Post by Admin on Jun 7, 2015 4:06:06 GMT
Licha ya Pemba na vumbi vilivyowatapakaa wale
wachawi, ila wote walitambulika kwa sababu ni
wakaazi wa eneo hilo na huwa wanafahamika kwa
michezo yao hiyo ya ingawaje hawakuwahi
kukamatwa!
Hakuna hata mchawi mmoja aliyekuwa na mpango
na Nyanzala, wote walikatiza kona mbele ya banda
litumikalo kuanikia dagaa wakielekea sasa kule
msalani.
Kule msalani nako, mambo yalikwishawiva. Mzee
Mtandii aliamua kuifanya kazi mwenyewe, aliingia
moja kwa moja msalani akifuatiwa na Nyembo,
akiwa na ‘vibumbasi’ vyake mkononi, akakitwaa
Kibuyu kile na baada ya manuizi tu akaanza kazi
ya kukizungusha huku akikipuliza kama firimbi.
Laahaulah!
Hakuna hata mchawi mmoja aliyepiga hata hatua
moja tangu kibuyu kilipoanza kuzungushwa.
Walipamiana na kutupwa ovyo, wale huku, hawa
kule. Vilio vyao vya kichawi vikaunguruma mle
auani huku wakitapatapa kutafuta msaada.
Iliwachukua muda mrefu wakihangaika hata
majirani pamoja na wanafamilia waliokuwa
wametawanyika, sasa wakarejea kushuhudia
mtanange ule. Walikuwa wakilia kwa uchungu,
fedheha, na kukata tamaa huku wakiomboleza
kutaka msaada.
Wakati mzee Mtandi akiendelea kucheza na kile
Kibuyu, ndipo Nyembo akatoka sasa huko msalani
na kuwakuta wachawi wale waliokuwa
wamezungukwa na kundi la watu, wakiendelea
kutapatapa kama wagonjwa walio taabani bin
Sambamaji.
Baada ya dakika kama kumi za kutapatapa pale
chini, ghafla wale wachawi wakajihisi ahueni
kidogo. Taabu zikawatoka kiasi, wakawa
wanatweta tu huku wanaangaliana wenyewe kwa
wenyewe. Vurugu na zogo kutoka kwa wakaazi
waliozidi kumiminika pale vilitishia usalama wao
maana kila mtu alikuwa akisema lake na kupanga
hukumu yake dhidi yao.
“KAA CHINI MWANGA MKUBWA WE!” Nyembo
alibwata huku akiwa amemtole macho Binti
Sambayu aliyekuwa amesimama akitaka kukimbia.
Binti sambayu alihisi kurejewa na nguvu hivyo
akaamini muda wa kutoweka umewadia. Haikuwa
hivyo. Hakujua kuwa ahueni ile imetokana na
Nyembo kumwambia mzee Mtandi kuwa aache
kidogo kuzungusha kile Kibuyu ili sasa aseme nao,
sasa kutokana na ujuaji wa Binti Sambayu ikambidi
Nyembo aliyekuwa amewasimamia wale wachawi
pale uani ampe ishara nyingine mzee Mtandi akiwa
kule msalani ili aendeleze kutoa kiminyo, naye bila
ajizi akaianza tena kazi ile iliyozua tabu kwa
wachawi wale. Walitaabika vilivyo, inaonekana
kiminyo kiliwazidia mpaka baadhi wakaanza
kutapika, huku wengine wakitokwa na haja kubwa
na ndogo palepale ikiwa ni ishara mbaya kwa
mchawi yeyote akikamatwa. Ishara ya kifo!
Kama haitoshi Nyembo akachukua mijedeli na
kuwagawia wananchi wenye hasira kali kisha
wakaanza kucharaza viboko vya nguvu, Wachawi
walihangaika na kulia mpaka wakabaki hoi ndipo
Nyembo akamwambia mzee Mtandi aache kidogo
kazi yake. Akawasogelea karibu wale wachawi na
kuwamwagia maji ya baridi kutoka katika ndoo
aliyotoka nayo mle msalani, kisha sasa akaanza
kusemanao kwa utulivu na umakini.
