Post by Admin on May 31, 2015 21:34:42 GMT
Ilipomlazimu mara mojamoja
kwenda kumsalimu Bi
Masonganya alikwenda japo
hakukaa muda mrefu,
na siku zote alizokaa huko muda
mwingi aliutumia
akiwa ndani tu na mama yake, kitu
kilichowazidish
ia hofu nduguze kuwa atakuwa
anarithishwa
uchawi tu…na hicho ndicho
kilichozidi kupalilia
uadui wao.
***
Sasa leo amekuja tena Kibondo
kwakuwa mzee
Mtandi amefariki, na makubaliano
ni kwamba
angezikiwa palepale Kibondo
hivyo ni lazima aje
amzike baba yake mdogo
(mjomba).
“Ilumbi…” Aliita Bi Chakupewa
ambaye ni dada
yake na mama Kaguba, kisha
akaaendelea kuongea
kabla hajaitikiwa. “…Nadhani we’
si’ mgeni wa
mambo ya humu ndani, sasa
imekuaje tena
unatuletea hiki kituko?”
Alihitimisha Chakupewa
huku akimsonta Nyembo kwa
kidole chake.
Wanafamilia wote wakajikuta
wametazamana.
“Ulitaka asije kumzika mzazi wake
aliyemlea kisa
magomvi yenu?” alijibu Ilumbi na
kukazia tena “…
nachojua mimi, Nyembo ni ndugu
yetu fullstop…
kama kuna makosa waliwahi
kufanya wazazi wake
basi sisi hayatuhusu kama
yasivyomuhusu yeye.”
“Nakwambia hivi Ilumbi kama
udugu leo utauzika,
ila huyu Nyembo humu ndani
hakai labda
mkamtafutie sehemu nyingine ya
kulala. Angalia
huko alipoingia tu majirani
wakaanza
kumzungumza, mnasababisha
familia yetu
ionekane ya kichawi, hivi tutaishi
vipi na jamii yetu
jamani? Alibwata mama Kaguba.
“Sasa unatutishia kuvunja udugu?
Aliyekuambia si’
tunashida na udugu nani? Udugu
wenyewe huu wa
nazi kukutania pakachani, acha
upumbavu wako
wewe…” Safari hii alibwata
Lubambi, mtoto wa
kiume marehemu. “…Iko hivi,
aliyekufa ni baba yetu
sisi japonanyi ni mjomba wenu.
Sasa kama
hamtaki tushiriki sote pamoja na
Nyembo wala
tusibabaishane tunaichukua maiti
na kwenda
kuizikia kwetu, kama ni uwezo
nasi’ pia tuko fiti!”
Majibu hayo ya Lubambi nd’o
kama yalichochea
vurugu, ikawa ni majibizano,
majigambo na kila
aina ya upuuzi mpaka baadaye
kabisa
walipouingilia ugomvi ule wazee
wengine kutoka
katika familia hiyo ambapo hekma
na busara zao
ziliwatuliza ndugu wale na
kuwapatanisha. Maneno
ya waze yaliwaingia sana akina
mama Kaguba
hasa pale waliposisitizwa kuwa
Nyembo hakuwa
mwenye hatia kamwe kwa kosa
lililofanywa na
wazazi huko nyuma, wakalainika
ukizingatia hata
ile hofu yao kuwa Nyembo alikuwa
akikabidhiwa
uchawi na marehemu Masonganya
ilikwishapotea
baada ya kupata ithibati mpya
kuwa kama ni
uchawi alikabidhiwa mtoto wao
wenyewe, Kaguba.
Kufikia hapo kidogo amani
ikarejea na shughuli za
maziko zikaendelea kupangiliwa.
Suluhu yao ikawa ni pigo kwa
kambi ya akina
Kaguba waliokuwa wakiombea
mzozo ule uwe
mkubwa ili maiti iondolewe mle
ndani ili Kaguba
apate nafasi ya kuingia kule
ufuoni akakichimbue
kile kibuyu kinachomzuia kutoka
nje ya nyumba
kwenda kuwanga.
Saa kumi Alasiri baada ya
kufanyika visomo vya
dua maalum na sala kwa maiti,
hatimaye jeneza la
mzee Mtandi likabebwa na
wanaume na kuelekea
makaburini kuzika. Wanawake
walibaki nyumbani
wakilisindikiza kwa macho jeneza
lile. Hakika kifo
kile kiliwachoma na kuwaingia
sana.
Hiyo nd’o ikawa safari ya mwisho
ya bwana
Mtandi.
