Post by Admin on May 31, 2015 21:29:05 GMT
Baada ya kukamilisha zoezi hilo,
Kungurume
akamlipa dereva teksi na
kumwacha aende zake
kwani kwa mujibu wa mganga,
wao walipaswa
kulala palepale. Kuwafahamisha
nyumbani kwao
haikuwa tabu kwani tangu
walipofika kwa Babu
hapo mtandao ulikuwa ukifanya
kazi.
******
Babu Gao akarejea katika ule
ukarimu wake wa
kawaida na wa kila siku.
Akawakirimu chakula
wageni wake, akawapa maji ya
kuoga huku yeye
akazianza sarakasi zake za
kumtibu mzee Mtandi
aliyekuwa hajarejewa na fahamu
muda wote ule.
Tiba ilikuwa kubwa na ngumu
sana, ilichukuwa
muda mrefu mpaka giza la usiku
likaingia, na hapo
Babu Gao akawaandalia wageni
wake sehemu ya
kulala. Walipolala, yeye
akaendelea na patashika
yake.
***
“Jamani kazi ni ngumu sana kama
nilivyokuambien
i tangu jana…” Babu Gao
aliwaambia akina mama
Kaguba baada ya kumka asubuhi.
“…Huyu bwana
kuna siri kubwa sana aliigundua
kuhusiana na hao
wachawi wenu, bahati mbaya
alipokuwa
akiwaelezeni ninyi hakujua kuwa
nyumba ile si
salama kujadili vitu hatari kama
vile…mle ndani
kuna wachawi kila kona…”
“Lakini Babu wakati mjomba
anatuhadithia habari
hiyo mpaka ikamkuta hali hii,
tulikuwa tumewatoa
nje watu wote wasiohusika.”
Mama Kaguba
alidakia.
“Una uhakika gani kuwa kati yenu
mliokuwa pale
sebuleni hakuna mchawi? Kwani
ninyi mlitegemea
kuwa yule mtoto mdogo Kaguba
angeweza kuwa
mchawi?” alisaili kwa umakini
Babu Gao.
“Mnh! Kwahiyo kuna mtu kati yetu
kule nyumbani
ni mchawi?” Alihoji kungurume.
“Sina maana hiyo, nilitaka tu
kukuonesheni kuwa
hamko makini na jambo hili
kwakuwa hamuujui
uchawi ninyi…iko hivi sasa, siku
ile mlipokuwa
mnaongea mambo haya mle ndani
palikuwa na
Paka amejilaza kwenye kiti, basi
yule hakua Paka
asilani!”
“Ama!” Alimaka Kungurume huku
akivuta
kumbukumbu ya siku ile.
“Alikuwa ni mwanaadamu yule
aliyejibadili na kuwa
kama Paka japo miaka yote
mmekuwa mkiamini
kuwa ni Paka wa kufugwa ila
hayati Masonganya
alikuwa akimtamua kama
mtumishi wake, na muda
mrefu huwa anawafatilia mambo
yenu. Sasa
aliposikia habari ile mbaya
akatoka nje na kwenda
kumpa taarifa Kaguba aliyekuwa
akicheza nje na
wenziwe’ Kaguba naye haraka
akawasilisha taarifa
ile kwa Binti Sambayu kwa njia
wazijuazo wenyewe
ndipo likatumwa pigo lile
lilomfanya mjomba wenu
awe hivi…ila tutajitahidi sana
kuhakikisha
anapona.”
“Tutashukuru sana Babu.”
“Vizuri!”
“Unajua nini Babu…” Kungurume
alianza kuongea
huku akitembeza macho yake
katika chumba kile
cha uganga. “…sisi hata hatukujua
ni kipi hicho
ambacho mjomba alikigundua
toka kwa hao
wachawi kwani alipofikia tu
kwenye pointi hiyo
nd’o akaanguka, sasa we’
unaweza kututajia hicho
alichokigundua?” Swali hilo
likamfanya Babu Gao
apikiche viganja vya mikono yake
na kisha
kuifumbata mikono yake kifuani.
