Post by Admin on May 31, 2015 21:31:51 GMT
Walitimka kwa kasi ya ajabu
mpaka nje ya viwanja
vile vya makaburi ambapo
hawakumuona kabisa
mzee Mtandi, hawakujua amepitia
njia gani.
Kutokana na hali ile ya kuogofya
hawakuendelea
kupoteza muda, wakaendelea
kukimbia na kuelekea
nyumbani kwa Babu Gao.
“Poleni jamani, nini hasa
kilichotokea maana
nimeshangaa kuona mgonjwa
amerudi mbio na
kupitiliza mpaka chumbani.” Mke
wa Babu Gao
aliwapokea akina Babu Gao
pamoja na Kungurume
ambao nao waliingia hapo
nyumbani kwa kasi ya
ajabu. Hakuna aliyemjibu mama
yule zaidi ya
kuendelea kutweta kwa mchoko na
kihoro, japo
hawakupumzika baada ya kusikia
kuwa mgonjwa
yuko ndani. Wote wakafuatana na
kuingia
chumbani kwa mgonjwa.
Wakamkuta mzee Mtandi akiwa
amelala kitandani
hoi bin taabani…hana hali, hana
kauli. Yaani
mgonjwa aliyekuja nyumbani huku
akikimbia ghafla
amekuwa hoi asiyeweza hata
kuinua mkono acha
kusimama!
Kungurume kila alipokumbuka
jinsi Babu Gao
alivyotaka kuwakimbia alitamani
hata amnase
kelbu lakini akahofia kuvuruga
mambo. Wakaanza
kumhudumia mzee Mtandi. Mpaka
kwenye saa nne
usiku hali haikuwa imetengemaa
ikawabidi waingie
tu kulala. Hakuna aliyelala zaidi ya
kuhesabu paa
tu.
Wakiwa bado wamejilaza vitandani
mwao ghafla
wakamsikia mtu akipita nje ya
nyumba huko
ambapo baada ya kusikia akipiga
ngoma kisha
akinena kwa sauti kubwa.
“TANZIA…TANZIA…
TANZIA Familia ya bwana GAO
aliye mganga
kiboko inasikitika kuwatangazia
kifo cha mteja
wake bwana mtandi Bin
Kalukalange kilichotokea
usiku wa kuamkia leo, maziko
yatafanyikia Kibondo
mjini.”
Tangazo hilo liliwafikia kila mmoja
mahala
alipolala…hofu mpya ikaibuka
hasa kwa akina
Kungurume ambao kioja cha
namna hiyo
kilishapata kuwakumba kwa
ndugu yao Bi
Nyanzala. Wote wakainuka baada
ya tangazo hilo
kuisha na kuingia chumbani kwa
mzee Mtandi.
Loohsalale!
Mzee Mtandi alikuwa amefariki.
Kilio kikaibuka
hapohapo. Babu Gao akajitahidi
kuwatuliza ili
ajaribu kuangalia kwenye
‘bainokyula’ yake…na
hata alipopiga ramli zake
zilimthibitishia kuwa
mzee Mtandi amekwishaaga
dunia. Simu
zikapigwa mjini kwa ndugu ambao
nao baada ya
kuangua vilio vikubwa
vilivyokusanya majirani,
walijipanga wakakodi gari na
kuufuata mwili wa
marehemu pamoja na akina mama
Kaguba.
********
“…hii siyo bure, kuna jambo zito
humu ndani. Na
wasipokuwa makini watatikitia
kama utitiri…”
aliongea Bi mkubwa mmoja
aliyehudhuria msibani
hapo kwa hayati Masonganya.
“Haswa! Maana ndani ya muda
mfupi tu
wamekufa watu watu. Alianza Bi
Masonganya,
akafuatia Nyanzala, na sasa
mjomba wao bwana
Mtandi…haiwezekani.” Waliungana
mikono akina
mama hao.
“Aaah kwa Mungu madogo hayo,
si ajabu kufa
watu watatu kutoka katika familia
moja…Mungu
hata akitaka kuwamaliza nchi
nzima kwa sekunde
hashindwi kamwe!” alijibu dada
mwingine huku
‘akiwabyeda’ wenziye.
“We’ mtoto mdogo huna ujuacho
kaa kimya!”
Wakati mjadala mzima ukuiendelea
huko uani kwa
akina mama, upande wa mbele wa
nyumba
wanaume nao walikuwa
wakizungumzia jambo
hilohilo mpaka walipokatizwa na
gari iliyokwenda
kufuata maiti. Ilikuwa ikirejea huku
imewasha taa
ikiwa ni ishara kuwa wamebeba
maiti. Wanaume
wakasimama mpaka Gari
ilipoegeshwa,
wakaisogelea na kusaidiana
kuupokea mwili wa
hayati Mtandi.
