Post by Admin on May 31, 2015 21:22:27 GMT
“Watangazie wachawi wote kuwa
jumatano
nitatoka na nitakuja kusikiliza
shida za kila mtu,
nadhani msiba utamilizika siku ya
jumanne hivyo
mpaka kufikia jumatano nitakuwa
nimepata nafasi
ya kukichimbua hicho Kibuyu…ila
kwa sasa
msiruke umbali mrefu, muishie
mikoa ya jirani tu…
nawatakia uwangaji mwema.”
Pamoja na Kaguba
kumuaga binti Sambayu ila
maswali kadhaa
yaliwafanya waendelee na mjadala
wao.
Waliendelea na majibizano kwa
umakini wa hali ya
juu kwa kuhofia kusikika na mtu
wa kawaida
maana kama angetokea mtu akiwa
macho
angeweza kuwasikia kwa kuwa
kwa muda ule
iliwabidi wawasiliane kama watu
wa kawaida tu
kwakuwa haikuwa rahisi kwao
kuwasiliana kwa
mtindo wao wa kichawi kwani
nyumba ile ilikuwa
imezindikwa.
Walipomaliza mazungumzo
wakaagana.
Mtoto Kaguba na Binti Sambayu
wakaagana na
kuachana wakiwa na matumaini ya
kukamilisha
mpango wao. Siku hiyo ilikuwa ni
Alkhamisi hivyo
ingewagharimu siku kama sita ili
kukipata kibuyu
chao.
***
Kulipopambazuka kila mmoja
aliamka na kuanza
kutekeleza majukumu ya kila siku,
wapo
waliokwenda kuchota maji, wapo
waliokuwa
wakipika huku wengine
wakisafisha nyumba na
wengine wakiwa wameketi tu
sebuleni. Watoto nao,
pamoja na Kaguba waliendelea na
majukumu yao
ya kucheza!
Mzee Mtandi alikuwa chumbani
kwake akiwa
amemakinika na kijitabu chake
kidogo ambacho
hupendelea sana kuandikia
kumbukumbu zake za
kila siku. Alikuwa akisoma hikina
kuandika kile,
alimuradi alijishughulisha na
alichokijua
mwenyewe. Alipoona amemaliza,
akakirejesha
kitabu chake kwenye mfuko wa
begi lake la nguo
na kutoka mle chumbani mpaka
uani.
“Jamani mi’ n’natoka kidogo kuna
pahala
ninakwenda mara moja, nitarejea
baadaye!” Mzee
Mtandi aliwaaga wapwa zake.
“Mjomba si’ ungesubiri stiftahi
kwanza?” alijibu
kwa kusaili Kungurume.
“Hapana, mtaniachia tu nikirudi
nitakula ninashida
na bwana mmoja hivi maeneo ya
stendi huko.”
Baada ya mazungumzo ya hapa na
pale Mzee
Mtandi akadandia baiskeli yake
mkangafu na
kuondoka. Hakwenda stendi kama
alivyodai, ila
kuna sehemu alikuwa ana shida
kubwa sana, shida
ambayo usiku kucha aliumaliza
akiifikiria.
Alipotimiza shida yake akapitia
kwenye mihangaiko
ya hapa na pale kisha akarejea
nyumbani ambapo
kabla ya kuingiza chochote
kinywani akaitisha
kikao cha familia nzima nzima.
Wote wakajumuika sebuleni.
“Nimekuiteni hapa wanangu, kuna
mambo mazito
kidogo nataka kukuelezeni…
naomba muwe na
staha na na utulivu wa hali ya
juu…” Alianza
kuongea Mzee Mtandi baada ya
kufungua na
kutuliza baraza. “…Kuna jambo
zito nimelivumbua,
jambo ambalo kama tutachelewa
kufanya ma’arifa
basi matokeo ya uvumbuzi wangu
wa hatari ni vifo
vyetu wenyewe, tutapitiana hapa
na kufa kama
wagonjwa wa kipindupindu.”
