Post by Admin on Jun 7, 2015 6:14:28 GMT
“Dah!! Umependeza kweli sitaibiwa huko na
wajanja,hebu ona ona mgongo wako utadhani huna
mamba ulivyopendeza,ona kifua chako mpenzi wangu
hapana nitaibiwa mke mie” Adam alikuwa akimtania
Bite huku akim funga zipu yake ya mgongoni
“Acha wivu mwanaume wewe,kaa ndani usubirie ya
kwako aniibe nani wataishia kutamani tu!!” alijibu Bite
huku akimun’gunya midomo yake ili lipstick aliyopakaa
ikae vizuri zaidi na kioo kikiwa mbele yake
“Nakupenda sana mke wangu,tambua hilo niliamua
toka moyoni mwangu na wala sijutii hata kidogo
najionamwenye bahati sana” Adam kwa sauti ya chini
iliyomaanisha anachokisema alimwambia Bite ambaye
alitulia tuli akamtazama Adam kisha akamkumbatia
na kumbusu.
“nakupenda pia nakupenda sana” Bite akamwambia
Adam halafu akatoka nje na kupanda teksi iliyokuwa
inamsubiri kwa nje na kuondoka,Adam hakuthubutu
kutoa hata pua yake nje kwani bado alikuwa na uoga
wa kurejea mikononi mwa watu wabaya
Majira ya saa tatu na nusu Bite tayari alikuwa
mlangoni akionyesha kadi yake ya mwaliko kwa watu
wa ulinzi kisha mwanadada kutoka kamati ya
maandalizi akamwongoza Bite kuelekea katika upande
ambao ndugu zake na mwanamke walikuwa
wamekaa,eneo la chini ya meza ya bwana na bibi
harusi mdogo.Bite alikuwa tayari kama ndugu wa
damu kwa Eveline walitokea kuheshimiana sana na
hawakuwahi kuingia katika malumbano makubwa
sana.
Amani ilitoweka katika meza ya bwana na bibi harusi
wadogo,Christian alikuwa amekosa utulivu mara kwa
mara alikuwa ananyanyua shingo yake aweze kuona
kitu Fulani ambacho hakuna aliyefahamu ni nini
kimemsibu
“Au kanaumwa tumbo?” alijiuliza matron huku akienda
kwenye ile meza kumsikiliza Chriss ana shida gani.
“Chriss ni nini baba umekuwaje?” alimuuliza baada ya
kumfikia
“nataka kwenda kwa mama” alijibu kwa sauti iliyojaa
manun’guniko sana
“subiri kidogo mtoto mzuri nitakupeleka sawa” matron
alimdanganya Chriss huku akiamini shida yake ilikuwa
kwenda kwa Reshmail,kidogo Chriss alitulia japo bado
hakuwa na katika hali ya uchangamfu kama awali
Muda wa kutoa zawadi ulipofika maharusi wote katika
jozi tatu walitakiwa kuwa mbele ya umati kwa ajili ya
kupokea zawadi zao.Christian na Loyce waliwekewa
viti wakakaa wakati Eve,Benny,Reshmail na Fredrick
walisimama wima kupokea heshima hizo
“heee! We mtoto vipi? Jamani huyu mtoto kulikoni”
yule mwanamke aliuliza baada ya kushikwa gauni lake
na Christian alipotaka kuondoka baaba ya kutoa
zawadi.
Bahati mbaya muziki ulikuwa umezimwa hivyo ukumbi
mzima ulishuhudia tukio hili la kushangaza
“mamaaaa!! Mamaaaa!!” Chriss alimpigia kelele
alipotaka kuondoka
“Chriss…….Christian……Christian wanguuuu!!! Jamani
ni mwanangu..ni mwanangu huyu” alipiga kelele
mwanamke huyu, alikuwa ni Bite na tayari akili yake
imemgundu Christian,watu wote waliamini
amechanganyikiwa lakini alikuwa anasisitiza bado
kwa maneno hayohayo.
Hakika mbele yake alikuwepo mwanaye
waliyepotezana zaidi ya nusu mwaka sasa na dalili za
kumpata zilikuwa zimeanza kufifia.
Mayowe yake yalivyozidi yakapoteza usikivu pale
ukumbini na kila mtu kuanza kujiuliza kulikoni eneo lile
“mama mama mama,huyu ni mwanangu…..Christian
jamani” Bite kwa sauti ya juu sana akaanza
kumwambia Eveline ambaye alikuwa amekodoa macho
kuangalia anachofanya Bite pale mbele
“kuna nini jamani” Reshmail alishindwa kujiuliza
akamvagaa Eve na kumuuliza
“huyu ni Christian,mtoto wangu jamani mtoto wangu
kabisa” alisisitiza Bite.