Muda wa mazishi ulipangwa kuwa
ni saa kumi
alasiri ya siku itakayofuata ili
kuwasubirisha
watoto wawili wa marehemu
waishio Kigoma mjini.
“Ebyomunyumba tebi totolwa,”
Alisema Kungurume
kuwaambia dada zake kwa
kutumia lugha ileile ya
marehemu mjomba wao. Naye
akiwa na maana
ileile kuwa wasiyaweke hadharani
mambo yao.
***
Siku iliyofuata majira ya saa tano
asubuhi
waliwasili watoto wawili wa
marehemu ambao ni
Lubambi na Ilumbi…pamoja nao
waliandamana na
Nyembo. Wafiwa walitoka
kuwapokea ndugu zao
hao huku wakilia lakini baada ya
akina Ilumbi
kuingia ndani tu sura za akina
mama Kaguba pale
nyumbani zikawabadilika kutoka
kwenye huzuni na
simanzi ya kufiwa na kuwa hasira
ya Nongwa,
hapakuwa na mazungumzo yoyote
zaidi ya
kupotezeana tu. Tatizo kubwa
likiwa ni Nyembo.
Nyembo pia ni mtoto wa hayati Bi
Masonganya
hivyo ni ndugu yao na akina
mama Kaguba japo
tofauti yao ni moja tu, wakati wao
wanamwita Bi
Masonganya mama, huyu Nyembo
yeye anamuita
Baba. Naama Bi Masonganya ni
baba yake kabisa
na Nyembo, na hivyo ni miongoni
mwa vimbwanga
vya hayati Bi Masonganya.
Watoto wote wa Bi Masonganya
walimchukulia
Nyembo kama ni kielelezo cha
uchawi uliokubuhu
wa mama yao kiasi cha kuwafanya
waoneshewe
vidole kila wakatizapo wakiwa na
Nyembo.
Wakamchukia sana kijana yule
kiasi cha
kumuanzishia mizozo na ghasia
za kila aina mpaka
hayati bwana Mtandi alipoamua
kumchukuwa na
kwenda kuishi naye Kigoma mjini
baada ya
kuombwa kufanya hivyo na dada
yake. Hiyo ikawa
ni neema kubwa kwa Nyembo
kwani alinusurika
kulelewa kichawi na pia akiwa
huko alibahatika
kusomeshwa mpaka kidato cha
sita na mzee
Mtandi, tofauti na nduguze
walioishia darasa la
nne na wengine la saba tu.
***
Kwa kawaida ya genge la wachawi
wa pale
Kibondo ni kwamba ni lazima kwa
kiongozi wao
mkuu kuwa na mke, hivyo
ilipolazimu kumsimika
ukuu huo hayati Bi Masonganya,
ililazimu pia
apewe mke japo naye ni
mwanamke. Mke huyu
alipaswa kumfanyia Bi
Masonganya kila ambalo
mke humfanyia mumewe japo
tendo kuu bila shaka
lisingewezekana kwakuwa wote ni
jinsia moja.
Haikuwa taabu kumpata mke
kwani mmoja wa
wachawi aitwaye bwana Kalombola
alimtoa binti
yake pekee kwa heshma kubwa ili
aoelewe na
mkuu wake huyo mpya. Binti huyo
aliitwa
Masunga.
Maisha yakaendelea huku bi
Masonganya akiwa ni
mume wa Bi Masunga, na wakati
huohuo akiwa ni
mke wa bwana Muhonge ambaye
ndiye baba yao
na akina Kungurume. Ilimlazimu Bi
Masonganya
kumchukua huyo mkewe na kuishi
naye nyumbani
kwake kitu ambacho kilipekea
usiri ulioligubika
jambo hilo kuvuja, ming’ono
ikashamiri kwa
majirani na hatimaye wilaya nzima
na baadaye
habari zikamfikia bwana Muhonge
kuwa mkewe
naye ni mume wa mtu. Ikawa ni
balaa kubwa,
mzozo na magomvi yaliibuka kwa
kasi na hicho
nd’o kilichopelekea kifo cha
kutatanisha kwa
bwana Muhonge. Hapo ndipo Bi
Masonganya
alipojinafasina kujitandaza na
mkewe huyo bila
kificho…kila mtu akaamini sasa.