Kimya kilitanda huku kila mmoja
akisikiliza kwa
makini, Mzee Mtandi
akaendelea.“…Siku zote hizi
ninyi mkiwa mmelala, mi’ huwa
naamka usiku na
kujaribu kuchunguza mwenendo
wa mjukuu wangu
Kagubamaana kwa sasa hakuna
asiyejua u-hatari
wake. Yapo mengi huwa
nayang’amua ila hili
nililoling’amua usiku wa kuamkia
leo ni kubwa na
la hatari zaidi…ni kweli kama
alivyosema
mwenyewe kuwa dawa za Babu
Gao zinamzuia
kukutana na wachawi wenziye, hilo
nimeligundua
baada ya kumshuhudia kwa jicho
langu akiongea
na Binti Sambayu kupitia dirishani,
na nimegundua
hila nzito walizozipanga ili
kutuangamiza sisi sote,
na hakika tusipokuwa makini
tutakufa sote hapa
na kwenda kutumikishwa huko
kwenye ulimwengu
usioonekana kama misukule.”
Vinyweleo
viliwatutumka kwa hofu
wanafamilia wale
waliokuwa kama kondoo
anayesubiri kuvamiwa na
chui akiwa hana msaada.
Wakati wanaongea walihakikisha
hakuna mtu
mwingine yeyote tofauti na wao tu
kama
walengwa wakuu, hata watoto wao
wadogo wa
rika la Kaguba hawakuruhusiwa
kuingia ndani.
Kama palikuwa na kiumbe
chochote
kinachoonekana basi labda ni yule
paka wao
wanayemfuga aliyekuwa amejilalia
zake juu ya
kochi. Na hata alipoona maongezi
yale yakiendelea,
Paka alijitokea zake nje.
“…Bahati nzuri ni kwamba mbali
ya mipango yao
ya kutudhuru, pia nimepata mbinu
kali ya
kuwaangamiza wote
wanaojihusisha na uchawi
kutoka katikamazungumzo yao
wenyewe…”
Aliendelea kuogea Mzee Mtandi
kiasi cha kuzidi
kuwamakinisha wanafamilia wote.
“…
Nilipowaambia nakwenda mara
moja stendi,
haikuwa hivyo. Nilikwenda kwa Bi
mkubwa mmoja
hivi kumuulizia juu ya wapi nitapa
majani
yanayoitwa vibumbasi maana hiyo
ni moja ya
kinga tutakayoitumia wakati wa
kuishika silaha kuu
ya maangamizi na kuumaliza huu
udhia
unaotutesa.”
Ni kweli mzee Mtandi aliushuhudia
mchezo mzima
kati ya Kaguba na binti Sambayu.
Sasa wakati
anaanza kuwapa habari ilivyokuwa
wakati
wakiwasiliana ndipo kikaibuka
kitimtim kipya.
Walishangaa tu kuona ghafla mzee
Mtandi
akinyamaza kimya kama
aliyezimwa kwa rimoti.
Na hapohapo akaonekana
kuishiwa nguvu, mara
akaanguka chini ‘PAAA’ macho
yakamtoka, povu
likimfumka mdomoni. Taharuki
ikawavaa
wanafamilia, ikawa ni
mshikemshike mpya.
Hakuna mtoto mdogo pale mpaka
asielewe
kilichotokea kuwa ni tukio la
kivamizi la kishirikina
lililoazimia kumzuia Mzee Mtandi
asitoe siri
aliyokuwa nayo, na hata ikibidi afe
nayo kifuani.
Watoto hawakukubali kumpoteza
mjomba wao
pamoja na siri yake kubwa yenye
lengo la kuwafaa
wote. Haraka teksi ikaendewa na
baada ya
makubaliano safari ya kuelekea
kwa Babu Gao
ikaanza. Pamoja na Mzee Mtandi
mwenyewe,
ndani ya teksi ukitoa dereva
aliingia pia Mama
Kaguba na Kungurume.
Wakati wanaondoka, yule paka
wao wa kufugwa
aliyetoka wakati walipokuwa
wakiendelea na mazungumzo yao
alirejea na kuketi palepale kwenye
kochi.
***
Safari ilikuwa mbaya na ya
matumaini tu maana
kila baada ya hatua kadhaa gari
iliwaharibikia, kila
dereva alipojaribu kutengeneza na
kuendelea na
safari walitembea umbali mfupi tu
kabla ya
kuharibikiwa tena. Wakati huo hali
ya Mzee Mtandi
ikizidi kuwa mbaya, hakuwa na
fahamu kabisa
hivyo alikuwa amebebwa tu kama
mzigo.
