Post by Admin on Jun 7, 2015 6:11:55 GMT
“bite mama!!”
“bee mama”
“mpeleke mtoto shule halafu baadaye mpeleke pale
zahanati akapimwe jana usiku amekohoa sana”
ilikuwa sauti ya Eveline akimpa maelekezo Bite ambaye
alikuwa mfanyakazi wake mpya na wa kwanza wa
ndani ya nyumba yake na mchumba wake.
Ratiba ya Bite ilikuwa ni kazi kuanzia asubuhi ya saa
mbili ambapo alikuwa akimpeleka Loyce {mtoto wa
kaka yake Benny} shuleni na kisha akirejea anaandaa
chakula cha mchana kwa siku ambayo Benny hurudi
nyumbani mchana na baada ya hapo humfuata Loyce
shuleni,kisha maandalizi ya chakula cha jioni na
majira ya saa kumi na mbili huaga na
kuondoka,ilikuwa kazi ambayo haikumtoa jasho Bite
na malipo ya shilingi laki moja kila mwezi
yalimtosheleza kabisa kupanga chumba kidogo
walicholipia shilingi 15000 kwa mwezi
“tunashukuru sana kwa ukarimu wenu bwana na bibi
Gwakisa Mungu awazidishie baraka katika kazi zenu”
alitoa shukrani za dhati Adam kwa niaba ya mke wake
wa bandia (Bite).
uchangamfu wake na wingi wa vituko ulifanya nyumba
ya Gwakisa iwe iwe yenye shangwe na tabasamu kila
siku,kitendo chake cha kuaga pale kilimsononesha
Gwakisa na mkewe lakini hawakuwa na jinsi, kutoka
mfukoni mwake aliwakabidhi shilingi laki mbili za
kuanzia maisha yao huko waendako
Tayari Adam alianza kumpenda kwa dhati Bite
uchapakazi wake na jinsi alivyomwokoa kutoka katika
kifo ulichangia sana lakini kiunganishi cha mtoto
Christian ndio ilikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao.
walivyohama katika nyumba yao ya kupanga walianza
rasmi kuishi maisha ya mke na mume Adam hakuwa
na amani hata kidogo na familia ya Reshmail hasa
baada ya kukuta katika nyumba hiyo ndogo
waliyohamia magazeti yaliyobandikwa kama
mapambo likisema;
“imani za kishirikina zamwondoa mheshimiwa
Manyama bungeni” alitamani sana kuisoma habari
hiyo kiundani iliyotoka takribani miaka mitano iliyopita
lakini ilikuwa imeandikwa inaendelea ukurasa wa pili
anbao haukuwepo pale ukutani
“Au walikuwa wanataka kunitoa kafara? Mungu
wangu!! Niliwakosea nini mimi” alijiuliza Adam wakati
wakiingiza yao ya Rambo ndani ya chumba hicho
kimoja kilichotenganishwa na pazia kufanya sebule na
chumba
Hisi hizo mbaya zikamfanya Adam aamue kuanzisha
rasmi uhusiano na mwanamke ambaye amezaa naye
mtoto pia aliyeokoa maisha yake bila kutarajia
mwanamke ambaye hajawahi kumkwaza,mwanamke
mpiganaji anayempa furaha tele kila siku
“Bite nataka uwe mke wangu”
“Mh!! Niwe mkeo mara ngapi mimi mkeo tayari jamani”
alijibu Bite huku akichezea ndevu za Adam ikiwa ni
siku ya pili tu tangia wahamie katika makazi hayo
mapya
“una utani wewe mbona ulikuwa hujaniambia wala
sijawahi kusikia ukiniita mume wako?
“sio lazima nikwambie tayari nina mtoto wako halafu
humu ndani kuna kitanda kimoja tena kidogo
tu,ulidhani chako mwenyewe!!!” aliuliza Bite kisha wote
wakacheka huku wakikumbatiana na kuangukia
kitandani
**** *******
Maisha ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa
yamebadilika sana akiwa anasubiri wakati baba yake
akimtafutia kazi itakayompendeza alifurahia mara zote
na Christian huku akiwa amewabadili watu wote
wanaomfahamu kwa ukaribu kutokea kumwita
Reshmail na sasa walimwita mama Christian na
alikuwa amejivika pete ya ndoa katika kidole chake
cha shahada ikwa na jina Adam na nyingine ndogo
akiwa amemvisha Christian ikiwa imeandikwa
Reshmail.
