Post by Admin on Jun 7, 2015 5:07:11 GMT
Miaka ilizidi kukatika wazo la Bi. Gaudencia kumtoa
Adam katika jumba lile lilikuwepo kichwani mwake
kwani udhaifu alioupata Reshmail pamoja na kashfa
mbaya anazozipata pale chuoni zilimsononesha sana
lakini ataanzia wapi kuificha aibu yake pale ambapo
Adam,akasababisha uovu wa mama huyu uwekwe
hadharani.
Ni jambo hilo lililomuumiza kichwa mama huyu.
"Reshmail na baba yake watanielewaje kwa mabaya
niliyowafanyia,nimeishusha heshima ya mume wangu
aliyekuwa na heshima kubwa bungeni" alizidi kuwaza
Huku Iringa maeneo ya Ruaha Adam alikuwa
anauanza mwaka wa tatu,akiishi kama nyumbani
kwake,lakini hakuridhika hata kidogo maisha hayo ya
ufungwa.
Miaka mitatu ilikuwa mingi sana "Mama na baba
yangu wanahisi niko wapi? vipi kuhusu mpenzi wangu
Reshmail,hapana imetosha nahitaji kutoka hapa,lakini
lazima nijiulize nitatoka vipi hapa katika ngome hii"
alijisisitiza Adam japo ulinzi madhubuti ulioongezwa
kutokana na kutoroka kwa Bite katika mazingira ya
kutatanisha pale ngomeni
***
Mwaka wa pili uliisha hivyohivyo kimateso makali
yaliyojawa na kumbukumbu mbaya na isingekuwa
kuhamishwa kwa darasa la sheria mwaka wa pili
kwenda katika maghorofa ya Mwanjonde chuoni hapo
basi Reshmail angefeli vibaya masomo yake kutokana
na msongo wa mawazo.
Akiwa mwaka wa tatu afya yake ilirejea tele kwani
hakuwa akiiona tena picha kubwa ya Adam machoni
pake hali hiyo ya afya kurejea ilizusha msemo mpya
tena,tofauti na mwanzo walivyosema ana Ukimwi,sasa
walisema "Akikonda ana virusi,akinenepa ameanza
kutumia dozi"
Yote hayo alituhumiwa Reshmail lakini kamwe
hakuwahi kuthubutu kunyanyua mdomo wake kujibu
vijembe hivyo yeye alikuwa mkimya huku akipambana
na masomo hadi alipoumaliza mwaka wake wa nne
vyema.
Mnamo mwezi wa kumi na moja familia yake yote
ilisafiri kuelekea jijini Mwanza kusheherekea kwa
pamoja mahafali ya mtoto wao,Eveline ambaye tayari
alikuwa kazini baada ya kuwa amemaliza miaka yake
mitatu chuoni na kufaulu vizuri pia alijumuika katika
kukamilisha furaha hii ya rafiki yake mpenzi huku
akiongozana na mchumba wake Benjamin Simon.
Reshmail alifurahishwa sana na ujio wa Eve kwani
alizidi kudhihirisha kuwa ni kiasi gani yeye ni rafiki wa
kweli.
Yalikuwa ni mahafali makubwa na ya kipekee kuliko
yote yaliyowahi kutokea ambapo chuo cha
Mt.Augustino kilifanya mahafali ya pamoja na matawi
yake yote Tanzania,yaani Iringa,Mtwara na Tabora.
Kwa ufupi yalikuwa yamefana.
Ni katika pirikapirika na pitapita za huku na huko za
sherehe hiyo ndipo Reshmail akiwa na Eveline ana
kwa ana anakutana na familia ya Adam yaani baba
na mama yake,aliwatambua kwa uwepo wa Rosemary
yule mdogo wake Adam.
Rosemary alikuwa ndio kwanza amehitimu shahada ya
elimu katika chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi
la mtwara hivyo yeye na familia yake pia walikuwepo
katika viwanja vya Raila Odinga kusheherekea
mahafali yale.
"Mchawi...mchawi!" alianza kupiga kelele mama yake
Adam wakati Reshmail akisogea taratibu katika eneo
walilokuwepo kwa furaha.