Kimya kikatawala.
“Siwezi kusema uongo kabisa
katika hili, ni
kwamba sijabahatika kukijua hicho
kitu. Hata haya
machache niliyowahabarisha
nimeyapata kwa
ufundi wangu wa hali ya juu,
niliingia kichwani
mwa mjomba wenu na kuanza
kuzisoma fikra zake
lakini habari niliyoipata ni ile kama
mliyokuwa nayo
ninyi, yaani niliishia palepale
alipoanguka tu.
Nadhani leo atazinduka na
tutakwenda kufanya
kafara kubwa makaburini ambapo
tukimaliza
atatuhabarisha yeye mwenyewe.
***
Asubuhi yote, na mchana kutwa
Babu Gao alikuwa
akishughulika na jambo lile zito
mpaka kwenye saa
kumi alasiri ndipo mzee Mtandi
akarejewa na
fahamu. Ilikuwa ni kazi nzito, kazi
ya kutibu huku
akipambana na nguvu za wachawi
zilizokuwa
zikimshambulia mara kwa mara
kiasi cha
kumvurugia kabisa kazi yake.
Baada ya Mzee
Mtandi kuzinduka akaachwa
apumzike, kisha
baadaye akapewa chakula na
kupelekwa kuoga
akiwa amebebwa. Afya yake
haikuwa mbaya sana
japo tatizo kubwa alilokuwa nalo
ni kutoweza
kutembea mwenyewe pamoja na
kupoteza
kumbukumbu…hakuwa na
kumbukumbu zozote za
kulichotokea. Hilo Babu Gayo
alilitarajia.
Saa moja magharib msafara wa
kwenda
makaburini ukaanza. Kungurume,
Mama Kaguba,
Babu Gao na Kanumba wake
wakiwa wamembeba
mzee Mtandi wakaongozana
kuelekea makaburini
ambapo zindiko kubwa liliratibiwa
kufanyika.
“Tukifika makaburini
hatutoruhusiwa kuongea
chochote labda kama
nitawaelekeza kufanya
hivyo,. Sawa?” Aliunguruma Babu
Gao.
“Ndiyo!” “…Tawire.” Walijibu.
“Kuna kazi ndogo tu kama ya
dakika kumi hivi
tutaifanyia juu ya kaburi. Tukifika
we’ bwana
Mtandi tutakuwekea kigoda juu ya
Kaburi kisha
utaketi, tutakupa kinu
kitakachokuwa na dawa
ndani yake, utakishikilia kwa
mikono yako miwili
halafu mimi nitatwanga dawa
itakayokuwa humo
kwenye kinu…” Walikuwa
wakimsikiliza kwa kina
Babu Gao akitoa maelekezo
maana walijua
wakifika huko makaburini
hawatopata nafasi ya
kuongea kama walivyopewa
hadhari mapema.
“…Nikishamaliza kutwanga tu
dawa utainuka na
kutoka hapo kaburini kisha dawa
hiyo
tutaichanganya kwenye kinu na
sote tutaioga na
kuinywa. Hapo tutakuwa
tumemaliza kazi yetu.”
Alihitimisha Babu Gao na
kuruhusu maswali kwa
ambaye hajaelewa, hapakuwa na
swali.
Wakatembea mpaka wakawasili
katika viwanja vya
makaburi. Japo alikuwa
amebebwa, mzee Mtandi
alisikia na kuelewa maelekezo yote
yaliyotolewa na
Babu Gao.
Viwanja vya makaburi vilikuwa
kimya kabisa,
upepo ukiiyumbisha miti kadhaa
iliyopandwa kwa
kulizunguka eneo hilo kiasi cha
kuyaangusha
majani dhaifu yaliyolegea. Wakati
huo giza
lilikwishaanza kutanda na kufanya
eneo hili la
makaburini kutisha haswa!