Hakuwa mtu wa kulialia tena wala msongo wa
mawazo haukumsumbua tena aliamini nafasi ya Adam
ilikuwa imezibwa vyema na Christian ambaye alikuwa
Adam mpya kwake. Walilala wote, walicheza wote na
kusimuliana mambo mbalimbali.alipoenda kusalimia
rafiki zake walienda wote Christian mkono wa kulia.
Harakaharaka Christian alijikuta akimpenda mno
Reshmail kuliko hata ilivyokuwa kwa mama yake
mzazi,maisha ya kifahari ya kwao Reshmail
yalimfanya Christian anawiri sana ungewakuta
wakicheza bustanini kama vile wanalingana umri
walibembea pamoja na kupigana kiuongouongo,kwa
ufupi waliishi maisha ya kusisimua kwa kila
aliyewaona.
Akiugua Reshmail ni Christian atamuuguza kwa kukaa
pembeni yake bila kutoka nje hadi apone hivyo hivyo
kwa Reshmail abaye alimwogesha na kumlisha.
Wakati huo Reshmail ndio alikuwa mwalimu wa
Christian akimfundisha kusoma na kuandika jambo
ambalo hata baba yake alilipenda na Christian
alikuwa mtu anayeelewa haraka akifundishwa
,reshmail alifurahia sana.
Baada ya kukaa na Christian mwezi sita reshmail kwa
mara nyingine Iringa kwa rafiki yake jambo kubwa
lililompeleka huko ni harusi ya rafiki yahe huyo
ambapo alitarajiwa kuwa matron wa kipenzi chake
hicho.
“shoga shughuli kesho kutwa hata haujaonekana
jamani au ndio mambo yetu yale haja ya kufanyiwa
make up….” Aliuliza kiutani.
Eve katika simu alipokuwa anaongea na Reshmail.
“Kesho asubuhi na mapema nakujua ,mume wangu
alikuwa na mafua ndio tatizo si unajua tena.”alijibu
Reshmail.
Haya mume huyo anavyoringiwa shauriro “alijibu Eve
.Christian alikuwa amependekezwa kuwa bwana harusi
mdogo pamoja na Loyce (mtoto wa kaka yake Benny).
“He unatoka mume wangu asiuze sura,na jinsi
alivyoandaliwa huku Dar es salaam ,utachoka
mwenyewe na simtoi mpaka siku ya
shughuli,atakayeruhusiwa kumuona ni bibi harusi
mdogo(Loyce) peke yake wakati wa kujifunza,sitaki
mwingine amuone mpaka siku yenyewe”alijibu
Reshmail kwa furaha.
“Haya umeshindwa ambao hatuna waume
tunalo,alijibu Eve kisha wakaagana.
Asubuhi ya siku iliyofuata majira ya saa nne asubuhi
tayari Reshmail,Christian,mpambaji pamoja na dereva
walikuwa ndani ya gari la baba yake (Resh)taratibu
safari ya Iringa ikaanza.
“Usitupeleke kwa kasi sawa eeh,alitoa malekezo
Reshmail na kukubaliwa na dereva kwa sababu
hawakuwa na haraka yeyote ila mbele yao yalikuwa
bado masaa mengi sana kabla ya harusi kufanyika.
Kwa mwendo wa kinyonga kabisa gar lilifika mbele ya
nyumba ya Eve majira ya saa nne usiku na hakuna
aliyekuwa ameschoka sana.Shamrashamra zilikuwa
kubwa sana maeneo ya pale kwa Eve kelele zilizidi
alipofika Reshmail, na kama alivyoaahidi kweli
alishuka yeye peke yake kutoka katika gari akifuatiwa
na dereva,urembo wake utadhani alikuwa amepembwa
tayari kuingia ukumbini.
