Post by Admin on Jun 7, 2015 5:00:54 GMT
Matokeo ya kidato cha sita yalipotoka hayakuwa ya
kushangaza sana kwa upande wake kwani alikuwa
amevuna alichokipanda. Reshmail alikuwa amepata
daraja la kwanza na ndivyo alivyotarajia,furaha yake
iliongezeka baada ya kumwona katika orodha Eveline
Maige rafiki yake kipenzi naye akiwa amepata daraja
la kwanza huku wakitofautiana pointi kadhaa.
Akiwa anajiandaa kumpigia simu tayari simu yake
iliwakawaka na kuandika "pacha" jina ambalo alikuwa
amemwandika Eve katika simu yake,badala ya
kuongea wote kwa pamoja wakaanza
kucheka,walicheka sana hadi simu ilipokatika. Zilikuwa
ni furaha kutoka moyoni,kwa nini wasifurahi wakati
ndoto zao zilikuwa zinatimia?
Tanzania Commission of Universities (T.C.U) ilipotoa
uchaguzi wa kwenda vyuoni Reshmail kama
alivyopenda alichaguliwa chuo kikuu cha mtakatifu
Augustine Mwanza kwa masomo ya sheria huku
Eveline Maige akipelekwa Mzumbe chuo kikuu kwenda
kuchukua masomo ya uhasibu shahada ya juu.
"Ndugu hakimu naomba kujitetea!" Eve alimtania Resh
utani wao wa shuleni siku walipokuwa wanaagana.
Walikuwa wametenganishwa hatimaye lakini
mawasiliano yao yalidumu
Kama alivyojiwekea kiapo chake cha kutopenda
hovyohovyo ni hivyohivyo alivyoingia pale
chuoni,hakuringia uzuri wake lakini hakutaka pia
usumbufu unaopitiliza kutoka kwa wanaume yaani
kwa kifupi alikuwa na msimamo mkali sana,ni rafiki
yake (Eve) pamoja na wazazi wake ambao wangeweza
kubashiri sababu hasa inayomfanya binti huyu awe
hivi na si mtu mwingine pale chuoni.
Maringo yake yalifichwa na werevu wake
darasani,kwani ilikuwa ni warembo wachache sana wa
aina yake waliofanya vizuri kimasomo,jambo hilo
lililowavutia waalimu wengi sana na wanafunzi ambao
wanapenda maendeleo kimasomo. Reshmail hakuwa
mtu wa mambo mengi hakunywa pombe wala kwenda
kumbi za starehe usiku starehe yake ilikuwa ni kusoma
na michezo.
Mnamo mwezi wa pili michezo ya FAWASCO ilipoanza
michezo hiyo inayohusisha vitivo vyote pale
chuoni,kwa maksudi alichaguliwa kuwa mhamasishaji
kwa wasichana wajibu alioufanya vizuri ipasavyo na
kikubwa zaidi akawa pia mdhamini mkubwa sana.
Moyo wake wa kujitolea uliwavutia sana wanadarasa
wenzake ambao baadhi walimpenda huku wengine
wakidai ana maringo, msimamo wa Reshmail ulibaki
palepale.
Mwaka wa pili pale chuoni ndio ulikuwa mbaya kwake.
Darasa walilolitumia mwaka wa pili wanafunzi wa
kitivo cha sheria,lililojulikana kama Mombasa Raha
kwa mbele lilikuwa na picha kubwa sana ya Adam
ambayo ilikuwa pembeni ya ubao wa kufundishia hiyo
ikimaanisha kwamba kila atakapoingia darasani
lazima aione,"ADAM THE GREAT" yaliandikwa
maandishi haya chini ya picha kubwa ya Adam.
Amani,ikatoweka kabisa moyoni mwake kumbukumbu
mbaya za kumpoteza mpenzi wake Adam zikaanza
kumrejea kwa kasi sana.Reshmail akaanza kujihisi
yeye ndiye chanzo cha yote hayo,tofauti na waalimu
wake hakuna mwanafunzi aliyemfahamu Adam zaidi
ya kujua tu historia ya yaliyomkuta na wengi
kuichukulia kama simulizi tu ya kusadikika. Reshmail
alianza kuwa mtoro darasani na hata alipoingia
badala ya kumwangalia na kumsikiliza
mwalimu,mawazo yake yote yalivutwa na picha ya
Adam yenye tabasamu pana mara zote aliamini
inamuangalia yeye na kumlaumu kwa kumkatisha
masomo yake kwa penzi la mtandaoni.
"Adam stop blaming me!!(Adam usinilaumu)" alipiga
kelele kwa nguvu Reshmail bila kujitambua.
Mwalimu alimshangaa na hakuelewa kilikuwa
kimemsibu nini "Is she dreaming? (Anaota?)" aliuliza
mwalimu Sijjo aliyekuwa anawafundisha somo la
mawasiliano (Communication skills),darasa zima
likacheka kwa fujo sana,lakini Reshmail alikuwa analia
huku akitetemeka sana,kwa ghadhabu akasimama na
kutoka nje.
