Zumbe
wote ni watoto wa
marehemu Bi Masonganya, na
Shumbana pamoja
na Ndugai ni wajukuu waliofariki
kwa awamu
tofautitofauti katika mazingira ya
kutatanisha!
“Kwanini sasa huwa mnauwaua
wenzenu hivi?”
“Siye usiku huwa tunakula nyama
za watu,
kwahiyo ikifika zamu yetu ya
kutoa chakula nd’o
mimi na bibi tulikuwa tunamuua
mtu mmoja kwa
ajili ya kumla usiku, na wengine
huwa hatuwaui ila
tu tunawachukua kwa ajili ya
kutufanyia kazi
ngumu za usiku,” Alijibu Kaguba.
“Tutawapataje hao watu
uliowaua?”
“Mnh…haiwezekani kuwatoa huko
labda ma’mdogo
Nyanzala tu nd’o bado hajakatwa
ulimi, ila naye
akikatwa hawezi tena kurudi
huku.”
Kimya kikapita.
“Haya nenda ukacheze.” Babu Gao
alimruhusu
Kaguba atoke nje, na alipotoka tu
Babu Gao
akawageukia wanafamilia na
kuwatupia swali.
“Mmeamini jamani? Mmemsikia
mwanenu
wenyewe?”
“Ndiyo Babu.”
“Basi hiyo nd’o hali halisi…mtoto
huyu ni hatari,
kila siku usiku kabla hajatoka
hutumia muda
mwingi yeye na wenziye
kuwachezeeni, hakika
huwasumbueni sana…” hakuna
aliyebishana na
Babu maana ni kweli mara nyingi
huamka wakiwa
hoi kama waliotoka shamba
kulima.
“…Nimemaliza kazi yangu, naomba
niondoke!”
“Tunashukuru sana kwa msaada
wako mkubwa
uliotupa…” alianza kuongea Mzee
Saadallah “…
lakini tunakuomba sana utusaidie
ili tulimalize
tatizo hili kivyovyote maana sasa
mbali ya
kumpoteza huyu mtoto pia
tunaweza hata
kuangamizwa na hao wachawi
ukoo mzima.”
“Wanyankole wana msemo wao
usemao ‘Omusote
oguli muntamu’ yaani ‘Nyoka
ndani ya mtungi wa
Udongo’wakiwa na maana kwamba
kumuua
unataka lakini hautaki kuharibu
mtungi wako wa
udongo…mnataka kuutoa uchawi
ndani ya nafsi ya
Kaguba, lakini hamtaki kumdhuru.
Jamani hili
jambo siyo dogo kama
mnavyodhani, wanaweza
kufa wengi hapa kama umakini na
hatua za
makusudi zisipochukuliwa. Na
hata kama
tutafanikiwa kuutoa uchawi huo
ndani yake bila
kumdhuru ila mkumbue wahenga
walinena
‘Chombo kilichopikiwa samaki,
hakiachi kunuka
uvumba’…” Alisema Babu Gao
akiwa na maana
kwamba hata kama watafanikiwa
kuutoa uchawi
ule ndani ya Kaguba,yawezekana
akabakia
nashombo ya uchawi huo. na
kumalizia. “…Mimi
kwa sasa sina msaada wowote
kwenu ila inabidi
niende kwanza kwangu nikaongee
na mizimu
yangu, sasa endapo kama itanipa
mbinu ya
kupambana na suala hili basi
tutawasiliana…kwa
leo nitawaachia dawa tu ambazo
mtaziweka
mlangoni, juu ya bati, na kwenye
pembe za
nyumba hii ili kumzuia mtoto huyu
asitoke usiku
kwenda kwa hao wafuasi wake ili
asije akawaeleza
mipango yetu, sawa?”
“Sawa babu, tunakusikiliza wewe
tu!”
