Post by Admin on Jun 7, 2015 4:26:17 GMT
Ni kweli nafasi zilikuwa zimejaa lakini pesa iliongea
nafasi ya mtu mwingine wakapewa wao tena
harakaharaka,huku mtendaji wa jambo hilo akiweka
shilingi laki mbili na nusu kibindoni.
Huku Resh na Eve wakipata nafasi katika ndege ya
Precision Air kiulaini,kwa mara ya kwanza Eve
anapanda ndege
"Mh! ushoga nao raha wakati mwingine” alijisemea
wakati muhudumu wa ndani ya ndege akitoa
maelekezo madogomadogo.
Ilikuwa kama safari ya kutoka Kimara Dar kwenda
Mbagala,tayari walikuwa jiji la Mwanza
"Eve rushwa tamu wewe,naamini haitaisha ona sasa
tupo Mwanza tayari"
Resh alimwambia Eve wakati wanasafisha macho yao
wajue nini cha kufanya baada ya kushuka kutoka
kwenye ndege.
"Hoteli yenu ni nzuri?" Eve alimuuliza muhusika
aliyekuwa ndani ya kigari kidogo kilichoandikwa
Millenium Hotels kilichokuwa hapo kwa lengo la
kutafuta wateja wanaotua na ndege uwanjani hapo,
"Ni nzuri sana hautajuta kuwa pale.”
"Mh! haya,Resh twende giza linaingia" Eve alimwita
Resh wakajitoma ndani ya gari na safari ikaanza.
"Darling umetoka kwenye michezo tayari pole mpenzi"
ulikuwa ujumbe mfupi kutoka kwa Adam kuja kwa
Resh,tabasamu pana likameza mdomo wake looh!
lilikuwa tabasamu lililoelezea furaha ya moyo.
Adam alituma ujumbe huo akijua Resh yupo shuleni
tena ilikuwa siku ya michezo ambayo Resh alipenda
kushiriki hasahasa mpira wa kikapu.
"Mamaaaaa!!"
Resh alipiga kelele ghafla gari ikayumba huku na
huko,dereva akajaribu kwa uwezo wake wote
kuirudisha barabarani "Paaaa!!" mlio mkubwa
ukasikika.
*******************
Adam alipokea ujumbe kutoka kwa Reshmail akiwa
maeneo ya kijiweni barabara ya lami kuelekea chuo
kikuu cha mtakatifu Augustino,kupitia shule ya
wasichana ya Ngaza.Adam alikuwa pamoja na rafiki
yake (Huha) katika pikipiki ya rafiki yao aliyekuwa
amewaazimisha wazungukiezungukie maeneo.
"Huha hebu endesha twende hapo Nyegezi kona kuna
mtu nataka kuonana naye mara moja"
Adam alimwomba Huha.
"Tayari Halima ametuma meseji mwambie hatuna
mafuta atufate na gari yake bwana"
Alitania Huha huku akianza kuiondoa pikipiki taratibu
"Ungejua hata usingesema wewe twende ukajionee
maajabu ya mwaka" alijibu Adamu huku pikipiki ikizidi
kushika kasi.
Ndani ya dakika tano tayari walikuwa Nyegezi kona
ambapo Huha alipaki pembezoni kidogo na barabara
iendayo stendi kuu ya Nyegezi jijini Mwanza,Adam
alielekea dukani kununua vocha,na Huha akasogea
pembeni kidogo aweze kuvuta sigara yake.
***
Dereva akiwa mwingi wa mawazo yake binafsi
yasiyomuhusu Reshmail wala Eve na hata kama
yangekuwa yanawahusu ule haukuwa muda muafaka
wa kuwaambia.
Macho ya Reshmail yalikuwa yamekutana na bango
kubwa lililoandikwa "KARIBU CHUO KIKUU CHA
MTAKATIFU AUGUSTINO" kwa hamu kubwa aliyokuwa
nayo ya kumwona Adam ambaye alikuwa pia
mwanafunzi ndani ya chuo hicho ndio sababu kuu ya
kujikuta akipiga kelele kwa nguvu hali iliyomshtua
dereva kutoka katika mawazo mazito na kujikuta
akiyumbisha gari huku na huko hadi ilipokutana na
pikipiki iliyokuwa imepakiwa pembezoni mwa barabara
na kuirusha umbali ambao si wa kutisha sana,
Iligeuka vurumai madereva wa teksi na bodaboda za
pikipiki walikuwa wakali sana hawakutaka kusikia la
mtu,wengine hasira za kukosa abiria tangu waingie
kijiweni asubuhi walizihamishia katika tukio hilo.
