Post by Admin on Jun 7, 2015 4:23:58 GMT
Ulikuwa mshikemshke wa ghafla pale shuleni mwalimu
aliamuru kila mmoja aje mstarini hata kama ni
mgonjwa,viranja walitii amri na kuita wanafunzi wote
kwa haraka hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyebaki
ndani ya bweni.
Wakiwa hawajui nini kinachoendelea mwalimu wa
zamu aliyeitwa Mwl.Chipeta alikuwa mbele ya
wanafunzi waliokuwa kimya kumsikiliza yeye.”Kabla
sijatoa tangazo hili,ni nani anatambua mwanafunzi
ambaye hayupo eneo hili? (Kimya)
"Nani anaumwa na amepewa ruhusa?" (Kimya)
"Kwa hyo wote mpo?" (Ndiooo)
"Haya mchepuo wa H.G.E wote pita mbele" aliamuru
mwalimu Chipeta na kwa haraka wakaanza kujongea
mbele.
"Mamaaaaa,"
ghafla kelele ilisikika kuna mwanafunzi aliyekuwa
mgonjwa alikuwa ameanguka chini kwa sababu ya
kizunguzungu.Ustaarabu ukatoweka pale ghafla kila
mwanafunzi akawa anasema lake,mara hivi mara vile.
Hata mwalimu Chipeta alitimua mbio kuelekea kwenye
tukio.
Ni wakat huohuo Joyce ambaye alikuwa kiranja
alipata mwanya wa kutuma ujumbe kwa Reshmail
kumpa taarifa.
*****
Roho ilikuwa inamdunda Reshmail kwa kasi
sana,aliamin kila kitu kitakuwa wazi na atafukuzwa
shule,
"Eve watanielewaje wazazi mie mh! nimerokoroga"
alijisemea Reshmail.
"Upo na steringi lazima tushinde haka kavita kadogo"
Eve alimpa moyo wa ujasiri Resh,"Naomba hiyo simu
si ina salio kidogo"
"Imo elfu tatu" Alijibu huku akimpa simu Eve.
"Sihitaji zote hizo natumia shiling 60 tu hapa"Alijibu
kwa jeuri Eve huku akionekana kujiamini zaidi.
"Sasa hyo 60 itafanya nini shogangu au umesema elfu
sitini?"Alitania Resh na wote wakajikuta wanacheka.
"Dakika tano nyingi majibu mazuri yatakuja,chukua
simu yako ikiingia meseji uisome mi nalala bibie tuliza
roho yako hii sio movie ya kihindi eti stering
anauwawa,hili picha la kichina stering anachomwa
kisu bado anapona" alimaliza Eve na kushusha kofia
yake ikafunika macho.
Ni kama alivyosema dakika tano zilikuwa nyingi sana
ujumbe kujibiwa
"Na ufanye kweli mi narekebisha mambo nyie tanueni
kwa raha zenu na pia kuhusu yule wa H.G.L vipi?"
ulisomeka ujumbe.
"Mungu wangu amakweli Eve steringi jamani yaani
kirahisi hvyo" alijisemea Resh kwa sauti ya chini
akidhani Eve amelala tayari "Futa sms ya huyo mjnga
nitamalizana nae" kwa saut ya kivivu Eve alimwambia
Resh.
****
Ndege ya Precion Air ilikuwa inaondoka kutoka
Musoma kwenda Dar-es-salaam kupitia Mwanza
majira ya saa kumi na moja wakati basi la KIMOTCO
lilifika saa kumi na nusu jioni,Resh aliona akipanda
gari anaweza kuchelewa kwa Adam Mwanza japo hata
umbali wa Musoma kwenda Mwanza
hakuufahamu."Resh ndege ya wapi tunapata sasa hv
jaman" Eve alimuuliza Resh wakiwa ndani ya 'Teksi’
kutokea stendi kuu ya Musoma maeneo ya Bweri.
"Tunajaribu steringi wangu"
"Haya!! utamu na uchungu wa mapenzi mwachie
aliyeyabeba" alitoa fumbo Eveline.
"Dereva dereva zuia kidogo tafadhali" ghafla Resh
alimwomba dreva naye bila hiana akazikanyaga breki
bila kuuliza kulikoni. Mbio mbio Resh akashuka
akaanza kutimua mbio kurudi nyuma huku akiwa peku
viatu ameacha garini Eve,Dereva na wananchi wengine
wakabaki kumshangaa.
****************************** **********
Mwalimu Chipeta aliongoza zoezi zima la
kumshughulikia mwanafunzi aliyeanguka pale
mstarini,shule ya Arusha international ilisifika sana
kwa kujali afya za wanafunzi hivyo tukio lile
lilisababisha Mwalimu Chipeta kumsahau kabisa
Bi.Gaudencia mama yake Reshmail na kwenda
kushughulika ipasavyo kwenye lile tukio,
Aliyekuwa ameanguka alikuwa Naomi Holela
mwanafunzi aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa
kifua na pale kilikuwa kimembana hasa kutokana na
baridi iliyokuwepo nje.
Gari ya shule ilifika haraka Mwalimu Chipeta na viranja
wawili pamoja na 'matron' walimsindikiza Naomi
hospitali.