Miezi sita ya ndoa hiyo ya ajabu,
hatimaye Bi
Masunga akapata ujauzito,
haikueleweka kirahisi
nini ambacho Bi Masonganya
alichomtenda Bi
Masunga mpaka kushika ujauzito
ule. Kama
aliyeitegemea hali ile, Bi
Masonganya kila siku
akawa anamuosha na kumfukiza
madawa ya kila
aina Masunga mpaka zilipotimu
siku zake za
kujifungua. Na alipojifungua,
Laahaullah mtoto
alitoka kafanana kila kitu na Bi
Masonganya(Baba
yake), yaani mpaka kucha. Tukio
hilo la ajabu
lilizagaa karibu kila kona ya
Kibondo kiasi cha
kumfanya mtoto aliyezaliwa
(Nyembo) kuwa mfano
wa kivutio cha watalii wa ndani
(wambea). Nyembo
alikuwa vizuri tu huku akipata
malezi kama
wapatayo nduguze wengine
aliowakuta japo kwake
yeye Bi Masonganya alikuwa ni
Baba.
Hicho ndicho kilichowafanya
watoto wa Bi
Masonganya kumchukia Nyembo
na kugombana
naye mara nyingi mpaka mama
Nyembo akawa
anaingilia na hatimaye
kusababisha ugomvi ule
kuwa mkubwa zaidi. Bi Masunga
alifariki Nyembo
alipokuwa na umri wa miaka
mitano na hapo ndipo
ilipomlazimu Bi Masonganya
amuombe kaka yake,
mzee Mtandi amchukue ili
kunusuru vurugu
zilizokuwa zikiendelea kuota
makucha. Nyembo
akahamishiwa Kigoma, huko
aliishi na mzee Mtandi
mwenyewe pamoja na watoto
wake kwa raha
mustarehe hata akasahau habari
za Kibondo.
Ilipomlazimu mara mojamoja
kwenda kumsalimu Bi
Masonganya alikwenda japo
hakukaa muda mrefu,
na siku zote alizokaa huko muda
mwingi aliutumia
akiwa ndani tu na mama yake, kitu
kilichowazidish
ia hofu nduguze kuwa atakuwa
anarithishwa
uchawi tu…na hicho ndicho
kilichozidi kupalilia
uadui wao.
ITAENDELEA...
mpaka nje ya viwanja
vile vya makaburi ambapo
hawakumuona kabisa
mzee Mtandi, hawakujua amepitia
njia gani.
Kutokana na hali ile ya kuogofya
hawakuendelea
kupoteza muda, wakaendelea
kukimbia na kuelekea
nyumbani kwa Babu Gao.
“Poleni jamani, nini hasa
kilichotokea maana
nimeshangaa kuona mgonjwa
amerudi mbio na
kupitiliza mpaka chumbani.” Mke
wa Babu Gao
aliwapokea akina Babu Gao
pamoja na Kungurume
ambao nao waliingia hapo
nyumbani kwa kasi ya
ajabu. Hakuna aliyemjibu mama
yule zaidi ya
kuendelea kutweta kwa mchoko na
kihoro, japo
hawakupumzika baada ya kusikia
kuwa mgonjwa
yuko ndani. Wote wakafuatana na
kuingia
chumbani kwa mgonjwa.
Wakamkuta mzee Mtandi akiwa
amelala kitandani
hoi bin taabani…hana hali, hana
kauli. Yaani
mgonjwa aliyekuja nyumbani huku
akikimbia ghafla
amekuwa hoi asiyeweza hata
kuinua mkono acha
kusimama!
Kungurume kila alipokumbuka
jinsi Babu Gao
alivyotaka kuwakimbia alitamani
hata amnase
kelbu lakini akahofia kuvuruga
mambo. Wakaanza
kumhudumia mzee Mtandi. Mpaka
kwenye saa nne
usiku hali haikuwa imetengemaa
ikawabidi waingie
tu kulala. Hakuna aliyelala zaidi ya
kuhesabu paa
tu.
Wakiwa bado wamejilaza vitandani
mwao ghafla
wakamsikia mtu akipita nje ya
nyumba huko
ambapo baada ya kusikia akipiga
ngoma kisha
akinena kwa sauti kubwa.
“TANZIA…TANZIA…
TANZIA Familia ya bwana GAO
aliye mganga
kiboko inasikitika kuwatangazia
kifo cha mteja
wake bwana mtandi Bin
Kalukalange kilichotokea
usiku wa kuamkia leo, maziko
yatafanyikia Kibondo
mjini.”