Japo ulikuwa ni mwezi mmoja tu tangu waanze
masomo ya mwaka wa pili lakini
tabu na mateso aliyokuwa ameyapata yalitosha
kumshawishi kuwa huenda amesoma hapo kwa miaka
kumi.Wazazi wake hawakuwa na la kufanya,Eveline
alibaki kumwonea huruma shoga yake huyu alijaribu
mara kwa mara kumpigia simu lakini haikuwa tiba ya
tatizo la Reshmail.
Ni kweli Reshmail asingeweza kujilazimisha kuwa na
furaha kwani ni yeye aliyemshawishi Adam awe nae
kimapenzi na ni yeye huyuhuyu alimshawishi Adam
aende kwao kwa ajili ya kujitambulisha na safari hiyo
ikawa ya mwisho ya Adam.
"Nikiwaambia waalimu wangu watanielewaje,na hata
wakinielewa itakuwaje wanafunzi wenzangu wakijua
siri hii? watajenga picha gani tena kuhusu mimi, mh!
niepushe na hali hi bwana,kama uliweza kuniondolea
mawazo haya hadi nikamaliza kidato cha sita vyema
hebu baba na sasa ondoa tena na hili jaribu zito
mbele yangu na jina lako lisifiwe."
aliweka ombi fupi Reshmail katika mawazo yake hayo.
Lilikuwa ni jambo gumu sana kwa Reshmail alikonda
sana na punde si punde maneno ya wakosaji
yakaanza tena "Mh! kumbe ndio maana anakataa
wanaume kumbe anaishi kwa matumaini maskini,dada
mrembo kama huyu" yalisikika maneno hayo katika
vijiwe vya wanafunzi pale chuoni.
Ilikuwa ni kero kubwa kila alipokatiza vidole
vilimwelekea yeye umaarufu wake wa awali kwamba ni
mrembo ukaongezeka maradufu karibia chuo kizima
lakini wakati huu ilikuwa ni sifa mbaya kwamba ana
virusi vya UKIMWI hata yeye aliyasikia maneno hayo
yalikuwa yakivuma kwa kasi,hakuwa na uwezo wa
kuzuia tetesi hizo
"Wangejua kwamba mi ni bikra na wanayoyasema yote
ni uongo,hata wasingenyanyua midomo yao michafu
kuropoka upuuzi huo,lakini bila Adam watajuaje?"
alijiuliza Reshmail akiwa chumbani mwake katika
hosteli ya Ngulelo aliyokuwa amepanga chumba
alichoishi peke yake. Marafiki zake taratibu wakaanza
kumtenga wakiamini ameathirika,hilo halikumuumiza
kichwa kwani alilitegemea sana hasa hasa dhana ya
unyanyapaa kwa waathirika iliyokuwa inatawala
chuoni hapo.
***
Bite alifanikiwa kutoroka katika ngome ile kubwa
aliyokuwa amehifadhiwa Adam. Kwa jinsi alivyokuwa
amezoeleka pale haikumchukua muda mrefu
kumshawishi mlinzi amfungulie geti atoke kidogo na
ndio ikawa jumla hakwenda mbali sana na mkoa wa
Iringa bali aliweka kambi yake maeneo ya Uyole
Mbeya mkoa uliopo jirani na Iringa ambapo kipesa
kidogo alichoondoka nacho pale ndani alifungua
kibanda chake sokoni na kupanga nyumba eneo jirani
la Igawilo akianzia maisha ya kulala chini hadi
aliponunua godoro.
Biashara ya kuuza nyanya na mbogamboga ilimkimu
sana maisha yake kwani wazo wala tegemeo lake
halikuwa kununua gari,au kujenga nyumba hapana
lengo lake lilikuwa uhai pekee,na shilngi elfu moja
alizozipata zilikuwa zinamtosha kabisa.
Alikuwa mchangamfu na mstaarabu sana,wateja
walivutika kwake kwa kasi kufaidi ukarimu wake katika
biashara.Tumbo lake lilianza kukua taratibu,kina
mama sokoni wakaanza kuhisi tayari Bite kapata
mjanja Mbeya amemjaza mimba,lakini miezi yake ya
kujifungua ndiyo ilifungua akili za waliokuwa na
maswali na kugundua kwamba ile mimba alikuja nayo
pale na sio kwamba aliipatia pale. Salama bin salmin
Bite alijifungua mtoto wa kiume miezi tisa ilipowadia.
"Mh! baba yake atafurahi tena alimpa jina pale tu
nilipomwambia nimeshika mimba" Bite kwa furaha tele
aliwaambia kina mama wa pale sokoni,akiwemo jirani
yake mama wawili,ni hao ndio walikuwa ndugu zake.
"Hongera Bite,sijui ndio unakuwa mama nani vile" Bite
alihojiwa na mama wawili
"Mwanangu anaitwa Christian" alijibu Bite huku
akibusu kichanga chake hicho ambacho kilikuwa
kinarusharusha miguu na mikono yake huku na huko.
Christian alizaliwa akiwa na afya tele na
hakusumbuliwa na magonjwa wakati wa ukuaji wake
mwaka wa kwanza,ilikuwa furaha kubwa kwa mama
yake.
**************