Post by Admin on Jun 7, 2015 6:03:02 GMT
Baridi kali ya Mbeya ilikuwa imemkataa motto wa Bite
(Christian) kwa hali hiyo alipotimiza miaka miwili
waliondoka na kurudi tena Iringa ambapo Bite alitaka
kukaa kidogo halafu aende Mwanza kuweka makazi
mapya huko.
Jambo la kushangaza licha ya baridi ya Iringa hali ya
Christian ilianza kuwa njema kama awali jambo
lililosababisha Bite aendelee kukaa katika mkoa huo.
Hadi anatimiza miaka mine hali yake kiafya ilikuwa
njema sana na tayari Bite alikuwa amesahau suala la
kwenda Mwanza. Akaanzisha genge la kuuza uji na
karanga mida ya jioni na mihogo ya kukaanga majira
ya asubuhi.
Ilikuwa biashara ndogo lakini iliyomuingizia kipato
kizuri tofauti na matarajio yake.aliweza kupanga
nyumba ya chumba kimoja na sebule aliyoishi na
mwanae kwa furaha sana tu bila masumbufu yoyote
hadi siku hiyo asubuhi alipokuwa anauza mihogo yake
ambapo wanaume wawili ambao sura zao hazikuwa
ngeni machoni pake walipofika eneo la biashara
yake.Aliwapokea kwa furaha sana na bashasha kama
wateja wengine aliozoeana nao.
”Bite tukuone pembeni kidogo samahani lakini’ wawili
wale walimvuta pembeni Bite
“mh! Mikopo asubuhi asubuhi hamna kwakweli
mtadhalilisha hizo suti zenu” aliongea Bite kwa utani
huku akiwafata walipo wawili hao
“funga biashara tunaondoka na ukithubutu kupiga
kelele au kukimbia nasambaratisha ubongo wako
nadhani hujawahi kufikiria kifo cha namna hiyo,hivyo
basi fanya kama unavyoagizwa” aliambiwa Bite na
wale wanaume huku mmoja akifunua koti lake jeusi la
suti na kumwonyesha Bite kitu ambacho hakujiuliza
mara mbili mbili kuwa ile ilikuwa ni Bunduki,
Kwa kuutambua uoga alioupata Bite,yule mwenye
bunduki alimbandika kitu mfano wa kishikizo cha nguo
na kumwambia “hiyo ni sound recorder nenda
ukawaambie wateja wako sisi ni ndugu zako
tumekuletea taarifa za msiba nitakuwa nakusikiliza
hapa, ole wako nasema ole wako usifuate maelekezo”
alipewa masharti hayo ya uongo Bite ambaye laiti
isingekuwa pensi yake ya jinsi ambayo huwa anavaa
kwa ndani ili kuhifadhia pesa zake za mauzo basi
mkojo uliopenya bila yeye kujua ungemwagika
palepale hadharani na wala asingepatwa ma aibu
yoyote ile.
Kama alivyoagizwa aliwaeleza wateja wake wawili
waliokuwa wanamalizia kuitafuna mihogo waliyokuwa
wameinunua,wakampa pole za dhati .
jasho lilikuwa linamtoka alitamani kutumia ishara
kuwaambia kwamba yupo katika hatari lakini
alipowazia mdomo wa bunduki alikaa kimya
kabisa,bila kificho Bite aliiogopa sana bunduki na
hakupenda kumwacha Christian katika umri ule.
Tayari akili ilisharudi nyuma akatambua hasa,hao
watu alikutana nao wapi,walikuwa ni baadhi ya
wafanyakazi katika ile ngome aliyekaa miaka miwili na
ni hao waliomleta Adam pale ngomeni
“nimekwisha mimi Beatrice” alijiwazia Bite huku
akitetemeka.
Baada ya kuifunga biashara yake aliwafuata akiwa na
mwanae amemshikilia mkono.
“nadhani unajua hatuhitaji mtoto!!! Tunakuhitaji wewe
tena sasa hivi” aligombezwa Bite na bila kujijua
akajikuta akimwacha mwanae pale
“Christian narudi sawa nisubirie pale sokoni sawa
mwanangu!