Wakaingia na kwenda mpaka
katikati ya makaburi,
Babu Gao akachagua kaburi moja
lilionesha kuwa
si la muda mrefu sana tangu
lihifadhi mtu ndani
yake. Haraka Kanumba wa Babu
akaweka kigoda
juu ya Kaburi hilo sambamba na
Kinu chenye dawa
kisha akarudi hatua moja nyuma.
Babu Gao
akasaidiana na Kungurume
kumnyanyua mzee
Mtandi na kumkalisha juu ya
kigoda kile juu ya
kaburi. Baada ya kuketi, mzee
Mtandi akakishika
kinu kwa mikono yake miwili na
hapohapo Babu
Gao akiwa amesimama kwa karibu
japo yeye
hakupanda juu ya kaburi, akainua
juu mchi wake
wa kutwangia na kuanza kuongea
maneno yake ya
kiganga. Wakati huo Mama
Kaguba, Kungurume,
na yule Kanumba walikuwa
wamesimama kwa
kulizunguka kaburi.
Baada ya Babu kumaliza kuongea
tu maneno yake,
akaanza kutwanga dawa iliyomo
ndani ya kinu
kilichoshikiliwa na mzee Mtandi
huku akiimba
nyimbo kwa lugha ya kiha.
Ghafla wakati Babu Gao akitwanga
dawa ile
kikaibuka kizaazaa kilichowafanya
wote wataharuki
mpaka Babu Gao mwenyewe.
Ilikuwa ni wakati Babu Gao
akitwanga ile dawa,
ndipo Kaburi lililokaliwa na mzee
Mtandi
lilipoachama kama mamba, na
wote wakashuhudia
Mzee Mtandi aliyekuwa ameketi
kwenye Kigoda
akizama na kupotelea ndani ya
kaburi pamoja na
kinu chake kisha kaburi
likajifunga.
Mama Kaguba alijikuta
amemshikila shati kwa
nguvu kaka yake hofu kuu
ikimkumba, wakati huo
Kanumba naye alikuwa
amehamanika na
kumuangalia Babu Gao aliyebaki
na mchi wake
mkononi asijue cha kufanya.
Ghafla!
Wakaanza kusikia kukurukakara
na vurugu
vikitokea ndani ya kaburi
aliliozama mzee Mtandi.
Ilikuwa ni kama vile uchukue
dumu kubwa halafu
uliwekee mawe madogo na kuanza
kulitikisa kwa
nguvu ndivyo zile vurugu mle
kaburini
zilivyozizima.
“YALAAAH…UWIIIII NAKUFAAA
JAMANI!” Sauti ya
mzee Mtandi ilisikika ikitokea mle
kaburini licha ya
kuwa kaburi lilikuwa limejifunga.
Babu Gao
uzalendo ukamshinda, akautupa
mwichi wake na
kutaka kukimbia ndipo haraka
Kungurume
akamrukia na kumkwida.
“Unataka kukimbia wapi?”
Kungurume alibwata.
“Tuondokeni jamani hii si hali ya
kawaida,” alijibu
Babu Gao. Kabla Kungurume
hajajibu lolote ndipo
tena mkanda ukaendelea. Kaburi
likajapasua
katikati halafu katikahali isiyokuwa
ya kawaida,
mzee Mtandi akarushwa kwa
nguvu kutokea mle
kaburini na kwenda angani, yeye
kule, kigoda na
kinu huko. Kisha akatua chini
kama kifurushi.
Kitokeo cha hapo mzee Mtandi
akainuka na kuanza
kutimua mbio kali, kufikia hapo
sasa akina
Kungurume pamoja na mganga
wao nao
wakatimka.
Mgonjwa aliyekuja amebebwa,
mara ghafla
ameondoka akikimbia kama
amefungwa mota
miguuni. Chezea kifo wewe!!!
Walitimka kwa kasi ya ajabu
mpaka nje ya viwanja
vile vya makaburi ambapo
hawakumuona kabisa
mzee Mtandi, hawakujua amepitia
njia gani.
Kutokana na hali ile ya kuogofya
hawakuendelea
kupoteza muda, wakaendelea
kukimbia na kuelekea
nyumbani kwa Babu Gao.