Nguvu zilimwisha Reshmail japokuwa hakuzimia lakini
alianguka chini,alishuhudia kila kitu lakini hakuweza
kuzungumza,ulikuwa mshtuko wa hali ya juu sana
haikuwa sherehe tena bali kasheshe,huku Bite na
mayowe yake huku Reshmail akiwa chini.
Wapiga picha hawakuwa mbali walilichukua hili tukio
kikamilifu tayari kwa kuuza katika vyombo vya habari.
Mwanamama mwenye nguo nyeusi alikuwa
anapambana kupenya katika msitu mkubwa wa watu
pale ukumbini,mwanzoni hakuwemo kwenye sherehe
“vimama vya Kiswahili navyo,hapo umbea tu ndo
amefata humu,akipigwa hapo au akikanyagwa
atamlalamikia nani”
mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa suti aliwaambia
wenzake huku wakimtazama mama huyo mwenye
baibui iliyovaliwa kwa staili ya ninja hasa hasa kwa
waumini wa dini ya uislamu anavyopambana kwa
juhudi ili apenye. Watu kwa huruma wakampisha, moja
kwa moja akiwa anakimbia kwa kasi alifika mbele ya
ukumbi akaanza kuzubaa na mara ghafla akakimbilia
alipolala Reshmail na kuanza kutikisa
“huyu maza vipi mwehu nini? Yaani mtu ameachiwa
hewa impige yeye anaenda kuweka usiku tena na
manguo yake” kijana mmoja aliyekuwa amevaa jinsi
kwa staili ya mlegezo aliwaambia wenzake
“tulia wewe huenda ni mamake huyo” alijibiwa na
wenzake
“reshmail amka amka mpenzi” alimwambia kwa sauti
ya chini.
**** ** ***
Wivu wa utani utani aliouonyesha mbele ya mke wake
ulukuwa unatoka moyoni mwake,Adam alihisi huko nje
labda kuna mjanja anamchukulia mke wake.
”ngoja nikamfumanie mtu leo” alijiwazia Adam huku
akipekua pekua nguo gani anaweza kuvaa iweze
kumziba sura yake asiweze kufahamika kwa urahisi
mbele za watu,’baibui’ ndio jibu alilopata,
harakaharaka akajitanda kwa ustadi,
Alifahamu vyema pesa ya mkewe ilipokuwa
inahifadhiwa akajichotea kiasi kilichotosheleza kwa
nauli “Mountain view” alijikumbusha jina la hotel
ambayo sherehe ilikua inafanyika,ni jina alilolikariri
kwenye kadi ya mwaliko.
Akiwa na baibui lake alipanda teksi ikamfikisha moja
kwa moja eneo la tukio,kukuru kakara aliyoikuta pale
ilimtia hofu kubwa sana aliamini lazima kuna kitu
kimeharibika eneo lile hakuwaza kitu kingine bali
usalama wa mkewe (Bite) moja kwa moja naye
alijichanganya humo ndani.
Tofauti ya malengo yake ya kumjulia hali
mkewe,macho yake yanakutana na Reshmail akiwa
sakafuni na vazi lake zuri la harusi,sura yake bado
ilikuwa haijasahaulika katika kumbukumbu za Adam.
Nguvu zilizokuwa zimemwisha Resh pale chini zilirejea
kwa kasi kutokana na kusikia sauti ya kiume kutoka
katika nguo za kike
“mamaaaaaaaaaaa!!!!” alipiga kelele kwa sauti ya juu
huku tayari akiwa amesimama wima akijaribu
kukimbia,kamera zikageukia eneo lao tena nyingi
zikimmulika mwanamke mwenye baibui (Adam).
Kabla hajakimbia Reshmail alidakwa mkono wake.
”Adaam……Adaaaam!!!” alipiga kelele kali zaidi wakati
huuu Reshmail. Adam alikuwa amejivua baibui kwa
upande wa usoni, akiwa hajapewa jibu lolote reshmail
palepale alifika Bite,
”Adam! Umefikaje hapa mume wangu…si ulisema
hauji…” Bite aliuliza
“nini? Nani? Umemwitaje? Na huyu ni…….” Hakuweza
kumalizi kauli yake wakati huu,mawazo yakauzidi
nguvu ubongo wake akazimia palepale.
Wakati huo Chriss alikuwa analia tu hajui
kinachoendelea, Eve na Benny walikuwa wanahaha
huku na huko bila kukumbuka kwamba alikuwa na
shera safi kabisa tena ya gharama za juu kabisa,
Benny ndio alikuwa kama tahira hajui hata pa kuanzia
alikuwa ameshtuka sana.
Ilikuwa kama vita vile lakini hakuna hata aliyejeruhiwa
wala aliyekuwa anapigana vilikuwa si vita vya risasi
bali vita vya mapenzi.
Wageni waalikwa waligeuza tukio hilo kuwa kama
filamu ya kusisimua lakini waliyokuwa wameianzia
katikati bila kujua ilianzia wapi na inaenda wapi.,nani
nyota wa filamu na nani adui.
***