Post by Admin on Jun 7, 2015 4:46:43 GMT
Siku ya tano polisi waliopewa jukumu la kufanya
upelelezi huo walirejea na taarifa yao huku
wakiambatana na ushahidi. Zilikuwa nguo aliyokuwa
amevaa Adam kwenda kanisani ikiwa na matundu sita
ya risasi na ikiwa imetapakaa damu pote, suruali
ilikuwa na matundu matatu ya risasi.
"Hapana hawezi kuwa Adam hata kidogo nasema
hawezi kuwa yeye" alifoka Manyama huku akiwa
wimawima mbele ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai jiji la Dar-es-salaam Chacha Boniphace au
maarufu kama Chacha B.
"Mheshimiwa lakini huu ni upelelezi wa awali
tunaendelea zaidi na zaidi tutazidi kutoa taarifa kadri
tunavyopata majibu mapya" alijieleza kwa utulivu bila
wasiwasi kabisa jambo ambalo kidogo lilirejesha
amani ya Manyama japo hofu tayari ilishaukumba
moyo wake kwamba huenda Adam ameuwawa tena
kikatili.
Ilikuwa ni shughuli pevu kwa Reshmail kuamini kile
ambacho alikuwa anaelezwa na baba yake kwamba
Adam anadhaniwa kuuwawa kwa risasi nane kisha
mwili wake hauonekani. Bi. Gaudencia tayari alikuwa
anaangua kilio kikubwa hata kabla maelezo
hayajaisha ikawa kazi kwa mumewe kumbembeleza.
"Mke wangu Adam hajafa ila inadhaniwa pia upelelezi
bado unaendelea jamani,ukilia hivyo unakuaribisha
msiba mama watoto sawa" alibembeleza mzee
Manyama huku amemkumbatia mkewe.
"Baba haiwezekani baba haiwezekani nguo za Adam
zipatikane katika hali hiyo halafu mnasema
hajafa,jamani Adam wangu wamemuua"
alipiga mayowe Reshmail ikamlazimu mzee Manyama
kufanya kazi mara mbili jambo ambalo lilimtoa jasho
mzee huyu.
"Reshmail mwanangu,tulia hiyo siyo taarifa rasmi
jamani ni majibu ya awali mbona mnanifanyia hivyo
au mnataka nipate presha nife?" alijieleza Manyama
huku akijifuta jasho kwa kutumia shati lake.
Reshmail mbio mbio akaondoka pale sebuleni akaanza
kuzipanda ngazi kuelekea chumbani kwake huku
akilia,mzee Manyama nae huyo nyuma yake.
"Reshmail mwanangu,njoo malkia wangu,njoo
mwanangu"
aliyazungumza hayo huku akimkimbiza kwa nyuma.
Wakati huo Bi. Gaudencia tayari alikuwa amenyamaza
kimya kabisa,akijaribu kupikicha macho yake.
Reshmail hakusimama hadi chumbani kwake
akajifungia,baba yake alibembeleza mpaka akachoka
hakupata jibu zaidi ya kilio cha kwikwi kutoka ndani.
"Baba Resh twende chumbani mume wangu,twende
utakaa hapa hadi saa ngapi cha msingi tumwombe
Mungu asije akajidhuru mwanetu"
Gaudencia alimnyanyua mumewe wakajikongoja
kuelekea chumbani kwao,Manyama akiwa amelegea
kabisa.
Asubuhi ya siku iliyofuata naibu waziri wa ulinzi na
usalama,alifika na msafara wake wa magari matano
kwa mbunge Manyama kuja kutoa pole ya kutokewa
tukio hilo lenye utata kwa mwenzao.
Shughuli ngumu iliyokuwa mbele yao ni jinsi gani
watawaeleza wazazi wake Adam ambao hadi dakika
hiyo waliamini Adam yupo salama na mwenye furaha
kwa mchumba wake Reshmail,Manyama alimuomba
waziri ashughulikie hilo suala na bila kupoteza muda
alinyanyua simu yake ya mkononi na kutoa taarifa
hiyo kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai
Mwanza pamoja na mawasiliano anayoweza kumpata
baba yake Adam.
Ilikuwa vigumu sana kwa baba Adam kuelewa
anachoelezwa lakini kwa kadri ya uwezo wake na
taaluma yake mkuu huyo alifanikiwa kumwelewesha
ambapo baba yake Adam aliondoka akiwa na
matumaini kwamba ipo siku Adam atapatikana.
Nyumba nzima ya kina Adam ilipooza sana dada yake
Adam (Rosemary) alikuwa analia muda wote kwa
uchungu hakuamini kwamba siku ile pale uwanja wa
ndege alivyosindikizwa na familia nzima ya
mhe.Manyama ndio ilikuwa mara ya mwisho kumwona
kaka yake kipenzi(Adam).
Uongozi wa polisi uliifikisha taarifa hiyo pale chuoni
ambao pia walipokea kwa simanzi kubwa.
"MAUAJI YA KUTISHA",
ndivyo mandishi meusi kabisa kwenye magazeti
mbalimbali yalisomeka,hali hiyo ilithibitisha kabisa
kuwa Adam hayuko hai tena.
Picha yake iliyoambatanishwa na habari hizo akiwa na
mtoto wa mbunge iliteka na kuumiza mioyo ya watu
wengi hasahasa vijana.
"Tumempoteza mwanasheria"
ndilo neno la pamoja walilosema wasomi wa chuo
kikuu cha mtakatifu Augustino Mwanza katika misa ya
pamoja kumwombea mema Adam kama yupo hai au
kumtakia pumziko jema la milele kama tayari Mungu
ameichukua roho yake,kila uso ulikuwa na simanzi
kubwa ilikuwa kama tamthilia.
Reshmail alikuwa kama zezeta,hamwelewi mtu
yeyote,roho yake ilimwambia kwamba mama yake
mzazi anahusika kwa namna moja au nyingine katika
tukio hili lililojaa utata.
Lakini ataanzia wapi kumweleza baba yake,atajisikiaje
mzee Manyama akigundua kwamba mke na mtoto
wake walikuwa katika ndoa haramu ya siri ndani ya
nyumba yake.
"Hapana sitaki kuongeza tatizo juu ya tatizo nitasubiri
liwalo na liwe,kama Mungu alimpanga Adam awe
wangu naapa sitaolewa na mwingine kamwe,lakini
kama hakuwa halali yangu basi ataletwa mwanaume
duniani kwa ajili yangu tena"
Alijipa ujasiri wa hali ya juu Reshmail huku
akijipigapiga kifuani.
"Nitarejea shule na nitasoma tena kwa bidii
sana,sitamwaza mwanaume yeyote tena alikuwa
Adam na atabaki kuwa Adam hadi Mungu aamue
tena"
aliendelea kujipa matumaini.
"Bibi yangu aliniambia maneno ya mdomo huumba
halisi,na nina uhakika ninachokiongea kwa mdomo
wangu Mungu ataniumbia"
Aliendelea kuongea huku machozi yakifumba macho
yake na kitambaa alichokuwa anatumia kujifuta
kilikuwa kimelowana tayari kwa wingi wa machozi
alikuwa kama yatima vile, Resh alikuwa akifungasha
baadhi ya mizigo yake tayari kwa kurejea shuleni
tena,tangu tukio la Adam kupotea hakuna
aliyetegemea hata siku moja Resh atawaza kurudi tena
shuleni kwani waziwazi akili yake ilionekana kuathirika
kwa kiasi kikubwa kwa kumpoteza Adam katika
mazingira yasiyoeleweka.
********