Post by Admin on Jun 7, 2015 6:09:59 GMT
Lwebe na kundi lake baada ya kumpiga risasi mbili
Adam waliamini katu asingeweza kunyanyuka kutoka
katika eneo lile,na hata angeweza kuinuka hakuwa na
pa kwenda hakuujua mkoa huo hata kidogo. Waliingia
ndani na kupiga simu kwa Bi.Gaudensia kwamba mtu
wake tayari ana risasi mbili mwilini
“msimuue jamani,tafadhali sana kesho naileta pesa
yenu mapema kabisa”
“nimechoshwa na ahadi zako mheshimiwa jiandae
kuchukua maiti yako siku yoyote utakayotaka utaikuta
nimeihifadhi na kama na kuizika nitakusaidia” alijibu
kwa ghadhabu kasha akakata simu
Bi Gaudencia akapiga tena
“nakusikiliza”
“basi nielewe kwa leo na hili ni ombi la mwisho
tafadhali usimuue kesho asubuhi sana nakuja
huko,ninaondoka huku saa nane usiku tafadhali”
alibembeleza
“na iwe hivyo atalala nje leo na hata kula hadi
utakapokuja
“sawa mkurugenzi” alijibu kwa unyenyekevu Gaudensia
Akini ya Bi.Gaudensia ilifanya kazi haraka haraka
akapekua kila kona katika chumba anacholala na
mumewe na kwa bahati nzuri kwa akakutana na kadi
ya benki ya mume wake ambayo alikuwa akifahamu
vizuri kabisa namba zake za siri.
Bila kupoteza muda akampigia dereva wake wa siri
ambaye huwa anampeleka Iringa naye haraka haraka
bila kuhoji akatii amri aliyopewa.bila Reshmail kujua
Bi.Gaudensia akaondoka majira saa saba usiku,nafsi
ilikuwa ikimuhukumu juu ya baya lolote litakalomkuta
Adam
“damu ya Adam ipo juu yangu”
“naenda kwa rafiki yangu ameugua ghafla “ mama
Reshmail alimuaga mlinzi wa getini
“sawa bosi” alijibu mzee yule wa makamo huku
akifunga geti baada ya mama kuwa ametoka nje
Kwa kasi ya ajabu gari iliondoka jijini Dar-es-salaam
kwa kuwa ilikuwa usiku sana vizingiti vya watu wa
usalama pamoja na foleni havikuwepo sana hivyo
dereva alikimbiza gari kwa kadri ya uwezo wake.
Breki ya kwanza ilikuwa ni katika benki ya C.R.D.B
maeneo ya Ubungo ambapo mama Reshmail alishuka
na kuvuta pesa kutoka katika akaunti ya akiba ya
mzee Manyama
Badala ya masaa matano kwa gari binafsi kufika
Iringa walitumia masaa matatu pekee
“mh!! Huku napo kijijini kweli huyo nae sijui ni
mgonjwa sasa usiku huu atapata wapi lifti ya gari”
Mama Reshmail alimwambia dereva wake alipoona
watu wawili wakisimamisha gari
“ah!! Ndo maisha ya Tanzania yalivyo” alijibu dereva
huku akiongeza zaidi mwendo wa gari hadi wakaifikia
ngome ya vigogo waliyokuwa wakiifuata
**** **** *****
Magari makubwa ya mizigo yatokayo Morogoro
kwenda Zambia na Malawi ndiyo yaliyotoa msaada
kwa Bite na Adam ambapo Bite alijitambulisha kama
mke wa Adam na kwamba wamevamiwa na
majambazi na mumewe (Adam) amepigwa risasi.
Laiti kama madereva wangekuwa watanzania kwa jinsi
walivyo waoga katu wasingewapandisha wawili hawa
lakini wakongomani wale ambao vita kwao ni jambo la
kawaida waliwachukua Adam na Bite hadi Iringa mjini
walipowaacha jirani kabisa na hospitali ya rufaa.
“bila RB hatupokei mgonjwa wa aina hii” alisema
muuguzi wa kike wa hospitali ile wakati Bite anajieleza.
