Post by Admin on Jun 7, 2015 4:47:42 GMT
"Baba kesho narejea shule si unajua tayari shule
imefunguliwa?" Reshmail alimkurupua mzazi wake
huyo kutoka alipokaa kwa mshangao
"Umesema nini malkia wangu!" alihoji Manyama huku
akiwa wima
"Narejea shule kesho" kwa msisitizo na tabasamu
alijibu Reshmail.
Mzee Manyama hakuamini kwani alikuwa akiwaza ni
namna gani atamshawishi mwanae aweze tena kurejea
shuleni baada ya matatizo yote yaliyojitokeza kwa
mchumba wake Adam ambaye hadi wakati huo bado
mwili wake ulikuwa haujapatikana wala taarifa yoyote
zaidi ya nguo zikiwa na matundu ya risasi na damu.
"asante sana mwanangu nakupenda sana" mzee
Manyama aliongea kwa furaha huku akimkumbatia
mwanae.
Tangu kupotea kwa Adam aliyehisiwa kuwa tayari
amekufa kulipokelewa kwa hisia tofauti na wananchi
huku asilimia kubwa ikiegemea upande wa imani
potofu za kishirikina wakihusisha tukio hilo na utajiri
alionao Mh. Manyama na uchaguzi uliokuwa mbele
yake.
**** *******
"Wamemtoa mwanangu kafara ili waongeze
utajiri,nilimwambia Adam aoe msukuma mwenzake
ona sasa,watoto wa siku hizi wabishi wanajifanya
wanajua sana na elimu yao inawadanganya"
mama yake Adam alikuwa analaani vikali mbele ya
mume wake wakiwa ndani ya nyumba yao maeneo ya
Igoma kwa 'one-way'
"Usiseme hivyo mama Adam kumbuka sisi ni
wakristu,tumwachie Mungu yeye ndio atajua nini cha
kufanya"
Babaye Adam alimtuliza mkewe huku
akimgongagonga mgongoni kwa kutumia kiganja cha
mkono wake wa kuume.
Mawasiliano baina ya familia hizi mbili ya Adam jijini
Mwanza na ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa
yamekatika licha ya baba yake Adam (mzee Michael)
kutangaza kuwa kutoka moyoni mwake amesamehe
yote yaliyotokea na anaamini ni mipango ya Mungu.
Lakini kinyongo kilionekana dhahiri kwa
matendo,upendo wa zamani haukuwepo tena jambo
hilo lilimfadhaisha sana mzee Manyama kiasi cha
kukondeana na kukosa umakini katika utendaji wake
wa kazi jambo lililoishusha sana heshima yake kama
mbunge aliyekuwa anaheshimika sana kuanzia
bungeni hadi jimboni kwake,
Wapinzani walitumia fursa hiyo kumchafua hasahasa
na kweli uchafu huo ukakubalika kwa wananchi kwa
ujumla Manyama hakuwa na lake tena pale,wananchi
walimpuuzia sana tofauti na zamani na hata hiyo
miaka miwili iliyobaki wananchi waliiona kama ni
mingi sana kuwa na kiongozi wa aina yake.
Kuliko fedheha yote hiyo Mh. Manyama kwa hiari yake
mwenyewe alipitisha kura ya maoni ya wananchi
kuhusu imani waliyonayo kwake kama mbunge wao.
Asilimia 70 ya waliopiga kura walidai hawana imani
naye huku asilimia kumi na nne tu ndio wakidai bado
wana imani naye na kura zilizobaki zikiharibika,rasmi
Manyama akawa ametolewa bungeni na katika
uchaguzi mdogo uliofanyika akachaguliwa mbunge
kutoka chama cha upinzani na maisha yakaendelea
huku Mh.Manyama akiendelea na biashara zake
mikoani.
* **
Adam akiwa pale bustanini alivamiwa ghafla na
wanaume wawili wa shoka wakiwa na bunduki,ishara
ya kidole mdomoni ilimfanya atulie tuli kisha
wakamwonyesha ishara kwamba awafuate alifanya
kama walivyotaka hadi kwenye gari iliyokuwa imepaki
pembeni kidogo ya nyumba yao Adam alishangazwa
sana na ukimya uliokuwepo hakuwepo mlinzi wala
mama mkwe wake.