Babu Gao akafungua tena kikapu
chake na kutoa
kibuyu kingine na vipande vya
magazeti ambavyo
alivitumia kufungia dawa fulani
nyeusi aliyoitoa
ndani ya vibuyu vyake,
akawafungia na
kuwakabidhi kisha baada ya
kuwapa maelekezo
akaondoka zake!
Wakazindika kila kona kama
walivyoelekezwa na
mganga kisha wakaendelea na
mambo mengine
kama kawaida.
***
Siku iliyofuata, tofauti na siku
zingine
wanafamiliawaliamka wakiwa na
nguvu na siha
njema.bila shaka dawa za Babu
Gao zilisaidia na
kuwafanya wasichezewe kichawi.
Shughuli za kila
siku zikaendelea kama kawaida
japo kwa simanzi,
hofu namashaka.
Sasa wakati mama Kaguba
akifagiafagia huku
wenziye wakiendea la mapishi
huko jikoni, ndipo
kikazuka kioja kingine cha mwaka.
SEHEMU YA NNE
“Mama…angalia hapo unapofagia,”
Kaguba
aliongea kwa kumtahadharisha
mama yake.
Kutokana na vimbwanga vya mtoto
yule, sasa
alikuwa si wa kupuuzwa kwa kila
anachotaka
kukisema.
“Kuna nini?” Alisaili mama Kaguba
huku akitupia
macho yake eneo hilo alilokuwa
akiliswafi.
“Hapo si nd’o mmechimbia ile
dawa mliyopewa na
yule Babu ili mnizuie nisitoke
usiku! Sasa ukifagia
vibaya utaifukua buree mwishowe
usiku nitatoka
tena.”
Heeh!
Yaani kumbe Kaguba alikwishajua
kuhusu dawa
zilizochimbiwa mahala pale kwa
siri kubwa? Tena
wakati babu Gao anatoa
maelekezo ya dawa ile
yeye alikuwa nje huko akicheza…
hii kali kuliko.
“We’ mtoto wewe! Nani
amekwambia kuwa kuna
dawa hapa?” Mama Kaguba
alimhoji mwanaye
huyo mtata, wakati huo na ndugu
kadhaa nao
wakisogea kusikiliza habari hiyo
mpya ya
kuchachafya ubongo.
“…halafu mama leo nasikia kichwa
kinaniuma
sana…jana wachawi wote walikuja
kunipitia lakini
wakashindwa kuingia ndani, na
mimi nikashindwa
kutoka kutokana na hiyo dawa
mliyoweka, sasa
wakawa wananiita kwa makelele
sana mpaka
nikashindwa kulala!” kabla
hajajibiwa akaendelea
mwenyewe “…unajua mi’ nd’o
mkubwa wao tangu
mlipomuua bibi maana
alishaganikabidhi vitunga
vyake vote vya uchawi. Mama mi’
mwenziyo ni
bosi we’ nidharau tuu.”
Majanga!
Mama Kaguba na nduguze
wakaangaliana kwa
kihoro. Kama ilivyo kwa mtoto
mwingine yeyote,
Kaguba alisimama na kutoka zake
nje kwenda
kucheza na wenzake bila ya kujali
athari ya
maneno yake aliyoacha
ameyabwata mbele ya
wazazi wake.
Hakuna kilichofanywa zaidi ya
kuendelea kuishi
kwa mashaka huku wakisubiri
kama Babu Gao
angerejea na mpya gani. Siku
kadhaa zikakatika
bila ya Babu Gao kurejea, japo
bilaya kupatwa na
mauzauza mengine yoyote kutoka
kwa Kaguba
wala kwa hayati Nyanzala.
***
“…mkuu tunaomba japo idhini
yako tu ili tumkate
kabisa ulimi Nyanzala maana
tunaona wazazi
wako wanaanza harakati za
kwenda kwa waganga,
sasa tusije tukamkosa,” Binti
Sambayu aliongea
kwa kumbembeleza Kaguba, akiwa
nje ya nyumba
baada ya kushindwa kuingia wala
kumtoa Kaguba
ndani kutoka na zindiko kali la
Babu Gao.