***Heeeeh!
Kungurume
akamlipa dereva teksi na
kumwacha aende zake
kwani kwa mujibu wa mganga,
wao walipaswa
kulala palepale. Kuwafahamisha
nyumbani kwao
haikuwa tabu kwani tangu
walipofika kwa Babu
hapo mtandao ulikuwa ukifanya
kazi.
******
Babu Gao akarejea katika ule
ukarimu wake wa
kawaida na wa kila siku.
Akawakirimu chakula
wageni wake, akawapa maji ya
kuoga huku yeye
akazianza sarakasi zake za
kumtibu mzee Mtandi
aliyekuwa hajarejewa na fahamu
muda wote ule.
Tiba ilikuwa kubwa na ngumu
sana, ilichukuwa
muda mrefu mpaka giza la usiku
likaingia, na hapo
Babu Gao akawaandalia wageni
wake sehemu ya
kulala. Walipolala, yeye
akaendelea na patashika
yake.
***
“Jamani kazi ni ngumu sana kama
nilivyokuambien
i tangu jana…” Babu Gao
aliwaambia akina mama
Kaguba baada ya kumka asubuhi.
“…Huyu bwana
kuna siri kubwa sana aliigundua
kuhusiana na hao
wachawi wenu, bahati mbaya
alipokuwa
akiwaelezeni ninyi hakujua kuwa
nyumba ile si
salama kujadili vitu hatari kama
vile…mle ndani
kuna wachawi kila kona…”
“Lakini Babu wakati mjomba
anatuhadithia habari
hiyo mpaka ikamkuta hali hii,
tulikuwa tumewatoa
nje watu wote wasiohusika.”
Mama Kaguba
alidakia.
“Una uhakika gani kuwa kati yenu
mliokuwa pale
sebuleni hakuna mchawi? Kwani
ninyi mlitegemea
kuwa yule mtoto mdogo Kaguba
angeweza kuwa
mchawi?” alisaili kwa umakini
Babu Gao.
“Mnh! Kwahiyo kuna mtu kati yetu
kule nyumbani
ni mchawi?” Alihoji kungurume.
“Sina maana hiyo, nilitaka tu
kukuonesheni kuwa
hamko makini na jambo hili
kwakuwa hamuujui
uchawi ninyi…iko hivi sasa, siku
ile mlipokuwa
mnaongea mambo haya mle ndani
palikuwa na
Paka amejilaza kwenye kiti, basi
yule hakua Paka
asilani!”
“Ama!” Alimaka Kungurume huku
akivuta
kumbukumbu ya siku ile.
“Alikuwa ni mwanaadamu yule
aliyejibadili na kuwa
kama Paka japo miaka yote
mmekuwa mkiamini
kuwa ni Paka wa kufugwa ila
hayati Masonganya
alikuwa akimtamua kama
mtumishi wake, na muda
mrefu huwa anawafatilia mambo
yenu. Sasa
aliposikia habari ile mbaya
akatoka nje na kwenda
kumpa taarifa Kaguba aliyekuwa
akicheza nje na
wenziwe’ Kaguba naye haraka
akawasilisha taarifa
ile kwa Binti Sambayu kwa njia
wazijuazo wenyewe
ndipo likatumwa pigo lile
lilomfanya mjomba wenu
awe hivi…ila tutajitahidi sana
kuhakikisha
anapona.”
“Tutashukuru sana Babu.”
“Vizuri!”
“Unajua nini Babu…” Kungurume
alianza kuongea
huku akitembeza macho yake
katika chumba kile
cha uganga. “…sisi hata hatukujua
ni kipi hicho
ambacho mjomba alikigundua
toka kwa hao
wachawi kwani alipofikia tu
kwenye pointi hiyo
nd’o akaanguka, sasa we’
unaweza kututajia hicho
alichokigundua?” Swali hilo
likamfanya Babu Gao
apikiche viganja vya mikono yake
na kisha
kuifumbata mikono yake kifuani.
Kimya kikatawala.