”Leo mkifanya mchezo mtakufa hapahapa…cha
msingi ili mpate msamaha ni lazima mtueleze kila
kitu, kila siri na kila mchezo mliokwishawahi
kuufanya hapa wilayani kwetu na kwingineko…
Mmenielewa?” Alibweka tena Nyembo.
Wakamuitikia kwa vichwa tu huku nyuso zao
wakiziinamisha chini kwa fadhaa. “…Kwanza
kabisa nataka mtueleze kwanini mliwachukua
kichawi akina Nyanzala na mzee Mtandi. Pili
mtutajie watu wote mliowahi kuwaua na tatu
mtueleze jinsi mlivyokuwa mkifanya kazi zenu za
kichawi hatua kwa hatua, Sawa?” Nyembo
alitamba. Muda huo akina mama Kaguba.
Kungurume, Ilumbi, na wengine walikwishajongea
eneo la tukio, wakiwa nyuma ya Nyembo
wakimwona kama mkombozi wao licha ya kuwa
mwanzo walimbeza na kumdhihaki.
“Simama juu we’ Binti Sambayu utoe maelezo!”
Alifoka Nyembo, na hapohapo akasimama Binti
Sambayu na kuanza kutoa maelezo huku umati
wote ukiwa kimya!
SEHEMU YA KUMI
“Mimi ni kweli mchawi wa siku nyingi ila
sikupenda kuwa mchawi jamani, nilirithishwa tu na
hayati Bi…”
“NITAKUADHIBU TENA WEWE? SITAKI STORI
HAPA, NATAKA UJIBU MASWALI YANGU
NILIYOKUULIZA.” Alifoka Nyembo na kumfanya
Binti Sambayu aanze kuelezea mambo mazito
yawahusuyo wachawi wa hapo Kibondo na sehemu
kadhaa wanazohusiana nazo kikazi.
“…Sisi ni wachawi ambao tulirithishwa tu uchawi
kutoka kwa wazazi, mababu, na mabibi zetu.
Uchawi wetu uko chini ya mzimu mkubwa uitwao
GULUGUJA, Tumefunzwa na kukuzwa katika
tamaduni za kichawi mpaka tukafuzu. Wengi wetu
tuliingizwa humu tungali watoto wadogo japo kuna
baadhi walishawishiwa na kuingizwa katika kikundi
chetu cha uchawi wakiwa watu wazima…” Umati
mkubwa uliofurika uani kwa hayati masonganya
uliokuwa kimya ukisikiliza, ulishitushwa na ujio wa
ghafla katika usiku ule wa mzee mmoja ambaye
baadhi walimtambua na baadhi wakiwa
hawajamtambua. Cha ajabu wakati mzee huyo
alipoingia tu mle uani, hapohapo binti Sambayu
akaanza kulia kwa sauti ya hofu na uchungu na
kuwafanya wengi kuogopa.
Mzee yule bila ya kusalimiana na yeyote, akakatiza
katikati ya watu, akamsogea binti Sambayu na
kumnyang’anya kibuyu kidogo alichokua
amekishikilia kisha akaingiza mkono kwenye
kikapu chake cha rangi ya kaki kilichoathiriwa na
uchafu mpaka kikaonekana ni cheusi, akakiweka
kile Kibuyu na kisha akatoa kitu kama mkufu hivi
uliosukwa kwa ukindu, akamvisha binti Sambayu
shingoni. Baada ya hapo akarejea mpaka
alipokuwa amesimama bwana Kungurume na
kumpa mkono huku akimsalimu. Alikuwa ni Babu
Gao.
“Msiogope jamani nimemvisha kitu kinachoitwa
Mkanyafe yaani mkufu wa kifo, endapo atadiriki
kusema uongo basi ataangamia na kufa hapahapa
yeye na wafuasi wake wote waliopo hapa na
waliopo huko majumbani mwao, kuna mambo
mengi na ya ajabu ambayo anapaswa kuyaongea
huyu mchawi…mimi nimetembea usiku huu kwa
miguu kutokea huko kwangu mbali ili kuja kushiriki
katika kuuona mwisho wao hawa watu wabaya.”
