Post by Admin on Jun 7, 2015 4:45:09 GMT
Ilikuwa jumapili moja tulivu sana baada ya kutoka
kanisani familia yote akiwemo pia Adam,baba yake
Reshmail aliongozana na mwanae kwenda mjini kwa
lengo kuu la kuonana na walimu mbalimbali wa
masomo ya ziada(Tution) watakaompendeza Reshmail
basi waweze kumfundishia nyumbani.
Huku nyuma alibaki Adam pamoja na mkwewe (Mama
Reshmail) baada ya kupata kifungua kinywa Adam
alimwaga mkwewe kuwa anaenda kuzungukazunguka
bustanini
"Tena nilitaka nikwambie leo unataka uondoke hata
bustanini hujawahi kufika,afadhali nenda mwanangu"
alijibu mama Reshmail.
Ulikuwa mpango kabambe uliosukwa na Bi.
Gaudencia,kwa dhumuni kuu la kumwondolea
mamlaka Adam ya kuwa na Reshmail. Kwa kuwatumia
vijana kutoka katika ngome ya vigogo,ngome maalum
iliyokuwa inatumiwa na watu wenye pesa zao kwa ajili
ya kuwatenda vibaya watu wanaoonekana kuingilia
mambo yao aidha kimapenzi au kibiashara.
Alipoaga anaenda bustanini Gaudencia alitumia fursa
hiyo kupiga simu kwa wanaume hao wa shoka ambao
tayari alikiwa ameelewana nao bei.
"Ndani ya dakika tano tutakuwa hapo” ndio jibu
lililotolewa upande wa pili
Bila kuongezea lolote Bi.Gaudencia alikata simu yake
na kutoka nje.
"Babu kwa mama Veneranda si unapajua?" alitoa
swali hlo Bi. Gaudencia kwenda kwa mlinzi wao wa
getini.
"Ndio si yule mama anayesuka pale mbele"
”Hapo hapo haya haraka nenda kaniangalizie kama
kuna foleni kubwa" aliamrisha Bi. Gaude na mlinzi
akatii amri hiyo haraka haraka akaondoka katika lindo
lake akaenda kutimiza amri ya bosi wake.
Baada ya dakika takribani kumi alirejea mlinzi yule
"Yupo mmoja tu anamaliziwa" alileta taarifa hiyo kwa
furaha.
"Haya mi ninatoka nimemwacha Adam ndani amelala
akiamka mwambie nimetoka kidogo" alisema mama
Reshmail huku akiondoka.
“sawa bosi nitamwambia”
Masaa mawili badae alirejea akiwa amesukwa tayari
nywele zake,ni muda huohuo Reshmail na baba yake
walikuwa wametoka mizungukoni, walimkuta
Gaudencia anatokea ndani.
"Babu Adam alivyoamka ameenda wapi? au
bustanini?"Aliuliza Gaudencia na kuongezea
"Maana nimegonga chumbani kwake kimya, hebu
Reshmail ingia ukamwangalie ndani mwake humo
huenda amelala bado" kwa mwendo wa maringo lakini
harakaharaka Reshmail alijongea ndani.
"Babu unasema Adam hajatoka?" Resh aliuliza baada
ya kurejea akiwa na hofu kidogo usoni.
"Hajatoka na mimi hapa sijatoka tangu mama
alipoenda kusuka na kumwacha Adam amelala"
alijieleza mlinzi yule jibu lililopokelewa kwa furaha na
Bi.Gaudencia.
Jambo gumu zaidi kwa ambao hawakujua janja ya
mama huyu ni kwamba simu ya Adam ilikuwa
haipatikani hali hiyo ilileta wasiwasi sana, walisubiri
huenda atarudi hadi jioni hali ilikuwa tete ndipo mzee
Manyama alipoamua kupiga simu kituo cha polisi
maeneo ya jirani kwa sababu alikuwa mbunge msako
ulianza usiku huohuo.
Siku tatu zilipita bila taarifa yoyote kutoka katika kituo
cha polisi,Reshmail alikuwa amepooza sana kupita
maelezo mara kwa mara alimpigia baba yake simu na
kuuliza kulikoni lakini jibu bado lilikuwa lilelile kuwa
hajapatikana.
"Mama niache tafadhali,tena niache nasema upuuzi
wako siutaki tena niache!" alifoka Reshmail pale mama
yake alivyomkuta amekaa sebuleni na kujaribu
kumpapasa huku akimpa pole ya kupotelewa na Adam
wake ghafla.
"Mwanangu usiwe na hasira kiasi hicho polisi
watafanikisha upelelezi na watamrejesha Adam akiwa
mzima wa afya" alibembeleza Bi. Gaudencia lakini
Reshmail hakujibu kitu akajiondokea akiwa ameuvuta
mdomo wake sana.
********