“Shoga tabia gain hiyo kupendeza kuliko bibi
harusi?”aliuliza eve kiutani baada ya Reshmail kuingia
katika chumba ambacho Eve alikuwa amehifadhiwa
akiwa na wapambaji wake.
“Hebu acha utani wako,kila mara unadhani tuko
shuleni?mwone,”alijibu Reshmail,Eve akajiziba mdomo
kwa aibu huku akiwatazama wapambaji wake
waliokuwa wamejizuia kucheka lakini uvumulivu
ukawashinda wakacheka kwa nguvu.
Chumba kile kikageuka kijiwa cha story kati ya
Reshmail na Eve ,stori zingine zilikuwa juu ya mume
wa Reshmail (Christian),shoga hadi pete?
“Sina utani mie mbona”?alijibu Resh huku wapambaji
wakiwa hawajui hata kinachoongelewa.
“Mama kuna mtu anataka kukuona,ilikuwa ni sauti ya
kike ikimueleza Eve.
“Heh!!ushazaa na wewe?”aliuliza kiutani
Reshmail.Mh!!niringe huyu ni msaidizi wangu tu wa
kazi anaitwa Bite,nampenda naye ananipenda pia.
“Sio kama mimi na Christian “alidakia Reshmail
ambaye tangu aingie chumba kilitawaliwa na vicheko.
“Bite humuwezi huyu anaitwa mam Christian ni rafiki
yangu tangu utotoni.
“Nafurahi kukufahamu mama Christian hata mimi.
Alitaka kuondelea kuongea Bite akakatishwa na Eve.
”Anayetaka kuniona nani huyo tena?,mwambie nina
mgeni" Bite akajiondokea bila kumalizia kauli yake.
Sherehe ilifana kuanzi kanisani lakini mambo yote
yalikuwa saa mbili usiku maharusi wadogo
walipokuwa wametangulia mbele wakifuatiwa na wana
ndoa wenyewe(Eveline na Benjamin)huku nyuma yao
Reshmail na Fredrick wakifunika kila kitu kwa pale
mbele Christian aliteka macho ya watu huku kamera
zimemulika yeye.
Tabasamu lake pana la wakati wote lililoonyesha
vishimo katika mashavu yake yote lilisababisha watu
wengine wahisi huenda sio kutoka Tanzania , suti yake
iliyoendana kabisa na mwili wake na viatu vyake pia
jinsi mkono wake ulivyokuwa umemshika kiustadi
Loyce (bi harusi mdogo) ulimfanya MC ashindwe
kukaa kimya “nani mwenyewe harusi,wa mbele,nyuma
au kati” aliuliza kwa mbwembwe
“mbeleeeeeeeee!!!.......nyumaa aaa!!!!” ndio majibu
yaliyosikika kutoka kwa wengi
“hayaa wageni waalikwa wanasema maharusi wa
katikati wamefunika sana” alidanganya MC
aliyefahamu wazi Christian na Reshmail wameteka
macho ya watu wengi pengine kuliko maharusi
wenyewe.
Picha zilipigwa kwa wingi lakini Christian
hakuonyesha wasiwasi wowote “mh!! Katoto kazuri
halafu kajanja hako” wanawake walikuwa
wakinon’gonezana huku wakimtazama Christian
anavyozidi kusonga mbele
“wamekatoa nje,baba yake ni mreno” alidakia mama
aliyesifika kwa umbea pale mtaani aliyejulikana zaidi
kwa jina la mama mwingi.hata hawakuhangaika
kujibishana nae kwani walishamzoea
Taratibu kabisa kwa mwendo wa kunyata jozi hizi tatu
za kuvutia ziligawanyika huku jozi mbili za wakubwa
zikienda katika meza kubwa kabisa na watoto
wakienda katika meza yao ndogo iliyokuwa
akimeremeta soda na vinywaji vingine baridi,
”kusema ukweli sherehe imependeza,siongei kama MC
bali kama ndugu Kidagaa Peter Kubalunga wengi
wananiita MC K.P” alichombeza Msema Chochote
(MC) na kushangiliwa sana na umati mkubwa
uliohudhuria sherehe hiyo