“haya mama alijibu Christian kwa furaha kwani alijua
amepata fursa kubwa na ya kipekee kwenda kucheza
na watoto wenzake pale mtaani
“ulidhani unaweza kutuzidi ujanja sisi,umepotea sisi
hatupimiki hata kidogo umeumia tena umeumia sana
aliambiwa Bite na wale wanaume wakiwa kwenye gari
kuelekea kwenye gari kuelekea kule katika ngome
jambo hilo Bite hakulitamani hata kidogo,japo
alimpata Christian kwa bahati mbaya lakini alikuwa
akimpenda sana kutoka moyoni na hakuwa tayari
kutenganishwa naye kwa namna yoyote ile.
Alijiuliza maswali mengi sana ni nani atakayempa
chakula mwanaye siku hiyo na nyingine
zitakazoendelea wakati yeye hayupo,michezo ya
kukimbizana aliyoipenda Chriss pia ilimtia hofu Bite na
kuhisi huenda mwanae anaweza kupoteza uhai wake
kwa kugongwa na gari.
Funda la hasira lilimkaba kooni alitamani kufanya
lolote lile wakati huo lile jambo liwe ndoto kwake,
machozi yaliyotoka ndio yaliyeyusha lile fundo japo
kidogo,hasira kali ilikuwa imemkaba Bite aliyekuwa
amekaa siti ya nyuma na jamaa mwenye Bunduki
katika koti lake lakini maskini hakuwa na la kufanya
hadi gari lilipoingia ndani ya ngome ile
* * * * *
Macho ya Reshmail yalitawaliwa na taswira ya yule
mtoto Christian, zilikuwa ni siku nyingi zimepita tangu
afungue album yake kumwangalia mpenzi wake
(Adam) aliyeaminika kuwa tayari ni marehemu.Ni
katika usiku huu alipokuwa akipitia album ya Eveline
ndipo tena anakutana na picha ya Adam ambayo yeye
(Adam) alimpa Eveline walipoenda Mwanza.
”Eveline,Eveline,Eve……….huyu hapa ni nani???”
“we umechanganyikiwa tena eti hebu acha mambo
yake ya ajabu huyu Adam” Alijibu Eve kwa uoga.
“ na tuliyemwona leo kule sokoni ni nani??” aliuliza
Reshmail
“we Reshmail jamani wanafanana Mungu wangu
mbona wamefana hivyo lakini eeh!! Eve alijikuta picha
ya mtoto Christian ikiumbika kichwani mwake na
Zangu kwa sababu nimekaa naye hadi saa nne
tumemsubiri huyo mama yake aje wapi!! Nikaona isiwe
shari ngoja nimpeleke polisi penye usalama kuepuka
balaa kumbe na nyie hamjui ni wa nani he!!” alitoa
maelezo hayo yule mama na kueleweka vyema kwa
Reshmail na Eveline.
“hicho kituo cha polisi umesema kipo wapi?” aliuliza
Eve
“kile pale kinaonekana hata kwa hapa,lile jingo la bluu
nyuma yake” alielekeza yule mama
Ndani ya dakika tano tayari Reshmail na shoga yake
walikuwa mbele ya mapokezi ya kituo cha polisi Iringa
mjini, na walikuwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao
ya kuhudumiwa ifike.
“nyie ni ndugu zake? Au mmoja wenu ndio mama
yake?”
“hapana sisi si ndugu zake ila……”aliishia njiani katika
maongezi yake Resh baada ya kukatishwa na yule
askari “ila nini? Yaani nyie wanawake wa siku hizi
suala la kujali watoto wenu hamtaki kabisa kulisikia
mnachojali ni urembo tu wa sura zenu”
“jamani sio kwamba kuna ndugu yake hapa kati yetu
ila sisi tumemkuta jana kule sokoni ndio tumemnunulia
chakula halafu tukajiondokea zetu,leo hii ndio tunapita
pale kwa mama Fred yule mwenye mgahawa yeye
ndiye ametupatia taarifa hiyo tukaona sio vibaya nasi
tukifika kumwona huyo motto” aliongea Eve
aliyeonekana kutokuwa na hofu na kituo cha polisi
lakini Reshmail alikuwa ana uoga kwa mbali kama vile
anatuhumiwa kwa lolote lile.