***
Saa tisa usiku, kundi kubwa la
wachawi
likiongozwa na Binti Sambayu
lilikusanyika kwa
kulizunguka kaburi alilozikwa
hayati Mtandi,
wakiwa watupu kama
walivyozaliwa. Ngoma na
nyimbo za kichawi zilirindima
kisawasawa, kila
mmoja alijiachia atakavyo bila ya
kujali ni athari
gani atakayoacha kutokana na
kubinuka akiwa
mtupu mbele ya wenziye ambao
wengine ni wa
jinsia tofauti na yake. Mbali ya
kuserebuka nyimbo
hizo pia kulikuwa na vinywaji na
vitoweo murua,
Damu na nyama za watu, pamoja
na pombe kali
vilihusika.
“Jamani mida inayoyoma, sasa
tutekeleze
kilichotuleta ili tutawanyike…karibu
mkuu!”
Aliongea Bi mkubwa mmoja
ambaye alitapakaa
vumbi kali ya makaburini kutokana
mtindo wa
kugaagaa wakati alipokuwa
akiserebuka.
Alipomaliza tu kuongea, wachawi
wote wakaketi
chini na hapo ndipo akasimama
Binti Sambayu na
kuanza kuongea.
“Bila kupoteza muda napenda
kuwapa salamu
kutoka kwa mkuu wetu Kaguba
anasema yuko
pamoja nasi na kwamba siku si
nyingi atajumuika
nasi na kutatua matatizo yetu
yote…” kufikia hapo
vigeregere vikazimama, kisha
akaendelea. “…
pamoja na hayo ni kwamba
tulikuwa tuwe na
mazoezi makubwa mawili hapa
leo. Moja ni
kumkata rasmi ulimi Nyanzala ili
aingizwe katika
daftari letu la kudumu la misukule,
na pili ni
kumfukua bwana Mtandi na
kumzindika kabla ya
siku yake ya kukatwa ulimi. Ila
kutokana na
maagizo toka kwa mkuu Kaguba
ni kwamba
hatutomkata ulimi leo Nyanzala
mpaka
atakapokuja mwenyewe hivyo
tutabakiwa na suala
hili moja tu la kumfukua huyu
bwana mjuaji!”
Alipomaliza tu kusema maneno
hayo binti
Sambayumara kijana mmoja
aliyekuwa
amejihifadhi kichawi chini ya
miembe akaibukia
akiwa amemshika mkono Nyanzala
na
kumkabidhisha kwa wachawi wale.
Nyanzala
aliyekuwa amevishwa kijigauni
chepesi huku
miguuni akiwa peku kama bata,
alikuwa
akitetemeka kama mtoto mwenye
homa.
Baada ya Nyanzala kuwekwa chini,
sasa
wakalisogelea Kaburi la hayati
bwana Mtandi na
kuanza kubinuka tena mahepe
yao. Dakika chache
tu Binti Sambayu akakipiga kwa
nguvu chungu
cheusi juu ya kaburi lile na
hapohapo kaburi
likapasuka na kuachia kijinjia
chembamba.
Macho ya Nyanzala aliyekuwa
ameketi jirani
kabisa, yalishuhudia kupitia katika
ufa huo
uliopasuka hapo kaburini
akichomoza maiti
aliyevaa sanda nyeupe. Kutokana
na upenyo huo
finyu hapo kaburini, maiti ilikuwa
ikichomoza kwa
tabu sana mpaka takribani dakika
tano maiti ikawa
juu ya kaburi.
Muda wote huo wale wachawi
walikuwa
wakiendelea kuimba kwa shangwe
huku wakicheza
na kufurahia tukio hilo. Maiti ile
haikuwa maiti ki-
ukweli maana ilipomwagiwa dawa
fulani kutoka
katika kibuyu kidogo cha binti
Sambayu hapohapo
ikainuka. Alikuwa ni Mzee Mtandi.
Mara macho ya Nyanzala
yakakutana na yale ya
mjomba’ake mzee Mtandi. japo
wote walikuwa
kama wapumbavu tu kwa jinsi
walivyopumbazwa
akili na madawa. Nyanzala
akaanza kulia japo bila
ya kutoa sauti.
Wakati mzee Mtandi akiwa
amesimama kama
mlevi wa dawa za kulevya,
akashituliwa kwa
kumwagiwa maji ya baridi
yakifuatiwa na mijeredi
ya nguvu! Akashituka kutokana na
maumivu yale,
na sasa akili zikawa zimeanza
kumreja…hicho nd’o
walichokuwa wakikitaka wale
Wachawi.
Kumzindua!
