Post by Admin on Jun 7, 2015 6:16:20 GMT
Ni katika nyumba ya Eveline. Reshmail akiwa mbele ya
Beti amepiga magoti akilia kwa uchungu
“Bite wewe ni mwanamke mwenzangu nionee huruma
kwa haya niliyopitia,nimeteseka sana, nimedhalilishwa
kwa ajili ya Adam, ni kwa ajili yake hadi leo mimi ni
bikra, kwa ajili yake familia yake imetuchukia,kwa ajili
ya Adam baba yangu haeshimiki tena mtaani
kwetu,Bite sitamani mwanaume yeyote
yule,ukininyan’ganya Adam na Christian mimi nitakufa
Bite, ni furaha gani utaipata kwa kifo changu kwa ajili
ya upendo?, sitajali huyu mtoto uliyezaa nae wala
sitaumizwa na ujauzito wake uliombebea, ninakuomba
Bite niache na mimi nipate furaha japo kidogo tu katika
siku zangu zilizobaki hapa ulimwenguni, nisaidie
niweze kurudisha upendo uliogeuka chuki kati ya
familia yangu na Adam. Bite uamuzi upo mikononi
mwako,ukikataa utaniumiza sana na nina uhakika
nitakufa na pendo langu kwa Adam”
Kilio kilimzuia kuendelea kuongea,lakini na yeye
mgongoni mwake alilowanishwa kwa machozi ya Bite
yaliyokuwa yanatililika muda wote wakati Reshmail
anaongea,kwa hali halisi alimwonea huruma lakini pia
kwa dhati kabisa aliwapenda Adam na Christian. Eve
na mumewe Benny walikuwa watazamaji,wenyewe
hawakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi yoyote yale.
Christian alikuwa ametulia kwenye kochi, hali ya
utulivu aliyokuwa nayo ilipita siku zote.
“Adam tulipokutana unapajua,yote tuliyofanya
unayajua,upendo wangu kwako nadhani unautambua
pia……labda sikupangwa kuwa wako milele ndio
maana aliyepangwa amejitokeza wakati
muafaka,asante kwa zawadi ya penzi lako,asante kwa
mtoto na huu ujauzito hii ni heshima kubwa kwako
milele,neno gumu ninaloweza kulisema sasa ni kuwa
kwa moyo mmoja nakuruhusu uendelee na
Reshmail,nayasema haya mbele ya mama yangu
Eveline”
Alizungumza Bite kisha akashindwa kujizuia kuangua
kilio kikuu kilichoamsha hisia za kila mtu pale ndani
wote wakadondosha machozi yao. Adam,Reshmail na
Bite wote kwa pamoja wakakumbatiana huku machozi
yao yakitua juu ya Christian aliyekuwa katikati
yao,ilikuwa ni picha ya kusisimua na kuumiza sana.
****** *****
Kilikuwa kikao kikubwa cha familia yao Reshmail,watu
wote muhimu walikuwemo kasoro mama wa familia
hiyo aliyesusia kikao,mzee
Manyama,Reshmail,Eve,Benny,Bit e,na Paskalina
walikamilisha kikao hichi,Christian alikuwa bustanini
akibembea.
Reshmail alikuwa anatoa siri nzito nzito za
kushangaza ambazo kwa namna kubwa kabisa zilitoa
taswira ya mambo yaliyokuwa yamefichika kwa muda
mrefu,uhusiano wa kimapenzi kati yake na mama yake
mzazi ulimwacha kila mtu mdomo wazi,Reshmail
aliomba msamaha kwa hilo na alieleweka na
kusamehewa. Ni katika usimuliaji wa upande wa Bite
kuhusu ngome ya vigogo iliyoleta fikra za mazingira ya
kupotea kwa kadi yake ya benki katika mazingira ya
utata mkubwa,Benny hakuongea neno kwani yeye
alikuwa kama mgeni tu katika mkutano huo.
Mzee Manyama alikuwa kimya akimtafakari mkewe
kwa maovu aliyoifanyia familia yake,kwa mateso
aliyompa Adam na kwa uvunjifu wa amani aliouleta
baina ya familia hizi mbili,kwa fedheha aliyomletea na
kumvunjia heshima yake bungeni na hata
mtaani,akiwa mwingi wa hasira alisimama bila kuaga
na kuelekea chumbani,kwa hali aliyokuwa nayo
Reshmail aliamua kumfata kwa nyuma ili asije kufanya
jambo baya huko anapoenda,hasira yake ilipokelewa
na na mwili wa mkewe ukiwa sakafuni,tayari alikuwa
maiti.