Safari iliendelea hivyohivyo
kimungumungu tu
mpaka walipofika katika moja ya
mapori kadhaa
ambapo ilikuwa wakilimaliza pori
lile tu
wangewasili nyumbani kwa Babu
Gao, ndipo
kilipoibuka Kimbunga kikali
kilichoishambulia ile
teksi mpaka ikazima.
Baada ya kimbunga kumalizika na
upepo kutulia
ndipo dereva akateremka ili
kutengeneza gari
yake,hilo likawa kosa kubwa!
SEHEMU YA TANO
Ilikuwa kama maigizo tu, mbele ya
macho ya
Kungurume na mama Kaguba pale
waliposhuhudia
dereva wao akiyeyuka na kupotea
punde tu mara
baada ya kuteremka garini.
Wakahaha na kuanza
kupiga makelele ya kutaka msaada
lakini hakuna
aliyewasikia. Ukimya uliendelea
kutuama eneo lile
laporini. Walipiga kelele mpaka
wenyewe wakatulia,
hakuna aliyetokea kuwahami.
Labda simu zao
zingewasaidia ili wawasiliane na
ndugu huko mjini
kama kungekuwa na mtandao
katika pori lile,
haikuwa hivyo!
Walikaa pale wakiwa ndani ya
teksi mbovu huku
dereva akiwa ametoweka kimiujiza
huku hali ya
mjomba wao ikizidi kudorora.
Ndipo baada ya
muda fulani ikatokea gari aina ya
Landrover.
Haraka Kungurume akajivisha
ujasiri maana yeye
nd’o mwanaume aliyebaki,
akateremka ndani ya
gari na kulipiga mkono gari lile
lililokuwa likipita
akidhamiria kuomba msaada. Cha
ajabu gari ile
iliwapita kama nyumba
inayoungua moto. Hakujua
ni nini hasa kilichopelekea hali ile
ya kutelekezwa
na gari ile.
Labda hawakumuona! Labda
walimuogopa
wakidhani ni mtego wa
majambazi, au nd’o hila za
akina Kaguba na Binti Sambayu.
Hakuna jibu
sahihi!Kungurume akabaki
amejishika kiunoni kwa
mikono yake iliyojazia huku
macho yake yakitalii
mazingira ya kijani kibichi
yaliyotawala pori lile.
Akarudi ndani ya gari huku
akitweta, akiwa
amepoteza kabisa matumaini.
“Mwenzangu, hali ngumu,”
Alisema Kungurume
akimwambiadada yake.
“Kivipi?”
“Kuna mawili tu yanayoonekana
hapa…tutampotez
a mjomba hapahapa mikononi
mwetu au
tutaangamia pamoja naye…”
“Mbona unanitisha kaka?” Kabla
Kungurume
hajajibu, ndipo ikaibuka tena gari
nyingine aina ya
Landcruiser. Haraka Kungurume
akateremka ili
kujaribu tena bahati. Akapunga
mkono wake ikiwa
ni ishara ya kuomba msaada.
Bahati ikawa yake,
gari ile ikasimama.
“Habari zenu wakuu?” Alisalimu
Kungurume.
“Nzuri, vipi kuna shida gani?”
Dereva wa gari ile
alijibu akiwa ndani ya gari yake
bila hata ya
kuteremka.
“Jamani tumepata matatizo, tuna
mgonjwa ndani
ya teksi yetu na tumeharibikiwa
hapa…hali ya
mgonjwa inazidi kuwa mbaya tu
tunaomba
msaada wenu tafadhali.
“Gari imeharibika kitu gani?”
“Kwakweli hata sijui
kilichoharibika.” Jibu hili
likamfanya dereva wa ile
Landcruiser aangaliane na
mtu aliyembeba.
“Dereva wa teksi hiyo yuko wapi?”
Swali hili sasa
kutoka kwa mtu aliyebebwa
kwenye ile Landcruiser
lilimfanya Kungurume ajigonge
asijue cha kujibu,
maana kama ataeleza ukweli kuwa
ametoweka
katika mazingira ya kutatanisha,
hakika asingepata
msaada kwani asingeaminika
kabisa na hata kama
angeaminika basi angekuwa
amekwishawatisha
sana watu hao. Baada ya fikra fupi
alijibu.
