Post by Admin on May 31, 2015 21:38:01 GMT
Alipohitimisha tu zoezi lile, haraka
akatoka mle
chumbani akiwa na kibuyu chake
mkononi,
akaelekea na mpaka uani kisha
akaingia chooni
ambako alianza kufanya kitu
kikubwa kuliko umri
wake.
Hatua zote anazozipitia Nyembo,
tangu kukifukua
kibuyu, na kukibeba tena kwa
ustadi wa kujikinga
na majani ya vibumbasi na
kukimbilia nacho
chooni alizipata kupitia maelezo
yaliyoandikwa na
bwana Mtandi katika kijitabu
chake cha
kumbukumbu(Diary). Mchana
kutwa wakati ndugu
wakishughulika na mambo
makubwa zaidi
kimuonekano hapo msibani,
Nyembo alikuwa
makini akisoma kitabu hicho cha
kumbukumbu
ambapo mbali ya mambo mengine
ikiwemo
madeni, ndipo akakumbana na siri
nzito ambayo
mzee Mtandi aliisikia kutoka kwa
Kaguba na Binti
Sambayu na kuiandika humo kabla
hajakutwa na
ile hali ya sintofahamu wakati
akiwasimulia akina
Kungurume bahati na majani
hayoya vibumbasi
aliyakuta humo kwenye begi.
Tabia hii ya
kujisomeasomea taarifa muhimu,
Nyembo
alijizoesha kupitia huko shuleni
alikokuwa anasoma
na pia alijifunza kupitia kwa mzee
Mtandi.
“Akkhhhhh….OHHHHKH KHAAA
NAKUFAAAAAAAAA.
” Sauti ya Kaguba ilivuma kwa kasi
kutokea
chumbani alikolala. Ilikuwa ni
kama mashetani
fulani yaliyompanda kichwani. bila
shaka ni
kutokana na kitendo kilichofanywa
na Nyembo
kuingia chooni na kile Kibuyu.
Watu wote
wakaamka kwa mshituko.
“HAAGHHAAAAAAA
HATARIIIIIIIIII…CHOOOONI.
NIFUNGULIENIIII NIKAUUUE.”
Kaguba aliendelea
kulalama kwa hasira kiasi cha
kuwafanya wakubwa
wote waingiwe na hofu na kihoro
cha kujua nini
kipo huko chooni.
Wote waliamka na kujumuika
pamoja isipokuwa
Nyembo tu nd’o hakuonekana
alikokwenda, hofu
mpya ikawakabili.
****
Kule makaburini nako mambo
yalikuwa yakiendelea
kama yalivyopangwa, tayari mzee
Mtandi
alikwishaanza kufanyishwa
mazoezi na tayari
alikuwa amekimbia karibu
mzunguko wa pili.
Wakati mzee Mtandi akikimbia
mzunguko wa tatu,
wachawi walishangaa ghafla
lilipotokea jambo
fulani lisilo la kawaida, pale
ambapo mzee Mtandi
badala aishie kwenye uzio wa
makaburi ambako
ndiko alipokuwa amewekewa
alama ya kuishia
katika mizunguko yote
anayokimbia, na alifanya
hivyo tangu mwanzo, sasa
alipitiliza kwa kasi ya
ajabu mpaka nje kabisa ya uga wa
makaburi
ambako kuna barabara inakatiza.
Kama haitoshi
mzee Mtandi akiwa katika kasi ya
ajabu
alitokomea gizani kabisa.
Wachawi wote wakajua
kilichotokea kuwa mzee
Saadallah amewakimbia, haikuwa
kitu cha kawaida
kwa msukule wao ambaye
wameshammwagia
dawa na kumpunguza akili
atoweke kwa mtindo
ule. Bila shaka kuna nguvu ya
ziada imetumika!
“Haiwezekani…kuna namna hapa.
MKIMBIZENIIIII,”
Alliongea kwa mshituko na
mashaka Binti
Sambayu.
“Mkuu ungemuangilia kwenye kioo
chako kwanza
maana sisi hatumuoni kwa upeo
wetu!” alijibu
kijana yule aliyemleta Nyanzala.
Wakati mjadala
ukiendelea ndipo ghafla tena
ilipowadhihirikia hali
mbaya zaidi kwao, ilikwa ni kama
vile wamewekwa
ndani ya boksi halafu mara
wabinuliwe juu chini,
mara kulia na kushoto.