“ulistahili hukumu hii” bila kushtuka alisema mzee
Manyama huku akimpisha Reshmail aingie humo
ndani.
*** ******* *****
Mapema baada ya mazishi ya mama yake mzazi
Reshmail akiongozana na Adam katika gari ya baba
yake,dereva akiwa Adam walifunga safari ya kwenda
Mwanza kwa wazazi wake (Adam).
“utabaki ndani ya gari nitatangulia mimi najua
watakuwa wakali hao lakini wakikuona ndipo mzizi wa
fitna utakapokuwa umekatwa” Reshmail alimpa
maelekezo Adam ambaye alikubali kwa ishara ya
kutikisa kichwa.
Gari ilipaki nje kidogo ya nyumba ya kina Adam,kama
walivyoelewana akashuka Reshmail akiwa
amependeza sana,akaifunga gari kwa kutumia rimoti
aliyoshuka nayo na kwa mwendo wa kunyata akaanza
kuusogelea mlango akausukuma akaingia
ndani,kupitia kwenye kioo Adm lishuhudi Reshmail
akitoweka machoni pake.
“umefata nini hapa we mchawi Adam hajakutosha
unamtaka na Rosemary ngoja sasa….Rose!!!!”
Aliita mama Adam,Reshmail akiwa anatabasamu
kwani alijua ni muda mfupi wote watakuwa na furaha
kubwa.
Akiwa bado hajaanza kuongea alishuhudia mama
Adam akimfuata na kisu huku Rosemary akifika pale
na mwiko mkubwa,wakati huu akili yake ilifanya kazi
haraka akaanza kukimbia lakini nguo yake ndefu
ilimsaliti baada ya kunasa kwenye geti la kutokea nje.
Kwa macho yake mawili Adam alishuhudia Reshmail
akiwa chini huku watu wawili wakimshambulia kwa
fujo,alijaribu kufungua mlango lakini ulikuwa
umewekwa ‘loki’ sauti yake haikuweza kusikika nje
alipigapiga vioo vya gari lakini hakuna aliyemsikia.
Alishuhudia damu nyingi sana ikiruka juu. Kwa akili ya
haraka haraka akakumbuka kushusha kioo akatokea
dirishani
“mamaaaaaaaaaaaaaaa!!!” Adam akaita kwa nguvu
palepale mama yake akageuka na kudondosha kisu
alichokuwa nacho,
”Adam mwanangu ni wewe!!!”
Alisema mama Adam huku aimfuata Adam ambaye
hakumjali bali alifika alipokuwa Reshmail
“Reshmail,Reshmail”
“ mama na dada mmemuua mke wangu jamani
mamaaaa!!” alilia Adam baada yakuona hajibiwi kitu.
”A.d….am!! ninaku….fa mume wangu….ninakufa kwa
furaha…..ni..meku..rudish…sha kwenu…naku…
panda..sana”
Reshmail aliongea kwa kujiumauma huku akivuja
damu,raia wengine walikuwa katika harakati za
kutafuta msaada lakini msaada mkubwa uliopatikana
ni wa polisi waliowatia nguvuni mama Adam na
mwanae Rosemary huku roho ya Reshmail ikimaliza
muda wake palepale Igoma jijini Mwanza.
kama usingekuwa ujasiri wa Adam basi tukio lile
lingegharimu maisha yake,tayari mama mkwe
amepotea,na sasa mpenzi wake Reshmail,mama na
mdogo wake wakitupwa jela kwa kesi ya mauaji.
**** **** **** *****
“mapenzi yamenipotezea muda wangu nimekuwa
mfungwa miaka mitano, mapenzi yameivunja vunja
familia yangu, mwanamke niliyempenda ametoweka
tayari tena mbele ya macho yangu,ni heri niisome hii
sheria vizuri zaidi ili ikiwezekana siku moja niwatetee
ndugu zangu walioko gerezani hao pekee ndio furaha
yangu, kamwe siwezi kuhangaika tena na watoto wa
hapa chuoni hata siku moja sidhani kama wana
maana sana kwangu nikithubutu tena huenda
yatakuwa makubwa zaidi ya awali.”
Alimaliza simulizi yake Adam.
……………MWISHO………………