Tangazo hilo liliwafikia kila mmoja
mahala
alipolala…hofu mpya ikaibuka
hasa kwa akina
Kungurume ambao kioja cha
namna hiyo
kilishapata kuwakumba kwa
ndugu yao Bi
Nyanzala. Wote wakainuka baada
ya tangazo hilo
kuisha na kuingia chumbani kwa
mzee Mtandi.
Loohsalale!
Mzee Mtandi alikuwa amefariki.
Kilio kikaibuka
hapohapo. Babu Gao akajitahidi
kuwatuliza ili
ajaribu kuangalia kwenye
‘bainokyula’ yake…na
hata alipopiga ramli zake
zilimthibitishia kuwa
mzee Mtandi amekwishaaga
dunia. Simu
zikapigwa mjini kwa ndugu ambao
nao baada ya
kuangua vilio vikubwa
vilivyokusanya majirani,
walijipanga wakakodi gari na
kuufuata mwili wa
marehemu pamoja na akina mama
Kaguba.
********
“…hii siyo bure, kuna jambo zito
humu ndani. Na
wasipokuwa makini watatikitia
kama utitiri…”
aliongea Bi mkubwa mmoja
aliyehudhuria msibani
hapo kwa hayati Masonganya.
“Haswa! Maana ndani ya muda
mfupi tu
wamekufa watu watu. Alianza Bi
Masonganya,
akafuatia Nyanzala, na sasa
mjomba wao bwana
Mtandi…haiwezekani.” Waliungana
mikono akina
mama hao.
“Aaah kwa Mungu madogo hayo,
si ajabu kufa
watu watatu kutoka katika familia
moja…Mungu
hata akitaka kuwamaliza nchi
nzima kwa sekunde
hashindwi kamwe!” alijibu dada
mwingine huku
‘akiwabyeda’ wenziye.
“We’ mtoto mdogo huna ujuacho
kaa kimya!”
Wakati mjadala mzima ukuiendelea
huko uani kwa
akina mama, upande wa mbele wa
nyumba
wanaume nao walikuwa
wakizungumzia jambo
hilohilo mpaka walipokatizwa na
gari iliyokwenda
kufuata maiti. Ilikuwa ikirejea huku
imewasha taa
ikiwa ni ishara kuwa wamebeba
maiti. Wanaume
wakasimama mpaka Gari
ilipoegeshwa,
wakaisogelea na kusaidiana
kuupokea mwili wa
hayati Mtandi.
Muda wa mazishi ulipangwa kuwa
ni saa kumi
alasiri ya siku itakayofuata ili
kuwasubirisha
watoto wawili wa marehemu
waishio Kigoma mjini.
“Ebyomunyumba tebi totolwa,”
Alisema Kungurume
kuwaambia dada zake kwa
kutumia lugha ileile ya
marehemu mjomba wao. Naye
akiwa na maana
ileile kuwa wasiyaweke hadharani
mambo yao.
***
Siku iliyofuata majira ya saa tano
asubuhi
waliwasili watoto wawili wa
marehemu ambao ni
Lubambi na Ilumbi…pamoja nao
waliandamana na
Nyembo. Wafiwa walitoka
kuwapokea ndugu zao
hao huku wakilia lakini baada ya
akina Ilumbi
kuingia ndani tu sura za akina
mama Kaguba pale
nyumbani zikawabadilika kutoka
kwenye huzuni na
simanzi ya kufiwa na kuwa hasira
ya Nongwa,
hapakuwa na mazungumzo yoyote
zaidi ya
kupotezeana tu. Tatizo kubwa
likiwa ni Nyembo.
Nyembo pia ni mtoto wa hayati Bi
Masonganya
hivyo ni ndugu yao na akina
mama Kaguba japo
tofauti yao ni moja tu, wakati wao
wanamwita Bi
Masonganya mama, huyu Nyembo
yeye anamuita
Baba. Naama Bi Masonganya ni
baba yake kabisa
na Nyembo, na hivyo ni miongoni
mwa vimbwanga
vya hayati Bi Masonganya.
Watoto wote wa Bi Masonganya
walimchukulia
Nyembo kama ni kielelezo cha
uchawi uliokubuhu
wa mama yao kiasi cha kuwafanya
waoneshewe
vidole kila wakatizapo wakiwa na
Nyembo.