Waliyumbishwa bila
kujielewa mpaka wakawa kama
walevi au
wanaojisikia ‘kizunguzungu’ huku
wengine
wakicheua nyama na damu za
watu walizokula na
kunywa. Nyanzala naye kama
aliyezinduliwa
kutoka usingizi akajikuta akili za
kibinaadamu
zikimrejea naye akatimua mbio
kali kama mjomba
wake, hakuna mchawi hata mmoja
aliyeweza
kumuangalia Nyamizi akitoweka
kwa jinsi
walivyokuwa wakiona maluweluwe
ya kubinuliwa
bila kujielewa.
***
“We’ Kaguba una nini lakini?”
Alisaili Bi
Chakupewa.
“Mamaaa na-ku-faa…nasikia
kizunguzungu
mamaaa!” Sasa Kaguba alianza
kuongea, na mara
akaanza kutapika. Kutokana na
vimbwanga vya
mtoto huyu kila mmoja akajua
labda pengine
alikuwa akijaribu kufanya ‘mchezo’
ndipo
akakutana na dawa zilizozindikwa.
“Ulikuwa unafanya nini lakini we’
mtoto?” Mama
Kaguba naye alihoji kwa woga.
“Mama nakufaaaa aakkkhh…
mjomba Nyembo
anatuuwa.” Aliendelea kulalama
Kaguba.
Baada ya Kaguba kumtaja
Nyembo, ndipo kila mtu
akawa kama aliyefungukiwa na
kitu kichwani kwani
muda wote wa tukio hilo, Nyembo
hakuwemo mle
ndani.
“Jamani kwani Nyembo yuko
wapi?” Alisaili Ilumbi.
“Tuwaulizeni ninyi mliyelala naye
huko ufuoni!”
alijibu Kungurume.
“YU-KO CHO-O-NI ANATAKA
KUNIMALIZAAA
AKKHH Uhuaakh!” Kaguba alijibu
haraka huku
akitoa milio ya ajabu isiyoeleweka
kabisa. Haraka
wote wakatoka mpaka uani
ambako giza nene
lililokuwa limetanda. Wakawasha
taa na kuelekea
mpaka huko chooni.
Hamad!
Wakakamkuta Nyembo akiwa
amesimama katikati
ya choo huku mikono yake miwili
ikiwa imeshika
kile kibuyu kilichozungushiwa
shanga nyingi kwa
juu huku kwa ndani kukiwa na vitu
vya ajabu na
kuogofya!
“Ilumbi mnaonaa? Mnaonaa? Si’
tuliwaambia sisi
kuwa huyu Nyembo si mtu mzuri
mkawa
mnamtetea!?” Alibwata kwa
ghadhabu Mama
Kaguba. Akina Ilumbi nao
wakajikuta wakiduwaa tu
na kumkodolea macho Nyembo
ambaye alikuwa
akikizungusha kile kibuyu chini
juu, juu chini, mara
kulia. Mara kushoto. Hakuna
aliyeelewa
akifanyacho zaidi ya kumuona
kuwa ni mchawi tu.
“Nyembo unafanya nini huku
chooni saa hizi na
hicho kibuyu?” Lubambi alimsaili
Nyembo kwa
kihoro na woga.
“Unamuuliza anafanya nini wakati
unamwona
anawanga kabisa hapo, au unataka
akuambie
anasali?” Alidakia Kungurume.
“Embu tulieni ninyi msiwe kama
majuha…ningekuw
a nawanga sasa inakuaje huyo
mtoto wenu
ambaye ndiye mkubwa wa
wachawi apige kelele
kiasi hicho?” Alijibu kwa kujiamini
Nyembo kiasi
cha kuwafanya wote mle chooni
wazidi kubutwaika.
Baada ya hapo Nyembo
akaendelea kukizungusha
kile Kibuyu chake, na hapohapo
wakaanza
kumsikia Kaguba akilia kwa sauti
huku
akiweweseka kama awali. Kufikia
hapo sasa mama
Kaguba chango la uzazi
likamshituka akajikuta
uzalendo ukimshinda akamvaa
Nyembo ili
amnyang’anye hicho kibuyu.
Wakaenda mweleka
mpaka chini, ikawa ni patashika ya
haja!