Babu Gao aliongea kwa sauti yake kavu na ya
kukoroma kisha akamuashiria Binti Sambayu
aendelee. Naam binti Sambayu akasimulia historia
yao ya kuingia kwenye uchawi na namna
wanavyoendesha shughuli zao hatua kwa hatua.
“Ndani ya hiki kibuyu kuna nini hasa kinachofanya
kiwe na nguvu na uwezo mkubwa kiasi hiki?”
Nyembo alimsaili binti Sambayu baada ya kutoa
historia yao ambayo haikuwa na umuhimu mkubwa
sana.
“Humo kuna dawa za mitishamba tu
zilizochanganywa na vitu vingine tofautitaofauti.”
“Ni vitu gani hivyo?”
“Aaa…hu.. ku..na nywele, mkaa na..” Kabla binti
Sambayu hajafikisha neno lake mwisho watu
walimshangaa akianza kuhangaika na kutapatapa
huku mikono yake akiipeleka shingoni kujaribu
kuuzuia ule Mkanyafe uliokuwa ukimkaba mpaka
akashindwa kuhema na kuanza kukoroma.
Alikoroma huku udenda ukimtoka na macho
yakimlegea mfano wa mtu anaye karibia kufa.
“We’ si nimekukanya kusema uongo? Sasa
unataka kufa si’ ndiyo eeh?” Babu Gao alimfokea
binti Sambayu ambaye sasa hakua hata na uwezo
wa kujibu zaidi ya kunyanyua mikono yake huku na
kule kutaka msaada. Haraka Babu Gao
akamsogelea na kufanya cha kufanya mpaka
mkufu ule ukalegeza.
“Narudia tena, ukithubutu kusema uongo hapa leo
utakufa…eleza ukweli wa kila kitu,” Alibwata Babu
Gao. Watu walijikuta wakishangilia kwa tukio lile
lililowafanya sasa waamini kuwa Wachawi
wampatikana. Kufikia hapo sasa binti Sambayu
akaamua kusema kila kitu kuhusiana na uchawi
wao akihofia kuuawa na mkufu wa Babu Gao.
“…Naomba msituue jamani, ninaahidi kuwa
hatutarudia tena mchzo huu wa uchawi, tumekoma
jamani. Nitaelea…nitaeleza kila kitu…” Alilalama
binti Sambayu huku akilia na kuendelea. “…ndani
ya Kibuyu hicho kuna mchanganyiko wa vitu vingi
sana. Kuna mafuta ya watu, ngozi za maalbino,
nyongo za koboko na za simba, kitovu cha mtoto
mchanga, moyo wa kondoo, utumbo wa
mwanamke mjamzito…”
“Vitu vyote hivyo huwa mnavipataje?” alidakia
Nyembo.
“…Huwatunwaua kwa hila watu tuwatakao,
tukishawaua ndipo usiku huwa tunawachoma na
kuwakamua mafuta yao, kama maiti ni ya
mjamzito huwa tunampasua tumbo tunamkata
utumbo wake, na kama ni ya mtoto huwa
tunachukua kitovu chake. Pia huwa tunazifukua
maiti za albino na kuchuna ngozi zao, hao Koboko
na Simba huwa tunawatega kichawi ambapo
tukishawakamata huwa tunachukua vitu kadhaa
ndani ya miili yao huku wakiwa hai…”
“Lengo la vitu vyote hivyo ni nini hasa?” Alisaili
tena Nyembo akiwa amewasimamia wale wachawi
na mijeledi yake.