Wakamchukia sana kijana yule
kiasi cha
kumuanzishia mizozo na ghasia
za kila aina mpaka
hayati bwana Mtandi alipoamua
kumchukuwa na
kwenda kuishi naye Kigoma mjini
baada ya
kuombwa kufanya hivyo na dada
yake. Hiyo ikawa
ni neema kubwa kwa Nyembo
kwani alinusurika
kulelewa kichawi na pia akiwa
huko alibahatika
kusomeshwa mpaka kidato cha
sita na mzee
Mtandi, tofauti na nduguze
walioishia darasa la
nne na wengine la saba tu.
***
Kwa kawaida ya genge la wachawi
wa pale
Kibondo ni kwamba ni lazima kwa
kiongozi wao
mkuu kuwa na mke, hivyo
ilipolazimu kumsimika
ukuu huo hayati Bi Masonganya,
ililazimu pia
apewe mke japo naye ni
mwanamke. Mke huyu
alipaswa kumfanyia Bi
Masonganya kila ambalo
mke humfanyia mumewe japo
tendo kuu bila shaka
lisingewezekana kwakuwa wote ni
jinsia moja.
Haikuwa taabu kumpata mke
kwani mmoja wa
wachawi aitwaye bwana Kalombola
alimtoa binti
yake pekee kwa heshma kubwa ili
aoelewe na
mkuu wake huyo mpya. Binti huyo
aliitwa
Masunga.
Maisha yakaendelea huku bi
Masonganya akiwa ni
mume wa Bi Masunga, na wakati
huohuo akiwa ni
mke wa bwana Muhonge ambaye
ndiye baba yao
na akina Kungurume. Ilimlazimu Bi
Masonganya
kumchukua huyo mkewe na kuishi
naye nyumbani
kwake kitu ambacho kilipekea
usiri ulioligubika
jambo hilo kuvuja, ming’ono
ikashamiri kwa
majirani na hatimaye wilaya nzima
na baadaye
habari zikamfikia bwana Muhonge
kuwa mkewe
naye ni mume wa mtu. Ikawa ni
balaa kubwa,
mzozo na magomvi yaliibuka kwa
kasi na hicho
nd’o kilichopelekea kifo cha
kutatanisha kwa
bwana Muhonge. Hapo ndipo Bi
Masonganya
alipojinafasina kujitandaza na
mkewe huyo bila
kificho…kila mtu akaamini sasa.
Miezi sita ya ndoa hiyo ya ajabu,
hatimaye Bi
Masunga akapata ujauzito,
haikueleweka kirahisi
nini ambacho Bi Masonganya
alichomtenda Bi
Masunga mpaka kushika ujauzito
ule. Kama
aliyeitegemea hali ile, Bi
Masonganya kila siku
akawa anamuosha na kumfukiza
madawa ya kila
aina Masunga mpaka zilipotimu
siku zake za
kujifungua. Na alipojifungua,
Laahaullah mtoto
alitoka kafanana kila kitu na Bi
Masonganya(Baba
yake), yaani mpaka kucha. Tukio
hilo la ajabu
lilizagaa karibu kila kona ya
Kibondo kiasi cha
kumfanya mtoto aliyezaliwa
(Nyembo) kuwa mfano
wa kivutio cha watalii wa ndani
(wambea). Nyembo
alikuwa vizuri tu huku akipata
malezi kama
wapatayo nduguze wengine
aliowakuta japo kwake
yeye Bi Masonganya alikuwa ni
Baba.
Hicho ndicho kilichowafanya
watoto wa Bi
Masonganya kumchukia Nyembo
na kugombana
naye mara nyingi mpaka mama
Nyembo akawa
anaingilia na hatimaye
kusababisha ugomvi ule
kuwa mkubwa zaidi. Bi Masunga
alifariki Nyembo
alipokuwa na umri wa miaka
mitano na hapo ndipo
ilipomlazimu Bi Masonganya
amuombe kaka yake,
mzee Mtandi amchukue ili
kunusuru vurugu
zilizokuwa zikiendelea kuota
makucha. Nyembo
akahamishiwa Kigoma, huko
aliishi na mzee Mtandi
mwenyewe pamoja na watoto
wake kwa raha
mustarehe hata akasahau habari
za Kibondo.
Ilipomlazimu mara mojamoja
kwenda kumsalimu Bi
Masonganya alikwenda japo
hakukaa muda mrefu,
na siku zote alizokaa huko muda
mwingi aliutumia
akiwa ndani tu na mama yake, kitu
kilichowazidish
ia hofu nduguze kuwa atakuwa
anarithishwa
uchawi tu…na hicho ndicho
kilichozidi kupalilia
uadui wao.
ITAENDELEA...