Wakati vurugu hiyo ikiendelea
mara ghafla
kikawakumba kioja kikubwa na
cha nguvu kuliko
hicho cha kumkuta Nyembo
akihangaika na Kibuyu
huko chooni. Wakati baadhi
wakiwa chooni, kuna
wengine walibaki wamesimama
uani. Sasa hao
nd’o walianzisha vurugu na kelele
zilizowatoa wote
kule chooni.
“UWIIIIIII JAMANIII BABU MTANDI
HUYOOO,”
Alipiga kelele Kilanga, mtoto
mdogo wa kike wa
Kungurume, waliokuwa uani hapo
wote
wakamshuhudia mzee Mtandi
akiingia ndani kwa
kasi. Kusikia kuwa mzee Mtandi
akitajwa
kuonekana, kikazuka kimuhemuhe
cha hali ya juu.
Wakasambaana wote na kukimbilia
ndani ambako
mzee Mtandi naye akaingia. Japo
Nyembo
alitegemea kutokea kwa jambo
zito kutokana na
maelezo yaliyoandikwa kitaalamu
kwenye kile
kitabu cha kumbukumbu lakini
naye kihoro
kikamkumba, akajikuta akitimka na
kuelekea ndani
huku kile kibuyu akikiacha kule
chooni kilipoanguka
tangu alipokumbwa na mama
Kaguba kilimponyoka
na kuanguka chini.
“WEEE LUBAMBI USIINGIE HUKO,
MJOMBA ND’O
AMEINGIA HUKO!” Chakupewa
alimhadhari
Lubambi asiingie chumbani
ambako mzee Mtandi
ameingia. Japo Lubambi alitaka
kumuona kama ni
kweli baba yake lakini hofu
iliyomvaa ilimsukuma
na kujikuta akikimbilia kule
waliposimama
nduguze. Haikuwa jambo jepesi
kumwona mzazi
wako aliyekufa na ukahakikisha
mmemzika halafu
ghafla atokee tena. Si rahisi hata
kidogo.
Mara tu baada ya Nyembo naye
kuingia ndani,
hakutaka kupoteza muda,
akawasogelea ndugu
zake ambao walijikuta wakipiga
kelele za
kumuogopa wakimwona tu kama
mchawi.
“Acheni upuuzi ninyi, nilichokuwa
nakifanya huko
chooni nd’o kimemrejesha mzee
Mtandi, sikutaka
kuwaambia mapema kwakuwa
tungeharibu
mpango mzima na yangetokea
kama yaliyotokea
wakati mzee Mtandi alipokuwa
akiwasimulia ninyi
alichokigundua…” Aliongea
Nyembo kwa kujiamini
kama ilivyo kawaida yake japo
ndiyo kabisa alizidi
kuwachanganya nduguze ambao
hawakumwelewa
kwanini alijua kuwa mzee Mtandi
aliyekufa na
kuzikwa kuwa angerejea? Na wapi
alikipata kile
kibuyu kilichofanya Kaguba awe
anapiga kelele.
Akaendelea Nyembo. “…haya
tujivisheni ujasiri,
tuingie chumbani tukajaribu
kumtuliza mzee
Mtandi ili tuzungumze naye na
endap…” Kabla
Nyembo hajafikisha neno lake
mwisho kikazuka
kizazaa kipya na cha kuogofya
zaidi.
Mlango wao wa kutokea uani
ulisukumwa kwa
nguvu, na hapohapo wote
wakamshuhudia
msichana akiingia kwa kasi kama
anayekimbizwa.
Wote kwa pamoja walimshuhudia
na kumfahamu,
alikuwa ni Nyanzala.
“UWIIIIIIII JAMANI
TUNAKUFAAA..NYANZALAAA!”
Alipiga kelele za woga mama
Kaguba, huku
akisaidiwa na nduguze wengine
akiwemo Ilumbi,
Chakupewa, na wajukuu. Hakika
ilikuwa ni siku ya
ajabu sana kwao, hakuna
aliyeelewa kama
anoyaona kweli matukio yale ya
ajabu au anaota.
Nyanzala naye akajikuta
akiwaogopa nduguze
waliokuwa wametaharuki kwa
kupiga makelele
huku wakiparamia meza na viti
vilivyokuwapo
sebule hapo. Akajikuta akikimbilia
chumbani
ambako ndiko alikokimbilia mzee
Mtandi!