“Hapana, msimkate kabisa ulimi
ma’mdogo wangu
mpaka n’takapokuja mwenyewe,”
Alijibu Kaguba
kwa kutokea ndani. Ilikuwa ni
usiku wa manane,
Kaguba akiwa dirishani kwa ndani
ya chumba huku
Binti Sambayu akiwa kwa nje
wakijibizanana.
“Pia tulimfuata usiku wa jana huyo
Babu Gao ili
tumpe hongo yoyote atupe dawa
ya kuziua nguvu
zile ndumba alizozindika lakini
amekataa
katakata.”
“Achaneni naye…”
“Sasa hali hii itakuwa mpaka lini
mkuu?”
“Muda si mrefu nitawatoka tu
hawa na huyo Babu
Gao nitamuua kwa mkono
wangu…kuna kibuyu
chenye uchawi na dawa zote kali,
bibi alikichimbia
chini ya kitanda chake, sasa
nashindwa kukifukua
kwakuwa kuna watu bado
wanalala humo
chumbani mwake walipopafanya
kama ufuo. ila
nikikipata tu hakuna
atakayethubutu kunisogelea…”
Alisema Kaguba.
“Sasa mkuu, kama hao nduguzo
watakigundua
hicho kibuyu itakuaje?”
“Itakuwa hatari sana maana hicho
ndicho chenye
nguvu zote za uchawi wa bibi…
kama watakipata
na kukichoma moto au
kukidumbukiza chooni basi
tutateketea wachawi wote wa
kambi yetu ya
Kibondo. Ila ondoa shaka hakuna
atakayeweza
kukisogelea maana mtu wa
kawaida akikigusa kwa
mkono wake bila ya kukishika kwa
majani ya
Vibumbasi, atapigwa na kitu mithili
ya radi kali na
kufa hapohapo.”
“Sawa mkuu.”
“Watangazie wachawi wote kuwa
jumatano
nitatoka na nitakuja kusikiliza
shida za kila mtu,
nadhani msiba utamilizika siku ya
jumanne hivyo
mpaka kufikia jumatano nitakuwa
nimepata nafasi
ya kukichimbua hicho Kibuyu…ila
kwa sasa
msiruke umbali mrefu, muishie
mikoa ya jirani tu…
nawatakia uwangaji mwema.”
Pamoja na Kaguba
kumuaga binti Sambayu ila
maswali kadhaa
yaliwafanya waendelee na mjadala
wao.
Waliendelea na majibizano kwa
umakini wa hali ya
juu kwa kuhofia kusikika na mtu
wa kawaida
maana kama angetokea mtu akiwa
macho
angeweza kuwasikia kwa kuwa
kwa muda ule
iliwabidi wawasiliane kama watu
wa kawaida tu
kwakuwa haikuwa rahisi kwao
kuwasiliana kwa
mtindo wao wa kichawi kwani
nyumba ile ilikuwa
imezindikwa.
Walipomaliza mazungumzo
wakaagana.
Mtoto Kaguba na Binti Sambayu
wakaagana na
kuachana wakiwa na matumaini ya
kukamilisha
mpango wao. Siku hiyo ilikuwa ni
Alkhamisi hivyo
ingewagharimu siku kama sita ili
kukipata kibuyu
chao.
***ITAENDELEA***
“Swali zuri, sasa iko hivi endapo
mtoto huyo
ataukataa uchawi huo basi
hutokea tu hatokifunga
kiganja chake cha mkono baada
ya kuwekea dawa
na huyo mchawi…na hapo
utamuona huyo mchawi
akiwa amekasirika kabisa na
huenda hata
akaondoka na kumwacha mtoto
akiumwa ovyo tu.