“haya yupo tumemuhifadhi na tumepeleka taarifa
kwenye vyommbo vya habari wataanza kutangaza
kama mama yake bahati mbaya haya atakuja
kumchukua na kama amemtelekeza akajiandae
kwenda kuishi kwa watoto yatima sisi hatuna uwezo
wa kuhifadhi watu hapa zaidi ya mahabusu” alijieleza
askari yule huku akijipepea joto kwa kutumia kofia
yake iliyochakaa
Majuma mawili yalipita bila mama wala ndugu wa
motto kupatikana licha ya kituo cha redio maarufu
mjini iringa cha Ebon fm kutangaza kila siku bila
kukoma
“Eve naenda kumchukua yule motto nafsi yangu
inanishauri hivyo na ni lazima nifate ambacho nafsi
yangu inaniamuru” Reshmail alimwambia Eve siku
moja wakiwa wamekaa sebuleni wakiangalia habari
katika luninga.Eve alikuwa amejenga tabia ya
kutobishana na rafki yake huyo kwani furaha yake
ilikuwa ni kumwona Reshmail akiwa na furaha tele
“lakini Resh,mama yake si atamtafuta ssana??”
“Eve yaani imetangazwa hivyo redioni na hajajitokeza
leo hii mie tu kumchukua ndipo ajitokeze? Looh! Acha
nae ahangaike kidogo” alijibu Reshmail kwa jeuri
“mh! Haya sikuwezi mwanasheria wangu”
Polisi hapakuwa na usumbufu ni wazi kwamba
walikuwa wamechoshwa na matukio ya watoto
kutelekezwa na wazazi wao pasipo sababu zilizo
wazi,hivyo kitendo cha Resmail kuamua kumchukua
Christian ilikuwa ahueni kwao.aliandiokishwa maelezo
mafupi tu kabla ya kuruhusiwa kondoka na mtoto
ambaye alikuwa dhaifu tayari kutokana na lishe duni
na upweke wa kutomuona mama yake kwa siku hizo
zote.
Reshmail alikuwa ameyafurahia sana maisha ya
Iringa,kampani kubwa kutoka Eveline na mchumba
wake ilibeba nusu ya furaha yake huku nusu nyingine
ikikamilishwa na uwepo wa Christian mikononi
mwake,mara kwa mara alipenda kuwa naye karibu
huku akimwita mume wako jambo lililompa faraja
kubwa moyoni
”Eve jamani nitakumiss kipenzi changu lakini nitarudi
tena asanteni sana kwa ukarimu wenu mlionionyesha
tangu mwanzo nimeishi kwa furaha kubwa sana hapa”
Reshmail aliyazungumza hayo alipokuwa anawaaga
Eve na Benny usiku ambapo kesho yake alitegemea
kurejea Dar-es-salaam akiwa ameandamana na
Christian mtoto aliyempata katika mazingira ya
kutatanisha
Kwa Christian safari ya kutoka Iringa kwenda Dar
ilikuwa safari yake ya kwanza ndefu zaidi kuwahi
kusafiri
Siku iloyofuata wawili hawa walikuwa ndani ya basi la
‘budget’ litokalo Mbeya kwenda Dar likipitia Iringa.
“Mama alisema baba yupo pale kwenye ile nyumba,
tushuke nikamsalimie!” Chriss aliongea hayo huku
akielekezea kidole chake kwenye jingo lililoonekana
kwa mbali mno kutokea pale barabarani na hapakuwa
na dalili ya kuishi mtu pale hivyo Reshmail
akachukulia kuwa ni akili ya utoto imemtuma Chriss
kuzungumza akaamua kupuuzia
“chriss alikwambia nani we muongo!!”
“alinambia mama siku moja hivi tulipita hapa ,halafu
mama alinikataza kusema uongo ni dhambi” alijieleza
Christian haraka haraka
“mh! Haya tutakiuja siku nyingine sawa mfalme
wangu” Reshmail alimjibu Chriss ili kumlidhisha kwa
aliyokuwa anasema
** ** ** **