***Makubwa!
ITAENDELEA
akatoka mle
chumbani akiwa na kibuyu chake
mkononi,
akaelekea na mpaka uani kisha
akaingia chooni
ambako alianza kufanya kitu
kikubwa kuliko umri
wake.
Hatua zote anazozipitia Nyembo,
tangu kukifukua
kibuyu, na kukibeba tena kwa
ustadi wa kujikinga
na majani ya vibumbasi na
kukimbilia nacho
chooni alizipata kupitia maelezo
yaliyoandikwa na
bwana Mtandi katika kijitabu
chake cha
kumbukumbu(Diary). Mchana
kutwa wakati ndugu
wakishughulika na mambo
makubwa zaidi
kimuonekano hapo msibani,
Nyembo alikuwa
makini akisoma kitabu hicho cha
kumbukumbu
ambapo mbali ya mambo mengine
ikiwemo
madeni, ndipo akakumbana na siri
nzito ambayo
mzee Mtandi aliisikia kutoka kwa
Kaguba na Binti
Sambayu na kuiandika humo kabla
hajakutwa na
ile hali ya sintofahamu wakati
akiwasimulia akina
Kungurume bahati na majani
hayoya vibumbasi
aliyakuta humo kwenye begi.
Tabia hii ya
kujisomeasomea taarifa muhimu,
Nyembo
alijizoesha kupitia huko shuleni
alikokuwa anasoma
na pia alijifunza kupitia kwa mzee
Mtandi.
“Akkhhhhh….OHHHHKH KHAAA
NAKUFAAAAAAAAA.
” Sauti ya Kaguba ilivuma kwa kasi
kutokea
chumbani alikolala. Ilikuwa ni
kama mashetani
fulani yaliyompanda kichwani. bila
shaka ni
kutokana na kitendo kilichofanywa
na Nyembo
kuingia chooni na kile Kibuyu.
Watu wote
wakaamka kwa mshituko.
“HAAGHHAAAAAAA
HATARIIIIIIIIII…CHOOOONI.
NIFUNGULIENIIII NIKAUUUE.”
Kaguba aliendelea
kulalama kwa hasira kiasi cha
kuwafanya wakubwa
wote waingiwe na hofu na kihoro
cha kujua nini
kipo huko chooni.
Wote waliamka na kujumuika
pamoja isipokuwa
Nyembo tu nd’o hakuonekana
alikokwenda, hofu
mpya ikawakabili.
****
Kule makaburini nako mambo
yalikuwa yakiendelea
kama yalivyopangwa, tayari mzee
Mtandi
alikwishaanza kufanyishwa
mazoezi na tayari
alikuwa amekimbia karibu
mzunguko wa pili.
Wakati mzee Mtandi akikimbia
mzunguko wa tatu,
wachawi walishangaa ghafla
lilipotokea jambo
fulani lisilo la kawaida, pale
ambapo mzee Mtandi
badala aishie kwenye uzio wa
makaburi ambako
ndiko alipokuwa amewekewa
alama ya kuishia
katika mizunguko yote
anayokimbia, na alifanya
hivyo tangu mwanzo, sasa
alipitiliza kwa kasi ya
ajabu mpaka nje kabisa ya uga wa
makaburi
ambako kuna barabara inakatiza.
Kama haitoshi
mzee Mtandi akiwa katika kasi ya
ajabu
alitokomea gizani kabisa.
Wachawi wote wakajua
kilichotokea kuwa mzee
Saadallah amewakimbia, haikuwa
kitu cha kawaida
kwa msukule wao ambaye
wameshammwagia
dawa na kumpunguza akili
atoweke kwa mtindo
ule. Bila shaka kuna nguvu ya
ziada imetumika!
“Haiwezekani…kuna namna hapa.
MKIMBIZENIIIII,”
Alliongea kwa mshituko na
mashaka Binti
Sambayu.
“Mkuu ungemuangilia kwenye kioo
chako kwanza
maana sisi hatumuoni kwa upeo
wetu!” alijibu
kijana yule aliyemleta Nyanzala.
Wakati mjadala
ukiendelea ndipo ghafla tena
ilipowadhihirikia hali
mbaya zaidi kwao, ilikwa ni kama
vile wamewekwa
ndani ya boksi halafu mara
wabinuliwe juu chini,
mara kulia na kushoto.
