Post by Admin on Jun 7, 2015 6:05:58 GMT
Nyumba tulivu kabisa ya mh.Manyama ililipuka kwa
furaha kwa kurejea kwa Reshmail akiwa mwenye
furaha tele “umetuletea na mjukuu!!” alitania mama
Resh.
”mtoto wa Eve huyu anamwita mama mdogo” Resh
naye akadanganya
“kazuri kweli kama………………” alisita kumalizia baba
yake
“ni kama Adam baba usiogope kufananisha
wamefanana kweli” alimtoa baba yake wasiwasi huku
akimkumbatia baba yake kasha mama yake.
“mh!! Tulikuwa wapweke kweli jamani dada” msaidizi
wa kazi za ndani aliyeitwa Fatuma alimwambia
Reshmail huku akimkumbatia na kumbusu shavuni
“na huyo mtoto kama mwanao vile hebu kaone”
aliendelea Fatuma
“sio kama wa kwangu ila ni wa kwangu humwoni
alivyonifanana?” alijibu kimzaha na wote wakacheka
kwa pamoja
** ***** *****
Hali ya sintofahamu iliwakumba wale wafanyakazi wa
lile jumba (ngomeni) alipokuwa anatunzwa Adam.
Mkuu wa ngome hiyo bwana Lwebe alikuwa na
ghadhabu kubwa sana,kila mbua alikuwa na
ghadhabu kubwa sana,kila kitu kilikuwa shaghala
baghala kila mara aliongea kwenye simu hukuakitoa
vitisho vikali sana na hata kutishia kuua.
Wafanyakazi hawakumwelewa lolote walizitambua
hasira za bosi wao huyo ambaye mara chache
anazokuwa katika hali kama hiyo humalizia hasira
zake kwa kutoa roho ya mtu
“mlete Adam hapa mara moja !!” aliamrisha huku
akijikuna ndevu zake kwa kutumia mdomo wa bunduki
aliyokuwa nayo
“maskini Adam sijui amekosa nini” alijiuliza aliyekuwa
anaenda kumwita. Bila wasiwasi wowote Adam
akamfikia Lwebe D kwa ishara ya mkono
akamwamrisha kumfuata,pamoja na mabaunsa wawili
waliotinga suti nyeusi .
lwebe hakuongea neno lolote hadi walipofika kwa
nje,tayari kigiza cha saa mbili kilikuwa kimetawala
“mlete na yule mwingine wa nyumba ya chini” alitoa
amri nyingine tena baada ya tano walioagizwa
wakarejea na mtu mwingine
“we kinyamkera una bahati sana aliyekuleta hapa
amesema haujasambaza taarifa zozote mbaya laiti
kama ungethubutu ningeiondoa shingo yako sasa hivi.
Nakuacha uende tena lakini tambua mtandao wangu
upo popote katika nchi hii sasa ole wako uthubutu
kunyanyua mdomo wako kutangaza ujinga” aliambiwa
yule binti aliyeletwa pale huku akionyeshwa njia ya
kutokea
“we kidume kwa jeuri ya bosi wako kujaribu
kunidhurumu pesa yangu wakati wewe unakula na
kulala bure hapa;lazima nimwonyeshe mimi ni nani na
ni wewe utakayeumia” aliongea Lwebe huku akipuliza
moshi wa sigara hewani.
**********
Ilikuwa ni mwezi mmoja tangu Bite arejeshwe kwenye
ile ngome lakini katika chumba kingine,hakuwa
msaidizi wa kazi tena bali mtuhumiwa na hakupata
fursa ya kuonana na Adam hata siku moja .
siku alipotolewa nje usiku na kwa mahesabu ya miaka
mitano ambayo Adam angekaa pale machale
yalimcheza,alivyopewa uhuru wa kuondoka hakwenda
mbali sana alifika eneo moja kwenye mtaro na kuanza
kusubiria ni nini kitatokea japo hakusikia vizuri
maneno lakini alisubiri hata vitendo
**********
Mkataba wa miaka mitano alioandikishana
Bi.gaudensia na Lwebe wa Adam kuhifadhiwa pale
ulikuwa umeisha tayari na miezi mitatu zaidi ilikuwa
imepita,suala hilo la kuchelewesha pesa lilimkera sana
Lwebe na pia ahadi za uongo kutoka kwa Gaudencia
zilichochea sana hasira za Lwebe kufikia hatua ya
kuamua kuzipooza kwa huyo Adam aliyehifadhiwa
hapo.
Ni usiku huo alipoamua kwa mkono wake mwenyewe
Adam duniani kama kisasi kwa Bi.Gaudensia
“paa!! Paa!!” mlio mkali wa risasi ulisikika na
kumzindua Bite ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi
pale kwenye mtalo, kidogo apige kelele lakini viganja
vya mkono wake vikawahi kuuziba haraka sana.
Hakusikia hata chembe ya kilio na baada ya dakika
kama saba akasikia milango imefungwa
Kwa ujasiri na tahadhari kubwa Bite akajisogeza hadi
karibu kabisa na eneo ambalo aliamini hakika ndipo
mlio wa risasi umetokea huku kichwani kwake akiwa
ana jibu la “nimesahau saa yangu” iwapo atakutana
au kushtukiwa na mlinzi, kwa hofu alizurura katika lile
eneo dakika tatu bila kuona chochoten”au wameingia
nae ndani??” alijiuliza bila kupata jibu
“koh!! Koh!! Alishtuliwa na sauti ya kikohozi nyuma
yake, mawazo yake alidhania ni mlinzi eneo lile lakini
alipogeukz hakuwa mlinzi tena ni mwili wa binadamu
ukiwa chini,hakutambua mara moja yule ni nani hadi
macho yake yalipolizoea giza la pale “Adam!!!!!”
“we ni nani??” alijibiwa kwa sauti ya chini sana
iliyokuwa inaunguruma kama mnyama anayechinjwa
“Bite mimi jamani Adam”
“ondoka watakuua hao Bite ondoka niache mi nife
hapa” alijibu Adam
“hapana Adam usife,usife Adam twende tukamtafute
mwanetu Chrstian anatamani sana kukuona,usife
Adam tafadhali” Bite alibembeleza
**********
Risasi mbili zilizopenya katika paja lake la kulia
zilikuwa zimemsababishia Adam kuvuja sana damu na
mbele yake alichokitarajia ni kifo hakuna kingine lakini
maneno ya Bite.
Nguvu zilirejea upya kabisa tena kwa kasi”Bite
ulijifungua, mtoto wangu yuko wapi? Ni wa kiume au
wa kike?” alihoji maswali mfululizo Adam huku
akijitutumua kusimama kwa nguvu alizokuwa
amezipata
“ni stori ndefu na hapa sio mahali pake tuondoke
tafadhali jitahidi kuna hatari kubwa kama unampenda
mwanao jitahidi tuondoke” aliongea Bite huku
akiuweka mkono wa Adam katika bega lake na kuanza
kumkongoja kutoka eneo lile huku (Adam) akitumia
mguu mmoja na ule uliojeruhiwa ukiwa juu juu.
Kutoka pale walipokuwa hadi barabarani haukuwa
umbali mrefu sana na walifanikiwa kufika,kwa giza
nene lililokuwepo hawakuweza kuonekana na mtu
yeyote,nguvu zilikuwa zinamwishia Adam kutokana na
kuvuja damu lakini alijikaza kijasiri sana na kuendelea
mbele
********* ******* *******