Na endapo mtoto huyo ataukubali
uchawi huo,
basi atakapoachiwa tu mkono
wake baada ya
kukunjuliwa kiganja chake na
kuwekewa ile dawa
ya kichawi, hapohapo huukunja
mkono wake na
kuifumbata vizuri dawa ile ambayo
hupotelea
katikati ya kiganja chake…hivyo
ndivyo ilivyokuwa
kwa Kaguba alipozaliwa, baada ya
kuupokea
uchawi ule akawa ni miongoni
mwao hivyo
haikuwa taabu kwake kujifunza
vitu vya jamii yake
hiyo ya kichawi maana wahenga
walinena;Kifara
nga hakifunzwi kuchakura,”
Alinena kwa utuo Babu
Gao.
Wanafamilia wakaanagaliana,
hakuna aliyekuwa na
cha kubisha maana ni kweli
marehemu Bi
Masonganya alikuwa akipenda
sana kumtembelea
mtoto wake yeyote punde tu mara
baada ya
kujifungua, na hata yeye mama
Kaguba aishiye
wilayani Kasulu alipojifungua huyo
Kaguba wake, Bi
Masonganya aliwasili huko na
haraka aliwahi
kumbeba mtoto yule kama ilivyo
ada, hakuna
aliyemzuia wala kumshitukia. Bila
shaka hapo
ndipo alipopata fursa ya kutenda
huo ufedhuli
wake!
“Uchawi aliokabidhiwa huyu mtoto
wenu ni
mkubwa sana, hivi sasa yeye
ndiye kiongozi mkuu
wa wachawi wote wa ukanda huu
wa magharibi
licha ya umri wake huo mdogo…na
ameshauwa
watu wengi sana ambao hata
mkitajiwa
hamtoamini,na hata huyu
aliyefariki juzi naye
amemalizwa na mtoto wenu huyo
kwa maelekezo
au tuseme maombi aliypewa na
mmoja kati ya
watendaji wake wakubwa wa
kichawi. Ila angalizo
tu kwenu ni kwamba mtoto huyo
bado ni mdogo
sana asiyetambua lolote na
anayeongozwa na kiini
tu cha uchawi kilichomo ndani
yake sasa
mkimwendea vibaya kwanza
hatowajibu lolote
kwani kuna muda anakuwa na akili
za kitoto kama
walivyo watoto wengine na pia
zitakapomjia akili
zake za kichawi anaweza hata
kuwateketeza
nyumba nzima…” Babu Gao akiwa
anaendelea
kuongea, uzalendo ukamshinda
mama Kaguba na
kuanza kulia kwa uchungu na
fadhaa! Ikaanzaa
sasa kazi mpya ya kumbembeleza.
“Hebu mleteni hapa huyo mtoto,”
aliagiza Babu
Gao, na hapohapo akatoka mtu
mmoja mpaka uani
walipokuwa wakicheza watoto
wengi. Akamchukua
Kaguba na kurejea ndani.
Cha ajabu, Kaguba aliingia huku
akirukaruka ki-
mchezo kama wafanyavyo watoto,
ila alipoingia tu
mle sebuleni na kutupa macho
yake kwa mganga,
hapohapo akaanza kulia kwa hofu
huku
akitetemeka kwa woga.
“Unalia nini sasa wewe?” Mzee
Mtandi alimhoji
Kaguba wakati alipofikishwa pale
sebuleni.
“Namuogopa huyo…naomba
mnisamehe
msinipige.” Kila mtu alielewa kuwa
mtoto Kaguba
ni mchawi na nd’o maana
ameweza hata
kumtambua mganga. Babu Gao
hakuongea lolote,
akaingiza mkono kwenye kile
kikapu chake akatoa
kitu kama kibuyu hivi akiwa
amekizungushia
shanga za rangi za njano,
nyekundu na nyeusi…
“Nami’ ninacho sasa ukileta
mchezo nitakuua sasa
hivi hapa, haya tueleze ukweli
kwanini umemuua
ma’mdogo Nyanzala?” Babu Gao
alimfokea na
kumtisha Kaguba.