“Siwezi kusema uongo kabisa
katika hili, ni
kwamba sijabahatika kukijua hicho
kitu. Hata haya
machache niliyowahabarisha
nimeyapata kwa
ufundi wangu wa hali ya juu,
niliingia kichwani
mwa mjomba wenu na kuanza
kuzisoma fikra zake
lakini habari niliyoipata ni ile kama
mliyokuwa nayo
ninyi, yaani niliishia palepale
alipoanguka tu.
Nadhani leo atazinduka na
tutakwenda kufanya
kafara kubwa makaburini ambapo
tukimaliza
atatuhabarisha yeye mwenyewe.
***
Asubuhi yote, na mchana kutwa
Babu Gao alikuwa
akishughulika na jambo lile zito
mpaka kwenye saa
kumi alasiri ndipo mzee Mtandi
akarejewa na
fahamu. Ilikuwa ni kazi nzito, kazi
ya kutibu huku
akipambana na nguvu za wachawi
zilizokuwa
zikimshambulia mara kwa mara
kiasi cha
kumvurugia kabisa kazi yake.
Baada ya Mzee
Mtandi kuzinduka akaachwa
apumzike, kisha
baadaye akapewa chakula na
kupelekwa kuoga
akiwa amebebwa. Afya yake
haikuwa mbaya sana
japo tatizo kubwa alilokuwa nalo
ni kutoweza
kutembea mwenyewe pamoja na
kupoteza
kumbukumbu…hakuwa na
kumbukumbu zozote za
kulichotokea. Hilo Babu Gayo
alilitarajia.
Saa moja magharib msafara wa
kwenda
makaburini ukaanza. Kungurume,
Mama Kaguba,
Babu Gao na Kanumba wake
wakiwa wamembeba
mzee Mtandi wakaongozana
kuelekea makaburini
ambapo zindiko kubwa liliratibiwa
kufanyika.
“Tukifika makaburini
hatutoruhusiwa kuongea
chochote labda kama
nitawaelekeza kufanya
hivyo,. Sawa?” Aliunguruma Babu
Gao.
“Ndiyo!” “…Tawire.” Walijibu.
“Kuna kazi ndogo tu kama ya
dakika kumi hivi
tutaifanyia juu ya kaburi. Tukifika
we’ bwana
Mtandi tutakuwekea kigoda juu ya
Kaburi kisha
utaketi, tutakupa kinu
kitakachokuwa na dawa
ndani yake, utakishikilia kwa
mikono yako miwili
halafu mimi nitatwanga dawa
itakayokuwa humo
kwenye kinu…” Walikuwa
wakimsikiliza kwa kina
Babu Gao akitoa maelekezo
maana walijua
wakifika huko makaburini
hawatopata nafasi ya
kuongea kama walivyopewa
hadhari mapema.
“…Nikishamaliza kutwanga tu
dawa utainuka na
kutoka hapo kaburini kisha dawa
hiyo
tutaichanganya kwenye kinu na
sote tutaioga na
kuinywa. Hapo tutakuwa
tumemaliza kazi yetu.”
Alihitimisha Babu Gao na
kuruhusu maswali kwa
ambaye hajaelewa, hapakuwa na
swali.
Wakatembea mpaka wakawasili
katika viwanja vya
makaburi. Japo alikuwa
amebebwa, mzee Mtandi
alisikia na kuelewa maelekezo yote
yaliyotolewa na
Babu Gao.
Viwanja vya makaburi vilikuwa
kimya kabisa,
upepo ukiiyumbisha miti kadhaa
iliyopandwa kwa
kulizunguka eneo hilo kiasi cha
kuyaangusha
majani dhaifu yaliyolegea. Wakati
huo giza
lilikwishaanza kutanda na kufanya
eneo hili la
makaburini kutisha haswa!
Wakaingia na kwenda mpaka
katikati ya makaburi,
Babu Gao akachagua kaburi moja
lilionesha kuwa
si la muda mrefu sana tangu
lihifadhi mtu ndani
yake. Haraka Kanumba wa Babu
akaweka kigoda
juu ya Kaburi hilo sambamba na
Kinu chenye dawa
kisha akarudi hatua moja nyuma.