Ni kweli yule muuguzi(nesi) alikuwa na haki zote za
kupingana na ujio ule kwani hali aliyokuwa nayo
Adam ilihitaji taarifa za polisi kwanza
“haa!!! Mama Christian, ni wewe hata siamini au
nakufananisha?”
wakati Bite akijiegemeza kwenye ukuta huku akiwa
amekata tama alishangaa kutambulika kwake na nesi
yule
“Mungu wangu mama wawili jamani!!!”
Baada ya kumkazia macho naye Bite akamtambua yule
nesi kuwa waliwahi kufanya nae biashara katika soko
la Uyole Mbeya na pia alikuwa jirani yake pale
alipokuwa anaishi,ulikuwa mshangao mkubwa sana
“ehe!! Kulikoni tena ndugu yangu yamekukuta yapi
tena mwenzangu?” alihoji nesi huku akiwa
amechangamka sana safari hii
“ni makubwa sana,lakini ningeupata msaada wako
kwanza kwa mume wangu ndio tungeongea vizuri
shoga” alijibu Bite akiwa na matumaini tele
“ondoa shaka shoga huduma mnaipata sasa hivi tena
huduma bora,daktari tunaheshimiana naye sana na
pia ni shemeji yangu” nesi aliongea hayo huku
wakisaidiana kumwingiza Adam ndani ya chumba cha
wagonjwa,hapakuwa na maswali mengi,undugu
ulitawala pale.
Adam akafanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa risasi
katika ambao haukuchukua hata hata nusu saa damu
na maji pia vikaongezwa katika mwili wake uliokuwa
dhaifu sana.kufikia majira ya saa kumi na moja alfajiri
Adam alikuwa amepata nafuu kubwa na aliweza
kutembea japo kwa kuchechemea
“shoga nikueleze wazi tu kwamba sisi pa kufikia hapa
Iringa mimi na mume wangu hatuna! Tangu niondoke
ghafla niliacha sijalipa kodi nina uhakika chumba sio
changu tena kwa hiyo pa kwenda hatujui” Bite
alimweleza hayo mama wawili baada ya kuwa
amemsogeza pembeni ili mtu mwingine asiweze
kusikia
“Ondoa shaka Bite mimi kwangu pana nyumba kubwa
tu!! Nimejengewa na mnyakyusa mmoja,nimemweka
kwenye kiganja kwangu mimi hasikii,haoni wala
hasemi,ni kaka yake na huyu daktari we mwenyewe si
umeona alivyowashughulikia haraka” kwa sauti ya
chini kabisa nesi alijibu
Wote watatu katika teksi wakaongozana hadi
nyumbani kwa nesi ni kweli nesi hakuwa na chembe ya
utani hata kidogo nyumba ile ilikuwa kubwa sana na
haikuwa haki kukaliwa na watu wawili pekee vilikuwa
ni vyumba sita pamoja na sebule
“karibuni! Karibuni sana! Nesi aliwakaribisha walipofika
nyumbani kwake.
“asante sana ndugu yangu ama kweli ishi na watu
uvae viatu” alisema Bite kwa upole sana
“usijali Bite tumeishi vizuri,hatukuwahi kugombana
hata siku moja,tumetwishana matenga ya nyanya kwa
nini sasa nishindwe kukutendea wema!!!” nesi alimtoa
hofu Bite
Chumba walichopewa kilikuwa kikubwa cha
kuwatosha kabisa,kitanda cha tano kwa sita kilikuwa
saizi yao kabisa.
Adam alishangazwa sana na wema huo wa nesi lakini
mshango wake uliongezeka maradufu baada ya
kukutana na mume wa nesi siku ambayo walikuwa
wakitambulishwa kwake kama shemeji zake yaani
ndugu zake Bite.mzee huyu wa kinyakyusa aliyeitwa
Gwakisa ni kama heshima ilipitiliza na kuwa kama
anawanyenyekea wawili hawa.
Adam alihudumiwa na yule daktari kana kwamba
alikuwa ni mgonjwa wa kisukari au alikuwa ni mtoto
wa mfalme,Adam alipata farijiko kubwa sana kuishi
pale
Bite kama kawaida alikuwa mwanamke wa kujituma
sana,ndani ya wiki moja tayari alikuwa amepata kazi
ya ndani katika nyumba nzuri waliyoishi wanafamilia
watatu, mwanaume na mke pamoja na mtoto wa
kama miaka mitatu wa kike aliyekuwa anasoma shule
ya awali
***** ****** ****** ******