"Uuuwii" alipiga makelele kwa sauti ya juu jambo
lililovuruga usikivu katika eneo lile na watu kuanza
kumwangalia yeye kama mtu aliyechanganyikiwa,
Reshmail na Eve walikuwa wameganda tu na mama
Adam akizidi kupiga kelele,
Jitihada za baba yake Adam kumtuliza mkewe
hazikufua dafu,mara ghafla mama Adam akakurupuka
akiwa na chupa iliyokuwa na soda ambayo
haijafunguliwa bado na kwa kasi akaenda kumkabili
Reshmail ambaye akili yake ni kama ilikuwa
imesimama na umati uliokuwa umemkazia macho kwa
kitendo cha kuitwa mchawi ulimzidishia hofu na
fedheha kwake, Eve alimshika mkono Reshmail na
kujaribu kumvuta watoke eneo lile lakini tayari mama
Adam alishawafikia na kwa nguvu kabisa akaituliza
chupa ile juu ya kichwa cha Reshmail palepale
akaenda chini huku damu nyingi ikimtoka kichwani.
Wanaume watatu akiwemo pia baba yake Adam
walifika na kumbeba juu juu,mama Adam ambaye
alionekana dhahiri kuwa bado hajaridhika na kipigo
alichotoa kwa Reshmail kwani bado alikuwa
anaangaza huku na huko kama palikuwa na silaha
nyingine. Alikuwa kama mwendawazimu.
Wengine walimbeba Rshmail ambaye joho lake la
kipekee kabisa lilikuwa limechafuliwa vibaya na vumbi
la uwanja wa mpirawa miguu wa Raila Odinga
ambapo ndio sherehe zilifanyika. Hali ya sintofahamu
ilitawala sherehe zile kwa takribani nusu saa nzima
hadi Reshmail alivyoondolewa na familia yake
kuelekea hospitali na mama Adam kutiwa katika nguvu
ya dola
***
Halikuwa jeraha kubwa sana nyuzi mbili zilipita katika
kichwa chake kushona jeraha lile
“kwa nini mama mkwe wako akutende hivi” eve
alimuuliza Reshmail akiwa pale kitandani
“ni haki yake hata kunipiga risasi mimi ni chanzo cha
maumivu haya wanayoyapata” alijibu Resh huku
akilazimisha tabasamu
“kwa hio hapa amenionea huruma sana mimi ni
sawasawa na muuaji tena wa kukusudia na haki
yangu ni kuuawa pia” aliendelea Reshmail huku akitoa
tabasamu hafifu tena
“usiseme hivyo mamii sio wewe uliyetaka iwe hivyo ni
Mungu pekee” aliongea kwa upole Eve huku
akivibinyabinya vidole vya Reshmail
“mama mwambie baba afatilie mama mkwe asije
kulazwa selo hata kwa saa moja hana kosa lolote”
Reshmail alimwambia mama yake alipoingia katika
chumba cha hospitali ya Agha khan aliyokuwaelazwa
kwa ajili ya matibabu maneno hayo yalimshangaza
sana mama yake aliyetegemea Reshmail atakuwa na
hasira ya kutendwa vile mbele ya hadhara
Nafsi ilikuwa inamsuta sana mama reshmail,moyo
uliomba msamaha lakini mdomo ulikuwa mzito sana
kufanya hivyo. Hali hiyo ilimkondesha sana na
kumkosesha raha ndani kwa ndani unene wake wa
asili uliyafunika yote hayo na hakuna aliyejua jambo
zito alilobeba mama huyu.
Kweli badala ya bwana na bibi Manyama kuegemea
upande wa mashtaka ili mama Adam apewe adhabu
la wao waliunga mkono kwamba Reshmail alikuwa na
makosa mahakama ikatupilia mbali mashtaka hayo na
mama Adam akawa huru,jambo hilo badala ya
kurudisha undugu liliongeza chuki na uadui
“si nilikwambia ukabisha?? Kama hawajamtoa
mwanetu kafara kwanini sasa wamekubali niachiwe
huru??” mama Adam alimwambia mumewe jambo
ambalo wakati huu hata yeye alikubaliana nalo kuwa
motto wao mkubwa wa kiume(Adam) alitendwa vibaya
na familia ya reshmail .
kuamini kwa mzee Michael baba yake Adam ni sawa
na familia nzima kuamini kabisa na sumu ya chuki
ikamwingia kila mwanafamilia na kuwa aadui
wakubwa wa familia ya mzee Manyama.
* * * * * * * * *