“Nisameheni Babu, mi’
nililazimishwa tu kumuua
kwakuwa yeye ndiye aliyemuua
Bibi!” Kaguba
alijibu huku akilia kwa sauti yenye
kitetemeshi cha
uoga.
“Ni kina nani hao
walokulazimisha?”
“Wale wachawi ninao waongozaga
usiku nd’o
waliniambia ni lazima tulipize
kisasi!”
“Umeshawaua watu wangapi?”
“awwwh..niii.. ni wengi tu!”
“Wataje haraka.”
“Dada Shumbana, mjomba
Makanya, kaka Ndugai,
mjomba Zumbe, ma’mdogo
Nyanzala na majirani”
Balaa!
Nyanzala, Makanya na Zumbe
wote ni watoto wa
marehemu Bi Masonganya, na
Shumbana pamoja
na Ndugai ni wajukuu waliofariki
kwa awamu
tofautitofauti katika mazingira ya
kutatanisha!
“Kwanini sasa huwa mnauwaua
wenzenu hivi?”
“Siye usiku huwa tunakula nyama
za watu,
kwahiyo ikifika zamu yetu ya
kutoa chakula nd’o
mimi na bibi tulikuwa tunamuua
mtu mmoja kwa
ajili ya kumla usiku, na wengine
huwa hatuwaui ila
tu tunawachukua kwa ajili ya
kutufanyia kazi
ngumu za usiku,” Alijibu Kaguba.
“Tutawapataje hao watu
uliowaua?”
“Mnh…haiwezekani kuwatoa huko
labda ma’mdogo
Nyanzala tu nd’o bado hajakatwa
ulimi, ila naye
akikatwa hawezi tena kurudi
huku.”
Kimya kikapita.
“Haya nenda ukacheze.” Babu Gao
alimruhusu
Kaguba atoke nje, na alipotoka tu
Babu Gao
akawageukia wanafamilia na
kuwatupia swali.
“Mmeamini jamani? Mmemsikia
mwanenu
wenyewe?”
“Ndiyo Babu.”
“Basi hiyo nd’o hali halisi…mtoto
huyu ni hatari,
kila siku usiku kabla hajatoka
hutumia muda
mwingi yeye na wenziye
kuwachezeeni, hakika
huwasumbueni sana…” hakuna
aliyebishana na
Babu maana ni kweli mara nyingi
huamka wakiwa
hoi kama waliotoka shamba
kulima.
“…Nimemaliza kazi yangu, naomba
niondoke!”
“Tunashukuru sana kwa msaada
wako mkubwa
uliotupa…” alianza kuongea Mzee
Saadallah “…
lakini tunakuomba sana utusaidie
ili tulimalize
tatizo hili kivyovyote maana sasa
mbali ya
kumpoteza huyu mtoto pia
tunaweza hata
kuangamizwa na hao wachawi
ukoo mzima.”
“Wanyankole wana msemo wao
usemao ‘Omusote
oguli muntamu’ yaani ‘Nyoka
ndani ya mtungi wa
Udongo’wakiwa na maana kwamba
kumuua
unataka lakini hautaki kuharibu
mtungi wako wa
udongo…mnataka kuutoa uchawi
ndani ya nafsi ya
Kaguba, lakini hamtaki kumdhuru.
Jamani hili
jambo siyo dogo kama
mnavyodhani, wanaweza
kufa wengi hapa kama umakini na
hatua za
makusudi zisipochukuliwa. Na
hata kama
tutafanikiwa kuutoa uchawi huo
ndani yake bila
kumdhuru ila mkumbue wahenga
walinena
‘Chombo kilichopikiwa samaki,
hakiachi kunuka
uvumba’…” Alisema Babu Gao
akiwa na maana
kwamba hata kama watafanikiwa
kuutoa uchawi
ule ndani ya Kaguba,yawezekana
akabakia
nashombo ya uchawi huo. na
kumalizia. “…Mimi
kwa sasa sina msaada wowote
kwenu ila inabidi
niende kwanza kwangu nikaongee
na mizimu
yangu, sasa endapo kama itanipa
mbinu ya
kupambana na suala hili basi
tutawasiliana…kwa
leo nitawaachia dawa tu ambazo
mtaziweka
mlangoni, juu ya bati, na kwenye
pembe za
nyumba hii ili kumzuia mtoto huyu
asitoke usiku
kwenda kwa hao wafuasi wake ili
asije akawaeleza
mipango yetu, sawa?”