Babu Gao
akasaidiana na Kungurume
kumnyanyua mzee
Mtandi na kumkalisha juu ya
kigoda kile juu ya
kaburi. Baada ya kuketi, mzee
Mtandi akakishika
kinu kwa mikono yake miwili na
hapohapo Babu
Gao akiwa amesimama kwa karibu
japo yeye
hakupanda juu ya kaburi, akainua
juu mchi wake
wa kutwangia na kuanza kuongea
maneno yake ya
kiganga. Wakati huo Mama
Kaguba, Kungurume,
na yule Kanumba walikuwa
wamesimama kwa
kulizunguka kaburi.
Baada ya Babu kumaliza kuongea
tu maneno yake,
akaanza kutwanga dawa iliyomo
ndani ya kinu
kilichoshikiliwa na mzee Mtandi
huku akiimba
nyimbo kwa lugha ya kiha.
Ghafla wakati Babu Gao akitwanga
dawa ile
kikaibuka kizaazaa kilichowafanya
wote wataharuki
mpaka Babu Gao mwenyewe.
Ilikuwa ni wakati Babu Gao
akitwanga ile dawa,
ndipo Kaburi lililokaliwa na mzee
Mtandi
lilipoachama kama mamba, na
wote wakashuhudia
Mzee Mtandi aliyekuwa ameketi
kwenye Kigoda
akizama na kupotelea ndani ya
kaburi pamoja na
kinu chake kisha kaburi
likajifunga.
Mama Kaguba alijikuta
amemshikila shati kwa
nguvu kaka yake hofu kuu
ikimkumba, wakati huo
Kanumba naye alikuwa
amehamanika na
kumuangalia Babu Gao aliyebaki
na mchi wake
mkononi asijue cha kufanya.
Ghafla!
Wakaanza kusikia kukurukakara
na vurugu
vikitokea ndani ya kaburi
aliliozama mzee Mtandi.
Ilikuwa ni kama vile uchukue
dumu kubwa halafu
uliwekee mawe madogo na kuanza
kulitikisa kwa
nguvu ndivyo zile vurugu mle
kaburini
zilivyozizima.
“YALAAAH…UWIIIII NAKUFAAA
JAMANI!” Sauti ya
mzee Mtandi ilisikika ikitokea mle
kaburini licha ya
kuwa kaburi lilikuwa limejifunga.
Babu Gao
uzalendo ukamshinda, akautupa
mwichi wake na
kutaka kukimbia ndipo haraka
Kungurume
akamrukia na kumkwida.
“Unataka kukimbia wapi?”
Kungurume alibwata.
“Tuondokeni jamani hii si hali ya
kawaida,” alijibu
Babu Gao. Kabla Kungurume
hajajibu lolote ndipo
tena mkanda ukaendelea. Kaburi
likajapasua
katikati halafu katikahali isiyokuwa
ya kawaida,
mzee Mtandi akarushwa kwa
nguvu kutokea mle
kaburini na kwenda angani, yeye
kule, kigoda na
kinu huko. Kisha akatua chini
kama kifurushi.
Kitokeo cha hapo mzee Mtandi
akainuka na kuanza
kutimua mbio kali, kufikia hapo
sasa akina
Kungurume pamoja na mganga
wao nao
wakatimka.
Mgonjwa aliyekuja amebebwa,
mara ghafla
ameondoka akikimbia kama
amefungwa mota
miguuni. Chezea kifo wewe!!!
Walitimka kwa kasi ya ajabu
mpaka nje ya viwanja
vile vya makaburi ambapo
hawakumuona kabisa
mzee Mtandi, hawakujua amepitia
njia gani.
Kutokana na hali ile ya kuogofya
hawakuendelea
kupoteza muda, wakaendelea
kukimbia na kuelekea
nyumbani kwa Babu Gao.
***Heeeeh!