Post by Admin on Jun 7, 2015 4:44:07 GMT
Vurumai lilisawazishwa haraka sana Adam na Huha
ndio waliokuwa wamiliki wa ile pikipiki iliyogongwa na
gari waliyokuwemo akina Reshmail.
"Jamani huyu hapa ni dada yangu,ndio alikuwa
amenipigia simu tuonane hapa naomba haya mtuachie
sisi"
Adam aliuambia umati ule ambao hasira zao zilikuwa
zimeanza kupoa na haraka walimwelewa wakaacha
kumzonga dereva.
Reshmail bila kupoteza muda akamwongoza Adam
wakaingia garini akampa pesa taslimu shilingi laki tatu
kwa ajiri ya matengenezo ya ile pikipiki naye Adam
akamkabidhi Huha kisha akajumuika na Eve pamoja
na Reshmail katika gari,huku Reshmail akiwaacha
watu hoi kwa uzuri wake wa asilia ambao hata Adam
alikuwa amechachawa nao na kukubaliana na ukweli
kwamba picha zilizotumwa zilikuwa za Resh kweli.
***
Bi Gaudensia alifika Dar-es-salaam majira ya saa tatu
usiku,bado alikuwa hajaridhika kumaliza siku yake bila
kuongea na mwanae,hivyo punde tu baada ya kuingia
chumbani mwake aliamua kujaribu kupiga namba za
simu za Reshmail ambazo zilikuwa hazipatikani siku
nzima.
Furaha aliyoipata ilikuwa haisimuliki,pale simu ilipoita
upande wa pili"Mh! kalala nini huyu?" alijiuliza simu
ilivyoita kwa muda mrefu bila kupokelewa,lakini mara
ikapokelewa
"Helow! samahani Reshmail amelala"
sauti ya kiume ilijibu baada ya kupokea kisha simu
ikakatwa na kuzimwa.
Mama Resh hakuamini kuwa amesikia sauti ya kiume
katika simu ya mwanae alidhani amekosea namba
lakini alipohakikisha zilikuwa zenyewe,wivu mkali
ukamshika,akajaribu kupiga mara nyingi lakini bado
hali ilikuwa ileile simu ilikuwa imezimwa usingizi
ulipaa,alitokwa na jasho,hisia mbaya zikamvuruga na
kufanya kichwa chake kiume sana,mama huyu alikuwa
amejisahau kabisa kuwa Reshmail ni mwanae wa
kumzaa, alizurura kama mtu anayetafuta kitu
ambacho amesahau alipokiweka pale
chumbani,alitamani kupiga kelele lakini aliamini
hazitasaidia kitu.
***
Reshmail akiwa usingizini Adam pembeni yake,yeye
(Resh) alikuwa hoi kwa uchovu wa safari na
misukosuko yote waliyopitia,na alipomaliza kuoga tu
na kupata chakula alisinzia,hata simu yake ilipoita
hakuisikia hata kidogo na hata angeisikia asingeweza
kunyanyuka kupokea
"Resh ni kipetito anapiga" Adam alimuuliza Resh
aliyekuwa hoi kitandani.
"Ah! ni rafiki yangu mwambie nimelala" alijibu kwa
taabu akiwa hata hajui anachokiongea.
Naye Adam bila kugundua kwamba Resh hajui
anachokisema na ile namba ni ya mama yake Resh
alipokea na kuzungumza
Kitendo cha Adam kumkuta Reshmail akiwa bado ni
bikra kilimzuzua sana,mapenzi yake kwa Halima
yalipungua sana na kuisha kabisa hatimaye.
Siku tatu mfululizo walizotumia pale Millenium Hotel
zilitosha kuvunjilia mbali penzi la Adam na Halima na
kujenga penzi imara kati ya Adam na Reshmail.
"Mwezi wa pili uje ujitambulishe nyumbani Adam yaani
siwezi kusubiri kwa kweli nakupenda Adam wewe ni
mwanaume wangu wa kwanza na ninakuahidi
nitajitunza kwa ajili yako"
Reshmail alikuwa anamsisitiza Adam siku alipokuwa
amewasindikiza uwanja wa ndege tayari kwa wawili
hawa kurejea Arusha shuleni.
"Mama anapiga! Eve" Resh alimwambia Eve pale simu
yake ilivyoita.
"He! usiniambie huyo ndio mama,sasa mbona ulikubali
niongee nae usiku ule? aliduwaa Adam.
"Eti! uliongea nae? Yesu wangu!"
alishtuka Resh lakini Eve akamshauri azime simu
kwanza mengineyo watajua mbele kwa mbele naye
Resh akatii amri hiyo haraka akaizima simu bila
kupokea Resh kwa kiasi kukuwa alikuwa amemzoea na
kumwamini Eve.
Adam,Resh,na Eve waliagana kama watu
waliofahamia na kukaa pamoja siku nyingi sana,Resh
alimkumbatia Resh alimkumbatia Adam kwa muda
mrefu hadi Eve alipowatenganisha na kuambiana
Kwaheri.
***
Ilikuwa imebaki miezi minne wafanye mtihani wa
kumaliza kidato cha tano,Resh akiwa amekolea katika
penzi la Adam na kusahau kuhusu Mama yake
ambaye alikuwa amezuiwa na mwanaye huyo kwenda
pale shuleni kumsalimia kwa madai kwamba yeye
(Reshmail) anataka ajikite zaidi katika masomo.