“Sawa babu, tunakusikiliza wewe
tu!”
Babu Gao akafungua tena kikapu
chake na kutoa
kibuyu kingine na vipande vya
magazeti ambavyo
alivitumia kufungia dawa fulani
nyeusi aliyoitoa
ndani ya vibuyu vyake,
akawafungia na
kuwakabidhi kisha baada ya
kuwapa maelekezo
akaondoka zake!
Wakazindika kila kona kama
walivyoelekezwa na
mganga kisha wakaendelea na
mambo mengine
kama kawaida.
***
Siku iliyofuata, tofauti na siku
zingine
wanafamiliawaliamka wakiwa na
nguvu na siha
njema.bila shaka dawa za Babu
Gao zilisaidia na
kuwafanya wasichezewe kichawi.
Shughuli za kila
siku zikaendelea kama kawaida
japo kwa simanzi,
hofu namashaka.
Sasa wakati mama Kaguba
akifagiafagia huku
wenziye wakiendea la mapishi
huko jikoni, ndipo
kikazuka kioja kingine cha mwaka.
SEHEMU YA NNE
“Mama…angalia hapo unapofagia,”
Kaguba
aliongea kwa kumtahadharisha
mama yake.
Kutokana na vimbwanga vya mtoto
yule, sasa
alikuwa si wa kupuuzwa kwa kila
anachotaka
kukisema.
“Kuna nini?” Alisaili mama Kaguba
huku akitupia
macho yake eneo hilo alilokuwa
akiliswafi.
“Hapo si nd’o mmechimbia ile
dawa mliyopewa na
yule Babu ili mnizuie nisitoke
usiku! Sasa ukifagia
vibaya utaifukua buree mwishowe
usiku nitatoka
tena.”
Heeh!
Yaani kumbe Kaguba alikwishajua
kuhusu dawa
zilizochimbiwa mahala pale kwa
siri kubwa? Tena
wakati babu Gao anatoa
maelekezo ya dawa ile
yeye alikuwa nje huko akicheza…
hii kali kuliko.
“We’ mtoto wewe! Nani
amekwambia kuwa kuna
dawa hapa?” Mama Kaguba
alimhoji mwanaye
huyo mtata, wakati huo na ndugu
kadhaa nao
wakisogea kusikiliza habari hiyo
mpya ya
kuchachafya ubongo.
“…halafu mama leo nasikia kichwa
kinaniuma
sana…jana wachawi wote walikuja
kunipitia lakini
wakashindwa kuingia ndani, na
mimi nikashindwa
kutoka kutokana na hiyo dawa
mliyoweka, sasa
wakawa wananiita kwa makelele
sana mpaka
nikashindwa kulala!” kabla
hajajibiwa akaendelea
mwenyewe “…unajua mi’ nd’o
mkubwa wao tangu
mlipomuua bibi maana
alishaganikabidhi vitunga
vyake vote vya uchawi. Mama mi’
mwenziyo ni
bosi we’ nidharau tuu.”
Majanga!
Mama Kaguba na nduguze
wakaangaliana kwa
kihoro. Kama ilivyo kwa mtoto
mwingine yeyote,
Kaguba alisimama na kutoka zake
nje kwenda
kucheza na wenzake bila ya kujali
athari ya
maneno yake aliyoacha
ameyabwata mbele ya
wazazi wake.
Hakuna kilichofanywa zaidi ya
kuendelea kuishi
kwa mashaka huku wakisubiri
kama Babu Gao
angerejea na mpya gani. Siku
kadhaa zikakatika
bila ya Babu Gao kurejea, japo
bilaya kupatwa na
mauzauza mengine yoyote kutoka
kwa Kaguba
wala kwa hayati Nyanzala.
