Post by Admin on Jun 7, 2015 4:02:16 GMT
Nyanzala naye akajikuta akiwaogopa nduguze
waliokuwa wametaharuki kwa kupiga makelele
huku wakiparamia meza na viti vilivyokuwapo
sebule hapo. Akajikuta akikimbilia chumbani
ambako ndiko alikokimbilia mzee Mtandi!
Kelele kali za akina mama Kaguba ziliweza kuvuma
sana kutokana na hali ya utulivu wa usiku mnene
kama ule kiasi cha kuwaamsha majirani ambao
baadhi wenye ujasiri walitoka na kuja kujumuika
nao kujua kilichotokea huku wale wenzangu na
mimi wakiishia kuchungulia madirishani mwao tu
kama njiwa manga. Majirani walizidi kumiminika,
na hapo ndipo walipokutana na kioja kile cha
mwaka, kwamba watu wawili kutoka katika familia
moja waliokufa na kuzikwa kabisa eti leo
wamefufuka na kurudi nyumbani, tena kwa
kufuatana.
Ilikuwa ni mtafutano.
Wakati hayo yakiendelea, Kaguba alikuwa ametulia
kimya, macho yakiwa yamembadilika na kuwa
mithili ya Paka. Alikuwa akiona mbali sana,
aliwaona wachawi wenzake wakiwa wametaharuki
ovyo baada ya kuhangaishwa sana kutokana na
mchezo uliokuwa ukifanywa na Nyembo katika kile
kibuyu. Sasa walikuwa wamepata ahueni tangu
kibuyu kilipoachwa peke yake chooni, wakawa
kama mazezeta hivi wasioelewa kilichowakumba,
na baada ya Binti Sambayu kupiga ramli yake
kupitia kibuyu akagundua yaliyowakuta,
akawaamuru wafuasi wake wote watawanyike,
wakawa wanatimka mbio kuelekea majumbani
huku yeye(Binti Sambayu) akifanza maarifa.
‘Kibuyu kipo chooni, kimbia haraka kakichukue na
umuangamize huyo Nyembo haraka, halafu
uwapoteze hao akina Nyanzala kabla hawajasema
chochote, nasi tuko njiani tunakuja hukohuko
vinginevyo tutakufa sote.’ Sauti ya Binti Sambayu
aliyekuwa akikimbia ilimjia waziwazi kichwani
Kaguba ikimtaka kukiwahi kibuyu kule chooni.
Hakuna aliyeisikiasauti ile zaidi ya Kaguba
mwenyewe.
‘Sawa’ Kaguba naye alijibu kwa kutuma hisia zake
moja kwa moja kwa Binti Sambayu. Kisha Kaguba
akakata mawasiliano hayo ya ki-hisia na kuanza
kutoka pale alipokuwa ameketi.
Alipofika sebuleni, Kaguba aliwaangalia
harakaharaka wazazi wake waliokuwa bado
wametaharuki kIsha kwa kasi ya kustaajabisha
akaanza kuelekea ulipo mlango wa kutokea nje ili
akakiwahi kibuyu chake. Haraka Nyembo akahisi
kitu cha hatari, damu ikamsisimka akajikuta
akiacha kuzungumza na nduguze, na kumuangilia
Kaguba ambaye alikuwa ameshakaribia kutoka nje.
Haraka, na kwa kasi ya umeme Kungurume
akatoka mbio ili amzuie Kaguba asitoke nje, lakini
alikwishamchelewa. Kaguba alikuwa
amekwishatoka uani.
******
Japo Kaguba alikwishatoka uani kabla ya kufikiwa
na Nyembo, lakini hakupata nafasi ya kuufikia
mlango wa chooni, Nyembo akawa ameshamfikia
na kumkumba kama mchezo wa mieleka. Kaguba
akaanguka chini na kuanza kugaagaa huku akilia
kwa sauti kiasi cha kuwapa hofu wakubwa kule
ndani ambao wote wakatoka kwa kasi ili wajue
Nyembo amemtenda nini. Walipotoka hawakuona
kilichotokea, zaidi ya kumwona Kaguba
akihangaika pale chini karibu na mlango wa
kuingilia chooni. Majirani waliojumuika walizidi
kuchanganywa na mchezo ule unaondelea kutukia!