Reshmail kwa maksudi akabadilisha namba yake ya
simu ili mama yake asiweze kumpata mara kwa mara
badala yake muda mwingi akawa anawasiliana na
Adam.
Mwezi wa pili ilikuwa ni likizo ya mwezi mzima kwa
wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita na pia
wakati huohuo wanafunzi wa chuo kikuu cha
mtakatifu Augustino huwa katika mapumziko mafupi
baada ya kumaliza muhula(Semister) ya kwanza.
**********************
Kwa Reshmail ulikuwa wakati muafaka wa
kumtambulisha Adam kwa wazazi wake jambo ambalo
aliamini lingesaidia kupunguza makali ya mama yake.
Tangu akiwa mtoto kamwe hakuwahi kuwakwaza
wazazi wake kwa sababu ya wanaume hata siku moja
hivyo alitegemea hawatampinga.
Ilikuwa siku ya furaha kubwa sana kwa Bi. Gaudencia
na familia yote kwa ujumla kumwona tena Reshmail
nyumbani baada ya miezi mingi tena akiwa mwingi wa
furaha. Lakini tofauti na mama yake alivyofikiria
kwamba mwanae huyo anafurahia kurudi katika
ulimwengu wao wa mapenzi haramu yeye(Reshmail)
alikuwa anafuraha ya kumtambulisha Adam ndani ya
siku chache.
Kwa kujua wazi kabisa mama yake atachukizwa na
maamuzi yake hayo,Reshmail aliamua kulifikisha hilo
mbele ya Mzee. Manyama ambaye ni baba yake.
"Kwa sababu ni uchumba tu na hakupeleki popote
hamna tatizo hata kidogo,mlete tu mwanangu mlete
una maamuzi mazuri sana sio kama wasichana
wengine wanafanya upuuzi kimyakimya mambo
yanapokuwa mabaya ndio wanasema" alijibu
mzee.Manyama huku akimshika mwanae huyo
shavuni,
Resh akatabasamu na kumkumbatia baba yake
"I love you dad(Nakupenda baba)" Resh akamwambia
kwa furaha tele mzazi wake huyo,huku moyoni
akijiaminisha kwamba hapatakuwa na kikwazo tena
kwa mama yake kwani baba ndiye kichwa cha familia.
Baada ya siku tano Adam aliwasili ndani ya kasri la
mbunge huyu.Alikuwa anaogopa na hakuamini kama
angepokelewa na kama angepokelewa alijua yatakuwa
mapokezi mabaya sana kwani katika simulizi
mbalimbali anazozisikia kwa watu zilimwonyesha
kwamba ni vigumu sana kwa wazazi kumwelewa
mtoto wa kike linapokuja suala la kumtambulisha
mwanaume kama mchumba wake.
"Da Rosemary nina hofu mie" Adam alimwambia dada
yake kipenzi waliyekuwa wameongozana naye
"Acha uoga bro mbona hata sisi babu yetu alikuwa
chifu? kwani chifu na mbunge nani zaidi" alitania
Rosemary kumwondoa hofu kaka yake.
Mapokezi waliyoyapata kutokea kituo kikuu cha
mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo
yaliwashangaza mno waliwakuta watu wa kuwapokea
na kwenda nao kwenye gari mbili walizokuja
nazo,waliwafikisha hadi getini ambapo kina dada
wawili kwa heshima kabisa waliwaongoza hadi
sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao,japo usoni
waliuficha mshangao wao lakini moyoni uliwajaa tele.
Adam akiwa ndani ya suti nyeusi wanazotumia
wanasheria katika shughuli zao na Rosemary aliyevaa
suti pia walielekezwa wapi walipo wazazi wa Reshmail
wakaenda kutoa salamu zao,ilikuwa ni hafla kubwa
sana ndugu,jamaa na marafiki wapatao miamoja
walikuwa wamealikwa na mheshimiwa huyu. Ilikuwa
kama harusi kwa asiyejua lakini ulikuwa utambulisho
tu.
Bwana na bibi Manyama walipendeza kwelikweli na
walikuwa na kila haki ya kuitwa wakwe na Adam.
Furaha ya Bi. Gaudencia ilificha chuki aliyokuwa nayo
moyoni dhidi ya Adam kwa kumchukua mwanae
ambaye ndio alikuwa anampa raha zote za dunia.
Hadi hafla inafikia tamati majira ya saa mbili usiku kila
mtu alikuwa amepata furaha kubwa sana,wabunge na
madiwani ambao ni marafiki wa karibu wa Manyama
walitoa zawadi nyingi kwa wawili hawa huku babu
yake Reshmail akitoa mawaidha yenye maana kubwa
sana katika maisha waliyotarajia kuyaishi Reshmail na
Adam siku za usoni.
Mzee Manyama kwa ombi la mwanae aliwasiliana na
wazazi wa Adam kuwa muda wa mapumziko ya siku
tano alizobakiza Adam amalizie katika familia
yake,hapakuwa na kinyongo wala kipingamizi
chochote walikubali kwa moyo mmoja na Adam
akaendelea kuishi pale huku dada yake akirejea
Mwanza kwa usafiri wa ndege ambao gharama zote
zilikuwa juu ya mheshimiwa Manyama.
Kila alipowasiliana na wazazi wake Adam hakusita
kuelezea upendo wa kipekee anaoupata kutoka familia
ya Reshmail hata wao walifarijika sana.
***********************