Kwa kawaida Wachawi wale
wakishamfufua mtu,
humfanyia madawa yao pamoja na
kumshitua kwa
maji ya baridi na mijeredi ili
kuiamsha akili yake
ambayo ilidorora mchana kutwa
tangu afukiwe
kaburini na ndugu zake wakiamini
amekwishakufa,
kisha zoezi linalofuata ni
kumfanyisha mazoezi.
Huwa wao wanasimama na
msukule wao karibu
na kaburi alilofukuliwa kisha
wanamuamuru
akimbie mpaka sehemu
waliyoweka alama yao
halafu anarejea tena mpaka walipo
wao…hufanya
hivyo kwa takribani mizunguko
mitano kabla
hawajamzuia na kuondoka naye
mpaka nyumbani
atakapofikishiwa kwa shughuli
nyinge zaidi. Hivyo
na mzee Mtandi naye akaamriwa
aanze kukimbia
kama ilivyo desturi!
***
Katika usiku huo mkubwa wakati
wachawi
wakifanya vitu vyao kule
makaburini, huku
nyumbani nako watu walikuwa
wamelala isipokuwa
Nyembo pekee aliyekuwa
amejiegesha katika
godoro lake aliloliweka juu ya
turubai kubwa
lilitandikwa chumbani humo.
Kilichomfanya awe
macho mpaka muda ule alikuwa
akihangaika
kuchimbua pale kilipochimbiwa
kile kibuyu cha
maangamizi cha hayati
Masonganya,
kilichomchelewesha na kumkawiza
kukifikia ni hofu
ya kushitukiwa na nduguze ambao
baadhi yao
walikuwa wamelala humohumo
chumbani.
Hakutaka kabisa kuonekana.
Aliendelea kuchimbua taratibu na
kwa umakini wa
hali ya juu mpaka alipokifikia kile
kibuyu. Alipofikia
hapo akaacha kidogo zoezi hilo.
Akaingiza mkono
katika mfuko wa koti lake akatoa
majani ya
‘Vibumbasi’ akayasambaza vizuri
mikononi mwake
na kisha akaingiza mkono katika
kijishimo
alichokichimba na kukitoa kile
kibuyu.
Alipohitimisha tu zoezi lile, haraka
akatoka mle
chumbani akiwa na kibuyu chake
mkononi,
akaelekea na mpaka uani kisha
akaingia chooni
ambako alianza kufanya kitu
kikubwa kuliko umri
wake.
***MNh! Kitu gani hicho?
kwenda kumsalimu Bi
Masonganya alikwenda japo
hakukaa muda mrefu,
na siku zote alizokaa huko muda
mwingi aliutumia
akiwa ndani tu na mama yake, kitu
kilichowazidish
ia hofu nduguze kuwa atakuwa
anarithishwa
uchawi tu…na hicho ndicho
kilichozidi kupalilia
uadui wao.
***
Sasa leo amekuja tena Kibondo
kwakuwa mzee
Mtandi amefariki, na makubaliano
ni kwamba
angezikiwa palepale Kibondo
hivyo ni lazima aje
amzike baba yake mdogo
(mjomba).
“Ilumbi…” Aliita Bi Chakupewa
ambaye ni dada
yake na mama Kaguba, kisha
akaaendelea kuongea
kabla hajaitikiwa. “…Nadhani we’
si’ mgeni wa
mambo ya humu ndani, sasa
imekuaje tena
unatuletea hiki kituko?”
Alihitimisha Chakupewa
huku akimsonta Nyembo kwa
kidole chake.
Wanafamilia wote wakajikuta
wametazamana.
“Ulitaka asije kumzika mzazi wake
aliyemlea kisa
magomvi yenu?” alijibu Ilumbi na
kukazia tena “…
nachojua mimi, Nyembo ni ndugu
yetu fullstop…
kama kuna makosa waliwahi
kufanya wazazi wake
basi sisi hayatuhusu kama
yasivyomuhusu yeye.”
“Nakwambia hivi Ilumbi kama
udugu leo utauzika,
ila huyu Nyembo humu ndani
hakai labda
mkamtafutie sehemu nyingine ya
kulala. Angalia
huko alipoingia tu majirani
wakaanza
kumzungumza, mnasababisha
familia yetu
ionekane ya kichawi, hivi tutaishi
vipi na jamii yetu
jamani? Alibwata mama Kaguba.
“Sasa unatutishia kuvunja udugu?
Aliyekuambia si’
tunashida na udugu nani? Udugu
wenyewe huu wa
nazi kukutania pakachani, acha
upumbavu wako
wewe…” Safari hii alibwata
Lubambi, mtoto wa
kiume marehemu. “…Iko hivi,
aliyekufa ni baba yetu
sisi japonanyi ni mjomba wenu.