Wakati Nyembo akiwa mle msalani akakiona kile
Kibuyu kikiwa palepale kilipoangukia, lakini alisita
kukigusa baada ya kukumbuka maelezo
aliyoyakuta kwenye kile kitabu kilichoandikwa na
mzee Mtandi ambaye sasa haijulikani aitwe hayati,
msukule, ama maiti wa zamani! Kilichomsitisha
Nyembo ni ni yale majani ya ‘Vibumbasi’…hakuwa
nayo maana yalisambaa ovyo wakati wa ile
mpishempishe. Kichwa kikamvurugika asijue la
kufanye. Kumbukumbu zikamjia kuwa kuna majani
kiasi aliyabakiza kwenye begi la mzee Mtandi kule
chumbani, lakini sasa angewezaje kutoka mle
maliwatoni na kumwacha Kaguba pale mlangoni
akiwa peke yake, yaani amwachie fisi bucha?
Haiwezekani.
Ambacho Nyembo hakukijua ni kwamba, kadiri
anavyopoteza muda kufikiria nini chakufanya
ndivyo genge la wachawi lilivyokuwa likizidi kuja
kwa kasi katika nyumba ile ili kukiwahi kibuyu
chao! Na kweli walibakiza kama mitaa miwili tu
kufika hapo.
Baada ya tafakuri ya muda, Nyembo akaamua
kutoka mpaka pale uani. Tayari uwanja ulifurika
uamati wa watu, majirani na ndugu. Wote
wakamlaki kwa macho tofautitofauti, wapo
waliomchukulia kama shujaa, na wapo waliohisi
labda naye ni mchawi tu. Hakujali!
“Nahitaji haraka majani ya vibumbasi yapo ndani
ya Begi la mzee Mtandi!” Maneno ya Nyembo
yakawafanya watu watazamane maana majani
hayo ni mashuhuri kwa mambo ya kishirikina tu
japo akina Kungurume wakakumbuka kauli ya
mzee Mtandi muda mfupi kabla hajakumbwa na
yale maswaibu, alipata kuwatamkia habari za
majani hayo, pia kauli hiyo ilimfanya Kaguba
amtazame kwa tahadhari sana Nyembo maana
kusikia anahitaji majani yale kukampa jibu kuwa
mtu huyo anaelewa hatua kwa hatua za kukitwaa
kibuyu na hata kutishia uchawi wao. Lakini
angefanyaje sasa? Akaanza kuizungusha akili yake.
“Ilumbi…au Lubambi, hebu nichukulie haraka hayo
majani kwenye begi ndani, Laa sivyo sote hapa
tutaangamizwa sasa hivi, nataka nikichukuwe
Kibuyu ila sasa sipaswi kukigusa bila ya majani
hayo,” Alisisitiza Nyembo baada ya kuona kama
haeleweki hivi. Lakini bado haikusaidia kitu ilikuwa
kazi bure tu, sawa tu na kumpiga konzi kinyago.
Kauli hiyo ya Nyembo ilipenya dirishani, na kuingia
mpaka chumbani, chini ya uvungu wa kitanda
walipojificha Nyamizi na mjomba wake. Sauti ya
Nyembo haikuwa ngeni masikioni mwa mzee
Mtandi hivyo Kauli hiyo ikamzindua na kumpa
ishara fulani, ishara ya hatari kuwa Kibuyu tayari
kipo chini ya himaya ya Nyembo na kwamba
anahitaji ‘vibumbasi’ vya kushikia. Kwa jinsi
anavyomjua Nyembo kwa utamaduni wake wa
kusomasoma hivyo hakupoteza muda kujiuliza
kuwa ametoa wapi taarifa za kibuyu kile hatari
maana alimtambua fika kuwa atakuwa alisoma tu
kumbukumbu alizoacha ameziandika kwenye kile
kijitabu chake. Na kwakuwa alitambua utata wa
jambo hilo hivyo ilimdhihirikia kuwa ingekuwa ni
vigumu kwa wengine kumuelewa. Akachomoka
tokea chini ya uvungu kama mshale, haraka
akasimama na kuanza kuangaza huku na kule,
akaliona begi lake likiwa limewekwa juu ya stuli,
akalisogelea na kulifungua.