”…utumbo wa mwanamke mjamzito huwa
tunauchanganya na madawa ya kienyeji kisha
tunafukia katika njia panda basi hapo kama kuna
mjamzito tuliyemkusudia, ataumwa uchungu na
kuhangaika bila kuzaa mpaka atafariki. Na hizo
nyongo za Koboko na Simba mara nyingi huwa
tunazitumia kuwasukumizia hasira watu tuwatakao
ambao hushindwa kujizuia na kujikuta wakifanya
mambo wasiyoyatarajia kama vile kuwa na nguvu
za ajabu na kumpiga mtu mpaka kumuua, au
kujinyonga mwenyewe nk. Kitovu cha mtoto
mchanga huwa tunakichangaya na majani
yatumikayo kupikia mboga ya mlenda kisha
tunamnuizia mtu tumtakaye ambapo baada ya
kukizika hicho kitovu katika kaburi la mlemavu
yeyote aliyepata kufariki, huku kwenu huyo
tuliyemfanyia hivyo ataanza kuumwa sana na
kukonda mfano wa muathirika wa Ukimwi, na hata
mkienda kumpima hospitali huonekana na ugonjwa
huo kumbe Laa!”
“Hebu tutajie majina ya watu mliowahi kuwauwa
hapa Kibondo, pia ututajie namna ya vifo
mlivyowaua…” Babu Gao alichombezaswali hilo
akiwa na lengo maalum la kuwafanya wakaazi
walichukulie lile tatizo kuwa si tu la akina mama
Kaguba, bali ni la kwao wote. Alikuwa na uhakika
kuwa wapo watakaouguswa na simulizi chafu za
binti Sambayu. Na kweli hapo ndipo kazaazaa
kilipoanza maana binti Sambayu alianza kutaja
majina ya watu waliokufa zamani na siku za
karibuni kwa vifo vya aina kwa aina. Baadhi ya
waliotajwa kuuawa kwa ajali barabarani, magonjwa
kama Ukimwi, vifo vya uzazi nk ndugu zao
walikuwapo hapo eneo la tukio. Wapo waliolia kwa
uchungu na wapo walioishia kutetemeka kwa hofu
na kwa hasira, ndipo wakajitokeza wananchi
wachache wenye ghadhabu na kuanza
kuwashambulia kwa mawe na mikoma wachawi
wale kiasi cha kuvuruga mjadala ule mtamu.
Wakati kichapo kikiendelea, ghafla wakaingia
askari polisi pamoja waliokuwa wamearifiwa juu ya
tukio hilo la ajabu. Walipofika tu wakaanza
kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiendelea
kuwasulubu wale wachawi, kisha baada ya utulivu
kurejea, wakabaki na watuhumiwa wa Uchawi
pamoja na wahanga wa tukio hilo pamoja na mzee
Mtandi aliyetolewa kule chooni alipokuwa
amesimama na Kibuyu chake ambapo walifanya
nao mahojiano ya awali na kuamua kuwachukua
na kwenda nao kituoni kwa ajili ya mahojiano
zaidi. Pamoja na Wachawi, ndani ya gari ya Polisi
waliingia akina Mzee Mtandi, Nyanzala na
Kugurume.
Mara tu baada ya Polisi kuondoka, Babu Gao
alikichukua kile kibuyu, akakifanya alivyojua na
kukilipua moto. Kilipiga mlipuko mkali kama bomu
kabla ya kuanza kuteketea mpaka kikaisha chote.
Wakati Kibuyu kikiteketea, Wachawi wote
waliokuwa ndani ya gari ya Polisi waliteketea na
kufa wote. Cha ajabu kuna baadhi ya watu
waliokuwa majumbani mwao, nao waliteketea
kama ilivyokuwa kwa wale wachawi hivyo kudhihiri
kuwa nao walikuwa ni wachawi tu japo siku ile
hawakutoka kwenda kuwanga.
Huo ukawa mwisho wa Wachawi wote wa wilayani
hapo.
Siku mbili baadaye baada ya Polisi kujiridhisha na
kilichotokea huku wakiendelea na uchunguzi,
waliwachia akina Nyamizi na mzee Mtandi ambao
walirejea kwenye jamii yao wakiwa na mengi ya
kusimulia familia zao.
TAMATI.