Sasa kama
hamtaki tushiriki sote pamoja na
Nyembo wala
tusibabaishane tunaichukua maiti
na kwenda
kuizikia kwetu, kama ni uwezo
nasi’ pia tuko fiti!”
Majibu hayo ya Lubambi nd’o
kama yalichochea
vurugu, ikawa ni majibizano,
majigambo na kila
aina ya upuuzi mpaka baadaye
kabisa
walipouingilia ugomvi ule wazee
wengine kutoka
katika familia hiyo ambapo hekma
na busara zao
ziliwatuliza ndugu wale na
kuwapatanisha. Maneno
ya waze yaliwaingia sana akina
mama Kaguba
hasa pale waliposisitizwa kuwa
Nyembo hakuwa
mwenye hatia kamwe kwa kosa
lililofanywa na
wazazi huko nyuma, wakalainika
ukizingatia hata
ile hofu yao kuwa Nyembo alikuwa
akikabidhiwa
uchawi na marehemu Masonganya
ilikwishapotea
baada ya kupata ithibati mpya
kuwa kama ni
uchawi alikabidhiwa mtoto wao
wenyewe, Kaguba.
Kufikia hapo kidogo amani
ikarejea na shughuli za
maziko zikaendelea kupangiliwa.
Suluhu yao ikawa ni pigo kwa
kambi ya akina
Kaguba waliokuwa wakiombea
mzozo ule uwe
mkubwa ili maiti iondolewe mle
ndani ili Kaguba
apate nafasi ya kuingia kule
ufuoni akakichimbue
kile kibuyu kinachomzuia kutoka
nje ya nyumba
kwenda kuwanga.
Saa kumi Alasiri baada ya
kufanyika visomo vya
dua maalum na sala kwa maiti,
hatimaye jeneza la
mzee Mtandi likabebwa na
wanaume na kuelekea
makaburini kuzika. Wanawake
walibaki nyumbani
wakilisindikiza kwa macho jeneza
lile. Hakika kifo
kile kiliwachoma na kuwaingia
sana.
Hiyo nd’o ikawa safari ya mwisho
ya bwana
Mtandi.
***
Saa tisa usiku, kundi kubwa la
wachawi
likiongozwa na Binti Sambayu
lilikusanyika kwa
kulizunguka kaburi alilozikwa
hayati Mtandi,
wakiwa watupu kama
walivyozaliwa. Ngoma na
nyimbo za kichawi zilirindima
kisawasawa, kila
mmoja alijiachia atakavyo bila ya
kujali ni athari
gani atakayoacha kutokana na
kubinuka akiwa
mtupu mbele ya wenziye ambao
wengine ni wa
jinsia tofauti na yake. Mbali ya
kuserebuka nyimbo
hizo pia kulikuwa na vinywaji na
vitoweo murua,
Damu na nyama za watu, pamoja
na pombe kali
vilihusika.
“Jamani mida inayoyoma, sasa
tutekeleze
kilichotuleta ili tutawanyike…karibu
mkuu!”
Aliongea Bi mkubwa mmoja
ambaye alitapakaa
vumbi kali ya makaburini kutokana
mtindo wa
kugaagaa wakati alipokuwa
akiserebuka.
Alipomaliza tu kuongea, wachawi
wote wakaketi
chini na hapo ndipo akasimama
Binti Sambayu na
kuanza kuongea.
“Bila kupoteza muda napenda
kuwapa salamu
kutoka kwa mkuu wetu Kaguba
anasema yuko
pamoja nasi na kwamba siku si
nyingi atajumuika
nasi na kutatua matatizo yetu
yote…” kufikia hapo
vigeregere vikazimama, kisha
akaendelea. “…
pamoja na hayo ni kwamba
tulikuwa tuwe na
mazoezi makubwa mawili hapa
leo. Moja ni
kumkata rasmi ulimi Nyanzala ili
aingizwe katika
daftari letu la kudumu la misukule,
na pili ni
kumfukua bwana Mtandi na
kumzindika kabla ya
siku yake ya kukatwa ulimi. Ila
kutokana na
maagizo toka kwa mkuu Kaguba
ni kwamba
hatutomkata ulimi leo Nyanzala
mpaka
atakapokuja mwenyewe hivyo
tutabakiwa na suala
hili moja tu la kumfukua huyu
bwana mjuaji!”
Alipomaliza tu kusema maneno
hayo binti
Sambayumara kijana mmoja
aliyekuwa
amejihifadhi kichawi chini ya
miembe akaibukia
akiwa amemshika mkono Nyanzala
na
kumkabidhisha kwa wachawi wale.