“Dereva baada ya kujitahidi
kutengeneza gari bila
mafanikio ndipo akapata lifti ya
kwenda mjini
kuendea sijui kifaa gani huko…
sasa sisi tuna
mgonjwa hatuwezi kuendelea
kukaa hapa wakati
hali ya mgonjwa ni mbaya na
amepoteza fahamu.”
Alidanganya Kungurume akichelea
kupoteza
msaada.
“Sasa huku mnampeleka wapi
mgonjwa wenu?
Kuna hospitali kweli huku?” alisaili
dereva.
“Huku tunampeleka kwa mganga
wa kienyeji.” Jibu
hilo pia likawafanya mtu na dereva
wake
waangaliane na kutikisa vichwa.
“Yaani kaka mbona unaoekana
kama ni msomi hivi
halafu unadriki kuamini mambo
haya ya
kishirikina?” Alihoji dereva.
“Kaka, Kitanda usichokilalia
huwajui Kunguni
wake…Laiti mngejua masaibu
tunayopitia mpaka
tumesalimu amri na kuja huku bila
shaka
mngetuonea huruma…imebidi
tufanye hivi tu.”
“Okay iko hivi kaka sisi hatuwezi
kuwapeleka huko
kwa mganga kwakuwa tuna
mambo ya muhimu
tunawahi mjini…sasa msaada
pekee tunaoweza
kukupeni ni kuwapakia kwenye
gari yetu na kurejea
nanyi mjini na tutukwenda
kuwaacha hospitalikama
hamtojali…Upo hapo?”
Duuh!
Haikuwa lengo kabisa, Kungurume
akashusha
pumzi nzito ya kushindwa kabisa.
Akawaomba
mabwana wale wamsubiri asogee
upande wapili
ilipo teksi akaongee nadada yake
amweleze kuhusu
msada huo wa kurejea mjini.
Wakamkubalia.
Baada ya Kungurume kuifikia teksi
yao na kuongea
na dada yake, wakashuka ndani ya
teksi na
kuisogelea ile Landcruiser. Baada
ya mama Kaguba
kusalimiana na watu wale, alijaribu
kuwasihi na
kuwabembeleza ili tu wawapeleke
huko kwa Babu
ambapo hapakuwa mbali
kutokeahapo walipo…na
ikibidi hata kwa kuwalipa. Mjadala
ukaanza upya
huku jamaa wakiwa na msimamo
wao uleule lakini
kama ilivyo falsafa ya hayati Albert
Mangwea
kwamba ‘Mwanaume kwa
mwanamke, ni sawa na
mfupa kwa fisi’ Dereva na patna
wake wakasalimu
amri, wakageuza gari na
kuisogeza usawa wa
teksi. Wakateremka na kusaidiana
kumbeba Mzee
Mtandi na kumpakia ndani ya gari
yao.
Wakaingia wote ndani ya gari
baada ya
kuhakikisha ile teksi wameifunga
vizuri. Dereva
akalitia moto gari, likawaka. Lakini
kila alipoigiza
gia ili waondoke gari iligoma
kuondoka. Hila za
kifundi zilimwisha dereva yule bila
ya mafaniko.
Gari iligoma kabisa kuondoka na
baada ya
purukushani ikazima kabisa.
Balaa!
Wakashuka wote na dereva akalala
chini ya
uvunguwagari kuangalia hitilifu,
lakini hakuliona
tatizo. Akaingia tena ndani ya gari
peke yake huku
wengine wakimsubiri nje wakati
akijaribu
kuendesha. Alipojaribu kuliwasha
likawaka.
Alipoliingizia gia likakubali na
kuondoka, wote
wakafurahi. Baada ya gari
kusimama
wakalisogelea na kuingia ndani ya
gari kwa ajili ya
safari.
Walipoingia tu, mchezo ukawa
uleule gari likatia
mgomo tena. Ndipo dereva
akageuka mbogo
baada ya kugundua kuwa watu
hawa hawakuwa
wa kawaida. Akawateremsha
pamoja na mgonjwa
wao licha ya maombi ya huruma
kutoka kwao.
Alipowateremsha tu gari likakubali
tena,
akaliwasha na kulitia
gia..akawachia vumbi tu.
Mama Kaguba alilia kwa uchungu,
japo haikufaa
kitu. Wakarejea kwenye teksi yao
na kusubiri
kadari ya Mungu tu iwakute
maana hawakuwa na
namna nyingine.
***ITAENDELEA***