Usingekuwa upole wa yule dereva basi mawe
waliyobeba wananchi yangeigeuza ile gari kuwa
mkweche. Eveline alitelemka garini kwenda kumsaidia
dereva kujitetea lakini Reshmail uoga ulimtawala
akawa amejibana kwenye viti vya nyuma vya ile gari
huku akitetemeka.
"Mh! Adam hawezi kukosa mwenyeji maeneo haya
ngoja nijaribu kumpigia,ah! hii safari imetawaliwa na
mikosi dah!" aliwaza Resh huku akichukua simu yake
kutoka katika kipochi chake.
Lakini kelele zilizokuwa pale aliamini hawezi
kusikilizana vizuri na upande wa pili,taratibu huku
akitetemeka alifungua mlango akashuka na kuanza
kutembea kuelekea pahali ambapo kidogo pametulia.
Zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wenye hasira eneo
lile wakageuza vichwa vyao kuangalia kazi ya Mungu
ilivyotendeka vyema katika mwili wa Reshmail,
Badala ya kumpigia kelele dereva,miluzi mikali
ikiongozwa na dereva mkongwe wa teksi eneo lile
ndugu Sanya Bonda ikahamia kwa Reshmail,
Resh akajifanya kama hasikii vile "Ilikuwa haki ya
dereva kupotea njia jamani" Bonda alisema kwa sauti
ya juu na kugeuza hasira za watu kuwa vicheko. Resh
taratibu akaufikia mti mdogo mbali na eneo la tukio
akabonyeza namba za Adam.
Simu iliita muda mrefu bila kupokelewa. Alipopiga
mara ya pili simu ilipokelewa.
"Helow Resh subiri nisogee pembeni nakupigia kuna
tatizo limenipata" alijibiwa na Adam katika simu.
"Hata mi....." kabla hajamalizia kauli yake Reshmail
simu ilikatwa akiwa bado anaduwaa kama dakika
mbili pembeni yake alizengea kijana mmoja ambaye
Resh hakutaka hata kumwangalia machoni,alijua ni
walewale waliokuwa wakipiga miluzi na kumwita
majina waliyotaka.
Resh taratibu akajisogeza pemben.
"Vipi dada mbona wanikimbia au mi nanuka halafu we
mrembo haya basi umebarikiwa sana najua unataka
kusifiwa" aliongea yule kijana lakini Resh hakujibu.
Simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mfumo wa
kimya(Silence mode) ilikuwa inatoa mwanga kuashiria
aidha kuna ujumbe umeingia au kuna simu
inaingia,lakini kwa jinsi alivyoandamwa na yule kaka
kwa maneno hata hakuweza kugundua.
Baada ya dakika kadhaa akaondoka yule kaka ndipo
kuangalia simu akagundua ilikuwa imeita mpaka
imekata na hakuwa mwingine bali ni Adam alikuwa
amepiga,harakaharaka akapiga tena.
Ulikuwa mshangao wa hali ya juu sana Reshmail
hakuamini alipomwona yule kijana aliyekuwa
ametokea pale dakika chache zilizopita kuelekea
kwenye zile vurugu ndio anapokea simu.
"Resh mbona nimekupigia hupokei mamaa"
alimshuhudia yule kaka akiongea kwenye simu huku
akirejea lile eneo kukwepa kelele,kama ilivyo kwa mtu
aliyenaswa na umeme Reshmail alikuwa ametulia tuli
na simu sikioni huku yule kaka akizidi kulikaribia eneo
lile
“Reshmail mbona huongei!!” aliendelea kuuliza bila
kupata majibu.
"Adam"
Alijitutumua Resh na kutamka akiwa jirani naye
kabisa,bila kujua yule kijana akaangusha simu yake
hakuamini msichana aliyetoka kuongea nae dakika
kadhaa ndio Reshmail wa Arusha.
*********
ITAENDELEA..............