Waliyumbishwa bila
kujielewa mpaka wakawa kama
walevi au
wanaojisikia ‘kizunguzungu’ huku
wengine
wakicheua nyama na damu za
watu walizokula na
kunywa. Nyanzala naye kama
aliyezinduliwa
kutoka usingizi akajikuta akili za
kibinaadamu
zikimrejea naye akatimua mbio
kali kama mjomba
wake, hakuna mchawi hata mmoja
aliyeweza
kumuangalia Nyamizi akitoweka
kwa jinsi
walivyokuwa wakiona maluweluwe
ya kubinuliwa
bila kujielewa.
***
“We’ Kaguba una nini lakini?”
Alisaili Bi
Chakupewa.
“Mamaaa na-ku-faa…nasikia
kizunguzungu
mamaaa!” Sasa Kaguba alianza
kuongea, na mara
akaanza kutapika. Kutokana na
vimbwanga vya
mtoto huyu kila mmoja akajua
labda pengine
alikuwa akijaribu kufanya ‘mchezo’
ndipo
akakutana na dawa zilizozindikwa.
“Ulikuwa unafanya nini lakini we’
mtoto?” Mama
Kaguba naye alihoji kwa woga.
“Mama nakufaaaa aakkkhh…
mjomba Nyembo
anatuuwa.” Aliendelea kulalama
Kaguba.
Baada ya Kaguba kumtaja
Nyembo, ndipo kila mtu
akawa kama aliyefungukiwa na
kitu kichwani kwani
muda wote wa tukio hilo, Nyembo
hakuwemo mle
ndani.
“Jamani kwani Nyembo yuko
wapi?” Alisaili Ilumbi.
“Tuwaulizeni ninyi mliyelala naye
huko ufuoni!”
alijibu Kungurume.
“YU-KO CHO-O-NI ANATAKA
KUNIMALIZAAA
AKKHH Uhuaakh!” Kaguba alijibu
haraka huku
akitoa milio ya ajabu isiyoeleweka
kabisa. Haraka
wote wakatoka mpaka uani
ambako giza nene
lililokuwa limetanda. Wakawasha
taa na kuelekea
mpaka huko chooni.
Hamad!
Wakakamkuta Nyembo akiwa
amesimama katikati
ya choo huku mikono yake miwili
ikiwa imeshika
kile kibuyu kilichozungushiwa
shanga nyingi kwa
juu huku kwa ndani kukiwa na vitu
vya ajabu na
kuogofya!
“Ilumbi mnaonaa? Mnaonaa? Si’
tuliwaambia sisi
kuwa huyu Nyembo si mtu mzuri
mkawa
mnamtetea!?” Alibwata kwa
ghadhabu Mama
Kaguba. Akina Ilumbi nao
wakajikuta wakiduwaa tu
na kumkodolea macho Nyembo
ambaye alikuwa
akikizungusha kile kibuyu chini
juu, juu chini, mara
kulia. Mara kushoto. Hakuna
aliyeelewa
akifanyacho zaidi ya kumuona
kuwa ni mchawi tu.
“Nyembo unafanya nini huku
chooni saa hizi na
hicho kibuyu?” Lubambi alimsaili
Nyembo kwa
kihoro na woga.
“Unamuuliza anafanya nini wakati
unamwona
anawanga kabisa hapo, au unataka
akuambie
anasali?” Alidakia Kungurume.
“Embu tulieni ninyi msiwe kama
majuha…ningekuw
a nawanga sasa inakuaje huyo
mtoto wenu
ambaye ndiye mkubwa wa
wachawi apige kelele
kiasi hicho?” Alijibu kwa kujiamini
Nyembo kiasi
cha kuwafanya wote mle chooni
wazidi kubutwaika.
Baada ya hapo Nyembo
akaendelea kukizungusha
kile Kibuyu chake, na hapohapo
wakaanza
kumsikia Kaguba akilia kwa sauti
huku
akiweweseka kama awali. Kufikia
hapo sasa mama
Kaguba chango la uzazi
likamshituka akajikuta
uzalendo ukimshinda akamvaa
Nyembo ili
amnyang’anye hicho kibuyu.
Wakaenda mweleka
mpaka chini, ikawa ni patashika ya
haja!