Nyanzala
aliyekuwa amevishwa kijigauni
chepesi huku
miguuni akiwa peku kama bata,
alikuwa
akitetemeka kama mtoto mwenye
homa.
Baada ya Nyanzala kuwekwa chini,
sasa
wakalisogelea Kaburi la hayati
bwana Mtandi na
kuanza kubinuka tena mahepe
yao. Dakika chache
tu Binti Sambayu akakipiga kwa
nguvu chungu
cheusi juu ya kaburi lile na
hapohapo kaburi
likapasuka na kuachia kijinjia
chembamba.
Macho ya Nyanzala aliyekuwa
ameketi jirani
kabisa, yalishuhudia kupitia katika
ufa huo
uliopasuka hapo kaburini
akichomoza maiti
aliyevaa sanda nyeupe. Kutokana
na upenyo huo
finyu hapo kaburini, maiti ilikuwa
ikichomoza kwa
tabu sana mpaka takribani dakika
tano maiti ikawa
juu ya kaburi.
Muda wote huo wale wachawi
walikuwa
wakiendelea kuimba kwa shangwe
huku wakicheza
na kufurahia tukio hilo. Maiti ile
haikuwa maiti ki-
ukweli maana ilipomwagiwa dawa
fulani kutoka
katika kibuyu kidogo cha binti
Sambayu hapohapo
ikainuka. Alikuwa ni Mzee Mtandi.
Mara macho ya Nyanzala
yakakutana na yale ya
mjomba’ake mzee Mtandi. japo
wote walikuwa
kama wapumbavu tu kwa jinsi
walivyopumbazwa
akili na madawa. Nyanzala
akaanza kulia japo bila
ya kutoa sauti.
Wakati mzee Mtandi akiwa
amesimama kama
mlevi wa dawa za kulevya,
akashituliwa kwa
kumwagiwa maji ya baridi
yakifuatiwa na mijeredi
ya nguvu! Akashituka kutokana na
maumivu yale,
na sasa akili zikawa zimeanza
kumreja…hicho nd’o
walichokuwa wakikitaka wale
Wachawi.
Kumzindua!
Kwa kawaida Wachawi wale
wakishamfufua mtu,
humfanyia madawa yao pamoja na
kumshitua kwa
maji ya baridi na mijeredi ili
kuiamsha akili yake
ambayo ilidorora mchana kutwa
tangu afukiwe
kaburini na ndugu zake wakiamini
amekwishakufa,
kisha zoezi linalofuata ni
kumfanyisha mazoezi.
Huwa wao wanasimama na
msukule wao karibu
na kaburi alilofukuliwa kisha
wanamuamuru
akimbie mpaka sehemu
waliyoweka alama yao
halafu anarejea tena mpaka walipo
wao…hufanya
hivyo kwa takribani mizunguko
mitano kabla
hawajamzuia na kuondoka naye
mpaka nyumbani
atakapofikishiwa kwa shughuli
nyinge zaidi. Hivyo
na mzee Mtandi naye akaamriwa
aanze kukimbia
kama ilivyo desturi!
***
Katika usiku huo mkubwa wakati
wachawi
wakifanya vitu vyao kule
makaburini, huku
nyumbani nako watu walikuwa
wamelala isipokuwa
Nyembo pekee aliyekuwa
amejiegesha katika
godoro lake aliloliweka juu ya
turubai kubwa
lilitandikwa chumbani humo.
Kilichomfanya awe
macho mpaka muda ule alikuwa
akihangaika
kuchimbua pale kilipochimbiwa
kile kibuyu cha
maangamizi cha hayati
Masonganya,
kilichomchelewesha na kumkawiza
kukifikia ni hofu
ya kushitukiwa na nduguze ambao
baadhi yao
walikuwa wamelala humohumo
chumbani.
Hakutaka kabisa kuonekana.
Aliendelea kuchimbua taratibu na
kwa umakini wa
hali ya juu mpaka alipokifikia kile
kibuyu. Alipofikia
hapo akaacha kidogo zoezi hilo.
Akaingiza mkono
katika mfuko wa koti lake akatoa
majani ya
‘Vibumbasi’ akayasambaza vizuri
mikononi mwake
na kisha akaingiza mkono katika
kijishimo
alichokichimba na kukitoa kile
kibuyu.
Alipohitimisha tu zoezi lile, haraka
akatoka mle
chumbani akiwa na kibuyu chake
mkononi,
akaelekea na mpaka uani kisha
akaingia chooni
ambako alianza kufanya kitu
kikubwa kuliko umri
wake.
***MNh! Kitu gani hicho?