Baada ya kulifungua na kupekuwapekuwa
akayatambua majani ambayo ni yeye mwenyewe
ndiye aliyeyaweka mle, yalibaki kidogo sana kiasi
cha kumpa jibu kuwa yalitumika baadhi. Akili ya
kibinaadamu ikaanza kumjia, akajuwa tu hata
kuponyoka kwao kule makaburini bila shaka
kulitokana na jitihada zilizofanywa pale
Nyumbani…bila shaka na Nyembo. Akayachukua
yale majani na kuanza kutoka nayo nje haraka.
Alipotoa uso wake tu pale uani, Loosalale uwanja
wote ulivurugika, kelele za taharuki kutoka kwa
majirani zikazizima, kila mmoja akiamini kuwa
mzee Mtandi alikwishakufa, vije tena awepo pale.
Ndugu nao utadhani nd’o wanamuona mzee wao
huyo kwa maraya kwanza, maana nao waliungana
na majirani wenzao na kukimbia ovyo. Wote
wakaelekea ulipo mlango mkubwa wa kuingilia na
kutokea uani ili watawanyike…na walipoukaribia tu
mlango, ndipo kilipozuka tena kizaazaa kipya na
cha kipekee!
Wakiwa hapo mlnango ndipo wakakutana uso kwa
macho na kundi kubwa la watu zaidi ya kumi.
Wengine wakiwa watupu kama walivyozaliwa huku
wengine wakiwa wamejivisha vibwaya vidogo
vilivyositiri sehemu nyeti tu za maungo yao, watu
hao wakiwa wamejipaka pemba nyekundu na
nyeupe katika miili yao, ukijumlisha na vumbi
zilizowatapakaa nd’o kabisa walizidi kutisha. Watu
hao ndiyo wale wachawi waliokuwa wakiserebuka
kule makaburini kabla mzee Mtandi na Nyanzala
kuwaponyoka na kufuatiwa na patashika
iliyowavuruga kabisa. Hawakuwa japo na chembe
ya aibu, maana akili zao zilikwishavurugika hivyo
kwao wao, Kibuyu nd’o kilikuwa cha muhimu kuliko
kitu chochote.
Hakuna aliyethubutu kuendelea kutoka nje, wote
waliokuwa wakimkimbia mzee Mtandi wakiamini
kuwa msukule umewatokea, wakajikuta wakipiga
kelele kwa nguvu huku wakirejea tena kulekule
walipotokea, ilikuwa ni bora kukumbana na mzee
Mtandi kuliko kuvaana na genge hili la wachawi
waliopagawa. Cha ajabu mzee waliporejea huku
uani hawakumwona tena mzee Mtandi ila
walikumbana na kioja kingine kilichowafanya
wachanganyikiwe zaidi. Walimshuhudia Nyanzala
akiwa anatokea mlemle ndani alikotokea mzee
Mtandi, japo yeye(Nyanzala) alionesha hofu na
woga wa haliya juu, alikuwa akitetemeka tu na
kuhema juujuu.
Taharuki mpya ikaibuka ikiwa ni kukimbia ovyo tu
bila muelekeo huku wakipamiana na kwenda
mieleka mpaka chini. Nyanzala alipowashuhudia
wale wachawi wakiingia kwa tambo mle ndani
akakimbia kwa kasi na kurejea kule chumbani
ambako alishindwa kubaki peke yake kwa woga
uliomvaa baada ya mzee Mtandi kutoka.
Licha ya Pemba na vumbi vilivyowatapakaa wale
wachawi, ila wote walitambulika kwa sababu ni
wakaazi wa eneo hilo na huwa wanafahamika kwa
michezo yao hiyo ya ingawaje hawakuwahi
kukamatwa!
****Mnh! Kaazi Kwel, Kwel!