Akiwa ndani gari Mwalimu Chipeta alisikia simu yake
ikitoa mlio wa kupokea ujumbe mwanzoni alipuuzia
kutokana na ubize uliokuwa ukimkabili lakini punde
alitoa simu yake na kufungua ujumbe ulioingia
"Niaje ticha mi Wa ukweli nipo na Resh mbali kimtindo
kama vipi rekebisha mambo huko mi nikija nakuletea
geto yule Amina wa H.K.L,niandalie tu mapene yangu"
uso wake ulisahau matatizo yote yaliyokuwa mbele
yake, ni muda mrefu sasa tangu Mwalimu Chipeta
muhitimu wa shahada ya elimu ya fasihi andishi katika
chuo kikuu cha Dodoma alikuwa amemfukuzia binti
mrembo wa kawaida tu Amina bila mafanikio tegemeo
lake alikuwa ni Eve au Wa ukweli kama walivyomzoea
,bila kupoteza muda Chipeta alifungua sehemu ya
ku'forwad' meseji na akaituma kwa Mwalimu Madege
ambaye wote lao lilikuwa moja, alikuwa ni mwalimu
Madege aliyeijibu ule ujumbe na kuulizia kuhusu yeye
na mpango wa kumpata binti wa H.G.L.
"Samahani wewe ndio mama yake na Reshmail
"Mwalimu Madege aliuliza baada ya Bi. Gaude kuingia
katika ofisi ya makamu mwalimu wa zamu .
"Ndio ni mimi baba"
"Kwanza samahan sana kwa usumbufu uliojitokeza"
"Usijali na mimi niwape pole kwa matatizo
yaliyojitokeza hapa"
"Tunashukuru ndio mambo ya shule haya,eeh! mama
nimepokea ujumbe sasa hivi kwamba mwanao yupo
katika mbuga za Serengeti ambapo wanafunzi watano
waliofanya vizuri walipelekwa kufanya utalii wa siku
tano" alidanganya mwalimu Madege.
"Jaman huyu mtoto mbona hakuniambia?... baba yake
atafurahi sana akisikia maendeleo ya mwanae"mama
Resh alijieleza kwa furaha iliyozidi wasiwasi aliokuwa
nao.
"Tuliwashtukiza hawakuwa na taarifa hata wao
wameshangaa mno" aliendelea kupanga maneno huku
akichorachora mezani kwa kutumia karamu isiyokuwa
na wino.
Moyo wa mama Reshmail uliridhika japo mwili ulikuwa
na kinyongo kwa kukosa haki yake. Ilimbidi siku hiyo
hiyo afunge safari kurudi jijini Dar na zawadi
alizokuwa amemletea mwanae zikiwa mikononi mwake.
* * * * * *
A.T.M ya N.B.C aliyoiona maeneo ya Nyasho
ilimkumbusha kuwa kadi yake ni 'VISA' inafanya kazi
mashine ya A.T.M ya benki yoyote bila kujali macho ya
watu alitimua mbio pekupeku hadi kwenye mashine
ambapo kwa bahati nzuri hapakuwa na foleni na
mtandao ulikuwepo "You can withdraw up to 1000000
with your A.T.M card daily N.B.C WE CARE"
kijitangazo kwenye kioo cha mashne kiliibua tabasamu
la Reshmail,na bila ajizi akabonyeza chaguo la kutoa
laki tano kwa mikupuo miwili na kutimiza kiasi cha
milioni moja.
kisha kwa mwendo wa mbio kama alivyoingia akatoka
akisindikizwa na miluzi ya wauza mitumba wa Nyasho
ambayo kwake haikuwa na madhara hata chembe
"Samahani safari yenu imeahirishwa tafadhali hadi
kesho asubuhi!" sauti nyororo ya mwanadada wa
mapokezi aliyehusika na masuala ya Booking
aliwaeleza mwanaume mmoja aliyekuwa na mpenzi
wake wakitegemea kusafiri muda mfupi ujao kwenda
Mwanza.
Sura zao zilizokuwa na furaha zililegea na kuwa kama
watakavyokuwa pindi wakipata wajukuu,"Haiwezekani
huu ni upumbavu tena ujinga ujinga ujinga,yani safari
yangu inahairishwa ghafla kama vile safari za
baiskeli,hapana sipo tayari nas...."
"shhhhh!!" kwa ishara ya kidole kimoja kuziba mdomo
alinyamazishwa yule baba aliyetaka kuugeuza ukumbi
ule uwanja wa mapambano na matusi.
Kwa ishara nyingine yule dada akamwita akasogea
pale alipo akamnon'goneza "Unawaona wale
wasichana wawili,mmoja kimada wa mtoto wa raisi
mwingne mtoto wa kamanda wa jeshi ni simu kutoka
ikulu,kwa usalama wako acha kelele" alimwambia
huku akimwelekezea walipo Resh na Eve.
Bila kuhoji huku uoga ukimtawala hadhi yake ikashuka
haraka haraka akamvuta mkewe wakaondoka
wakawapisha kwa mbali Resh na Eve kama vile
wanatema cheche za moto.
****************************** ******
ITAENDELEA...............