***
“…mkuu tunaomba japo idhini
yako tu ili tumkate
kabisa ulimi Nyanzala maana
tunaona wazazi
wako wanaanza harakati za
kwenda kwa waganga,
sasa tusije tukamkosa,” Binti
Sambayu aliongea
kwa kumbembeleza Kaguba, akiwa
nje ya nyumba
baada ya kushindwa kuingia wala
kumtoa Kaguba
ndani kutoka na zindiko kali la
Babu Gao.
“Hapana, msimkate kabisa ulimi
ma’mdogo wangu
mpaka n’takapokuja mwenyewe,”
Alijibu Kaguba
kwa kutokea ndani. Ilikuwa ni
usiku wa manane,
Kaguba akiwa dirishani kwa ndani
ya chumba huku
Binti Sambayu akiwa kwa nje
wakijibizanana.
“Pia tulimfuata usiku wa jana huyo
Babu Gao ili
tumpe hongo yoyote atupe dawa
ya kuziua nguvu
zile ndumba alizozindika lakini
amekataa
katakata.”
“Achaneni naye…”
“Sasa hali hii itakuwa mpaka lini
mkuu?”
“Muda si mrefu nitawatoka tu
hawa na huyo Babu
Gao nitamuua kwa mkono
wangu…kuna kibuyu
chenye uchawi na dawa zote kali,
bibi alikichimbia
chini ya kitanda chake, sasa
nashindwa kukifukua
kwakuwa kuna watu bado
wanalala humo
chumbani mwake walipopafanya
kama ufuo. ila
nikikipata tu hakuna
atakayethubutu kunisogelea…”
Alisema Kaguba.
“Sasa mkuu, kama hao nduguzo
watakigundua
hicho kibuyu itakuaje?”
“Itakuwa hatari sana maana hicho
ndicho chenye
nguvu zote za uchawi wa bibi…
kama watakipata
na kukichoma moto au
kukidumbukiza chooni basi
tutateketea wachawi wote wa
kambi yetu ya
Kibondo. Ila ondoa shaka hakuna
atakayeweza
kukisogelea maana mtu wa
kawaida akikigusa kwa
mkono wake bila ya kukishika kwa
majani ya
Vibumbasi, atapigwa na kitu mithili
ya radi kali na
kufa hapohapo.”
“Sawa mkuu.”
“Watangazie wachawi wote kuwa
jumatano
nitatoka na nitakuja kusikiliza
shida za kila mtu,
nadhani msiba utamilizika siku ya
jumanne hivyo
mpaka kufikia jumatano nitakuwa
nimepata nafasi
ya kukichimbua hicho Kibuyu…ila
kwa sasa
msiruke umbali mrefu, muishie
mikoa ya jirani tu…
nawatakia uwangaji mwema.”
Pamoja na Kaguba
kumuaga binti Sambayu ila
maswali kadhaa
yaliwafanya waendelee na mjadala
wao.
Waliendelea na majibizano kwa
umakini wa hali ya
juu kwa kuhofia kusikika na mtu
wa kawaida
maana kama angetokea mtu akiwa
macho
angeweza kuwasikia kwa kuwa
kwa muda ule
iliwabidi wawasiliane kama watu
wa kawaida tu
kwakuwa haikuwa rahisi kwao
kuwasiliana kwa
mtindo wao wa kichawi kwani
nyumba ile ilikuwa
imezindikwa.
Walipomaliza mazungumzo
wakaagana.
Mtoto Kaguba na Binti Sambayu
wakaagana na
kuachana wakiwa na matumaini ya
kukamilisha
mpango wao. Siku hiyo ilikuwa ni
Alkhamisi hivyo
ingewagharimu siku kama sita ili
kukipata kibuyu
chao.
***ITAENDELEA***