Wakati vurugu hiyo ikiendelea
mara ghafla
kikawakumba kioja kikubwa na
cha nguvu kuliko
hicho cha kumkuta Nyembo
akihangaika na Kibuyu
huko chooni. Wakati baadhi
wakiwa chooni, kuna
wengine walibaki wamesimama
uani. Sasa hao
nd’o walianzisha vurugu na kelele
zilizowatoa wote
kule chooni.
“UWIIIIIII JAMANIII BABU MTANDI
HUYOOO,”
Alipiga kelele Kilanga, mtoto
mdogo wa kike wa
Kungurume, waliokuwa uani hapo
wote
wakamshuhudia mzee Mtandi
akiingia ndani kwa
kasi. Kusikia kuwa mzee Mtandi
akitajwa
kuonekana, kikazuka kimuhemuhe
cha hali ya juu.
Wakasambaana wote na kukimbilia
ndani ambako
mzee Mtandi naye akaingia. Japo
Nyembo
alitegemea kutokea kwa jambo
zito kutokana na
maelezo yaliyoandikwa kitaalamu
kwenye kile
kitabu cha kumbukumbu lakini
naye kihoro
kikamkumba, akajikuta akitimka na
kuelekea ndani
huku kile kibuyu akikiacha kule
chooni kilipoanguka
tangu alipokumbwa na mama
Kaguba kilimponyoka
na kuanguka chini.
“WEEE LUBAMBI USIINGIE HUKO,
MJOMBA ND’O
AMEINGIA HUKO!” Chakupewa
alimhadhari
Lubambi asiingie chumbani
ambako mzee Mtandi
ameingia. Japo Lubambi alitaka
kumuona kama ni
kweli baba yake lakini hofu
iliyomvaa ilimsukuma
na kujikuta akikimbilia kule
waliposimama
nduguze. Haikuwa jambo jepesi
kumwona mzazi
wako aliyekufa na ukahakikisha
mmemzika halafu
ghafla atokee tena. Si rahisi hata
kidogo.
Mara tu baada ya Nyembo naye
kuingia ndani,
hakutaka kupoteza muda,
akawasogelea ndugu
zake ambao walijikuta wakipiga
kelele za
kumuogopa wakimwona tu kama
mchawi.
“Acheni upuuzi ninyi, nilichokuwa
nakifanya huko
chooni nd’o kimemrejesha mzee
Mtandi, sikutaka
kuwaambia mapema kwakuwa
tungeharibu
mpango mzima na yangetokea
kama yaliyotokea
wakati mzee Mtandi alipokuwa
akiwasimulia ninyi
alichokigundua…” Aliongea
Nyembo kwa kujiamini
kama ilivyo kawaida yake japo
ndiyo kabisa alizidi
kuwachanganya nduguze ambao
hawakumwelewa
kwanini alijua kuwa mzee Mtandi
aliyekufa na
kuzikwa kuwa angerejea? Na wapi
alikipata kile
kibuyu kilichofanya Kaguba awe
anapiga kelele.
Akaendelea Nyembo. “…haya
tujivisheni ujasiri,
tuingie chumbani tukajaribu
kumtuliza mzee
Mtandi ili tuzungumze naye na
endap…” Kabla
Nyembo hajafikisha neno lake
mwisho kikazuka
kizazaa kipya na cha kuogofya
zaidi.
Mlango wao wa kutokea uani
ulisukumwa kwa
nguvu, na hapohapo wote
wakamshuhudia
msichana akiingia kwa kasi kama
anayekimbizwa.
Wote kwa pamoja walimshuhudia
na kumfahamu,
alikuwa ni Nyanzala.
“UWIIIIIIII JAMANI
TUNAKUFAAA..NYANZALAAA!”
Alipiga kelele za woga mama
Kaguba, huku
akisaidiwa na nduguze wengine
akiwemo Ilumbi,
Chakupewa, na wajukuu. Hakika
ilikuwa ni siku ya
ajabu sana kwao, hakuna
aliyeelewa kama
anoyaona kweli matukio yale ya
ajabu au anaota.
Nyanzala naye akajikuta
akiwaogopa nduguze
waliokuwa wametaharuki kwa
kupiga makelele
huku wakiparamia meza na viti
vilivyokuwapo
sebule hapo. Akajikuta akikimbilia
chumbani
ambako ndiko alikokimbilia mzee
Mtandi!
***Makubwa!
ITAENDELEA