Safari yao ilikwenda mpaka Iringa gari iliyokuwa na
vioo vyeusi 'tinted' ilimzuia Adam kujua ni wapi
alipo,gari ilizimishwa ndani ya jumba kubwa sana
ambapo alipelekwa kwenye chumba kikubwa tu,hofu
kubwa ilimtawala hakujua kwa nini yuko
pale,hakupigwa wala kupewa bughudha yoyote,hali
hiyo ilzidi kumshangaza
"au ndio wachuna ngozi" alijiuliza Adam kwa hofu tele.
Hayo ndio masharti ambayo mama Reshmail alitoa
kwa vijana aliowapa tenda hiyo ya kumtorosha Adam
pale nyumbani. Shida yake haikuwa kumtesa Adam
bali kumweka mbali na mwana (Reshmail) ambaye
alikuwa amempagawisha ipasavyo katika mapenzi ya
jinsia moja.
Suala la pesa halikuwa tatizo hata kidogo alichohitaji
ni kutimiziwa alichotaka. Mkataba wa miaka mitano
ndio alioingia na watu hawa kukaa na Adam bila
kumruhusu kutoka nje ya jingo.
Bi Gaudencia aliamini kwamba kwa kutokomea Adam
mbele ya uso wa Reshmail ilikuwa fursa nzuri ya
kurudisha tena uhusiano wake na Reshmail ambao
ulikuwa unaelekea kufa lakini kinyume chake alikuwa
ameibua chuki kubwa baina yake na mwanae “heri
wote tukose kama ni hivyo” alijiapiza mama Reshmail
baada ya kuona dalili za kumshawishi Reshmail
hazipo tena
Alikuwa ni Reshmail mwingine kabisa mkasa
uliomkumba ulimbadilisha sana na kuitanua akili yake
sana,Eveline naye alisikitishwa na yaliyomkumba
shoga yake akajitahhdi sana kuwa karibu naye kumpa
moyo huku akijiepusha sana kufanya vitendo ambavyo
vitamkumbusha Resh jinsi alivyoweza kukutana na
Adam.
Ni katika kujiepusha na kumkera rafiki yake huyo
kipenzi Eveline akajikuta amefuta picha za uchi na
filamu za ngono katika kompyuta yake akawa si mtu
wa kutoroka shule,hakuwa tena mtu wa wanaume na
hatimaye akawa Eveline wa kuigwa na wanafunzi
wenzake jambo hilo liliwaduwaza sana wanafunzi pale
shuleni lakini ndio hivyo Eve alikuwa amekubali
mabadiliko katika maisha yake.
Juhudi zao katika masomo ziliendelea kuwaweka
katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri mtihani wao wa
mwisho. Hawakuyazungumzia tena yaliyopita tena
walijadili mapya na yanayowanufaisha
"Eveline wewe ni kama dada yangu nakupenda sana"
"Nakupenda pia Reshmail umebadili maisha yangu
moja kwa moja nina maisha mazuri sasa" alijibu Eva
kwa upole huku akimwangalia Reshmail aliyekuwa
anaishusha chandarua yake aweze kulala. Ni kweli
walitokea kupendana wawili hawa.
"Hivi Resh una mpango bado wa kusomea uhasibu mi
lazima niwe mhasibu"
"Mh! unavyojiaminisha utadhani tumefaulu tayari"
alijibu Resh.
"He! mi najua sisi kufaulu kwetu sio swali ni jibu,swali
ni je tunaenda chuo gani na kusomea nini."
alijiaminisha Eveline.
"ok! nilidhani nitasomea uhasibu lakini kwa heshima ya
Adam nitasomea sheria" alijibu Reshmail kwa furaha.
"Mh! na upole wako huo na mambo ya kutoa hukumu
wapi na wapi? mwenzio naangalia ankara" alisema
Eva.
"Wala hata siendi kuhukumiana naenda kwa heshima
tu" alisisitiza Reshmail.
"Mh! haya mheshimiwa hakimu napenda kujitetea
kama ifuatavyo"
Eve alitania akifuatiwa na kicheko kikubwa kutoka kwa
Reshmail.
* * ***************