Post by Admin on Jun 7, 2015 6:00:42 GMT
Siku mbili alizokaa pale hospitali hakuja hata
mwanafunzi mmoja kutoka pale chuoni kuja kutoa pole
kwa Reshmail wote waliogopa wakiamini alikuwa
mshirikina .
Eve hakukubaliana hata kwa mbali na shutuma hizo
kwani alimwamini sana Reshmail hivyo aliendelea
kuwa pale hospitalini pamoja na mchumba wake
kumuuguza Reshmail ambaye alitoka siku tatu
baadaye.
“baba mimi nitaenda na Eve kwake nitakaa siku tano
ndio nitakuja huko” Reshmail alimpa taarifa hiyo baba
yake naye hakupinga kwani amani aliyokuwa nayo
Resh akiwa na Eve ilikuwa kubwa mno hali iliyowapa
faraja hata wazazi wake hivyo walimruhusu bila
kusita.
Siku hiyohiyo walipanda ndege kwa gharama za
mchumba wa Eveline aitwaye Benjamin
Simon,kuelekea Iringa ambapo Eve alikuwa amepata
ajira katika benki ya N.B.C tawi la hapo.
Maisha yao yalikuwa mazuri sana kwani Benny
alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari hivyo katika
majukumu waliweza kusaidiana na upendo wa dhati
kati yao ulipendezesha zaidi nyumba yao.Reshmail
alivutiwa sana na maisha hayo na kumkumbuka sana
Adam wake “laiti angekuwepo tungeishi hivi siku moja
“ alijiwazia Reshmail wakati akiwaangalia Eve na
Benny wakiwa kwenye kochi wamebebana kwa furaha
huku wakitaniana
Ilikuwa jioni moja Reshmail na Eve wakiwa katika
mizunguko ya hapa na pale mizunguko ambayo kwa
namna moja au nyingine iliibua ghafla safari ya
kuingia sokoni,waliingia hapo kununua matunda
matunda,zilikuwa zimepita siku tano na tofauti na
alivyowahaidi wazazi wake hata hakuwa amefikiria
kurudi Dar maisha ya Iringa yalikuwa yamempendeza
sana .
“Eveline ona eveline jamani angalia kale katoto!!!”
Reshmail alimgusagusa begani Eveline huku
akimwonyesha kikundi fulani cha watoto pale sokoni
“wewe achana hao machokoraa walionikwapua pochi
langu sina hamu nao hata kidogo,kisimu changu cha
mchina na shilingi elfu thelathini zikapotelea hewani
looh!! Wabaya hao” aliongea kwa hasira Eve huku
akisitisha zoezi la kula chungwa aliliokuwa anafanya
kwa wakati ule.
“mh!! Eve jamani achaga uongo yaani katoto kama
kale jamani hebu kaone kale kadogo “Reshmail alizidi
kusisitiza lakini Eve alionyesha bado ana uoga na
uchungu moyoni wa kuibiwa vitu vyake na watoto
aliowaita machokoraa
“Reshmail shauri zako vitakuliza hivyo we endelea
kusema ni vitoto………..mh!! Resh lakini kale kadogo
kazuri kweli” aliongea Eve alipokaona kale katoto
ambako Reshmail alisisitiza sana.
“toto zuri jamboo!!”
“sijambo shkamoo!!” kalijibu katoto kale kwa
uchangamfu sana baada ya Reshmail na Eve
kukasogelea na kukasalimia.
“marahaba mtoto mzuri mbona upo hapa! Mwenyewe
au hawa ni kaka zako?” Resh alimuuliza
“a a sio kaka zangu mi namsubiri mama ameondoka
na watu wameenda huko amesema anarudi nimsubiri”
alijibu tena kwa sauti ya kitotototo
“umekula??” aliuliza Eve.
“looh!! Eve hujaacha tu maswali yako ya kichoyo ya
uchagani kwenu mh! Unataka aseme amekula ili
umnyime au ?” Reshmail alimshushua Eve kiutani
“mh! Limeniganda shoga,una mashushu wewe!!”
alijibu Eve kiaibuaibu huku akimpa yule mtoto
chungwa lililokwisha menywa tayari.
“mama anarudi saa ngapi??” Reshmail alimuuliza yule
mtoto tena
“sijui nimemsubiri hata hajaja amenipa chai tu
akaondoka na wale wanaume wawili” alijieleza vizuri
motto yule
“mh!! Mjini mjini tu katoto kanajieleza utadhani mtu
mzima dah!” Eve alimnon’goneza Reshmail
“haya twende ukale eti motto mzuri!” Reshmail
alimwambia yule motto naye akakubali kwa ishara ya
kichwa,akiwa pekupeku akafuatana na Reshmail hadi
kwenye mgahawa ulioandikwa “MAMA FRED
MGAHAWA” uliokuwa pembeni kidogo ya soko kuu la
Iringa.
“utamsalimia mama eeh!!” baada ya kumnunulia
chakula walilipa na kumuaga
“haya mamdogo!” alijibu yule mtoto
“unaitwa nani vile”Eve akamuuliza
“naitwa Christian motto wa mama Bite” alijibu na wote
kwenye mgahawa wakacheka
Kuifananisha na picha ya Adam, dimplez za yule
mtoto zilimfananisha kabisa na Adam, achilia mbali
rangi yake ya maji ya kunde na ucheshi wake.
"Eve hapana,mbona kesho naenda kumtafuta
Christian ili nimjue baba yake
anavyofanana,haiwezekani kufanana kwa kiasi hchi
hapana "Aliongea Resh huku akiifunika album ile .
Eve alikubaliana naye na siku iliyofuata majira ya saa
nne,walikuwa katika hoteli ya yule mama ambapo
walimwacha Christian.
"Nyie watoto ni kesi gani hyo mmetaka kuniachia jana"
mama mnene kiasi mmiliki wa mgahawa wa Mama
Fred aliwapokea kwa maneno hayo makali huku
akifunga kanga yake vizuri kiunoni.
Resh na Eve hawakuwa na jibu la kutoa walidhani
amewafananisha labda
"Mama ni nini tena,mbona sisi...." alijaribu kujieleza
Eve huku akiishiwa maneno ya kujieleza.
"Mmenitekelezea mtoto hapa anaanza kunililia hapa
usiku he! jamani mnataka mniuwe kwa presha mkurya
wa watu mie" aliongea kwa ghadhabu na mshangao
mkubwa sana yule mama.
"Mama sisi tumempata hapo sokoni,ndio kumleta
hapa kwako kwa ajili ya kupata chakula tu mama
yangu" Reshmail alinyanyua mdomo wake na
kuzungumza kwa sauti iliyojaa mshangao pia.
"He! mauzauza gani haya jamani,mi nimempeleka pale
kituo cha polisi usiku uleule ndugu
****************************** ********