Post by Admin on Jun 7, 2015 4:48:55 GMT
Maisha yaliendelea vyema sana tu japo yalikuwa
maisha ya mashaka Adam aliruhusiwa kuongea na
kuuliza kila kitu kasoro swali moja tu "Kwa nini niko
hapa?",ndio hakuruhusiwa kuliuliza hata kwa
mbali,watu wote pale hawakuwa na ubaya nae hata
kidogo,hawakumtesa,hakugombezw a wala hakufanya
kazi,alipewa huduma zote za msingi,aliweza kutoka
nje na kwenda bustanini lakini nje ya geti
hakuruhusiwa.
Tayari aliyazoea maisha haya lakini kumbukumbu ya
jinsi alivyochukuliwa ndani ya jumba la wakweze bila
kupata msaada wowote ule "Nani atakuwa nyuma ya
haya yote mlinzi alikuwa wapi? Mama Resh je?"
alijiuliza sana bila kupata wa kumpa jibu.
"Hivi unaitwa dada nani vile?" Adam alimuuliza dada
mmoja ambaye kila baada ya siku tatu alikuja kufanya
usafi katika chumba chake.
"Naitwa Beatrice Cosmas niite Bite" alijibu huku
anafuta vioo kwa dirisha la chumba cha Adam.
"Una jina zuri wewe mh!"Alisanifu Adam.
"Asante wewe ni Adam eeh!" aliongezea yule binti
huku akiwa ameacha shughuli yake aliyokuwa
anafanya.
"Ndio mimi ni Adam! samahani nikuulize maswali
machache"
"Uliza tu lakini sitakujibu sasa hivi"
"Kwa nini?"
"We uliza yote ndo nitakwambia kwa nini"
"Hivi hapa ni wapi? kwa nani? na kwa nini nipo
hapa?"
"Ndio hayo matatu tu?...sawa nitakujibu kwa sharti
dogo sana yaani"
"Sharti gani hilo mi nipo tayari"alitoa uhakika Adam
bila hata kulijua sharti lenyewe.
"Sikia Adam sina haja ya kuzunguka zunguka nina
mwaka wa pili hapa kitu kinaitwa mwanaume katika
mwili wangu ni kama ndoto sasa ni wewe wa kutii kiu
yangu na mimi nitajibu maswali yako" alijieleza
Bite,jambo ambalio lilikuwa zito na la kumshangaza
Adam.
"Mh! au ndo mtego tena kutoka kwa Reshmail? dah!
ikiwa hivyo nitaaibika kweli mimi"Alijiwazia Adam kwa
mashaka makubwa kabla ya kujibu.
"Basi utakuja kunijibu baadaye!" alisema Adam.
"Haya usiku na wewe jiandae" alijibu na kuaga Bite.
Hayawi hayawi mara yakawa usiku wa saa tatu,Bite
tayari ndani ya chumba cha Adam ndani ya khanga
moja peke yake.
"Haya nipe nikupe hakuna longolongo hapa"
alizungumza Bite.
"Subiri taratibu basi,sikiliza" alianza kujitetea Adam
wakati Bite anajisogeza kitandani,Adam alikuwa
amechelewa tayari joto la Bite lilipenya katika mwili
wake na kumchanganya hadi kujikuta akifanya
kinyume na alivyotarajia kwamba atafanikiwa kutegua
mtego wa Bite badala yake alikuwa ameshafanya
mapenzi na Bite.
Kwa Bite ulikuwa ushindi mkubwa sana kwani tangu
aletwe hapo kuwa msaidizi wa kazi za ndani ya
vyumba hakuwahi kutoka nje ya jengo hilo,sio
kwamba alikuwa amefungwa hapana kila kitu
kilikuwepo ndani kila siku pia alikuwa ameridhika
kuwa hapo.
"Hapa ni Iringa,nimejibu swali lako la kwanza
tuendelee tena nikujibu swali la pili na tatu" alisema
Bite kwa shauku kubwa sana.
"Hapana Bite imetosha kwa leo sijisikii vizuri,siku
nyingine basi sawa!" alidanganya Adam na Bite
hakuwa mbishi akambusu Adam shavuni
akajiondokea zake.
Ilimchukua takribani siku tano Bite kugundua kwamba
tayari ameshika ujauzito jambo ambalo
halikuruhusiwa katika jumba hilo na alipewa onyo kali
wakati anaingia hapo. Kwa usalama wake na Adam
alifikiria suala la kutoroka lakini haya yote aliyafanya
baada ya kuongea na Adam na kumweleza hali halisi.
Ni katika wasaa huo alimweleza Adam chanzo
ambacho kinaweza kuwa kimemsababishia yeye
kuwepo pale
"Umemchukulia kigogo mpenzi wake,umemendea
mtoto wa kizito au umemkataa kimapenzi mtu
maarafu" hizo ndizo zilikuwa baadhi ya sababu
alizoorodheshewa na Bite,lakini kwake yeye aliona
hakuna hata moja inayomuhusu kwani wazazi wote
wawili wa Reshmail walimpenda sana hakuwa tayari
kuweka hisia kwamba pengine moyoni wanamchukia.
"Usijali lakini hutakaa milele humu,huwa unafika
Muda aliyekuweka humu akiridhika unatoka.
"Nitamlea mtoto,napenda watoto hata kama
usipokuwa mpenzi au mume wangu nitampenda sana
na nitamwita....."
"Christian akiwa mvulana au Christina akiwa
msichana" alidakia Adam ambaye kwa mbali alianza
kumtamani Bite kimapenzi.
* * *
Biashara za baba yake zilikuwa zinaendelea vizuri na
skendo lake lilikuwa linafifia taratibu. Hadi anamaliza
kidato cha sita Reshmail mapenzi kwa wazazi wake
yalikuwa palepale na japo hakutaka kumwongelea
Adam jena alikuwa na picha yake waliyopiga pamoja
siku moja kabla ya tukio lile la kushangaza na
kuumiza.
Reshmail kwa ruhusa ya wazazi wa Eveline alienda
nae mpaka kwao ambapo walikaa wote kwa siku tano
kisha akarejea tena Arusha.
Urembo wa Reshmail ulipagawisha kila mwanaume na
hata baba yake ilifikia kipindi akakiri kwamba kweli
pale alizaa mtoto mmoja wa kipekee na kweli alikuwa
wa kipekee. Mama Resh bado alikuwa na matamanio
lakini kwa sasa alimwogopa sana Reshmail tofauti na
miaka mingi iliyopita.
"Baba na mama wiki ijayo nataka kwenda Mwanza
kwa wazazi wa Adam" Resh alitoa hoja yake wakiwa
mezani wanakula.
"Wapi? Mwanza! hawatakuelewa mwanangu utakuwa
kwa maksudi kabisa unafufua shari iliyopoa tayari"
Kwa busara tele na upole mzee Manyama alimweleza
mwanae ambaye pia aliyapokea kwa nidhamu ya hali
ya juu na kichwa chake kuyakubali kuwa yana maana
kubwa ndani yake.
"Nimekuelewa baba sitaenda tena" alijibu kwa
unyenyekevu sana Reshmail.
* * * *